By Julius Bett

LIVE: Ligi Kuu Bara

18/01/17 Reverse order Timestamp format


 1. Heka heka za mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Simba na Yanga zinaendelea katika mitaa mbalimbali

  JB Julius Bett
 2. Simba imewasili tayari

  JB Julius Bett
 3. Simba wakiondoka uwanja wa ndege

  JB Julius Bett
 4. Simba wakiingia kwenye basi lao

  JB Julius Bett
 5. tizi la simba

  JB Julius Bett
 6. Yanga ikijifua tayari kwa mchezo dhidi ya Simba

  JB Julius Bett
 7. Mechi ya Azam v Mbeya City kuchezwa usiku kwenye Uwanja wa AzamComplex, Chamazi

  JB Julius Bett
 8. Wachezaji wa Yanga wakitoka uwanjani

  JB Julius Bett
 9. Kiungo wa Yanga, Tshishimbi akimtoka Kichuya wa Simba katika mchezo wa Ngao ya Jamii

  JB Julius Bett
 10. Mashabiki wa Simba wamenoga kinoma

  JB Julius Bett
 11. Mashabiki wa Yanga wamelipuka

  JB Julius Bett
 12. Wachezaji wa Yanga, Simba hao

  JB Julius Bett
 13. Mtu aende mpira ubaki

  JB Julius Bett
 14. Mashabiki Yanga, Simba wachangamkia tiketi za mechi ya watani wa jadi

  JB Julius Bett
 15. Angalia mwenyewe changamkia tiketi bei poa kabisa

  JB Julius Bett
 16. Hapa Papy Tshishimbi kule Haruna Niyonzima unakoseja sasa kuwepo uwanjani mechi tamu kama hiii

  JB Julius Bett
 17. Mageti mawili Yanga imewaambia mashabiki wake 12,000 wanaoingia kwenye mechi hiyo wawahi mapema huku Simba nao ikiwahamasisha wa kwao hivyohivyo. Lakini serikali imesisitiza kwamba tiketi zichapishwe kulingana na uwezo wa Uwanja na isizidi hata nukta.

  JB Julius Bett
 18. GUMZO kubwa la mechi ya leo Jumamosi ni uwezo wa Uwanja wa Uhuru kuhimili wingi wa mashabiki wa Simba na Yanga. Ni miaka 10 sasa tangu mechi ya watani hao ilipochezwa kwa mara ya mwisho kwenye Uwanja huo wa Serikali.

  JB Julius Bett
 19. Hili limepelekea mtanange huo wa heshima zaidi nchini kupelekwa Uhuru wenye uwezo wa kubeba mashabiki 22,000 tu, hivyo kuwanyima fursa mashabiki 38,000 ambao wangeweza kuingia uwanjani kama mchezo ungekuwa Taifa.

  JB Julius Bett
 20. Mageti yatakayotumika ni mawili, yote yenye mfumo wa tiketi za kielektroniki. Mageti hayo yana jumla ya milango midogo 20 ya kuingilia hivyo kutoa fursa ya watu wengi kuingia ndani ya muda mfupi. Mageti mengine mawili yaliyopo mbele ya uwanja wa Uhuru, yatatumika kwa mashabiki waliokata tiketi za VIP.

  JB Julius Bett
 21. Kwa wale wa mzunguko, wataingilia geti la nyuma ya uwanja wa uhuru (in door), ambalo linaelekea kwenye uwanja wa ndani wa Taifa. Geti jingine ni lile la kuingilia mashabiki wa Yanga la Uwanja wa Taifa. Mageti hayo mawili yatatumiwa na mashabiki zaidi ya 20,000 watakaokata tiketi za mzunguko.

  JB Julius Bett
 22. Licha ya udogo wa Uwanja wa Uhuru, Polisi zaidi ya 350 watakuwepo kuhakikisha usalama unakwenda vizuri. Kwa mechi zinazochezwa Taifa, Maofisa hao wa Polisi huwa 400.

  JB Julius Bett
 23. Okwi amefunga mabao nane kwenye Uwanja wa Uhuru je leo ataona nyavu za Yanga

  JB Julius Bett
 24. Ajib amefunga mabao matano katika Ligi Kuu hadi sasa magoli hayo amefunga kwenye viwanja tofauti. Je leo ataifunga timu yake ya zamani

  JB Julius Bett
 25. 'Tetemeko la Kati'.

  Ndiyo ni tetemeko la kati. Unadhani nini kitatokea wakati kocha Joseph Omog wa Simba akiwaweka katikati Jonas Mkude na James Kotei halafu mbele yake kushoto na kulia akawaweka viungo wengine; Haruna Niyonzima, Mohammed Ibrahim na Mzamiru Yassin? Unadhani hakutakuwa na tetemeko katikati ya uwanja, iwapo kocha George Lwandamina wa Yanga akijibu mapigo naye akaamua kuwapanga viungo; Papy Kabamba 'Tshishimbi', Thabani Kamusoko, Raphael Daud, Pius Buswita na Said Juma 'Makapu'. Wenye uwezekano mkubwa wa kuanza ni Tshishimbi, Buswita na Daudi. Eneo hili ndilo linalotwajwa kushika hatma kubwa ya mchezo huo ambao una historia kubwa zaidi nchini.

  JB Julius Bett
 26. Mchina apagawisha mashabiki wa Simba utawapenda

  JB Julius Bett
 27. Yanga kwa sebene ulazima uwakubali leo hatoki mtu hapa

  JB Julius Bett
 28. Mashabiki Yanga, Simba waonyesha soka si uadui hata kidogo

  JB Julius Bett
 29. Mwamuzi Simba

  Simba huenda ikatembelea nyota ya Mwamuzi, Elly Sasii ambaye katika mechi zao nne alizohusika, ni moja tu ambayo wamepoteza. Sasii ambaye ni mwamuzi bora wa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara, amekuwa na bahati na Simba katika mechi alizochezesha kama mwamuzi wa kati na hata zile alizokuwa mwamuzi wa akiba.

  JB Julius Bett
 30. Kikosi cha Simba leo

  28)Aishi Manula (18)Erasto Nyoni (15) Mohamed Hussein (6)Juuko Murushid (17)Method Mwanjali (3)James Kotei (25)Shiza Kichuya (19)Mzamiru Yassin (7)Emmanuel Okwi (11)Laudit Mavugo (8)Haruna Niyonzima SUB (30) Emmanuel Mseja (21)Ally Shomari (13)Said Hamisi (22)John Bocco (20)Jonas Mkude (24)Mwinyi Kazimoto (29) Nicholas Gyan

  JB Julius Bett
 31. Tiketi zipo TFF yawaita mashabiki kwenda uwanjani

  JB Julius Bett
 32. Omog rekodi nzuri

  Tangu Omog alipokabidhiwa kikosi cha Simba, Julai mwaka jana, amekutana na Yanga mara nne lakini ni kama ana zali kwani hajawahi kupoteza mchezo wowote. Inafurahisha sana. Rekodi zinaonyesha Omog amekuwa mbabe kwelikweli mbele ya Yanga. Katika mechi hizo, ameshinda moja na kupata sare tatu. Katika sare hizo mbili zikwenda kwenye mikwaju ya penalti na akashinda. Habari njema kwa watu wa Simba ni kwamba Omog hajawahi kupoteza kwa Yanga hata akicheza pungufu. Mechi mbili za Oktoba Mosi mwaka jana alipata sare ya bao 1-1 na Februari mwaka huu alishinda 2-1, zote akiwa pungufu. Mechi nyingine ilikuwa ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi ambapo Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti kisha kufanya hivyo tena katika pambano la Ngao ya Hisani.

  JB Julius Bett
 33. Lwandamina bado

  Kocha huyu Mzambia bado ana wakati mgumu na mechi za watani. Tangu amepewa kazi ya kuifundisha Yanga mwishoni mwaka jana amekutana na Simba mara tatu na zote ameambulia patupu.

  Amepata sare mbili moja katika nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi na nyingine katika pambano la Ngao ya Hisani. Lwandamina alipoteza pambano moja la Ligi Kuu Februari mwaka huu.

  JB Julius Bett
 34. Lwandamina, Omog wamekwenda shule

  Kimsingi Omog na Lwandamina ni makocha wa daraja la juu, ndani ya Ligi Kuu Bara. Omog amewahi kutwaa Kombe la Shirikisho Afrika wakati huo akiifundisha AC Leopard ya Congo-Brazaville wakati Lwandamina alifika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na Zesco.

  Omog ana leseni B ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA). Sio kocha wa mchezo mchezo. Kwa upande wa Lwandamina amepiga kitabu ile mbaya kwani ana leseni A ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

  JB Julius Bett
 35. Simba: Aishi Manula, Erasto Nyoni, Tshabalala, Juuko Murshid, Method Mwanjali (C), James Kotei, Mzamiru Yassin, Haruna Niyonzima, Laudit Mavugo, Emmanuel Okwi, Shiza Kichuya.

  JB Julius Bett

 36. Kichuya yupo

  Pamoja na macho yote kuwatazama Okwi na Ajib, rekodi zinaonyesha kuwa staa wa Simba, Shiza Kichuya ndiye hatari zaidi kwenye mechi za watani kwa sasa akiwa amefunga mara zote mbili alizocheza katika michezo ya Ligi Kuu. Kichuya aliifungia Simba bao la kusawazisha Oktoba mwaka jana kabla ya kufunga la ushindi wakati Yanga ikifa 2-1 Februari mwaka huu.

  JB Julius Bett
 37. Basi la Yanga limewasili kwenye Uwanja wa Uhuru

  JB Julius Bett
 38. Basi la Simba limeingia uwanjani sasa

  JB Julius Bett
 39. Mashabiki wa Yanga wakiwa jukwaani Uwanja wa Uhuru

  JB Julius Bett
 40. Mashabiki wa Simba wakiwa wamejitokeza Uwanja wa Taifa

  JB Julius Bett
 41. Basi la Simba baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Uhuru

  JB Julius Bett
 42. Makonde yamerushwa na walinzi wa timu za Simba na Yanga maarufu kama Makomandoo wakati klabu hizo mbili zilipokuwa zinaingia uwanjani kabla ya pambano lao kuanzia kwenye uwanja wa Uhuru, saa 10.00 jioni.

  JB Julius Bett
 43. Yanga (4-3-3): Youthe Rostand, Juma Abdul (C), Gadiel Michael, Andrew Vincent, Kelvin Yondani, Papy Tshishimbi, Raphael Daud, Pius Buswita, Ibrahim Ajib, Obrey Chirwa, Geofrey Mwashiuya.

  Simba (4-4-2): Aishi Manula, Erasto Nyoni, Mohamed Hussein, Juuko Murushid, Method Mwanjali, James Kotei, Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, Emmanuel Okwi, Laudit Mavugo, Haruna Niyonzima

  JB Julius Bett
 44. Timu zinaingia uwanjani zimejipanga tayari kwa kusalimiana


  JB Julius Bett
 45. Yanga inawakosa Ngoma, Kamusoko, Tambwe katika mchezo wa leo

  JB Julius Bett
 46. Nahodha wa Yanga leo ni Kelvin Yondani, wakati Simba ni method Mwanjali

  JB Julius Bett
 47. Ajib ndiye kinara wa ufungaji wa Yanga akiwa na mabao matano wakati Simba kinara wa ufungaji ni Okwi na mabao nane

  JB Julius Bett
 48. Simba inaanza mpira

  JB Julius Bett
 49. Dakika kwanza, Mavugo anapiga shuti linalokwenda juu

  JB Julius Bett
 50. Simba imeanza mechi kwa kasi kulishambulia lango la Yanga

  JB Julius Bett
 51. Simba wanamiliki mpira kwa kucheza pasi nyingi, lakini wakiwa kwenye upande wao

  JB Julius Bett
 52. Dakika ya 5: Yanga 0-0 Simba

  JB Julius Bett
 53. Kipa wa Yanga, Rostand anaokoa krosi ya Elasto Nyoni

  JB Julius Bett
 54. Dakika 6: Ajib anaotoa. Yanga inacheza mpira wa kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza

  JB Julius Bett
 55. Dakika 7:Juma Abdul anapiga faolu lakini ameshindwa kuwa na madhara langoni mwa Simba

  JB Julius Bett
 56. Dakika 10: Yanga 0-0 Simba. Timu zote zinajaribu kucheza mpira katikati

  JB Julius Bett
 57. Chirwa na Juuko wanaonyesha ubabe wa hali ya juu

  JB Julius Bett
 58. Dakika 11: Yanga inapata faulo inayopigwa na Ajib, lakini inaokolewa na mabeki wa Simba

  JB Julius Bett
 59. Ushindani mkubwa katika mchezo huu hadi sasa upo kwa beki wa SImba, Juuko dhidi ya Mzambia Chirwa wa Yanga wawili hawa mara kadhaa wamekuwa wakishinda kwa nguvu na ushindani wa hali ya juu

  JB Julius Bett
 60. Dakika 16: Yanga 0-0 Simba. Kipa wa Simba, Aishi Manura anabadilisha glovu zake

  JB Julius Bett
 61. Dakika 18: Simba inapata kona lakini krosi ya Okwi inaapa juu ya goli la Yanga

  JB Julius Bett
 62. Haruna Niyonzima wa Simba leo anakibarua kizito mbele ya swahiba wake Juma Abdul wa Yanga upande wa kushoto wa Simba

  JB Julius Bett
 63. Dakika 20: Yanga 0-0 Simba

  JB Julius Bett
 64. Dakika 22; Okwi anakosa bao kwa mpira wa kichwa kupaa juu. Yanga inajibu mapigo kwa shuti la Mwashiuya kupanguliwa na kipa wa Simba

  JB Julius Bett
 65. Yanga sasa imeanza kujiamini na kulishambulia lango la Simba wakitumia upande wa Mwashiuya

  JB Julius Bett
 66. Niyonzima amebadili upande ametoka kushoto na kuja upande wa kulia huku Kichuya akienda eneo lake

  JB Julius Bett
 67. Yondani alitaka kufanya makosa baada ya kusubili mpira utoke nje, lakini Mavugo aliuwahi na kupiga goli kabla ya Dante kuokoa

  JB Julius Bett
 68. Tshishimbi anapiga shuti la umbali wa mita 18, lakini kipa Manura anafanya kazi nzuri kuokoa mpira na kuwa kona

  JB Julius Bett
 69. Chirwa amemtoka Mohamed Hussein na kupiga shuti lililopita golini na mpira kutoka nje

  JB Julius Bett
 70. Hadi dakika 35: Kocha wa Yanga, Lwandamina amefanikiwa kwa mbinu zake baada ya kuwashika vilivyo Simba katikati ya uwanja

  JB Julius Bett
 71. Ajib anachezewa vibaya na Kotei

  JB Julius Bett
 72. Dakika 40: Yanga 0-0 Simba. Tshishimbi amefanikiwa kukata mawasiliano ya Muzamiru na safu yake ya ushambuliaji jambo linalowapa nafuu mabeki wa Yanga

  JB Julius Bett
 73. Dakika 45; Yanga 0-0 Simba. Imeongezwa dakika moja kabla ya kulipulizwa kwa filimbi ya mapumziko

  JB Julius Bett
 74. Mapumziko Yanga 0-0 Simba

  JB Julius Bett
 75. Hadi sasa kutokana na ubora wa vikosi vya timu zote. Lwandamina amefanikiwa kutokana timu yake kushambulia na vizuri na kupiga mashuti mengi yaliyolenga lango kulinganisha na Simba

  JB Julius Bett
 76. Kocha wa Simba, Omog anatakiwa kuzungumza na washambuliaji wake katika dakika 45 wameshindwa kupiga shuti lolote lililolenga lango pamoja na kumiliki mpira kwa asilimia 55 dhidi 45 za Yanga

  JB Julius Bett
 77. Timu zinarudi uwanjani tayari kuanza kwa kipindi cha pili

  JB Julius Bett
 78. Kipindi cha pili kimeanza hakuna mabadiliko kwa timu zote

  JB Julius Bett
 79. Beki wa Yanga, Andrew Vincent 'Dante' amefanikiwa kumzibiti vilivyo mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi hadi sasa

  JB Julius Bett
 80. Niyonzima ameumia baada ya kugongana na Juma Abdul ikiwa nje kidogo ya eneo la 18 la Yanga

  JB Julius Bett
 81. Okwi anapiga faulo hiyo inagonga ukuta wa Yanga na kurudi uwanjani. Dakika 50: Yanga 0-0 Simba

  JB Julius Bett
 82. Dante na Okwi leo ni mwendo wa Chama na Mogella

  JB Julius Bett
 83. John Bocco anapasha kwa upande wa Simba

  JB Julius Bett
 84. Chirwa anatoa pasi kwa Ajib anatoa kwa Mwashiuya anapiga shuti linalopanguliwana Manura na kuwa kona

  JB Julius Bett
 85. Simba wamemtoa Mavugo nafasi yake inachukuliwa na Bocco

  JB Julius Bett
 86. Gooooooooo Kichuyaaaaaaaaa anaipatia Simba bao la kuongoza dakika 57

  JB Julius Bett
 87. Kichuya anafunga bao hilo baada ya krosi ya Okwi kupanguliwa na kipa wa Yanga na kumkuta Nyoni aliyerudisha mpira uwanjani na kumkuta Kichuya aliyetumbukiza mpira wavuni

  JB Julius Bett
 88. Goooooo, Chirwa anaisawazishia Yanga dakika 60

  JB Julius Bett
 89. Yanga ilipata bao hilo baada ya Yondani kupiga mpira mrefu uliomkuta Ajib ambaye alitoa pasi kwa Mwashiuya aliyepisha krosi ya chini iliyompita Manura na kumkuta Chirwa aliyetumbukiza mpira wavuni

  JB Julius Bett
 90. Yanga wanafanya mabadiliko wanamtoa Mwashiuya na kuingia Martin

  JB Julius Bett
 91. Bao la Simba limedumu kwa dakika tatu kabla ya Yanga kusawazisha na kufanya timu zote kuanza kujipanga upya

  JB Julius Bett
 92. Dakika 65: Yanga anamtoa Raphael Daud anaingia Pato Ngonyani

  JB Julius Bett
 93. Mabao yote lile la Yanga na Simba limetokana na uzembe wa makipa kushindwa kuzuia krosi zilizopita katikati ya magoli yao

  JB Julius Bett
 94. Ajib amepewa kadi ya njano

  JB Julius Bett
 95. Dakika 69: Ajib anapiga shuti la moja kwa moja akiunganisha krosi ya Tshishimbi

  JB Julius Bett
 96. Martin anaikosesha Yanga bao baada ya shuti lake kupanguliwa na kipa Manura na kuwa kona

  JB Julius Bett
 97. Kichuya amethibisha yeye ndiye kiboko ya Yanga

  Pamoja na macho yote kuwatazama Okwi na Ajib, rekodi zinaonyesha kuwa staa wa Simba, Shiza Kichuya ndiye hatari zaidi kwenye mechi za watani kwa sasa akiwa amefunga mara zote mbili alizocheza katika michezo ya Ligi Kuu.

  Kichuya aliifungia Simba bao la kusawazisha Oktoba mwaka jana kabla ya kufunga la ushindi wakati Yanga ikifa 2-1 Februari mwaka huu.

  JB Julius Bett
 98. Simba imemtoa Kotei nafasi yake imechukuliwa na Jonas Mkude dakika 76

  JB Julius Bett
 99. Dakika 78: Yanga 1-1 Simba

  JB Julius Bett
 100. Baada ya mabao timu zote zinaonekana kucheza kwa umakini zaidi na kushambulia kwa kushtukiza

  JB Julius Bett
 101. Kama matokeo yatakuwa hivi, Lwandamina atakuwa akiendeleza rekodi yake ya kutoifunga Simba tangu alipotua Yanga

  JB Julius Bett
 102. Dakika 87: Yanga 1-1 Simba. Simba imemtoa Muzamiru ametoka ameingia Said Ndemla

  JB Julius Bett
 103. Kocha wa Simba, atakuwa akiendeleza rekodi yake ya kutopoteza dhidi ya Yanga. Rekodi zinaonyesha Omog amekuwa mbabe kwelikweli mbele ya Yanga. Katika mechi hizo, ameshinda moja na kupata sare tatu. Katika sare hizo mbili zikwenda kwenye mikwaju ya penalti na akashinda.

  JB Julius Bett
 104. Dakika 90 zimeongezwa mbili Yanga 1-1 Simba

  JB Julius Bett
 105. Kona inapigwa na Ajib

  JB Julius Bett
 106. Mpira umekwisha Yanga 1-1 Simba

  JB Julius Bett
 107. Msimamo Ligi Kuu Tanzania Bara 2017-2018

  P W D L F A PTS

  1. Simba 8 4 4 0 20 5 16

  2.Yanga 8 4 4 0 11 4 16

  3.Azam 8 4 4 0 6 2 16

  4.Mtibwa 7 4 3 0 7 3 15

  5.Singida 7 3 3 1 6 4 12

  6.Mbeya 8 3 2 3 9 8 11

  7.Prisons 7 2 4 1 8 6 10

  8.Lipuli 7 2 3 2 4 4 9

  9.Ndanda 7 2 3 2 4 4 9

  10.Mbao 7 1 4 2 8 9 7

  11.Mwadui 7 1 3 3 7 12 6

  12.Njombe 7 1 2 4 3 9 5

  13.Ruvu 7 0 5 2 3 12 5

  14.Majimaji 7 0 4 3 4 7 4

  15.Stand 7 1 1 5 3 10 4

  16.Kagera 7 0 3 4 3 7 3

  JB Julius Bett
 108. Msimamo Ligi Kuu Tanzania Bara 2017-2018

  P W D L F A PTS

  1. Simba 8 4 4 0 20 5 16

  2.Yanga 8 4 4 0 11 4 16

  3.Mtibwa 8 4 4 0 7 3 16

  4.Azam 8 4 4 0 6 2 16

  5.Singida 8 3 4 1 6 4 13

  6. Lipuli 8 3 3 2 6 5 12

  7. Mbeya 8 3 2 3 9 8 11

  8. Prisons 7 2 4 1 8 6 10

  9.Ndanda 8 2 3 3 5 6 9

  10.Mbao 8 1 4 3 9 11 7

  11.Mwadui 8 1 4 3 8 13 7

  12.Kagera 8 1 3 4 5 8 6

  13. Njombe 8 1 3 4 3 9 6

  14.Majimaji 8 0 5 3 5 8 5

  15.Stand 8 1 2 5 3 10 5

  16.Ruvu 7 0 5 2 3 12 5

  * Kabla ya mechi ya leo Jumatatu

  JB Julius Bett
 109. Mechi ya Prisons dhidi ya Ruvu Shooting inaendelea kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya

  JB Julius Bett
 110. Dakika 19, Mohamed Rashid anaipatia Prisons bao la kuongoza baada ya kumtoka beki wa Ruvu Shooting, Yusuph Nguya na kupiga shuti lililomshinda kipa Bidii Hussein na kujaa wavuni

  JB Julius Bett
 111. Dakika 24: Prisons 1-0 Ruvu Shooting

  JB Julius Bett
 112. Dakika 30: Prison 1-0 Ruvu Shooting. Wageni Shooting wanajitaidi kushambulia kusaka bao la kusawazisha, lakini washambuliaji wake wanakosa utulivu wanapofika langoni mwa Prisons

  JB Julius Bett
 113. Ruvu Shooting inashikiria mkia katika msimamo wa ligi ikiwa haijashinda mchezo wowote tangu kuanza kwa ligi hiyo. imefunga mabao matatu (3) na kufungwa 12 katika mechi saba

  JB Julius Bett
 114. Mshambuliaji wa Ruvu, Abdulrahaman Musa aliyekuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita hajafunga bao lolote katika mechi saba zilizopita

  JB Julius Bett
 115. Dakika 40: Prisons 1-0 Ruvu Shooting

  JB Julius Bett
 116. Kama Prisons itashinda mchezo huu itafikisha pointi 13 na kuishusha Singida United katika nafasi ya 5 kwa tofauti ya mabao ya kufunga

  JB Julius Bett
 117. Dakika 45 mapumziko: Prisons 1-0 Ruvu Shooting. Bao la Mohamed Rashid ndiyo kitu pekee kilicholeta tofauti ya mchezo huu hadi sasa baada ya timu zote kucheza mpira mwingi katikati ya uwanja, na kutengeneza nafasi chache za kufunga

  JB Julius Bett
 118. Kipindi cha pili kimeanza. Prison 1-0 Ruvu Shooting

  JB Julius Bett
 119. Dakika 50: Prisons 1-0 Ruvu Shooting, bado timu zote mbili zinaendelea kucheza mpira wa nguvu, lakini zinashindwa kutengeneza nafasi za kufunga

  JB Julius Bett
 120. Dakika 60: Prisons 1-0 Ruvu Shooting

  JB Julius Bett
 121. Dakika 70: Ruvu imechangamka kusaka bao la kusawazisha

  JB Julius Bett
 122. Kipa wa Prisons anaumia anapatiwa matibabu uwanjani

  JB Julius Bett
 123. Prisons imemtoa Eliuter Mpepo nafasi yake kuchukuliwa na Julius Kwanga. Mabadiliko ambayo bado hayajaisaidia Prisons kwani Ruvu Shooting wanaliandama lango lao

  JB Julius Bett
 124. katika pindi cha pili Ruvu Shooting ilipata kona nne mfululizo, lakini wameshindwa kuzitumia

  JB Julius Bett
 125. Dakika 75; Ruvu inamtoa Baraka Mtui nafasi yake kuchukuliwa na Said Dilunga

  JB Julius Bett
 126. Dakika 80: Ruvu wanaendelea kulisakama lango la Prisons lakini bado washambuliaji wake wanakosa umakini kwenye umaliziaji

  JB Julius Bett
 127. Salum Kimenya wa Prisons anapewa kadi ya njano dakika 82, inakuwa faulo ambayo inashindwa kutumiwa vizuri na Ruvu Shooting

  JB Julius Bett
 128. Dakika 85: Prisons 1-0 Ruvu Shooting

  JB Julius Bett
 129. Prisons inamtoa Fredy Kichudu nafasi yake inachukuliwa na Salum Bosco dakika 85

  JB Julius Bett
 130. Usahihi aliyetoka Prisond ni Fredy Chudu na siyo Fredy Kichudu

  JB Julius Bett
 131. Dakika 88: Prisons 1-0 Ruvu. Kama mechi itakwisha hivi basi Prisons itakuwa inashinda mchezo wake wa kwanza nyumbani tangu kuanza kwa msimu huu

  JB Julius Bett
 132. Dakika 90 sasa zimeongezwa dakika tano. Prisons 1-0 Ruvu

  JB Julius Bett
 133. Mpira umekwisha Prison 1-0 Ruvu Shooting

  JB Julius Bett
 134. Msimamo Ligi Kuu Tanzania Bara 2017-2018

  P W D L F A PTS

  1. Simba 8 4 4 0 20 5 16

  2.Yanga 8 4 4 0 11 4 16

  3.Mtibwa 8 4 4 0 7 3 16

  4.Azam 8 4 4 0 6 2 16

  5.Prisons 8 3 4 1 9 6 13

  6.Singida 8 3 4 1 6 4 13

  7.Lipuli 8 3 3 2 6 5 12

  8.Mbeya 8 3 2 3 9 8 11

  9.Ndanda 8 2 3 3 5 6 9

  10.Mbao 8 1 4 3 9 11 7

  11.Mwadui 8 1 4 3 8 13 7

  12.Kagera 8 1 3 4 5 8 6

  13.Njombe 8 1 3 4 3 9 6

  14.Majimaji 8 0 5 3 5 8 5

  15.Stand 8 1 2 5 3 10 5

  16.Ruvu 8 0 5 3 3 13 5

  JB Julius Bett
 135. Mechi ya Singida United v Yanga imeanza ikiwa dakika 5, lakini timu zote mbili zimekosa utulivu katika mchezo huu hakuna shambulio lolote la maana lililofanywa

  JB Julius Bett
 136. Dakika 6; Singida 0-0 Yanga

  JB Julius Bett
 137. Dakika 10: Singida 0-0 Yanga; Mpira unachezwa katikati zaidi hadi sasa hakuna shuti lolote lililolenga lango la timu yoyote

  JB Julius Bett
 138. Dakika 12: Ajib anakosa bao kwa mpira wake wa adhabu kutoka juu kidogo ya goli la Singida

  JB Julius Bett
 139. Mwashiuya anapoteza nafasi nzuri ya kuifungia Yanga baada ya shuti lake kutoka nje wakati kipa wa Singida, Manyika akiwa hayupo golini

  JB Julius Bett
 140. Yanga wamekuwa hatari zaidi wakipitisha mashambulizi yao kutokea upande wa kushoto, lakini bado wanakosa umakini katika umaliziaji

  JB Julius Bett
 141. Dakika 20: Singida 0-0 Yanga; Timu zote zimejaza viungo hivyo muda mwingi mpira umekuwa ukichezwa katikati ya uwanja

  JB Julius Bett
 142. Kaseke ameshindwa kutumia vizuri nafasi mbili alizozipata kuipatia Singida bao la kuongoza

  JB Julius Bett
 143. Dakika 22: Yanga inapata mpira wa adhabu nje kidogo ya eneo la 18,baada ya Mwashiuya kuangushwa

  JB Julius Bett
 144. Ajib anapiga faulo hiyo ni eneo linafanana na lile alilofunga bao dhidi ya Stand United, lakini ukuta wa Singida unakuwa makini kuokoa hatari hiyo.

  JB Julius Bett
 145. Beki wa Singida, Salum Kipaga anafanya kazi kubwa kumdhibiti mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa

  JB Julius Bett
 146. Dakika 27: Singida 0-0 Yanga

  JB Julius Bett
 147. Dakika 30: Singida 0-0 Yanga

  JB Julius Bett
 148. Dakika 35: Singida 0-0 Yanga; Mabeki wa SIngida wamefanikiwa kuwadhibiti livyo washambuliaji wa Yanga, Ajib, Chirwa pamoja na kuhakikisha Tshishimbi hapati muda mwingi wa kukaa na mpira.


  JB Julius Bett
 149. Bado dakika tano kabla ya mapumziko Singida 0-0 Yanga

  JB Julius Bett
 150. Mshambuliaji wa Singida, Daniel Usingimana alipata nafasi nzuri lakini shuti lake limedakwa na kipa wa Yanga

  JB Julius Bett
 151. Dakika 45; zimeongezwa dakika mbili kabla ya mapumziko

  JB Julius Bett
 152. Singida wanatumia udhaifu wa beki wa Yanga, Hassan Kessy anayecheza mechi yake ya kwanza msimu huu kupitisha mashabulizi yao

  JB Julius Bett
 153. Mapumziko Singida 0-0 Yanga

  JB Julius Bett
 154. Matokeo katika michezo mingine hadi sasa mapumziko

  Njombe 0-0 Mbao

  Ndanda 0-0 Mtibwa

  Kagera 1-0 Prisons

  JB Julius Bett
 155. Kipindi cha pili kinaanza: Singida 0-0 Yanga

  JB Julius Bett
 156. Kaseke anapewa kadi ya njano kwa kujiangusha

  JB Julius Bett
 157. Dakika 50: Singida 0-0 Yanga

  JB Julius Bett
 158. Dakika 50: Singida inapata kona ya pili

  JB Julius Bett
 159. Kona ya tatu kwa Singida, lakini wenyeji hao pamoja na kuwa na wachezaji warefu bado wameshindwa kutumia mipira ya juu kuipenya ngome ya Yanga yenye mabeki wafupi Yondani na Andrew Vicent

  JB Julius Bett
 160. Ubovu wa nyavu unataka kuzua utata, lakini umakini wa mwamuzi unasaidia kuweka mambo sawa na kukataa bao hilo la Singida United dakika 55.

  JB Julius Bett
 161. Yanga inamtoa Mwashiuya na kuingia Emmanuel Martin dakika 58

  JB Julius Bett
 162. Dakika 63: Singida 0-0 Yanga; Kocha Pluijm amefanikiwa kuifundi kuwadhibiti viungo wa Yanga

  JB Julius Bett
 163. Kocha wa Singida anamtoa Deus Kaseke mwenye kadi ya njano na nafasi yake kuchukuliwa na Michelle Katsvairo

  JB Julius Bett
 164. Chirwa anapewa kadi ya njano kwa kujiangusha katika eneo la penalti dakika 66; Singida 0-0 Yanga

  JB Julius Bett
 165. Dakika 70: Singida 0-0 Yanga

  JB Julius Bett
 166. Beki Salum Kipaga ameumia na kutolewa nje kwa upande wa Singida nafasi yake inachukuliwa na Rolland Msonjo. Dakika 72: Singida 0-0 Yanga

  JB Julius Bett
 167. Dakika 75: Kigi Makassi wa Yanga anafanyiwa faulo

  JB Julius Bett
 168. Kipa wa Yanga ameumia yupo chini pamoja na mshambuliaji wa Singida wote wawili wanafanyiwa matatibabu uwanjani

  JB Julius Bett
 169. Dakika 81: Kwenye uwanja wa Namfua kila timu inaokana kulizika na matokeo hivyo zinacheza kwa umakini

  JB Julius Bett
 170. Singida inamuingiza Atupele Green kuchukua nafasi ya Usengimana dakika 82

  JB Julius Bett
 171. Dakika 87: Baadhi ya mashabiki wameanza kuondoka kwenye Uwanja wa Namfua

  JB Julius Bett
 172. Yanga wanamtoa Pato Ngonyani anaingia Raphael Daud dakika 88

  JB Julius Bett
 173. Dakika 6 za nyongeza kwenye Uwanja wa Namfua. Singida 0-0 Yanga

  JB Julius Bett
 174. Mpira umekwisha Singida United 0-0 Yanga; Njombe 0-0 Mbao; Ndanda 0-0 Mtibwa; Kagera 1-1 Prisons

  JB Julius Bett