#Bajeti2018

23/10/15 Reverse order Timestamp format


 1. Lowassa - Ifakara - Sumaye: Kenya, Nigeria, Zambia wananchi wamefanya maamuzi ya kuondoa vyama tawala madarakani kwa kuwa vilikuwa haviwajali

  JB Julius Bett
 2. Lowassa akihutubia Ifakara

  JB Julius Bett
 3. LOWASSA- IFAKARA

  Si ajabu ajabu tukasikia siku ya kura mawasiliano nchi nzima yakakatika…hizi zote ni njama
  Sumaye
  JB Julius Bett
 4. LOWASSA- IFAKARA

  Utawala wa CCM umebakiza siku 2….tumetembea nchi nzima, watu wanataka mabadiliko
  Sumaye
  JB Julius Bett
 5. LOWASSA- IFAKARA

  Kazi ya polisi ni kulinda usalama wa wananchi…..tunataka wananchi wawe na uhuru wa kuamua kile wanachokitaka…hii nchi inatawaliwa na kwa ubeberu. Watu wananyanyaswa bila sababu
  Sumaye
  JB Julius Bett
 6. LOWASSA- IFAKARA

  Tusiogope Watanzania kubadilisha chama, tunataka tubadilishe chama. Tutaweka Chadema madarakani kwa miaka mitano, tuwapime kama wamefanikiwa. Kama bado, tuwatoe madarakani
  Sumaye
  JB Julius Bett
 7. LOWASSA-IFAKARA

  Kenya, Nigeria, Zambia wananchi wamefanya maamuzi ya kuondoa vyama tawala madarakani kwa kuwa vilikuwa haviwajali

  Sumaye

  JB Julius Bett
 8. LOWASSSA -IFAKARA

  Chukua mtu wa CUF, NCCR au Chadema uende naye akusaidia kupiga kura kama unahitaji msaaada. Usiokoteze mtu kwenye vituo. Chukua mtu unayemwamini akusaidie kupiga kura kama utashindwa.

  Sumaye

  JB Julius Bett
 9. CCM- JANGWANI

  Utaratibu wa kumpata mgombea urais mwaka huu ulitumika 1995, haujawahi kurekebishwa
  JK
  JB Julius Bett
 10. CCM- JANGWANI

  Nilifanya kampeni 2005 nilikuwa hoi kweli, lakini Magufuli ana nguvu bado
  JK
  JB Julius Bett
 11. CCM- JANGWANI

  Sipendi kulaumiwa kuwa chama kinaendeshwa vibaya
  JK
  JB Julius Bett
 12. CCM- JANGWANI

  Sina wasiwasi kuwa Watanzania watakuchagua Magufuli...anazo sifa zote
  JK
  JB Julius Bett
 13. CCM- JANGWANI

  Ni muadilifu, ni mwaminifu maana ukijumlisha vyote hivyo unanoga zaidi
  JK
  JB Julius Bett
 14. CCM- JANGWANI

  Ameahidi kupambana na rushwa. Hajamung'unya kutaja rushwa
  JK
  JB Julius Bett
 15. CCM- JANGWANI

  Magufuli ni mpenda watu, asiyechoka kufanya kazi. Ni makini
  JK
  JB Julius Bett
 16. CCM- JANGWANI

  Anapenda vijana na ameonyesha namna atakavyokabiliana na matatizo yao ikiwa ni pamoja na kuboresha shule
  JK
  JB Julius Bett
 17. CCM- JANGWANI

  Ameainisha vitabu vitakavyopatikana na mikopo ya vyuo vikuu
  JK
  JB Julius Bett
 18. CCM- JANGWANI

  Nilikuta mikopo ni 15,000 kwa wanafunzi wa elimu ya Juu na sasa ni 98,000 na zaidi...
  JK
  JB Julius Bett
 19. CCM- JANGWANI

  Ajira kwa vijana-Magufuli anatengeneza mazingira mazuri ili awamu yake iwe ya viwanda. Viwanda vitaongeza ajira. Ni nani kama magufuli?
  JK
  JB Julius Bett
 20. CCM- JANGWANI

  Atatengeneza mazingira mazuri ya wafanyabiashara kwa kuwa anatengeneza uchumi wa viwanda
  JK
  JB Julius Bett
 21. CCM- JANGWANI

  Magufuli amesema atatetea akina mama, kwa nini msimpe kura?
  JK
  JB Julius Bett
 22. CCM- JANGWANI

  Magufuli anajali michezo...atatetea walemavu na wasanii.
  JK
  JB Julius Bett
 23. CCM- JANGWANI

  Atatutoa hapa na kuiwezesha Tanzania kufuzu Kombe la Dunia na la Afrika
  JK
  JB Julius Bett
 24. CCM- JANGWANI

  Anajali wafugaji na wafugaji kwa amaana kama asingesoma, angekuwa anafuga huko Usukumani na mkewe Janet
  JK
  JB Julius Bett
 25. CCM- JANGWANI

  Sifa za Magufuli jamani ni nyingi...Nadhani tuishie hapo ili Magufuli apate wasaa
  JK
  JB Julius Bett
 26. CCM- JANGWANI

  Nimalize kwa kusema tarehe 25 jitokezeni kupiga kura. Amani itakuwepo, hapatatokea chochote
  JK
  JB Julius Bett
 27. CCM- JANGWANI

  Wamekwenda kushtaki na wameshindwa. Mahakama imethibitisha mahali pa kupigia kura si pa kufanyia mikutano
  JK
  JB Julius Bett
 28. CCM- JANGWANI

  Ninawapongeza Wana-CUF, Chadema, ACT na wasio na chama
  Magufuli
  JB Julius Bett
 29. CCM- JANGWANI

  Nimetembea umbali wa KM 46,221 Tanzania
  Magufuli
  JB Julius Bett
 30. CCM- JANGWANI

  Watanzania wote wanaichukia rushwa. Nami nitasimama kidete kupambana na rushwa
  Magufuli
  JB Julius Bett
 31. CCM- JANGWANI

  Natambua kuwa Watanzania wanaichukia rushwa...Mwalimu Nyerere alishawahi kusema rushwa na hongo ni adui mkubwa kuliko vita
  Magufuli
  JB Julius Bett
 32. CCM- JANGWANI

  Rushwa inatakiwa kushughulikiwa kama uhaini. Nitamtanguliza Mungu mbele ili nchi hii iwe ya neema kwa wote
  Magufuli
  JB Julius Bett
 33. CCM- JANGWANI

  Ninafahamu umuhiwa muwa kuwa na viwanda...bila viwanda, hakuna ajira
  Magufuli
  JB Julius Bett
 34. CCM- JANGWANI

  Mazingira ya kuwa na viwanda yako vizuri sasa. Pamoja na changamoto ya umeme iliyopo, gesi itamaliza tatizo hili
  Magufuli
  JB Julius Bett
 35. CCM- JANGWANI

  Viwanda vinahitaji watu wa kufanya kazi. Hilo si tatizo. Wasomi wapo wa kutosha
  Magufuli
  JB Julius Bett
 36. CCM- JANGWANI

  Tumejipanga kwa awamu ya Tano kukabiliana na msongamano katika barabara za jiji la Dar es Salaam
  Magufuli
  JB Julius Bett
 37. CCM- JANGWANI

  Tutapanua Mwai Kibaki Road
  Magufuli
  JB Julius Bett
 38. CCM- JANGWANI

  Kuna fedha zaidi ya Dola 117milioni kuboresha Tandale, Mburahati, Mwananyamala, Keko, Mbagala, Yombo, Kijichi na Makangarawe kwa kiwango cha lami, taa nk
  Magufuli
  JB Julius Bett
 39. CCM- JANGWANI

  Pale Ubungo tutajenga barabara ya juu yaani ghorofa.. tumeshasaini mkataba wa zaidi ya sh100bilioni
  Magufuli
  JB Julius Bett
 40. CCM- JANGWANI

  Nawahakikishia madereva mikataba yao na wamiliki nitaishughulikia mlipwe kwa haki
  Magufuli
  JB Julius Bett
 41. CCM- JANGWANI

  Tunataka ushuru kwa wajasiriamali tuondoe. Tutapanga maeneo kwa ajili ya wafanyabiashara
  Magufuli
  JB Julius Bett
 42. CCM- JANGWANI

  Mniletee wabunge waliotambulishwa hapa na JK
  Magufuli
  JB Julius Bett
 43. CCM- JANGWANI

  Waendesha bajaji na bodaboda tutawaandalia njia maalum ya kuingia mjini ili nao wawe na uhuru wa kuingia katikati ya DSM
  Magufuli
  JB Julius Bett
 44. CCM- JANGWANI

  Mimi kwangu ni kazi tu.Kwangu ni kazi tu. nafahamu shida za Watanzania
  Magufuli
  JB Julius Bett
 45. CCM- JANGWANI

  Nimeamua kufanya kazi kweli kweli. Nitashughulikia maji
  Magufuli
  JB Julius Bett
 46. CCM- JANGWANI

  Dar inatakiwa kupata maji lita 500milioni na sasa inapata lita300milioni tu
  Magufuli
  JB Julius Bett
 47. CCM- JANGWANI

  Kuna mradi unakuja tutaingiza maji lita 750milioni jiji la Dar. Nichagueni
  Magufuli
  JB Julius Bett
 48. CCM- JANGWANI

  Wafanyakazi mimi sio mkali..nimesimamia miradi ya barabara, mafuriko jamani huo ni mkali? Hapana, nadhani nilikuwa natimiza wajibu. Hakuna cha ukali hapo
  Magufuli
  JB Julius Bett
 49. CCM- JANGWANI

  Lakini watu wafanye kazi kwa amaana asiyefanya kazi na asile
  Magufuli
  JB Julius Bett
 50. CCM- JANGWANI

  Nataka kuboresha maslahi ya wafanyakazi. Kodi ni asilimia 11 na tunataka tuishishe chini ili wafanyakazi wapate unafuu
  Magufuli
  JB Julius Bett
 51. CCM- JANGWANI

  Mimi ni rafiki wa wafanyakazi, nitahakikisha maslahi yanalindwa
  Magufuli
  JB Julius Bett
 52. CCM- JANGWANI

  Lakini kuna wafanyakazi wala rushwa...hata ukiwalipa sh10milioni kwa mwezi wataiba tu. Hawa wataishia hapahapa Dar, simwamishi
  Magufuli
  JB Julius Bett
 53. CCM- JANGWANI

  Sadaka yangu kwa Watanzania, nataka kuwafanyia kazi. Nitapambana na mafisadi. Nilipoteuliwa tu, wamekimbia chama
  Magufuli
  JB Julius Bett
 54. CCM- JANGWANI

  Rais wa awamu ya nne na ya awamu ya tatu waliwateuwa watu wasiowafahamu.
  Magufuli
  JB Julius Bett
 55. CCM- JANGWANI

  Waliwateuwa watu waliowashauri vibaya..Kikwete uliweka watu wengine serikalini ambao hawafai na wametuchelewesha. hawafai
  Magufuli
  JB Julius Bett
 56. CCM- JANGWANI

  Si mnataka niseme? Nazungumza kwa uwazi
  Magufuli
  JB Julius Bett
 57. CCM- JANGWANI

  Ukabila, udini, vyama tuviweke pembeni, mnichague mimi
  Magufuli
  JB Julius Bett
 58. CCM- JANGWANI

  Tutasomesha wanafunzi bure, uwezo huo upo
  Magufuli
  JB Julius Bett
 59. CCM- JANGWANI

  Ninawashukuru sana, mnichague kwa maana HAPA NI KAZI TU
  Magufuli
  JB Julius Bett
 60. Mfuasi wa CCM akishangilia kwenye kampeni za uchaguzi

  JB Julius Bett
 61. Wafuasi wa CCM wakiwa Uwanja wa Jangwani katika kampeni za uchaguzi mkuu zinazoendelea nchini

  JB Julius Bett
 62. HOTUBA YA LOWASSA: Tuheshimu sheria na kanuni, tupige kura kwa Amani na Utulivu
  JB Julius Bett
 63. HOTUBA YA LOWASSA: Matatizo yaliyotokea Kenya hayakutokana na kuondelewa kwa KANU, Watanzania tuepukane na madai ya udanganyifu

  JB Julius Bett
 64. HOTUBA YA LOWASSA: Watanzania wamechoshwa na ahadi hewa za CCM…Watanzania sasa wanataka mabadiliko ya uhakika

  JB Julius Bett
 65. HOTUBA YA LOWASSA: CCM na serikali yake imeshindwa kuwapa wananchi maisha bora

  JB Julius Bett
 66. HOTUBA YA LOWASSA: Tutadhibiti matumuzi ya serikali na kupunguza makongamano yasiyo ya lazima, tutaanzisha wizara maalum ya kusimamia gesi na mafuta

  JB Julius Bett
 67. HOTUBA YA LOWASSA: Tutasimamia utawala bora na kuhakikisha haki inatendeka, serikali itaunda tume maalum kupendekeza kima cha chini cha mishahara sekta binafsi na serikalini

  JB Julius Bett
 68. HOTUBA YA LOWASSA: Nitahakikisha suala la michezo na utamaduni linasimamiwa, japo Tanzania inafanya vizuri kwenye sanaa ya muziki lakini bado juhudi zinahitajika kuinua michezo mingine

  JB Julius Bett
 69. HOTUBA YA LOWASSA: Mimi nawaheshimu Watanzania na nina muogopa Mungu, nawaahidi nitawatumikia kwa uaminifu, Tanzania inaweza tukichagua mabadiliko

  JB Julius Bett
 70. KUNA MAISHA BAADA YA UCHAGUZI: Wafanyabiashara wa Soko la Karume, Dar es Salaam, Athanas Mtunda (kushoto) na Said Muhidin wakiwa na furaha jana kuonyesha kuwa siasa si uadui. Picha na Said Khamis

  JB Julius Bett
 71. KAMPENI ZA LALA SALAMA: Mzunguko wa Samaki Samaki jijini Mwanza.

  Picha na Michael Jamson

  JB Julius Bett
 72. KAMPENI ZA LALA SALAMA: Polisi wakiwazuia wafuasi wa Chadema, waliotaka kuleta vurugu baada ya mabango ns bendera zao kushushwa eneo la Samaki Samaki Mwanza. PICHA| MICHAEL JAMSON

  JB Julius Bett
 73. CHADEMA- JANGWANI: Mkutano wa kufunga kampeni za Ukawa waanza Jangwani na sasa Mgombea Lowassa anazungumza ili awahi safari ya Arusha ambako atapiga kura kesho.

  JB Julius Bett
 74. CHADEMA- JANGWANI

  Rais bora ni yule mwenye maono na si jambo la kubahatisha wala kutisha watu
  Lowassa
  JB Julius Bett
 75. CHADEMA- JANGWANI

  Rais ni mtu mweye uwezo wa kutoa dira ya taifa na hivyo anatakiwa mtu aliyejiandaa kwa ajili ya kazi hiyo.
  Lowassa
  JB Julius Bett
 76. CHADEMA- JANGWANI

  Mnayo fursa kufanya yale yaliyofanywa na mataifa mengine kama Kenya, Zambia na Malawi katika kubadilisha utawala.

  Lowassa
  JB Julius Bett
 77. CHADEMA- JANGWANI

  Natambua uongozi ni dhamana na kwamba namuogopa Mungu, nawaheshimu watanzania, nitawatumikia kwa nguvu zangu zote.

  Lowassa
  JB Julius Bett
 78. CHADEMA- JANGWANI:

  Amemalizia kwa kuwaomba kura watanzania na kuwashukuru wote kwa kujitokeza na kumuunga mkono katika kampeni zake, na sasa mzee Kingunge Ngombale Mwiru anazungumza na wananchi.

  JB Julius Bett
 79. CHADEMA- JANGWANI

  Huko nyuma tulifaniliwa kujenga nchi…lakini hivi karibuni hasa awamu hii ya nne mambo yanakwenda vibaya

  Kingunge
  JB Julius Bett
 80. CHADEMA- JANGWANI

  Wananchi wanataka maisha bora, ila CCM wameshindwa

  Kingunge
  JB Julius Bett
 81. CHADEMA- JANGWANI

  Kikwete aliahidi maisha bora kwa kila Mtanzania, mnayapata?

  Kingunge
  JB Julius Bett
 82. CHADEMA- JANGWANI

  Tumeuliza Arusha, Mbeya, Tanga mmeyapata maisha bora? Wamesema hawajayapata
  Kingunge
  JB Julius Bett
 83. CHADEMA- JANGWANI

  Tatizo lao kubwa baada ya kukaa madarakani kwa miaka 54, uongozi wa chama umechoka

  Kingunge
  JB Julius Bett
 84. CHADEMA- JANGWANI

  CCM wamekuwa wakitoa ahadi nyingi lakini utekelezaji ni mdogo ndiyo maana vitu vingi vinauzwa kwa bei kubwa.
  Kingunge
  JB Julius Bett
 85. CHADEMA- JANGWANI

  Wanajiandaa kuchakachua kura ili Magufuli awe Rais, wakishindwa watumie vyombo vya usalama.
  Kingunge
  JB Julius Bett
 86. CCM-MWANZA Mkutano wa kufunga kampeni za CCM Uwanja wa Kirumba Mwanza umeanza kwa burudani kutoka Yamoto Band

  JB Julius Bett
 87. CHADEMA- JANGWANI: Kingunge amemaliza kuongea na sasa mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Maalim Seif Shariff Hamad anaongea.

  JB Julius Bett
 88. UKAWA-JANGWANI Wafuasi wa Ukawa katika mkutano wa kufunga kampeni za Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa viwanja vya Jangwani

  JB Julius Bett
 89. CHADEMA- JANGWANI: Seif anasema hana wasiwasi na kwamba kura zikipigwa, hata wakiiba Rais atakuwa Lowassa.

  JB Julius Bett
 90. CHADEMA- JANGWANI

  Nawaambia wananchi wa Tanzania, acheni woga nendeni mkapige kura. Nataka nikamwambie Mheshimiwa Rais Kikwete, leo unateua makatibu wakuu na kuwaapisha?

  Maalim Seif
  JB Julius Bett
 91. CHADEMA- JANGWANI

  Msivae sare za vyama vyetu kwa kuwa CCM wamenunua sare zetu iliwazivae kesho ili sisi tuonekane kuwa ndiyo tunaofanya fujo siku ya uchaguzi.

  Maalim Seif
  JB Julius Bett
 92. CHADEMA- JANGWANI

  Pia, kesho mawakala lazima wawepo vituoni wakati wa kupigakura na kujumlisha kura hatutaki kuona suala la Tume kujumlisha kura peke yao.

  Maalim Seif
  JB Julius Bett
 93. CHADEMA- JANGWANI: Maalim Seif amemaliza kuhutubia na sasa Mgombea mwenza Juma Duni Haji anazungumza.

  JB Julius Bett
 94. CHADEMA- JANGWANI: Duni amewaambia wanajeshi kukataa amri watakazopewa ili kupigana na raia. Asema yeye, Lowassa na Maalim Seif, licha ya kunyanyaswa, kudharauliwa wanakwenda Ikulu kuwatendea wema wananchi.

  JB Julius Bett
 95. CHADEMA- JANGWANI

  Hatutamuonea mtu wala kumnyanyasa mtu, nendeni mkapige kura kwa amani na tukutane Ikulu.
  Duni
  JB Julius Bett
 96. CHADEMA- JANGWANI

  Nitazungumza mambo machache sana kwa niaba ya chama.
  Mbowe
  JB Julius Bett
 97. CHADEMA- JANGWANI

  Nawashukuru wananchi kuwapokea wagombea wetu katika kampeni zao.

  Mbowe
  JB Julius Bett
 98. CHADEMA- JANGWANI

  Chadema na vyama vyote vya ukawa tunaheshimu sheria za nchi na mahakama ili nchi iweze kutawalika.
  Mbowe
  JB Julius Bett
 99. CHADEMA- JANGWANI

  Unapokuja na sheria na mahakama inatafsiri sheria ina maana unawahamisha watu kwenye makazi yao.

  Mbowe
  JB Julius Bett
 100. CHADEMA- JANGWANI

  Mahakama haijatuzuia kulinda kura zetu. Tutazilinda kura zetu kwa kuwa hatuiamini Tume ya Taifa ya uchaguzi.
  Mbowe
  JB Julius Bett
 101. CHADEMA- JANGWANI

  Tutalinda vituo nje ya mita 200 kama sheria inavyosema.
  Mbowe
  JB Julius Bett
 102. CHADEMA- JANGWANI

  Tunajua leo usiku wamepanga kugawa pesa nchi nzima, hivyo tukeshe leo tukilinda uhuru wetu.

  Mbowe
  JB Julius Bett
 103. CHADEMA- JANGWANI

  Kwa namna ambavyo tumeiona nchi ushindi ni dhahiri. Kama chama tmejiandaa kukusanya matokeo nchi nzima, hatutaingoja Tume itukusanyie matokeo.
  Mbowe
  JB Julius Bett
 104. CHADEMA- JANGWANI

  Hatujakatazwa kushangilia ushindi, hivyo tukipata matokeo tutawatangazia wananchi ili waweze kushangilia ushindi wao.

  Mbowe
  JB Julius Bett
 105. CHADEMA- JANGWANI

  Kama matokeo ya Tume yatafanana na yetu tutakubaliana na matokeo hayo ila kama yatatofautiana hatutayakubali matokeo hayo.

  Mbowe
  JB Julius Bett
 106. CHADEMA- JANGWANI: Mbowe amemaliza kuongea na sasa mwenyekiti mwenza wa ukawa James Mbatia amekaribishwa kuongea na wananchi.

  JB Julius Bett
 107. KAMPENI ZA LALA SALAMA: Mfuasi wa CCM akiwa kwenye mkutano wa wa kufunga kampeni za chama hicho Musoma Mjini. Picha na Beldina Nyakeke

  JB Julius Bett
 108. CCM-MWANZA: Mgombea mwenza wa urais kupitia CCM, Samia Suluhu Ali anaanza kuhutubia mkutano wa kufunga kampeni za CCM, Kirumba Mwanza

  JB Julius Bett
 109. CCM-MWANZA:Watanzania wote kesho tukamchague Dk John Pombe Magufuli kwa maendeleo ya Watanzania - SAMIA

  JB Julius Bett
 110. CHADEMA- JANGWANI

  Tulikubaliana vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi na Tume ya Uchaguzi tutengeneze utaratibu wa maridhiano lakini wenzetu wamekataa.

  Mbatia
  JB Julius Bett
 111. CCM-MWANZA: Mabadiliko ni kusema na kutenda, anayeweza kufanya hivyo ni Chama cha Mapinduzi - Samia

  JB Julius Bett
 112. CCM-MWANZA: Chagueni Chama cha Mapinduzi chenye nia ya kudumisha Muungano, kuimarisha Mapinduzi ya Zanzibar - Samia

  JB Julius Bett
 113. CHADEMA- JANGWANI

  Sasa kwa kuwa wamekataa, kesho tukipiga kura ushindi ni wetu, watake au wasitake.

  Mbatia
  JB Julius Bett
 114. CHADEMA- JANGWANI

  Kenya walikabidhiana madaraka kwa amani baada ya chama tawala kuridhika kuwa upinzani ulishinda. Jakaya Mrisho Kikwete unamuogopa nini wakati alikuwa rafiki yako?

  Mbatia
  JB Julius Bett
 115. CHADEMA- JANGWANI

  Edward Ngoyai Lowassa kwa kuwa ni mcha Mungu ameshakusamehe yote uliyomtendea.
  Mbatia
  JB Julius Bett
 116. CHADEMA- JANGWANI

  Gari ya Tanroads imekamatwa Njombe leo ikiwa na kura zilizopigwa kwa Magufuli, nawaambia CCM na Usalama wa Taifa mmeshashindwa kwa hila.
  Mbatia
  JB Julius Bett
 117. CHADEMA- JANGWANI

  Msimruhusu mtu msiyemjua apige kura kituoni kwenu, na kama Lubuva anakubaliana na shinikizo la CCM basi awe tayari kuungana naye kwenye Mahakama ya Uhalifu wa Kivita, ICC mjini The Hegue.

  Mbatia
  JB Julius Bett
 118. CHADEMA- JANGWANI

  Tumejitahidi kuweka historia mwaka huu kwa kufanya kampeni za kistaarabu kuliko wenzetu wa CCM.
  Mbatia
  JB Julius Bett
 119. CHADEMA- JANGWANI

  Zamani wapinzani tulikataliwa kwa kigezo cha kukosa uzoefu. Ila hadi sasa tuna watu wengi wenye uzoefu kama Mbowe, Taslima, Kingunge, Lowassa na Sumaye.

  Mbatia
  JB Julius Bett
 120. CCM - MWANZA

  Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM anaanza kuongea hivi sasa viwanja vya Kirumba, Mwanza

  JB Julius Bett
 121. CCM - MWANZA

  Nawashukuru wananchi kwa uwingi wenu, naomba uwingi huu tuanze kuutafsiri katika masanduku ya kura kesho - Rais Kikwete
  JB Julius Bett
 122. CHADEMA- JANGWANI

  Sheria ya mita 200 ilikuwepo miaka mingi, lakini kwa nini mwaka huu suala hili limepewa kipaumbele na kutiliwa mkazo zaidi?

  Taslima
  JB Julius Bett
 123. CHADEMA- JANGWANI: . Taslima amemaliza kuzungumza na sasa meneja wa kampeni John Mrema anasema zipo taarifa vijana wa JKT kesho watavalishwa nguo za polisi na kupewa majukumu ya kulinda raia na mali zao. Amewataka wasikubali.

  JB Julius Bett
 124. CHADEMA- JANGWANI: Sasa mgombea urais Edward Lowassa anawaombea kura wagombea ubunge jijini Dar es Salaam.

  JB Julius Bett
 125. CCM-MWANZA

  Hakuna ubabe katika CCM, tumeendesha utaratibu wetu kwa kufuata Katiba na kura zilimuangukia Magufuli - Rais Kikwete
  JB Julius Bett
 126. CHADEMA- JANGWANI: Kampeni zimefungwa rasmi viwanja vya Jangwani Jijini Dar es Salaam. Tukutane kesho kwenye taarifa mbalimbali za uchaguzi.

  JB Julius Bett
 127. CCM-MWANZA

  Katika nchi yenye matatizo makubwa ya rushwa, mnatakiwa kiongozi mwenye rekodi nzuri ya uaminifu - Rais Kikwete

  JB Julius Bett
 128. CCM-MWANZA

  Tatizo la kwenye Richomond tulikubaliana sote tukodishe mitambo kutoka nje, sikuhusika kwenye kampuni gani ilete hiyo mitambo, tatizo la Richmond, kanuni hazikuzingatiwa - Rais Kikwete

  JB Julius Bett
 129. CCM-MWANZA

  Katika uteuzi, suala la afya tulilizingatia, na Dk Magufuli alikidhi vigezo vyote vya afya - Rais Kikwete
  JB Julius Bett
 130. Vijana wakielekea katika Viwanja vya Jangwani kuhudhulia mkutano wa kufunga kampeni za mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.

  JB Julius Bett
 131. CCM-MWANZA

  Nimepata ushauri kwa Watanzania mbalimbali, nitakapo ingia Ikulu, nitaufanyia Kazi - Dk Magufuli
  JB Julius Bett
 132. CCM-MWANZA

  Nimekutana na kero nyingi, kero kubwa ni ya maji na katika Ilani yetu, inasisitiza kwamba awamu ya tano, ajenda zake ni kushughulikia matatizo ya maji - Dk Magufuli
  JB Julius Bett
 133. CCM-MWANZA

  Tunampango wa kuhakikisha tunakuwa na umeme wa uhakika, hatuwezi kuongelea kuwa na viwanda kama hatuna umeme wa uhakika - Dk Magufuli
  JB Julius Bett
 134. CCM-MWANZA

  Nitaulinda na kudumisha Muungano wetu, huu ni Muungano uliotufanya Watanzania tukae kwa amani na usalama - Dk Magufuli
  JB Julius Bett
 135. CCM-MWANZA

  Nimegundua vijana wanataka mabadiliko ya haraka, nawahakikishia atakayeweza kwenda na kasi ya vijana ni Magufuli - Dk Magufuli
  JB Julius Bett
 136. CCM-MWANZA

  Tunataka tuongeze wigo wa ajira kutoka asilimia tisa hadi asilimia 40, hii inawezekana, tumewahi kufanya hilo kwenye wizara ya ujenzi - Dk Magufuli
  JB Julius Bett
 137. CCM-MWANZA

  Tuna mpango wa kupanua viwanja vya ndege kwenye mikoayote mikubwa ikiwemo na Kiwanja cha ndege cha Mwanza - Dk Magufuli
  JB Julius Bett
 138. CCM-MWANZA

  Tutaanzisha mfuko wa wasanii kusimamia na kulinda haki za wasanii - Dk Magufuli
  JB Julius Bett
 139. CCM-MWANZA

  Rais Jakaya Kikwete amefunga mkutano wa kuhitimisha kampeni za urais za Chama Cha Mapinduzi
  JB Julius Bett
 140. CCM-MWANZA

  Rais Kikwete akiwa na mgombea wa urais kupitia CCM, Dk John Magufuli wakati wanaingia Uwanja wa Kirumba kwenye mkutano wa kufunga kampeni za CCM. Picha na Blog ya Michuzi

  JB Julius Bett
 141. UKAWA-JANGWANI

  Wafuasi wa Ukawa kwenye mkutano wa kufunga kampeni Uwanja wa Jangwani leo.

  JB Julius Bett
 142. KAMPENI ZA LALA SALAMA: Mgombea ubunge wa Chadema Bunda Mjini, Esther Bulaya alianguka akiwa jukwaani leo katika mkutano wa kufunga kampeni, amesema yuko salama.

  JB Julius Bett
 143. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu masuala mbalimbali ya Uchaguzi Mkuu, ikiwemo kusisitiza mwisho wa kampeni za uchaguzi huo kuwa ni leo saa 12: 00 jioni. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Emmanuel Kawishe.

  JB Julius Bett
 144. Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki na Balozi wa Papa nchini, Francisco Padila akiongoza ibada ya Misa Takatifu iliyofanyika leo katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mandaka Jimbo la Moshi, ibada hiyo ilifanyika ili kuwapa nafasi waumini kushiriki Uchaguzi Mkuu kesho jumapili.

  JB Julius Bett
 145. DP-IRINGA

  Mgombea Ubunge Jimbo la Iringa Mjini kwa tiketi ya DP, Roberth Kisinini akiwa ndani ya mkokoteni unaokokotwa na Punda akihutubia wananchi wa Manispaa ya Iringa katika mkutano wake wa kufunga kampeni uliofanyika eneo la stendi kuu ya mabasi , Iringa leo. Picha na Said Ng`amilo

  JB Julius Bett
 146. Waumini wa dini ya Kiislamu wakiomba dua kwenye swala maalum ya kuombea amani katika Uchaguzi Mkuu unaofanyika kesho, swala iliyofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Lumumba, mjini Unguja.

  JB Julius Bett
 147. CCM-MWANZA

  Mgombea wa urais kupitia CCM, Dk John Magufuli akihutubia mkutano wa kufunga kampeni Mwanza.

  JB Julius Bett
 148. KAMPENI ZA LALA SALAMA: Wafuasi wa Ukawa Uwanja wa Jangwani kwenye mkutano wa kuhitimisha kampeni.

  JB Julius Bett
 149. Kamanda wa polisi Mkoa Arusha, Liberatus Sabas amesema jeshi hilo limebaini uwepo wa vikundi vilivyojipanga kufanya vurugu na kuvionya kuacha mara moja.

  JB Julius Bett
 150. Hali ilivyo kwenye baadhi ya vituo vya kupiga kura leo asubuhi.

  JB Julius Bett
 151. KUTOKA MBAGALA KIZUIANI; Wapiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Kizuiani wameanza kufika kituoni hapo kuazia majira ya saa 11.00 asubuhi na wamepanga utaratibu wa kupeana namba.

  JB Julius Bett
 152. WAKAZI wa Mtaa wa NHC, Mugumu Jimbo la Serengeti wakiwa kwenye foleni asubuhi hii wakisubiri vituo kufunguliwa.

  JB Julius Bett
 153. HALI ya usafiri kwenye Kituo cha Daladala Mbezi Mwisho asubuhi ya leo.

  JB Julius Bett
 154. Kituo cha Sekondari MAdiba, Segerea, wapiga kura wamefika tangu saa 11.00 alfajiri

  JB Julius Bett
 155. BAADHI ya changamoto kwenye vituo vingi hadi sasa ni baadhi ya wananchi kutohakiki majina yao mapema, wengi wao wanafanya zoezi hilo asubuhi hii.

  JB Julius Bett
 156. KUTOKA Kituo cha Shule ya Msingi Magufuli ambapo mgombea urais kupitia CCM, Dk John Magufuli anatarajiwa kupiga kura yake baadaye leo.

  JB Julius Bett
 157. KUTOKA NYAMAGANA, MWANZA; Kituo cha Sekondari ya Nyabulogoya hakijaanza kupiga kura kutokana na mawakala wa vyama kuchelewa, maofisa wa NEC wanasema hawawezi kuabza mpaka wafike

  JB Julius Bett
 158. HALI ya usafiri kituo cha mabasi Kibaha Maili Moja leo asubuhi

  JB Julius Bett
 159. KITUO cha mabasi Nane Nane Mbeya kikiwa kitupu

  JB Julius Bett
 160. WASIMAMIZI wa Kituo cha Tabata Mtambani wakionesha wapiga kura masanduku matupu kabla ya kuanza kwa zoezi la kupiga kura.

  JB Julius Bett
 161. Mkazi wa Mtaa wa Mkoani Kibaha, William Mganga (83) akipiga kura yake leo asubuhi, vituo vingi vimetoa kipaumbele kwa wapiga kura wazee na wanawake wajawazito.

  JB Julius Bett
 162. Mgombea wa urais wa TLP, Maximillian Lyimo ameshindwa kupiga kura yake leo Kituo cha Njia Panda baada ya kwenda bila kitambulisho cha kura.

  JB Julius Bett
 163. MADUKA ya Soko Kuu Mwanza yakiwa yamefungwa leo asubuhi

  JB Julius Bett
 164. Mgombea wa urais wa Zanzibar kupitia CCM, Dk Ali Mohamed Shein akipiga kura katika Kituo cha kupigia kura kilichopo Shule ya Msingi Bungi, Wilaya ya Kati, mkoa wa Kusini Unguja. Picha na Ikulu Zanzibar

  JB Julius Bett
 165. HALI ilivyo Barabara ya Morogoro, Makutano ya Ubungo Mataa

  JB Julius Bett
 166. Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha TLP, Macmillan Lyimo akizungumza na waandishi wa habari nje ya kituo cha kupigia kura cha Gharani kilichopo katika Kata ya Njia Panda, Vunjo, mkoani Kilimanjaro baada ya kukataliwa kupiga kura kituoni hapo kutokana na kutokuwa na kitambulisho cha mpigakura. Picha na Dionis Nyato

  JB Julius Bett
 167. MKAZI wa Mtaa wa Nundu, Jimbo la Ilemela ameshindwa kupiga kura baada ya kukuta picha tofauti na yake kwenye daftari la Wapiga kura. Picha iliyokutwa kwenye daftari ni ya mwanamke.

  JB Julius Bett
 168. Mkazi wa Bagamoyo akipiga kura kwenye Kituo cha Tanesco, wanawake wenye watoto, wazee na wanawake wajawazito walipewa kipaumbele

  JB Julius Bett
 169. #UchaguziTanzani, Dar es Salaam tulivu

  JB Julius Bett
 170. Mgombea urais wa TLP, Macmillan Lyimo amepiga kura yake muda mfupi uliopita, asema hapakuwa na fomu namba 19 lakini kitambulisho alikuwa nacho.

  JB Julius Bett
 171. Mkazi wa Ukonga Mombasa, Amina Duka akipiga kura kwenye kituo cha kupigia kura cha Efatha, Dar es Salaam. Picha na Anthony Siame

  JB Julius Bett
 172. Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli akipiga kura katika kituo cha kupigia kura kilichopo Shule ya Msingi Magufuli, Chato Mkoani Geita. Picha na Adam Mzee

  JB Julius Bett
 173. Mgombea wa ubunge Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe akiwa kwenye foleni ya kupiga kura katika Kituo cha OTTU

  JB Julius Bett
 174. Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akipiga kura katika kituo cha kupigia kura cha Garagara, mjini Unguja, Zanzibar. Picha na Salim Shao

  JB Julius Bett
 175. KUTOKA SEGEREA: Mgombea ubunge tiketi CUF, Julius Mtatiro ameilalamikia NEC kwa kuacha jina la mgombea wa Chadema kwenye jimbo hilo ambaye walishakubaliana aondolewe kwenye orodha ya wagombea.

  JB Julius Bett
 176. Mgombea mwenza wa urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan akipiga kura katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Kiembe Samaki Unguja, Zanzibar. Picha na Salim Shao

  JB Julius Bett
 177. Mgombea wa urais wa chama cha ADC, Chifu Yemba akipiga kura katika kituo cha kupigia kura kilichopo Buguruni jijini Dar es Salaam. Picha na Venance Nestory

  JB Julius Bett
 178. Mgombea wa urais wa chama cha NRA, Janken Kasambala akipiga kura katika kituo cha kupigia kura kilichopo Shule ya Sekondari Binti Mussa, Kata ya Kiwalani jijini Dar es Salaam. Picha na Venance Nestory

  JB Julius Bett
 179. Mgombea urais wa chama cha ACT- Wazalendo, Anna Mghwira akipiga kura katika kituo cha kupigia kura kilichopo Shule ya Msingi Kibaoni, mkoani Singida. Picha na Gasper Andrew

  JB Julius Bett
 180. Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa akipiga kura kwenye kituo cha kupigia kura kilichopo katika Shule ya Msingi Ngarash, Kata ya Engutoto wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha. Picha na Filbert Rweyemamu

  JB Julius Bett
 181. Mgombea urais kwa tiketi ya Chaumma, Hashim Rungwe akipiga kura katika kituo cha kupigia kura kilichopo Shule ya Msingi Ushindi, Mikocheni jijini Dar es Salaam. Picha na Said Khamis

  JB Julius Bett
 182. Mgombea mwenza wa urais wa Chadema, Juma Duni Haji akipiga kura kwenye kituo cha kupigia kura kilichopo Malindi Unguja, Zanziabar. Picha na Salim Shao

  JB Julius Bett
 183. Mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Ngoyai Lowassa akiongea na waandishi baada ya kupiga kura.

  JB Julius Bett
 184. Mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Pombe Magufuli ashiriki kupiga kura Chato na kuzungumza na waandishi wa habari.

  JB Julius Bett
 185. KUTOKA MUSOMA: Kituo cha kupigia kura Musoma, Shule ya msingi wapiga kura wamelalamikia baadhi ya vijana kukaa kituoni muda mrefu bila kupiga kura matokeo yake wanawafanyia fujo hali hiyo imelazimisha polisi kuwasimamia wanaolalamikiwa wapige kura kisha kuondolewa kituoni.

  JB Julius Bett
 186. Manzese wapiga kura, wafurahishwa na amani kituoni

  JB Julius Bett
 187. Mgombea Mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Samia Suluhu atimiza wajibu wake kupiga kura Zanzibar

  JB Julius Bett
 188. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipiga kura katika kituo cha kupiga kura kilichopo kwenye Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kibaoni wilayani Mlele, mkoani Katavi. Picha | Ofisi ya Waziri Mkuu

  JB Julius Bett
 189. Mwangalizi Mkuu wa EU, Judith Sargentini anasema kumekuwa na hali ya utulivu katika vituo 400 vilivyotembelewa na waangalizi wa EU nchi nzima.

  JB Julius Bett
 190. ZANZIBAR: Jimbo Kijitoupele kura za ubunge zimeleta matatizo hivyo uchaguzi umesimamishwa wa nafasi ya ubunge

  JB Julius Bett
 191. TANGA: Wafanyabiashara wa pikipiki (bodaboda) tarafa ya Maramba wilayani Mkinga mkoani Tanga, wamesema leo hawatarudi katika vituo vyao hadi matokeo yatakapotolewa.

  JB Julius Bett
 192. Kazi ya kuhesabu kura ikifanyika katika kituo kilichopo Shule ya Msingi Musoma, Jimbo la Musoma Mjini, mkoani Mara.

  JB Julius Bett
 193. MUSOMA: Usafiri wa daladala Musoma mjini umeadimika, watu wengi wanatumia usafiri wa pikipiki ambao nao ni wa kusuasua

  JB Julius Bett
 194. UBUNGO: Hakuna biashara inayoendelea maeneo ya Ubungo mataa

  JB Julius Bett
 195. Zoezi la kuhesabu kura limeanza shule ya Msingi Mkuranga

  JB Julius Bett
 196. Mwangalizi Mkuu wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Mataifa Judith Sargentini amesema amepokea ripoti kutoka kwa waangalizi 140 waliopita kwenye vituo 500 Tanzania wakisema uchaguzi umefanyika kwa amani na utulivu

  JB Julius Bett
 197. MJI MWEMA: Katika kituo cha kupiga kura shule ya msingi Mji Mwema, wapiga kura watatu walivaa sare ya vyama na hivyo kuamliwa na walinzi wakavue sare hizo ili waje wapige kura, wananchi hao walitii agizo hilo na kuvua sare hizo.

  JB Julius Bett
 198. Mawakala wa kituo cha Stand ya zamani Jimbo la Kondoa Mjini wakisaini fomu ya kuthibitisha kuwa kazi imeisha katika hali ya usalama

  JB Julius Bett
 199. KILINDI: Asilimia kubwa ya vituo katika kata ya Jaila na Mswaki wilaya ya Kilindi vimeshafungwa na wasimamizi wapo ndani wakianza zoezi la kuhesabu kura.

  JB Julius Bett
 200. Wasimamizi katika Jimbo la Mbagala wanahesabu vitabu kufahamu vingapi vimetumika na vingapi vimebaki.

  JB Julius Bett
 201. UKONGA: Katika kkituo cha Kitunda Jimbo la Ukonga baadhi ya watu walichelewa na muda wa kupiga kupiga ulishapita na vituo kufungwa saa 10. Watu hao waliwabembeleza askari na wasimamizi waruhusiwe kupiga kura lakini walikataliwa hivyo kuondoka.

  JB Julius Bett
 202. Zoezi la kuhakiki kura kituo cha Sedeco Jimbo la Serengeti likiendelea.

  JB Julius Bett
 203. LULINDI: Jimbo la Lulindi wananchi wameshindwa kupiga kura ya nafasi ya ubunge hivyo uchaguzi wa nafasi hiyo umeahirishwa, ni baada ya kukosewa majina ya mgombea wa CUF katika wa CUF katika karatasi ya kupigia kura.

  JB Julius Bett
 204. MWANZA: Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Tito Mahinya anasema kuanzia saa 6:00 usiku wataanza kutoa matokeo ya jumla ya udiwani Jimbo la Nyamagana.

  JB Julius Bett
 205. Maandalizi ya Chadema kwa ajili ya mkutano na waandishi Millenium Tower

  JB Julius Bett
 206. ARUSHA: Msimamizi wa kituo cha Olkiken wilaya ya Longido mkoani Arusha alifunga kituo hicho ilipofika saa 10 ingawa wapiga kura walikuwa kwenye foleni hali iliyozua malalamiko. Hadi sasa wananchi bado wapo kituoni wakisubiri kupiga kura ingawa shughuli zilishafungwa.

  JB Julius Bett
 207. Kazi ya kuhesabu kura ikifanyika katika kituo cha kupigia kura kilichopo Kata ya Buguruni jijini Dar es Salaam. Picha na Venance Nestory

  JB Julius Bett
 208. MOSHI: Gari la mmoja wa makampeni meneja wa mgombea ubunge Jimbo la Moshi vijijini (CCM), Dk Cyrill Chami, limeshambuliwa na kuharibiwa vibaya na wananchi wakilishuku kuwa na kura bandia.

  JB Julius Bett
 209. Wananchi wa kata ya Uwanjani wakiwa kwenye uwanja wa Moira wa shule ya msingi Tunduma wakisubiria matokeo, polisi wamewaambia wakusanyike hapo baada ya kuona wanasogea na kujikusanya jirani na vituo vya kupigia kura.

  JB Julius Bett
 210. TUNDUMA: Wananchi Jimbo la Tunduma wamenza kusimama kando kando mwa vituo vya kuhesabia kura na kila gari linalopita jirani na vituo wanazuia na kulirudisha lilikotoka. Wanasema hawamuamini mtu yeyote anaekatiza eneo hilo.

  JB Julius Bett
 211. TEMBONI: Kituo cha shule ya msingi Temboni hadi sasa watu zaidi ya 400 hawajapiga kura majina yao hayaonekani kwenye daftari, zoezi limesitishwa watu wameambiwa watawanyike wamegoma.

  JB Julius Bett
 212. Baadhi ya wakazi wa Kinyerezi wakimhoji askari Magereza katika kituo cha shule ya msingi Mount Pleasant baada ya kuona gari ndogo mabayo imeelezwa kuwa ni ya mlinzi inaingizwa ndani ya kituo hicho wakati kura zinahesabiwa ndani. Waliingia ndani na kupekua gari hilo.

  JB Julius Bett
 213. NYAMAGANA: Kituo cha shule ya msingi Mbugani Jimbo la Nyamagana kuna vijana wanalinda kura

  JB Julius Bett
 214. LINDI: Mkazi wa kijiji cha Kiangara wilaaya ya Liwale mkoani Lindi Abreheman Mkopora anashikiliwa na polisi kwa tuhuma ya kutaka kujiandikisha mara mbili.

  JB Julius Bett
 215. SERENGETI: Zoezi la kuhesabu kura Jimbo la Serengeti linaendelea, shamrashamra baadhi ya mitaa ikianza licha ya mvua kubwa inayonyesha.

  JB Julius Bett
 216. KARATU: Karatu waanza kuhesabu kura katika madarasa ya shule hakuna umeme wanatumia tochi.

  JB Julius Bett
 217. KIGOMA: Kigoma Kusini hali ni shwari, watu wapo wajumbani wanasubiri matokeo, hata baa hazina watu mji umetulia.

  JB Julius Bett
 218. Zoezi la kuhesabu kura linaendelea kituo cha Uwanja wa soko Mageuzi Jimbo la Shinyanga mjini.

  JB Julius Bett
 219. KAWE: Zoezi la kuhesabu kura bado linaendelea katika vituo mbalimbali vya Jimbo la Kawe.Katika kituo cha Bunju A, zoezi la kuhesabu kura za urais lilirudiwa baada ya wakala wa CCM kutoridhishwa na matokeo ya mgombea wake.

  JB Julius Bett
 220. Msimamizi wa kituo cha skuli ya Mtambile, jimbo la Mtambile, mkoa wa Kusini Pemba, Hafidhi Said Ali akionyesha tochi itakayotumika usiku wa kuhesabu kura kituoni hapo.

  JB Julius Bett
 221. ARUMERU: Kata ya Maivo kituo cha sokoni Jimbo la Arumeru watu bado wako kwenye foleni wanapiga kura na hii ni baada ya majina zaidi ya 200 kukosekana kwenye orodha ya wapiga kura.

  JB Julius Bett
 222. TUNDUMA: Mawakala Jimbo la Tunduma wanyang'anywa simu na wasimamizi baada ya kubainika wakirusha matokeo kwa wenzao nje. Na kutokana na hali hiyo wananchi wameanza kukusanyika kwa wingi jirani na vituo vya kuhesabia kura huku wakiimba nyimbo za vyama vyao.

  JB Julius Bett
 223. MVOMERO: Wasimamizi katika kituo cha shule ya msingi Wami Sokoine wakitumia simu za tochi na karabai kwa ajili ya uhesabuji kura.

  JB Julius Bett
 224. IFAKARA: Polisi wapiga mabomu ya machozi baada ya vijana kufanya fujo kwa kurusha mawe juu ya majengo ya shule ya msingi Mhola.

  JB Julius Bett
 225. MUSOMA: Polisi watumia mabomu ya machozi kutawanya wananchi wanaovunja kituo cha kuhesabia kura cha Kigera, Musoma Mjini wakipinga matokeo yanayotangazwa

  JB Julius Bett
 226. ARUMERU: Msimamizi mkuu wa kituo cha Arumeru Magharibi, Fidelis Lumato amesema kuwa wanashukuru wamemaliza uchaguzi salama bila vurugu hivyo wanaomba wananchi waendelee hivyo hadi kesho asubuhi atakapotangaza matokeo ya jumla.

  JB Julius Bett
 227. CHADEMA: Dosari za uchaguzi Katavi, Kimara na Pemba zinadhihirisha kuwa uchaguzi huu si huru na haki

  JB Julius Bett
 228. CHADEMA: Imethibitika kuwa tulichokibashiri kimetokea. Hivyo tuna haki ya kulinda kura zetu.

  JB Julius Bett
 229. MATOKEO URAIS Z’BAR: ZEC yatangaza kuwa Jimbo la Fuoni; Dk Shein (CCM) amepata kura 889 wakati Maalim Seif (CUF) akiwa na kura 429. Waliojiandikisha kupiga kura jimbo katika jimbo hilo ni 1,822, waliopiga kura ni 1,397.

  JB Julius Bett
 230. MATOKEO URAIS Z'BAR: Hadi sasa ZEC imetangaza matokeo ya urais katika majimbo ya Fuoni na Kiembesamaki na Shein (CCM) anaongoza dhidi ya Maalim Seif (CUF)

  JB Julius Bett
 231. MATOKEO URAIS Z'BAR: Kwa mujibu wa NEC, Dk Shein (CCM) ameongoza katika jimbo la Kiembesamaki kwa kura 4,413 dhidi ya 2,986 za Maalim Seif (CUF)

  JB Julius Bett
 232. UCHAGUZI 2015: Wagombea urais wa vyama vya CCM na Chadema wanachuana vikali kwa mujibu wa matokeo ya awali yanayotangazwa kwenye vituo mbalimbali nchini

  JB Julius Bett
 233. UCHAGUZI 2015: Matokeo ya uchaguzi ngazi ya Rais yataanza kutangazwa kwa awamu ya kwanza saa tatu asubuhi, saa sita mchana, saa tisa na saa 12 jioni.

  JB Julius Bett
 234. KIMARA: Wananchi vituo vya EDP Royal Kimara Stop Over A na B, Dar waanza kupiga kura leo asubuhi baada ya kuahirishwa jana kutokana na upungufu wa vifaa

  JB Julius Bett
 235. KIGOMA: Matokeo ya awali Kigoma Mjini: Mgombea ubunge wa ACT, Zitto Kabwe anaongoza, Urais: John Magufuli wa CCM anaongoza.

  JB Julius Bett
 236. UCHAGUZI TANZANIA: Mpigakura Kandido Mnemela akiweka karatasi kwenye sanduku la kura katika Kituo cha Majengo, Mpwapwa mkoani Dodoma jana. Picha na Habel Chidawali

  JB Julius Bett
 237. UCHAGUZI TANZANIA: Maduka yakiwa yamefungwa eneo la Soko Kuu, Kata ya Pamba jijini Mwanza kutokana na Uchaguzi Mkuu uliofanyika jana nchi nzima. Picha na Michael Jamson

  JB Julius Bett
 238. Mtu mwenye ulemavu akipata msaada kuingia katika kituo cha kupiga kura N.I.T Mabibo jijini Dar es Salaam jana. Azam TV

  JB Julius Bett
 239. MWANZA: Barabara ya jiji la Mwanza yafungwa asubuhi hii huku polisi wakiendelea kupiga mabomu ya machozi kuwatawanya watu wanaofuatilia matokeo.

  JB Julius Bett
 240. UCHAGUZI TANZANIA: Tume ya Taifa ya Uchaguzi yaanza kutangaza matokeo ya awali ya uchaguzi

  JB Julius Bett
 241. Wapiga kura wakiwa kituo cha majumuisho ya kura kwa ZEC na NEC (Gombani Stadium) wakisubiri kutangaziwa matokeo ya majimbo matano ya wilaya ya Chake Chake.

  JB Julius Bett
 242. Msimamizi wa uchaguzi Arumeru Magharibi akizungumza na waangalizi wa EU.

  JB Julius Bett
 243. IRINGA: Matokeo ya awali Iringa mjini ubunge Mchungaji Peter Msigwa kashinda.

  JB Julius Bett
 244. UCHAGUZI TANZANIA: Nec yatoa matokeo ya awali ya urais katika majimbo ya Paje Kusini, Makunduchi na Lulindi. Mgombea wa CCM, Dk John Magufuli anaongoza.

  JB Julius Bett
 245. UCHAGUZI TANZANIA: Matokeo ya jumla ya uchaguzi jimbo la Longido mkoani Arusha yanatarajiwa kutangazwa majira ya saa tisa mchana kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi Felix Kimario.

  JB Julius Bett
 246. Kura za baadhi ya kata za Handeni mjini zikishushwa asubuhi hii ili kujumlishwa.

  JB Julius Bett
 247. UCHAGUZI TANZANIA: Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Magu, Ntiniki Paul akiendelea kupokea matokeo kutoka kata za wilaya hiyo katika ukumbi wa halmashauri ya Magu.

  JB Julius Bett
 248. Wakazi wa Tabata Mawenzi wakitafuta majina yao walipokwenda kupiga kura katika kituo kilichopo katika ofisi ya Serikali za Mitaa ya Kimanga Daraja, Dar es Salaam jana. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 249. Jimbo la Tunduma

  Ubunge: Mwakajoka Frank (Chadema) 32,442, Frank Sichalwe (CCM) 17,220, James Mwakalonge(TLP) 85, Reddy Makuba (ACT Wazalendo) , 319.

  Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Tunduma, Halima Mpita ametangaza matokeo hayo.

  JB Julius Bett
 250. Jimbo la Tarime Mjini

  Ubunge: Ester Matiko(Chadema) 20,017, Michael Kembaki(CCM), 14, 025, Deogratias Meck(ACT-Wazalendo) 356.

  Msimamizi mkuu wa Uchaguzi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Juma Mwajombe amemtangaza Matiko kuwa mshindi katika Jimbo hilo
  JB Julius Bett
 251. Baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi jimbo la Kilombero wakibeba maboksi yenye kura wakati wa tukio la kujumlisha kura kutoka kata mbalimbali. Maboksi ya kura yanakusanywa ukumbi wa Halmashauri ya wilaya Kilombero mkoani Morogoro.

  JB Julius Bett
 252. Baadhi ya masanduku ya kura yakiwa yanaendelea kufikishwa katika ofisi za halmashauri ya wilaya ya Mvomero kutoka katika vituo.

  JB Julius Bett
 253. Jimbo la Siha

  Ubunge: Dk Godwin Mollel (Chadema) 22,746 na Aggrey Mwanry (CCM) 18,584.

  Msimamizi wa Uchaguzi, Rashid Kitambulio amemtangaza Dk Mollel kuwa mshindi wa jimbo hilo ambalo mbunge wake alikuwa ni Aggrey Mwanry (CCM).


  JB Julius Bett
 254. Jimbo Buyungu

  Ubunge: Bilago Samson Chadema), 23,041 na Christopher Chiza(CCM) 22,934

  JB Julius Bett
 255. UCHAGUZI TANZANIA: Mgombea ubunge wa Chadema Bilago Samson amefanikiwa kunyakua Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma kwa kura 23041. Jimbo hilo lilikuwa chini ya CCM kupitia Waziri Christopher Chiza aliyepata kura 22934.Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Kakonko, Jaina Msangi ametangaza matokeo hayo

  JB Julius Bett
 256. Wanachama wa CUF wakiwa wamekusanyika katika eneo la Mtendeni mjini Unguja, Zanzibar wakisubiri kutangaziwa mshindi wa kiti cha Urais katika Uchaguzi MKuu uliofanyika jana nchi nzima. Picha na Salim Shao

  JB Julius Bett
 257. UKONGA: Askari wa kutuliza ghasia wameongezwa kituo cha majumuisho ya kura jimbo la Ukonga baada ya zoezi la kuhesabu kura kurudiwa tena.

  JB Julius Bett
 258. UCHAGUZI TANZANIA: Jeshi la polisi mkoani Mtwara wilaya ya Tandahimba linawashikilia watu 8 kwa tuhuma za kuvamia na kubomoa nyumba ya msimamizi wa uchaguzi jimbo la Nanyamba.

  JB Julius Bett
 259. UCHAGUZI TANZANIA: Mgombea ubunge wa Chadema jimbo Shinyanga Patrobas Katambi amegoma kuendelea kusikiliza kutangazwa kwa matokeo na msimamizi wa uchaguzi Kalinjuna Lewis, kwa madai kuwa hana imani na matokeo hayo na kuamua kutoka ukumbini na wapambe wake wakati matokeo ya kila kituo yakiendelea kusomwa. Hadi sasa bado hajatangazwa mshindi

  JB Julius Bett
 260. KUTOKA ZANZIBAR: Kumekuwa na hali tete kwenye baadhi ya maeneo visiwani Zanzibar baada ya Chama cha Wananchi (CUF) kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwawanaongoza kwenye matokeo ya urais, juhudi za kuipata Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuzungumzia jambo hilo zinaendelea. Tutaendelea kuwajuza.

  JB Julius Bett
 261. UCHAGUZI TANZANIA: Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewataka wanachama wake wapuuze matokeo yanayotangazwa kwenye mitandao ya kuijamii na vyombo amabayo havina mamlaka

  JB Julius Bett
 262. WANANCHI wa Manispaa ya Musoma wakishangilia ushindi wa mbunge mteule wa jimbo hilo, Vedastus Mathayo

  JB Julius Bett
 263. MATOKEO YA UBUNGE: Jimbo la Monduli limechukuliwa na Julius Kalanga (Chadema), Joshua Nassar ameshinda tena Arumeru Mashariki, Jimbo la Serengeti limekwenda kwa Marwa Ryoba (Chadema)


  JB Julius Bett
 264. MATOKEO YA UBUNGE: Jumanne Kishimba (CCM) ameshinda Jimbo la Kahama Mjini, Steven Masele ameshinda Jimbo la Shinyanga Mjini, Hussein Bashe ameshinda Jimbo la Nzega Mjini na Silvestry Koka ameshinda Jimbo la Kibaha Mjini.

  JB Julius Bett
 265. MATOKEO YA UBUNGE: Esther Bulaya (Chadema) ameshinda ubunge Jimbo la Bunda Mjini na kumuangusha Steven Wasira, huku Jaffar Michael akishinda ubunge kwa tiketi ya Chadema Jimbo la Moshi Mjini.

  .

  JB Julius Bett
 266. MATOKEO UBUNGE: Anthony Mavunde (CCM) ametangazwa kuwa mshindi wa ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Joram Hongoli (CCM) akishinda Jimbo la Njombe Kaskazini, Edwin Sanda (CCM) ametangazwa mshindi Jimbo la Kondoa Mjini na Dotto Biteko (CCM) ameshinda ubunge Jimbo la Bukombe.

  JB Julius Bett
 267. MATOKEO ya ubunge Iringa Mjini kutangazwa kesho baada ya kuchelewa kupatikana kwa matokeo ya kituo cha Kata ya Ruaha.

  JB Julius Bett
 268. Mwamvuli wa Waangalizi wa Ndani wa Uchaguzi (CEMOT) umesema kuwa sehemu kubwa ya vituo vya kupigia kura vilijitahidi kuwahi kuanza kuhesabu kura mara tu baada ya muda wa upigaji kura kukamilika.

  JB Julius Bett
 269. TANZIA: Msimamizi wa uchaguzi Kata ya Pagwi, wilayani Kilindi Rajabu Nkungua amefariki dunia baada ya gari alilokuwa akitumia kusafirisha kura kutoka Ngazi kwenda Halmashauri kupinduka.

  JB Julius Bett
 270. Vurugu na mabomu ya machozi yalidumu kwa takribani saa tatu katika eneo linaloizunguka ofisi ya Kata ya Charambe, Mbagala ambako wananchi walikuwa wanasubiria matokeo huku mkoani Tanga polisi walilazimika kuwatimua kwa mabomu wananchi waliokuwa wakishangilia baada ya mgombea wao kushinda.

  JB Julius Bett
 271. Ubunge jimbo la Bukoba Mjini : Wilfred Lwakatare (Chadema) kura 28, 112 na kumshinda Balozi Khamis Kagasheki (CCM) aliyepata kura 25, 565

  JB Julius Bett
 272. UBUNGE NYAMAGANA: NEC yamtangaza mgombea ubunge Nyamagana, Stanislaus Mabula (CCM) kuwa mshindi baada ya kupata kura 81,170 dhidi ya kura 79,280 za Ezekiel Wenje (Chadema).

  JB Julius Bett
 273. UBUNGE NYAMAGANA: CCM imeshinda Kata 14 kati ya 18 za udiwani katika Jimbo la Nyamagana huku Chadema kikiambulia Kata Nne, hivyo CCM itaunda Halmashauri ya Nyamagana.

  JB Julius Bett
 274. UBUNGE NYAMAGANA: Mbunge mteule Stanslaus Mabula ameahidi kuanza majukumu yake kwa kuwaunganisha wananchi wa Jimbo lake na kuwawezesha wajikomboe kiuchumi.

  JB Julius Bett
 275. UBUNGE VUNJO: NEC yamtangaza James Mbatia (NCCR Mageuzi) mshindi katika kinyang’anyiro cha kuwania ubunge jimbo la Vunjo baada ya kupata kura 60,187 dhidi ya Augustine Mrema (TLP) aliyepata kura 6,416 na Innocent Shirima wa CCM (16,617)

  JB Julius Bett
 276. UBUNGE MOSHI VIJIJINI: NEC yamtangaza Anthony Komu (Chadema) mshindi katika kinyang’anyiro cha kuwania ubunge jimbo la Moshi Vijijini kupitia Chadema kuwa mshindi dhidi ya waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami (CCM).

  JB Julius Bett
 277. UBUNGE MOSHI VIJIJINI: Kwa mujibu wa NEC, Anthony Komu (Chadema) amepata kura 55,813 huku mpinzani wake wa karibu Dk Cyril Chami (CCM) akipata kura 24,415. Hivyo Komu ndiye mbunge mteule

  JB Julius Bett
 278. UDIWANI KUNDUCHI: Mgombea wa Udiwani kata ya Kunduchi kupitia tiketi ya CHADEMA atafuna karatasi ya matokeo ya uchaguzi. AzamTV

  JB Julius Bett
 279. Mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Picha na Said Khamis

  JB Julius Bett
 280. Mawaziri na Wabunge walioanguka.

  JB Julius Bett
 281. UCHAGUZI TANZANIA: Polisi wakiwa wamewaweka chini ya ulinzi vijana waliowakamata eneo la Mlandege, Mjini Unguja, Zanzibar kwa madai ya kuhusika na vurugu jana. Na Mpigapicha Wetu

  JB Julius Bett
 282. CHANGAMOTO ZA UCHAGUZI MKUU: Mawakala na wasimamizi wa kituo cha kupiga kura cha Shule ya Msingi Mbugani C2 wakijumlisha kura kwa kutumia taa ya sola, kama walivyokutwa juzi usiku katika Jimbo la Nyamagana jijini Mwanza. Picha na Michael Jamson

  JB Julius Bett
 283. MULEBA: Polisi mjini Muleba watumia mabomu ya machozi leo asubuhi kuwatawanya wananchi wanaoandamana kupinga matokeo ya ubunge jimbo la Muleba Kusini baada ya mgombea wa CCM, Prof Anna Tibaijuka kutangazwa mshindi mapema leo.

  JB Julius Bett
 284. Tume tunafanya kazi kwa kujipanga na utaratibu. Mshindi atashinda kwa kadiri ya kura zinazokuja kwetu. Matokeo yatatangazwa jinsi yanavyokuja.
  Jaji Damian Lubuva, Mwenyekiti NEC
  JB Julius Bett
 285. UBUNGE KIGOMA: Hadi sasa matokeo hayajatangazwa, wananchi kutoka kata za Nguruka, Kazuramimba, Uvunza na kata nyingine za jirani wamekusanyika wakishinikiza kupata matokeo hayo. Kutokana na hali hiyo askari polisi wametanda katika eneo hilo ili kuhakikisha hali ya usalama inatawala.

  JB Julius Bett
 286. UBUNGE KAWE: Mkurugenzi msaidizi wa Jimbo la Kawe, Onesmo Kayamba amesema matokeo ya ubunge kwa jimbo hilo yatatangazwa saa 8 mchana.

  JB Julius Bett
 287. UBUNGE TEMEKE: Baadhi ya wakazi wa Temeke wakizima moto katika Ofisi za kata ya Sandali baada ya vijana waliokuwa wakipinga matokeo ya mgombea udiwani wa kata hiyo kwa tiketi ya CCM, Abel Tarimo ambaye aliibuka mshindi, kuchoma moto ofisi hizo.

  JB Julius Bett
 288. UBUNGE TEMEKE: Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Photidas Kagimbo amesema anasubiri wasimamizi wa uchaguzi wakamilishe kazi ya majumuisho ili atangaze matokeo muda wowote kuanzia sasa.

  JB Julius Bett
 289. UBUNGE MBAGALA: Fomu 104 za matokeo katika jimbo la Mbagala zinadaiwa kutoonekana huku fomu 84 ndizo zinazoonekana,hali hiyo imepelekea kuwapo kwa malalamiko mengi kutoka kwa mawakala wa vyama vya siasa.

  JB Julius Bett
 290. UBUNGE NYAMAGANA: Mgombea wa Jimbo la Nyamagana kwa tiketi ya Chadema, Ezekiel Wenje amepinga matokeo ya jimbo hilo baada ya kushindwa huku akilalamika kuibiwa kura kwa sababu taratibu za kuhesabu zilikiukwa.

  JB Julius Bett
 291. MABASI mawili ya Kampuni ya Zacharia Express yanayofanya safari zake Tarime-Mwanza yameharibiwa kwa kupondwa na mawe jana mchana kwa kile kinachoelezwa ni ushabiki wa kisiasa, taarifa ya polisi yasema.

  JB Julius Bett
 292. Ujumbe wa waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya (EU) umesema uchaguzi ulikuwa na ushindani, ulipangwa vema lakini kumekuwa na jitihada hapakuw ana uwazi wa kutosha kutoka wa baadhi ya watendaji wa uchaguzi.


  JB Julius Bett
 293. MATOKEO YA UBUNGE: Halima Mdee ametangazwa kuwa mshindi wa kiti cha ubunge Jimbo la Kawe, Dar es Salaam

  JB Julius Bett
 294. Abdala Mtolea wa CUF ametangazwa kuwa mshindi wa Jimbo la Temeke na kumuangusha aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo, Abbas Mtemvu

  JB Julius Bett
 295. MATOKEO Jimbo la Iringa Mjini: Mchungaji Peter Msigwa ametangazwa mshindi wa ubunge wa jimbo hilo baada ya kupata kura 43,154 dhidi ya kura 32,406 za Fredrick Mwakalebela wa CCM

  JB Julius Bett
 296. Ukawa sasa imetwaa majimbo matano kati ya 10 ya jijini Dar es Salaam ikiwa ni mara ya kwanza kutwaa zaidi ya majimbo matatu tangu mwaka 1995

  JB Julius Bett
 297. Mtwara: Ina jumla ya kata 18, CUF imeshinda kata nane, CCM saba na Chadema tatu

  JB Julius Bett
 298. UBUNGE KINONDONI: NEC yasema usiku huu, mgombea wa CCM, Idd Azzan amepata kura 65, 964.

  JB Julius Bett
 299. UBUNGE KINONDONI: NEC yasema usiku huu, mgombea wa CUF, Maulid Mtulia amepata kura 70, 337.

  JB Julius Bett
 300. BUNGE KINONDONI: NEC imemtangaza rasmi mgombea wa CUF, Maulid Mtulia kuwa mshindi wa ubunge katika jimbo la Kinondoni baada ya kumshinda mbunge anayemaliza muda wake, Idd Azzan.

  JB Julius Bett
 301. Polisi mkoani Geita wakionyesha silaha mbalimbali za jadi zilizokamatwa usiku wa kuamkia Oktoba 25 katika Kijiji cha Bulela, Kata ya Bulela.Picha na Mpiga Picha Wetu

  JB Julius Bett
 302. UCHAGUZI TANZANIA: Jimbo la Kilindi ambalo lipo katika Mkoa wa Tanga, lina jumla ya kata 21. Kata zilizofanikiwa kufanya Uchaguzi Mkuu ni 20.

  JB Julius Bett
 303. Polisi wapongezwa kusimamia uchaguzi bila kutumia nguvu

  JB Julius Bett
 304. JB Julius Bett
 305. NEC asubuhi hii wanaendelea kutangaza matokeo ya awali ya urais kwenye majimbo ambayo yamekamilisha kuhesabu kura

  JB Julius Bett
 306. PWANI: Jeshi la polisi mkoani Pwani linawashikilia vijana 22 wilayani Rufiji kwa tuhuma za kufanya fujo na kufunga barabara

  JB Julius Bett
 307. MOSHI: Kundi la wananchi wameichoma moto ofisi ya serikali kata ya Njoro Manispaa ya Moshi,wakipinga matokeo ya udiwani yaliyompa ushindi mgombea wa Chadema, Jomba Koyi.

  JB Julius Bett
 308. Wananchi wakizima moto baada ya jengo la Ofisi ya Kata ya Sandali iliyopo Temeke Mikoroshini kuchomwa na watu wasiojulikana waliokuwa wakishinikiza matokeo ya udiwani wa kata hiyo yatangazwe, Dar es Salaam jana. Picha na Omar Fungo

  JB Julius Bett
 309. UCHAGUZI 2015: Matokeo ya ubunge Jimbo la Mbagala jijini Dar es Salaam bado hayajatangazwa, msimamizi wa uchaguzi jimbo hilo amesema wanatarajia kutangaza leo mchana.

  JB Julius Bett
 310. UCHAGUZI 2015: NEC leo imeendelea kutoa matokeo ya awali ya urais majimbo mengine 51 ambapo Dk. John Magufuli anaendelea kuongoza akifuatiwa na Edward Lowassa.

  JB Julius Bett
 311. UCHAGUZI Z’BAR WAFUTWA: Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum Jecha leo ametangaza kufuta Uchaguzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na matokeo yake kwasababu haukuwa huru na haki, Televisheni ya ZBC imeripoti.

  JB Julius Bett
 312. Lowassa: Hatukubaliani na matokeo ya uchaguzi NEC

  JB Julius Bett
 313. Msemaji wa Kambi ya Kampeni ya CCM, January Makamba amesema wanajiandaa kukata rufaa kupinga matokeo kwenye majimbo ya Kawe na Iringa Mjini kwasababu hawakuridhika na utaratibu wa kuhesabu kura ulivyoenda.

  JB Julius Bett
 314. Mgombea wa urais Zanzibar kupitia CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amekutana na waandishi wa habari na kusema mwenyekiti wa ZEC hana mamlaka ya kufuta uchaguzi na matokeo yake na wanawasiliana na taasisi za kimataifa kupata msaada juu ya jambo hilo.


  JB Julius Bett
 315. Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM, January Makamba amesema CCM inashangazwa na kauli za Ukawa kwamba hawakubali matokeo ya urais yanayotangazwa na Tume, wamewataka upinzani kuwa na utamaduni wa kukubali wanaposhindwa.

  JB Julius Bett
 316. Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva anatoa ufafanuzi kuhusu kufutwa uchaguzi na matokeo yake huko Zanzibar

  JB Julius Bett
 317. Hakuna taarifa zozote za dosari za upigaji wa kura za rais wa Jamhuri ya Muungano ambazo zimepokelewa toka Zanzibar hivyo mchakato wa rais wa Jamhuri unaendelea kama ulivyopangwa – Jaji Lubuva

  JB Julius Bett
 318. Mwamvuli wa Waangalizi wa Ndani wa Uchaguzi (CEMOT) umesema kuwa sehemu kubwa ya wagombea wa ubunge na udiwani walioshindwa walikubaliana na matokeo ya kura walizopata.

  JB Julius Bett
 319. Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba anahojiwa na kituo cha televisheni cha Azam TV kuhusu tamko la ZEC kufuta uchaguzi wa Zanzibar muda huu.

  JB Julius Bett
 320. UCHAGUZI 2015: Serikali ya Marekani imetoa wito kwa Zanzibar kuondoa tamko la kufuta uchaguzi lililotolewa na ZEC leo, taarifa ya Ubalozi huo nchini yasema.

  JB Julius Bett
 321. Hali ya usalama imerejea katika Wilaya ya Rungwe baada ya kukumbwa na vurugu kwa siku mbili mfululizo zilizotokana na ushabiki wa kisiasa.

  JB Julius Bett
 322. Taarifa ya Waangalizi wa Uchaguzi wa Ndani (Cemot), yaeleza kuwa robo ya walioshindwa sawa na asilimia 27, wamepinga matokeo

  JB Julius Bett
 323. UBUNGE KIGOMA KUSINI: Mgombea wa NCCR-Mageuzi, David Kafulila apata kura 33,382.

  JB Julius Bett
 324. UBUNGE KIGOMA KUSINI: Mgombea wa CCM, Hasna Mwilima apata kura 34, 453.

  JB Julius Bett
 325. UBUNGE KIGOMA KUSINI: Msimamizi wa uchaguzi, Ruben Mfume amemtangaza Hasna Mwilima (CCM) kuwa mshindi dhidi ya Davidi Kafulila wa NCCR-Mageuzi aliyekuwa anaetetea kiti chake.

  JB Julius Bett
 326. UBUNGE KIGOMA KUSINI: Mfume amesema matokeo yamechelewa kutokana mvutano baina ya wagombea; Mwilima akitaka kura zihesabiwe upya huku Kafulila akipinga.

  JB Julius Bett
 327. UBUNGE KIGOMA KUSINI: Kafulila amepinga kutangazwa matokeo hayo akisema muafaka haukuwa umepatikana, asema atakata rufaa kuyapinga.

  JB Julius Bett
 328. UCHAGUZI TANZANIA: Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu leo amesema hali ya usalama nchini ipo vizuri, awataka wananchi wasifanye fujo katika kushangilia matokeo yatakapotangazwa.

  JB Julius Bett
 329. Polisi wamejipanga kuwadhibiti wale wanaojiandaa kufanya fujo baada ya kutangazwa matokeo ya urais’’
  IGP Mangu
  JB Julius Bett
 330. UCHAGUZI TANZANIA: Watu 106 wafikishwa Mahakama ya Wilaya Moshi leo kwa tuhuma za kuvamia na kuteketeza kwa moto ofisi ya Serikali ya Kata ya Njoro jana wakipinga matokeo ya udiwani.

  JB Julius Bett
 331. UCHAGUZI 2015: Serikali ya Uingereza leo imetoa wito kwa Zanzibar kuendelea kutoa matokeo ya uchaguzi kwa kuwa ulikuwa huru na wa haki,Taarifa ya Ubalozi huo nchini yasema.

  JB Julius Bett
 332. UCHAGUZI 2015: NEC mchana huu imekamilisha kutangaza matokeo ya urais katika majimbo yote 264, sasa wanahakiki kabla ya kutangaza mshindi.

  JB Julius Bett
 333. Tume ya Taifa ya Uchaguzi imemtangaza Dk John Magufuli kuwa ndiye mshindi wa kiti cha urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumapili ya Oktoba 25, mwaka huu.

  JB Julius Bett
 334. UCHAGUZI TANZANIA: Rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan ni miongoni mwa watu waliowasili Ukumbi wa Diamond Jubilee kushuhudia kukabidhiwa cheti Rais Mteule Dk John Magufuli leo.

  JB Julius Bett
 335. UCHAGUZI TANZANIA: Rais Jakaya Kikwete awasili Ukumbi wa Diamond Jubilee kushuhudia kukabidhiwa cheti Rais Mteule Dk John Magufuli.

  JB Julius Bett
 336. UCHAGUZI TANZANIA: Rais Mteule Dk John Magufuli na aliyekuwa mgombea mwenza wake Samia Suluhu Hassan wawasili Ukumbi wa Diamond Jubilee kwa ajili ya kukabidhiwa cheti ushindi.

  JB Julius Bett
 337. UCHAGUZI TANZANIA: Wagombea urais wa Chadema Edward Lowassa na Hashim Rungwe wa Chauma wasusia sherehe za kukabidhiwa cheti cha ushindi Dk John Magufuli wa CCM.

  JB Julius Bett
 338. UCHAGUZI TANZANIA: Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva amemkabidhi cheti cha ushindi wa kiti cha urais, Dk John Pombe Magufuli Ukumbi wa Diamond Jubilee.

  JB Julius Bett
 339. UCHAGUZI TANZANIA: Wagombea wengi wa urais wamejitokeza kwenye zoezi la kukabidhiwa cheti mshindi wa kiti cha urais, Dk John magufuli isipokuwa kwa wagombea wa Chadema, Edward Lowassa na Chauma, Hashim Rungwe na TLP, Macmillan Lyimo

  JB Julius Bett
 340. Shamra Shamra za kusherehekea ushindi wa Dk Magufuli sasa zimehamia ofisi ndogo za makao makuu ya CCM, Lumumba, na sasa rais Jakaya Kikwete anaongea

  JB Julius Bett
 341. Naungana na wenzangu hasa mwenyekiti wangu wa Chama cha Mapinduzi kumshukuru Mungu katika siku hii muhimu – Dk Magufuli

  JB Julius Bett
 342. MKONO WA SHERIA: Watu 38 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi K isutu wakikabiliwa na mashtaka manne likiwamo la kutoa vitisho vya shinikizo kwa msimamizi atoe matokeo ya Ubunge ya Mbagala bila ya kufuata utaratibu na kuchoma maboxi 11 ya kupigia kura na karatasi za kupigia kura zenye thamani ya Sh 2.2 milioni.

  JB Julius Bett
 343. Wanaharakati wa maswala ya jinsia kupitia taasisi ya Ulingo Tanzania, wamesema uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka huu haukuwa huru na haki kwa sababu wanawake wengi walikosa haki yao ya msingi ya kuchagua na kuchaguliwa kwa sababu ya vurugu mbalimbali za kisiasa.

  JB Julius Bett
 344. Askari wa JWTZ wakifanya mazoezi ya gwaride katika Uwanja wa Uhuru jana kwa ajili ya Sherehe za kumwapisha Rais Mteule.

  JB Julius Bett
 345. Sitta, Zungu kuvaana uspika

  Wakati Bunge la Kumi na Moja likitarajiwa kuanza vikao vyake wiki ijayo mjini Dodoma, Samuel Sitta na Anne Makinda, waliokalia kiti cha Spika wa mabunge mawili yaliyopita, wanatajwa kuwamo kwenye mchuano mwingine wa kuwania nafasi hiyo ya kuongoza chombo hicho cha kutunga sheria.

  Majina ya makada hao wawili wa CCM, ambao mwaka huu hawakugombea ubunge kwenye majimbo yao, ni miongoni mwa watu kadhaa wanaotajwa kuwania kuongoza Bunge la 11 ambalo linatarajiwa kuanza vikao vyake wiki ijayo.

  JB Julius Bett
 346. Wagombea sita Zanzibar waandika barua UN

  JB Julius Bett
 347. #Zanzibar

  Wagombea wa urais wa Zanzibar wa vyama sita, wamemwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN), Ban Ki Moon kumwomba asaidie kutatua mgogoro wa Zanzibar uliotokana na kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.

  JB Julius Bett
 348. Katibu Mkuu wa Chaumma, Ali Omar Juma: “Tunataka matokeo ya Zanzibar yatangazwe, pia tunataka mgogoro huu umalizwe na Jumuiya ya Mataifa iingilie kati na tunaomba kamati ya wataalamu kuchunguza na kupata ushahidi wa uchaguzi wa Zanzibar ulivyokwenda.”

  JB Julius Bett
 349. Tangu kufutwa kwa matokeo Novemba 28 na Jecha, hali ya kisiasa Zanzibar bado haijatulia huku wananchi wakiwa na hofu ya kutokea kwa vurugu licha ya wanasiasa kuwatuliza wafuasi wao kila mara.

  JB Julius Bett
 350. KATUNI POLITIKSI #Mwananchi04Novemba2015 #UchaguziTanzania

  JB Julius Bett
 351. TB Joshua, marais wanane Afrika kushuhudia kuapishwa Magufuli

  JB Julius Bett
 352. PICHA: Muhubiri Maarufu Duniani TB joshua wa Nigeria akiwa na mwenyeji wake Rais Mteule wa awamu ya tano Dk John Magufuli mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa jijini Dar es Salaam jana jioni

  JB Julius Bett
 353. TB Joshua, marais wanane Afrika kushuhudia kuapishwa Magufuli

  JB Julius Bett
 354. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, marais watakaohudhuria shughuli ya kuapishwa kwa Dk Magufuli ni Robert Mugabe (Zimbabwe), Yoweri Museveni (Uganda), Paul Kagame (Rwanda), Jacob Zuma (Afrika Kusini), Joseph Kabila (DRC), Uhuru Kenyatta (Kenya), Filipe Nyusi (Msumbiji) na Edgar Lungu (Zambia).

  JB Julius Bett
 355. Kuapishwa Magufuli

  Malawi itawakilishwa na Makamu wa Rais, Saulos Chilima wakati Namibia ikiwakilishwa na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Netumbo NandiNdaitwah. China itawakilishwa na Makamu Mwenyekiti wa chama tawala cha CPC. Nchi nyingine ambazo zimethibitisha kushiriki na ambazo zitawakilishwa na kati ya makamu wa rais, waziri mkuu, spika au balozi ni Burundi, Comoro, Angola, Botswana, Lesotho, Madagascar na Mauritius.

  JB Julius Bett
 356. Maandamano ya Chadema yakwama

  JB Julius Bett
 357. CUF kuipinga CCM mahakamani

  JB Julius Bett
 358. Chama cha Wananchi (CUF) kimetangaza kwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi katika majimbo sita, kutokana na kile ilichoeleza ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi.

  JB Julius Bett
 359. Ndesamburo: Naona fahari kuwaangusha mawaziri wa JK

  JB Julius Bett
 360. Mpambano viti maalumu kuvikutanisha vyama vitatu

  JB Julius Bett
 361. Wabunge wa viti maalumu wanaotarajiwa kupatikana ni 112, sawa na asilimia 40 ya wabunge 264 wa majimbo, ambao watajumuika na 10 wa kuteuliwa na Rais, watano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Spika (ikiwa atachaguliwa kutoka nje ya wabunge) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

  JB Julius Bett
 362. Vyama vitatu kati ya 22 vya siasa vilivyoshiriki kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, ndivyo vyenye uhakika wa kupata wabunge wa viti maalumu ambao majina yao yatatangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kesho.

  JB Julius Bett
 363. Wanachama wa Chadema waachiwa kwa dhamana

  JB Julius Bett
 364. Wanachama watano wa Chadema pamoja na watu wengine watatu wasio raia wa Tanzania wanaokabiliwa na mashtaka ya makosa ya uhalifu wa kimtandao, wameachiwa kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti waliyopewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

  JB Julius Bett
 365. Rais Jakaya Kikwete akiwa kwenye mazungumzo na katibu mkuu wa CUF ambaye ni makamu wa kwanza wa Rais wa serikali ya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Ikulu jijini Dar es Salaam jana.

  Picha na Ikulu

  JB Julius Bett
 366. MBEYA: Aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Mbeya mjini kupitia CCM, Sambwee Shitambala, leo amesema kuwa anakubaliana na ushindi alioupata mgombea wa Chadema, Joseph Mbilinyi (Sugu) na kumtaka kuweka chini itikadi za vyama na kwa pamoja kusogeza mbele maendeleo ya jiji la Mbeya.

  JB Julius Bett
 367. KUAPISHWA MAGUFULI: Viongozi, wageni waalikwa wanawasili uwanja wa Uhuru asubuhi hii kuhudhuria sherehe za kuapishwa Dk. John Magufuli kuwa Rais wa awamu ya 5.

  JB Julius Bett
 368. Rais wa Zimbabwe Mh Robert Mugabe, amewasili Uwanja wa uhuru tayari kwa shughuli ya kumuapisha Mh Dk John Magufuli

  JB Julius Bett
 369. Waziri Mkuu wa Ethiopia naye amewasili Uwanjani, tayari kwa shughuli ya kumuapisha Mh John Magufuli

  JB Julius Bett
 370. Tayari Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, naye amewasili Uwanja wa uhuru kwa shughuli ya kumuapisha Mh John Magufuli

  JB Julius Bett
 371. KUAPISHWA MAGUFULI: kutoka uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ni sherehe za kuapishwa kwa Rais wa awamu ya 5 Tanzania Dk John Joseph Magufuli

  JB Julius Bett
 372. KUAPISHWA MAGUFULI: Jaji Mkuu Othman Chande na Viongozi wa dini wameelekea katika jukwaa la kiapo

  JB Julius Bett
 373. KUAPISHWA MAGUFULI: Rais Mteule, John Magufuli na makamu wa rais mteule, Samia Suluhu Hassan wamepanda kwenye jukwaa la kiapo.

  JB Julius Bett
 374. KUAPISHWA MAGUFULI: Rais Mteule, John Magufuli na makamu wa rais mteule, Samia Suluhu Hassan wamepanda kwenye jukwaa la kiapo.

  JB Julius Bett
 375. KUAPISHWA MAGUFULI: Rais Kikwete amewasili kwenye uwanja wa Uhuru tayari kwa ajili ya sherehe za kuapishwa kwa Dk. Magufuli, kisha atamkabidhi rasmi madaraka.

  JB Julius Bett
 376. KUAPISHWA MAGUFULI: Zoezi la kupiga mizinga 21 limemalizika na gwaride maalum linaendeela kujipanga.

  JB Julius Bett
 377. KUAPISHWA MAGUFULI: Bendera ya rais inashushwa muda huu, kisha DK Magufuli ataapishwa rasmi.

  JB Julius Bett
 378. KUAPISHWA MAGUFULI: Rais mteule John Pombe Magufuli anaanza kula kiapo

  JB Julius Bett
 379. RAIS MPYA: Dk John Pombe Magufuli ameshakula kiapo na sasa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano.

  JB Julius Bett
 380. Makamu wa rais mteule, Samia Suluhu Hassani ameshaapishwa na sasa rasmi anakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza nchini kushika wadhifa huo

  JB Julius Bett
 381. Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeiry anasoma dua hivi sasa.

  JB Julius Bett
 382. ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania, Muadhama Polycap Kadinali Pengo anasoma sala kwa niaba ya Baraza la Maaskofu Tanzania.

  JB Julius Bett
 383. Rais aliyemaliza muda wake, Jakaya Kikwete na aliyekuwa makamu wake, Dk Muhamed Ghalib Bilal wanasindikizwa na gari maalum kwenda jukwaa kuu baada ya kumaliza shughuli ya kuapishwa Rais Dk Magufuli.

  JB Julius Bett
 384. RAIS MPYA: Rais Dk John Pombe Magufuli anapewa heshima ya kupigiwa mizinga 21 muda huu

  JB Julius Bett
 385. Rais Dk Magufuli anakagua gwaride rasmi lililotengeneza umbo la Alpha kuashiria kuanza kwa utawala wake.

  JB Julius Bett
 386. BURUDANI mbalimbali za ngoma zinaendelea hivi sasa kutoka vikundi mbalimbali vya sanaa.

  JB Julius Bett
 387. WAKATI shughuli zikielekea ukingoni, Rais Dk John Magufuli anaomba kuongea kidogo na Watanzania.

  JB Julius Bett
 388. Nawashukuru viongozi wa dini ambao wameshiriki kwa njia moja ama nyingine katika kuliombea taifa letu - Rais DK Magufuli.
  JB Julius Bett
 389. Namshukuru Mungu kwa kutajilia uvumulivu hasa kwa wenzetu wa Zanzibar ambao wanapita katika kipindi kigumu - DK Magufuli
  JB Julius Bett
 390. Tutafanya kazi kwa juhudi zote kwa maendeleo ya taifa letu, natambua tunajukumu la dhati katika kuwatumikia Watanzania - Dk Magufuli
  JB Julius Bett
 391. Kilicho mbele yetu ni kuwatumikia Watanzania wote bila kujali itikadi, sasa hapa Kazi Tu - Dk Magufuli
  JB Julius Bett
 392. SHUGHULI za kuapishwa kwa Rais Dk John Magufuli zimefikia tamati na sasa rais Magufuli anaondoka Uwanja wa Uhuru.

  JB Julius Bett
 393. PILIKA PILIKA ZA LEO: Mzee Nassoro Salum akiendesha baiskeli huku akiwa amempakia mtoto wake Yusuph wakizunguka katika mitaa mjini Singida leo ambaye amedai anamjengea mazingira mazuri kuja kuwa rais wa Tanzania ifikapo mwaka 2050. Picha na Gasper Andrew

  JB Julius Bett
 394. Rais John Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na wageni waalikwa kutoka ndani na nje ya nchi wawasili Ikulu, jijini Dar es Salaam

  JB Julius Bett
 395. Wakazi wa kata ya Ipembe mjini Singida wakiangalia matangazo ya moja kwa moja ya luninga (TV) yaliokuwa yakionyesha hafla ya kuapishwa kwa Rais wa awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli iliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Picha na Gasper Andrew

  JB Julius Bett
 396. KAZI IMEANZA: Rais Dk John Magufuli ameitisha rasmi Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanza shughuli tarehe 17 mwezi huu na anatarajia kupendekeza jina la Waziri Mkuu tarehe 19 Novemba likaridhiwe bungeni. Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amesema leo.

  JB Julius Bett
 397. Rais Dk John Magufuli ameitisha rasmi Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanza shughuli tarehe 17 mwezi huu na anatarajia kupendekeza jina la Waziri Mkuu tarehe 19 Novemba likaridhiwe bungeni. Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.

  JB Julius Bett
 398. Rais Dk John Magufuli amemteua George Masaju kuwa mwanasheria Mkuu wa Serikali na ataapishwa kesho saa nne asubuhi.

  JB Julius Bett
 399. MARUFUKU SAFARI ZA NJE: Rais Dk. Magufuli leo amepiga marufuku watendaji kusafiri nje ya nchi, akasimu majukumu kwa mabalozi hadi itakapoamuliwa vinginevyo.

  JB Julius Bett
 400. MECHI YA KIRAFIKI: Timu ya Soka ya Wanawake Twiga Stars yawafunga wenzao wa Malawi bao 2-0 Dar leo katika mchezo wa kumuaga Ester Chabruma wa Twiga anayestaafu.

  JB Julius Bett
 401. MGOGORO WA KISIASA Z’BAR: Baraza Kuu la Chama Cha Wananchi CUF leo limesema mgogoro wa kisiasa Visiwani utamalizwa kwa ZEC kutangaza matokeo, mshindi kuapishwa.

  JB Julius Bett
 402. MGOMO UJERUMANI: Mgomo wa wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Lufthansa waingia siku ya tatu leo wakidai mafao bora ya kustaafu. Ndege 929 zasitisha safari zake.

  JB Julius Bett
 403. MGOGORO ZANZIBAR: Wawakilishi wateule 27 wa CUF kutoka Z’bar wapinga jijini Dar leo uamuzi wa ZEC kufuta ushindi wao kwa kuwa walishapewa vyeti vya ushindi.

  JB Julius Bett
 404. MAGUFULI ASHTUKIZA: Rais John Magufuli mchana huu amefanya ziara ya ghafla katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar, apita kwenye wodi kuangalia wagonjwa.

  JB Julius Bett
 405. SIASA: Chama kipya cha siasa, Tanzanian Patriotic Front (TPF-Mashujaa) kimepata usajili wa muda kuanzia leo, Msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi atangaza.

  JB Julius Bett
 406. Sitta: Nina sifa zote kuongoza Bunge lijalo

  JB Julius Bett
 407. Makamu wa rais, mama Samia Suluhu Hassan akabidhiwa ofisi rasmi na Dk Bilal

  JB Julius Bett
 408. ZIARA YA MAGUFULI MUHIMBILI: Rais Dk John Magufuli ameifuta Bodi ya Hospitali ya Muhimbili leo, pia amemsimamisha kazi na kumuhamishia wizarani aliyekuwa kaimu mkurugenzi wa hospitali hiyo.

  JB Julius Bett
 409. Serikali mkoani Mbeya leo imetoa hati miliki za kimila 2,800 kwa wakulima wa Wilaya ya Mbarali ili kuwawezesha kukopesheka na kupata mtaji wa kufaya kilimo cha mpunga.

  JB Julius Bett
 410. JENGO LA KIHISTORIA LAANGUKA: Jumba la Kihistoria la Maajabu la Beit al Ajaib lililopo Mji Mkongwe, Zanzibar limeporomoka baadhi ya kuta zake leo, hii ni mara ya pili kwa kuta za jengo hilo kuporomoka. Hakuna maafa yoyote kwa binadamu zaidi ya uharibifu wa mali.

  JB Julius Bett
 411. JUMBA LAANGUKA Z’BAR: Jumba la kihistoria la maajabu, Bait Al Ajaib (House of Wonder) liliopo Mji Mkongwe, Zanzibar limeporomoka baadhi ya kuta zake leo.

  JB Julius Bett
 412. KIWANDA CHAZINDULIWA: Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi leo amezindua Kampuni ya Avic-Shantui Tanzania Ltd ya kuuza mitambo ya kilimo na ujenzi yakiwamo matingatinga.
  Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam, Mzee Mwinyi alisema hatua ya kampuni kuja kuwekeza nchini ni matunda ya urafiki wa muda mrefu wa nchi mbili Tanzania na China.

  JB Julius Bett
 413. UBUNGE LUDEWA: Wagombe watatu kati ya kumi wanaoomba kuteuliwa na CCM kuwania ubunge Jimbo la Ludewa wamejitoa katika mchakato huo mchana huu, mmoja kati ya wagombe hao, Johnson Mgimba amesema amechukua uamuzi huo kwa maslahi ya wananchi wa Ludewa.

  JB Julius Bett
 414. UVUVI HARAMU. Jeshi la polisi mkoani Mtwara kwa kushirikiana na Marine Park pamoja na kikosi maalumu cha taifa kinachoshughulikia uhifadhi wa mazingira pamoja na bahari wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa mbalimbali wanaojihusisha na uvuvi haramu katika bahari ya Hindi. PICHA NA HAIKA KIMARO

  JB Julius Bett
 415. MGOGORO ZANZIBAR: Rais wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Salmin Amour Juma na Makamu wa Rais Mstaafu, Dk Mohamed Ghalib Bilal leo wameongezwa katika kikao cha kusaka suluhu visiwani Zanzibar baada ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa rais na wawakilishi.

  JB Julius Bett
 416. MGOGORO ZANZIBAR; Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amemtaka rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kutangaza hali ya hatari visiwani Zanzibar, endapo suala la kurudia uchaguzi ama kutangazwa kwa mshindi wa kiti cha urais likishindikana.

  JB Julius Bett
 417. MBIO ZA USPIKA: Spika wa zamani, Samwel Sitta na waziri wa zamani wa mambo ya ndani, Dk Emmanuel Nchimbi ni miongoni mwa makada tisa wa CCM waliochukua fomu leo kuomba kuteuliwa kugombea uspika Bunge lijalo.

  JB Julius Bett
 418. MLIPUKO LEBANON: Watu 43 wauawa Ijumaa, zaidi ya 200 waumia katika mashambulio 2 ya mabomu ya kujitoa mhanga kwenye makazi ya watu mjini Beirut, maofisa wasema.

  JB Julius Bett
 419. MBIO ZA USPIKA CCM: Mbunge mteule wa Ilala Mussa Azzan Zungu achukua fomu leo ofisi ndogo za CCM Lumumba kuomba kuteuliwa kuwania Unaibu Spika wa Bunge la 11.

  JB Julius Bett
 420. MBIO ZA USPIKA CCM: Spika wa Bunge la 10 Anne Makinda asisitiza kutogombea Uspika Bunge la 11 baada ya utumishi uliotukuka serikalini, asema anawaachia wengine.

  JB Julius Bett
 421. MGOMO URAFIKI: Wafanyakazi leo wameendelea na siku ya pili ya mgomo licha ya uongozi kuwataka warejee sehemu zao za kazi na kutishia kuchukua hatua kwa wakaidi.

  JB Julius Bett
 422. MGOGORO Z’BAR: Mgombea urais Zanzibar (CUF), Maalim Seif Hamad leo amefanya mazungumzo Dar na aliyekuwa mgombea wa Chadema, Edward Lowassa na viongozi wengine wa Ukawa kuhusu mgogoro wa kisiasa.

  Wasema watakutana na waandishi wa habari Jumapili kueleza walichojadili.

  JB Julius Bett
 423. UGAIDI UFARANSA: Polisi waua magaidi 8; Wanajeshi 1,500 wasambazwa eneo la tukio mjini Paris; Serikali yatangaza hali ya hatari nchi nzima.

  JB Julius Bett
 424. UGAIDI UFARANSA: Waasi wa Islamic State wamedai kuhusika na shambulio mjini Paris ambayo yameua zaidi ya watu 120.

  JB Julius Bett
 425. KUTOKA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM ->Benchi la ufundi la TanzanIa, Mkwasa, Kibadeni na Peter Manyika

  JB Julius Bett
 426. KUTOKA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM, ni wachezaji wa akiba wa Tanzania wakiwa kwenye benchi lao

  JB Julius Bett
 427. Tuishangilie kwa nguvu, tujivunie Taifa Stars #TanzaniaVsAlgeria #TanzaniaKwanza #Uzalendo

  JB Julius Bett
 428. SHUGHULI IMEANZA HARAKA HARAKA. ->Mbwana Samatta amekosa nafasi/goli ya wazi mwanzoni mwa mchezo #TanzaniaVsAlgeria #TanzaniaKwanza

  JB Julius Bett
 429. TAIFA STARS Vs Algeria kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar .Ni mechi muhimu kusaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia la 2018.

  JB Julius Bett
 430. MBIO ZA USPIKA: CCM yafunga mchakato leo kwa wanachama 21 kuchukua fomu za uspika, mmoja akiwania unaibu. Kamati Kuu yapanga kukutana Dodoma kesho kuwajadili.

  JB Julius Bett
 431. PIGO CHADEMA: Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo ameuawa leo mjini Katoro kwa sababu zinazohusishwa na siasa. Mganga Mkuu Geita athibitisha.

  JB Julius Bett
 432. MAUAJI GEITA: Jeshi la polisi linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema, Alphonce Mawazo aliyeuawa jana.

  JB Julius Bett
 433. MOTO HANDENI: Moto uliozuka leo alfajiri wateketeza nyumba mbili Kata ya Kibaoni wilayani Handeni, Tanga; Zimamoto wafika kutoa msaada, taarifa zaidi baadaye.

  JB Julius Bett
 434. UBUNGE LULINDI: Jerome Bwanausi wa CCM atangazwa mshindi Jimbo la Lulindi mkoani Mtwara kwa kupata kura 17,715 kwenye uchaguzi uliofanyika jana, NEC yaeleza.

  JB Julius Bett
 435. MAAJABU KAHAMA: Wachimba madini 5 kati ya 6 waliofukiwa na kifusi kwa siku 41 machimbo ya nyangarata -Kahama, waokolewa hai usiku wa kuamkia leo, polisi waeleza

  JB Julius Bett
 436. MBIO ZA USPIKA: CCM wampitisha Job Ndugai kuwania uspika baada ya Abdula Mwinyi na Dk Tulia Ackson kujitoa kuwania nafasi hiyo, Nape Nnauye aeleza mchana huu.

  JB Julius Bett
 437. HUDUMA ZA MRI ZASITISHWA: Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imesitisha kuanzia leo huduma ya vipimo ya MRI iliyokuwa imetengemaa siku chache zilizopita kwa ajili ya matengenezo zaidi.

  Write an update...

  JB Julius Bett
 438. BUNGE LA 11: Katibu wa Bunge Dk.Thomas Kashilila asubuhi hii amemteua Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge kuwa M/kiti wa uchaguzi wa Spika unaofanyika leo.

  JB Julius Bett
 439. ‪#‎KUTOKADodoma‬

  NDUGAI: "Nimekuwa mbunge kwa vipindi 3, naamini nina uwezo na uzoefu niliopata chini Mh Msekwa, Sitta na Makinda" ‪#‎UchaguziWaSpika‬

  JB Julius Bett
 440. UCHAGUZI WA SPIKA: Wabunge wameanza zoezi la kupiga kura kumchagua spika wa kuliongoza Bunge la 11 asubuhi hii mjini Dodoma.

  JB Julius Bett
 441. #KUTOKADodoma

  UCHAGUZI WA SPIKA: Wabunge wamepata mapumziko mafupi kusubiri zoezi la kuhesabu kura, kikao kurejea saa 6:15 mchana huu ili kutangazwa mshindi wa kiti hicho.

  JB Julius Bett
 442. NDUGAI SPIKA MPYA: Wabunge leo wamchagua Mbunge wa Kongwa (CCM), Job Ndugai kuwa Spika mpya wa Bunge la 11 akiwashinda wagombea wengine 7 wa kiti hicho.

  JB Julius Bett
 443. BUNGE LA 11: Katibu wa Bunge Dk.Thomas Kashilila amemuapisha Mbunge wa Kongwa (CCM), Job Ndugai kuwa Spika mpya wa Bunge la 11 mchana huu mjini Dodoma.

  JB Julius Bett
 444. UCHAGUZI 2015: Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhan Kailima ametangaza jumla ya majina 1393 ya Madiwani wa Viti Maalumu kwa vyama 5 leo jijini Dar.

  JB Julius Bett
 445. NYARA ZANASWA DAR: Watanzania 2 wamekamata wakiwa na zaidi ya Kobe 200 katika Uwanja wa Ndege Dar wakitaka kuwasafirisha kwenda Malaysia, Polisi yathibitisha leo.

  JB Julius Bett
 446. BUNGENI DODOMA: Kikao cha Bunge kinaendelea jioni hii kwa wabunge wateule kuendelea kula kiapo cha uaminifu.

  JB Julius Bett
 447. UNAIBU SPIKA: Wabunge wa CCM wamemteua Dk Tulia Ackson kugombea nafasi ya Unaibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  JB Julius Bett
 448. BOMOABOMOA DAR: Manispaa ya Kinondoni leo imeanza zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa bila kufuata utaratibu kwenye maeneo ya wazi huko Mwenge jijini Dar.

  JB Julius Bett
 449. KESI YA PONDA: Korti ya Morogoro leo yaahirisha kutoa hukumu ya kesi ya jinai inayomkabili Kiongozi wa Taasisi za Kiislamu Sheikh Ponda Issa Ponda hadi Novemba 30 mwaka huu.

  JB Julius Bett
 450. Ndugu na jamaa wa wabunge wakiimba kwa furaha katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma baada ya wabunge wao kuapishwa. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 451. Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchema akila kiapo cha utii mbele ya Spika wa Bunge, Job Ndugai katika ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 452. Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Joyce Mukya akila kiapo cha utii mbele ya Spika wa Bunge, Job Ndugai katika ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 453. HUDUMA ZA AFYA: Mfuko pensheni wa PSPF umeingia ubia na Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa na sasa wanatoa fao la huduma za afya kwa wanachama wa hiari wa PSPF.

  JB Julius Bett
 454. HOTUBA YA RAIS: Vyama vinavyounda Ukawa wamwandikia Spika Job Ndugai barua kutaka kujua uhalali wa Rais John Magufuli kuhutubia Bunge bila matokeo Rais wa Zanzibar kujulikana.

  Wamesema kuwa hawatakubali Katiba ivunjwe kwa kumruhusu Dk Shein kuingia bungeni wakati muda wake wa kushika madaraka ulishapita. Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwenye mkutano wa pamoja wa Ukawa.

  JB Julius Bett
 455. WAZIRI MKUU ATAJWA: Spika Job Ndugai leo mjini Dodoma amtaja Kassim Majaliwa kuwa mteule wa Rais Magufuli katika nafasi ya Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya 5.

  JB Julius Bett
 456. . UTEUZI WA WAZIRI MKUU: Bunge laahirishwa kwa dakika 45 kuwapa fursa wabunge kutafakari uteuzi wa mbunge Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu kabla ya kumthibitisha.

  JB Julius Bett
 457. KUTOKA DODOMA


  --> Mwanasheria mkuu wa Serikali George Masaju anawasilisha hoja ya serikali ya kumthibitisha Waziri Mkuu Mteule Kassim Majaliwa

  JB Julius Bett
 458. KUMTHIBITISHA WAZIRI MKUU: Wabunge wa CCM, William Lukuvi (Ismani); Jenista Mhagama (Peramiho); Dk. Hamis Kigwangalla (Nzega Vijijini); Kangi Lugola (Mwibara) na Andrew Chenge (Bariadi Magharibi) wachangia hoja ya AG na kuunga mkono.

  JB Julius Bett
 459. KUMTHIBITISHA WAZIRI MKUU: Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah atoa utaratibu ambapo wabunge watatakiwa kupiga kura za NDIYO au HAPANA ili kumthibitisha Waziri Mkuu mteule, Kassim Majaliwa.

  JB Julius Bett
 460. KUMTHIBITISHA WAZIRI MKUU: Wabunge wameshapiga kura na sasa zoezi la kuhesabu kura limeanza rasmi ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.

  JB Julius Bett
 461. KUTOKA DODOMA: Mchakato wa uchaguzi wa nafasi ya Naibu Spika bungeni unaendelea hivi sasa wagombea Magdalena Sakaya (CUF) na Dk Tulia Ackson (CCM) wanaomba kura kwa wabunge.

  JB Julius Bett
 462. KUTOKA BUNGENI: Mgombea wa nafasi ya Naibu Spika kupitia CCM DK Tulia Ackson amemaliza kuomba kura hata hivyo amekuwa akikatizwa na kelele kutoka kwa baadhi ya wabunge.

  JB Julius Bett
 463. UTEUZI WAZIRI MKUU: Wabunge mjini Dodoma wamemthibitisha kwa kura 258 za ndio Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wabunge 91 wamepiga kura ya hapana.

  JB Julius Bett
 464. MAJALIWA ATHIBITISHWA: Bunge limemthibitisha Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu kwa kura 258 (73.5%). Kura 91 (25.9) zimepinga uteuzi wake, kuapishwa kesho.

  JB Julius Bett
 465. Dk TULIA NDIYE UNAIBU SPIKA: Ashinda kwa kura 250 (71.2%) dhidi ya mpinzani wake Magdalena Sakaya (CUF) aliyepata kura 101 (28.8%). Dk Tulia ameshaapishwa.

  JB Julius Bett
 466. Waudumu wa Bunge wakiwa wamebeba masanduku ya kura za wabunge walizopiga kumchaguwa Waziri Mkuu mteule, Majaliwa Kassim Majaliwa wakizipeleka kuhesabiwa, mjini Dodoma leo hii. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 467. Watumishi wa Bunge wakifanya kazi za kuhesabu kura zilizopigwa na wabunge kuidhinisha jina la Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano,mjini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 468. Waziri Mkuu mteule, Majaliwa Kassim Majaliwa akipongezwa na wabunge kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo mjini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 469. Waziri Mkuu mteule, Majaliwa Kassim Majaliwa akiwashukuru wabunge kwa kumuidhinisha kushika wadhifa huo, bungeni mjini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 470. Waziri Mkuu mteule, Majaliwa Kassim Majaliwa (kulia) akiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju wakitoka katika ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 471. KESI YA MATTAKA: Korti ya Kisutu leo yawakuta na kesi ya kujibu aliyekuwa Mkurugenzi Shirika la Ndege (ATCL), David Mattaka na wenzake 2 katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi.

  JB Julius Bett
 472. WAZIRI MKUU KUAPISHWA: Wageni waalikwa waendelea kuwasili Ikulu Ndogo ya Chamwino, Dodoma tayari kwa hafla ya kuapishwa kwa Waziri Mkuu Mteule, Kassim Majaliwa.

  JB Julius Bett
 473. KIAPO CHA WAZIRI MKUU: Waziri Mkuu Mteule, Kassim Majaliwa awasili ukumbini muda huu tayari kwa zoezi la kula kiapo mbele ya Rais Dk. John Magufuli.

  JB Julius Bett
 474. KIAPO CHA WAZIRI MKUU: Rais Dk. John Magufuli awasili ukumbini tayari kwa hafla ya kumuapisha Waziri Mkuu Mteule, Kassim Majaliwa.

  JB Julius Bett
 475. KIAPO CHA WAZIRI MKUU: Waziri Mkuu-Mteule Kassim Majaliwa ala kiapo mbele ya Rais Magufuli Ikulu ndogo Dodoma leo baada ya kuteuliwa, kuidhinishwa na Bunge.

  JB Julius Bett
 476. KIAPO CHA WAZIRI MKUU: Viongozi wa serikali na wageni waalikwa wanampongeza Waziri Waziri Mkuu kwa kuteuliwa na kiapo, na kumtakia heri katika majukumu yake mapya.

  JB Julius Bett
 477. KIAPO CHA WAZIRI MKUU: Rais Magufuli, Waziri Mkuu Majaliwa, viongozi wengine wa serikali na wageni waalikwa washiriki zoezi la upigaji picha za pamoja kwa ajili ya kumbukumbu.

  JB Julius Bett
 478. UZINDUZI WA BUNGE: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju atoa hoja ya kutengua kanuni ili kuwaruhusu viongozi wa kitaifa kuingia Bungeni kushuhudia Rais Magufuli akihutubia Bunge.

  JB Julius Bett
 479. BOMOABOMOA KINONDONI: Manispaa leo imesema zaidi ya nyumba 20 zimebomolewa katika operesheni ya kubomoa nyumba zilizojengwa maeneo ya wazi, hifadhi za barabara.

  JB Julius Bett
 480. Shughuli ya ubomoaji Mbezi Beach BLock J

  JB Julius Bett
 481. Nyumba 20 zimebomolewa katika operesheni ya kubomoa nyumba zilizojengwa maeneo ya wazi, hifadhi za barabara.

  JB Julius Bett
 482. Shughuli ya ubomoaji Mbezi Beach BLock J

  JB Julius Bett
 483. Shughuli ya ubomoaji Mbezi Beach BLock J

  JB Julius Bett
 484. BOMOABOMOA KINONDONI: Manispaa leo imesema zaidi ya nyumba 20 zimebomolewa katika operesheni ya kubomoa nyumba zilizojengwa maeneo ya wazi, hifadhi za barabara.

  JB Julius Bett
 485. UZINDUZI WA BUNGE: Rais John Magufuli awasili Bungeni mjini Dodoma mchana huu kwa ajili ya kulihutubia na kulizindua Bunge la Kumi na Moja.

  JB Julius Bett
 486. Wabunge wa Ukawa wapiga kelele za kumtukuza na kumsifu Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad wakati Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein akiingia Bungeni.

  JB Julius Bett
 487. UZINDUZI WA BUNGE: Spika wa Bunge Job Ndugai aamuru wabunge wa upinzani watoke nje baada kutotii amri iliyowataka wanyamaze, kuketi. Watii, watoka nje ya ukumbi.

  JB Julius Bett
 488. UZINDUZI WA BUNGE: Spika wa Bunge Job Ndugai amkaribisha Rais John Magufuli kulihutubia na kulizindua Bunge baada ya wabunge wa Upinzani kutoka nje ya ukumbi.

  JB Julius Bett
 489. UZINDUZI WA BUNGE: Rais Magufuli amesema serikali yake haitavumilia kikundi chochote kitakacho vuruga amani ya nchi, kuwashughulikia wote wakatakaobainika.

  JB Julius Bett
 490. UZINDUZI WA BUNGE: Rais Magufuli ataja kero mbalimbali zilizotajwa na wanachi wakati wa kampeni na kuwataka wote waliochaguliwa kupitia CCM wanashiriki kutafuta ufumbuzi.

  JB Julius Bett
 491. UZINDUZI WA BUNGE: Rais Magufuli aahidi Bungeni leo kuwa ataupatia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa Zanzibar kwa kuimarisha mazungumzo baina ya vyama vya CCM na CUF.

  JB Julius Bett
 492. UZINDUZI WA BUNGE: Rais Magufuli awataka wawekezaji ambao wameuziwa viwanda lakini hawajaanza uzalishaji kuanza kuviendeleza mara moja, aonya watakaoshindwa sheria kutumika kuwapa wengine.

  JB Julius Bett
 493. UZINDUZI WA BUNGE: Rais Magufuli asema ahadi yake ya kukifanya kilimo, ufugaji na uvuvi kuwa wa kisasa ipo palepele. Asema serikali itaboresha bei za mazao.

  JB Julius Bett
 494. UZINDUZI WA BUNGE: Rais Magufuli asema Bungeni leo serikali yake itahakikisha elimu bure tangu shule ya msingi hadi sekondari inatolewa bure, mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu inatolewa kwa wakati.

  JB Julius Bett
 495. UZINDUZI WA BUNGE: Rais John Magufuli asema Bungeni leo serikali yake itawashughulikia wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya, ataka wananchi wamuombee.

  JB Julius Bett
 496. Rais John Magufuli akilihutubia bunge mjini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 497. KUTOKA DODOMA:


  Rais John Magufuli akilihutubia Bunge mjini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 498. PICHA: ‪#‎KutokaBungeniDodoma‬

  Wabunge wa kambi rasmi ya upinzani wakitoka Bungeni baada ya kuamrishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai baada ya kupiga kelele wakimtaja Maalim Seif, wakati wakipinga Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein , Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi, Seif Ali Idi na Spika wa Baraza la Wawakilishi kuingia bungeni, mjini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 499. Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia wakiwa wameimalisha ulinzi ndani ya ukumbi wa bunge. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 500. UZINDUZI WA BUNGE: Rais Magufuli asema ameamua kuunda Mahakama ya rushwa na ufisadi ili kurahisisha mapambano dhidi ya rushwa, awataka wabunge wamuunge mkono.

  JB Julius Bett
 501. Wabunge wa upinzani wakitoka Bungeni baada ya kuamrishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai baada ya kupiga kelele wakimtaja Maalim Seif, wakati wakipinga Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein , Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi, Seif Ali Idi na Spika wa Baraza la Wawakilishi kuingia bungeni, mjini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 502. UZINDUZI WA BUNGE: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atoa hoja ya kuahirisha bunge mjini Dodoma jioni hii, yaridhiwa, laahirishwa hadi Januari 2016.

  JB Julius Bett
 503. ANGLIKANA NYANDA ZA JUU KUSINI WAPATA ASKOFU MPYA: Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Nyanda za Juu Kusini limemweka wakfu leo Askofu Julius Lugendo kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo.Ibada ya Misa ya kumweka wakfu Askofu Lugendo imeendeshwa na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo nchini Dk Jacob Chimeledya.Askofu Julius Lugendo anawekwa wafu kuchukua nafasi ya Askofu John Mwela anayestaafu baada ya kuhudumu kwenye Dayosisi hiyo tangu mwaka 1999.

  Wakati huohuo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abass Kandoro amemwakilisha Rais Dk John Magufuli kwenye sherehe hizo.


  JB Julius Bett
 504. MAZISHI YA MAWAZO: Uongozi wa Chadema umesema leo kuwa unatarajia kufungua shauri Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kesho kuomba tafsiri ya mahakama baada ya polisi kuzuia mwili wa marehemu Alphonce Mawazo kwa maziko.

  JB Julius Bett
 505. MANUSURA WA MGODI: Mmoja wa manusura wa machimbo ya Nyangalata waliofukiwa kwa siku 41 amefariki leo baada ya kupata matatizo ya kupumua, daktari athibitisha.

  JB Julius Bett
 506. SHEREHE ZA UHURU:Rais John Magufuli ameamua siku ya Uhuru tarehe 9 Disemba iwe siku ya kufanya usafi wa mazingira na hakutakiwa na gwaride. Wananchi wote wataenda kufanya usafi na ameagiza wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi waandae vifaa.

  Amesema fedha zilizokuwa zimeandaliwa kwa ajili ya sherehe hizo zitapelekwa kwenye eneo lenye mahitaji ya kuhudumia wananchi..

  JB Julius Bett
 507. MZOZO Z'BAR: Kikao cha wagombea urais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad (CUF), Dk. Ali Mohamed Shein (CCM) kimeendelea tena leo Ikulu, Zanzibar kutafuta ufumbuzi baada ya matokeo ya uchaguzi kufutwa.

  JB Julius Bett
 508. UHALIFU: Mbeya. Raia wawili wa nchini uganda wanashikiliwa na polisi kwa mkoani Mbeya kwa kosa la kupatikana na bastola yenye risasi 14 na funguo za pingu.

  Kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa juzi katika mpaka wa Kasumulu wilayani Kyela wakielekea nchi jirani Malawi.

  JB Julius Bett
 509. UJANGILI: Mbeya. Raia wa kigeni wanne kutoka China, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya wakikabiliwa na mashtaka matatu ya uhujumu uchumi.

  Washtakiwa hao Song Leo (33), Xiao Shaodan (29), Chen Jianlin (34) na Hu Liang (30) wamepandishwa kizimban leo baada ya kukamatwa na nyara za Serikali ambazo ni pembe za faru 11 zenye thamani ya Sh 902.8 milioni. Kesi hiyo inaendelea kusikilizwa kesho.

  JB Julius Bett
 510. MICHUANO YA CECAFA: Kili Stars yasonga hatua ya robo fainali michuano ya Cecafa leo baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Rwanda.

  JB Julius Bett
 511. MAZISHI YA MAWAZO: Kesi ya kuomba kuondolewa amri ya polisi inayozuia kuagwa kwa mwili wa Alphonce Mawazo wa Chadema yaanza kusikilizwa Korti Kuu Mwanza leo.

  JB Julius Bett
 512. Papa Francis kutua kwa kishindo Nairobi leo

  JB Julius Bett
 513. KESI YA UCHAGUZI: Aliyekuwa mgombea ubunge Kyerwa, Benedict Mutungirehi (Chadema) afungua kesi Korti Kuu Bukoba leo kupinga ushindi wa Innocent Bilakwate (CCM)

  JB Julius Bett
 514. AMRI YA DC: DC Kinondoni P. Makonda awatupa rumande maofisa ardhi zaidi ya 10 kwa saa 6 Kawe kwa kuchelewa kufika eneo walilopatana. Asema kesho watarudi kazini

  JB Julius Bett
 515. Kiongozi wa kanisa la katoliki duniani Papa Francis amewasili nchini Kenya na kupokelewa na Rais @UKenyatta

  JB Julius Bett
 516. Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kesho mchana inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi iliyofunguliwa na ndugu wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo wakipinga zuio la polisi kuchukua na kuaga mwili wa Mawazo kwa maelezo ya kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu.

  JB Julius Bett
 517. #‎ZIARA‬: Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd, Francis ‪#‎Nanai‬ akikabidhi gazeti la ‪#‎Mwananchi‬ kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya ‪#‎Magufuli‬ iliyopo ‪#‎Chato‬

  JB Julius Bett
 518. MINZIRO ATUA PANONE: Kocha wa zamani wa Klabu za JKT Ruvu na Yanga, Felix Minziro amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuifundisha timu ya Panone FC ya jijini Moshi. Panone inashiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL)

  JB Julius Bett
 519. UAMUZI WA KORTI: Mahakama ya Bunda leo yawafutia wafuasi 3 wa Chadema shtaka la unyang'anyi wa silaha kwa kukosekana ushahidi. Wabakiwa na kesi ya wizi wa simu.

  JB Julius Bett
 520. POLISI WATIMULIWA: Jeshi la Polisi Kigoma limewafuta kazi askari 3 kwa kusambaza taarifa za uongo dhidi ya viongozi wao mitandaoni, RPC Ferdinand Mtui asema leo

  JB Julius Bett
 521. WAZIRI MKUU BANDARINI: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa afanya ziara ya kushtukiza bandarini Dar leo. Awaita TPA, TRA kikaoni kujadili changamoto kuhusu ufanisi na mapato

  JB Julius Bett
 522. HUKUMU YA MAHAKAMA: Korti wilayani Mbeya yawahukumu wakazi 2 wa Uyole kifungo cha miaka 7 kila mmoja kwa kuvunja na kuchoma nyumba ya waliyemtuhumu kwa uchawi.

  JB Julius Bett
 523. Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa leo ameamuru kukamatwa kwa maafisa kadhaa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na wengine kufukuzwa kazi baada ya kufanya ziara ya kushtukiza Bandarini na kukuta uozo . Maafisa hao wametakiwa kusalimisha hati zao za kusafiria, nah ii imekuja baada ya kugundulika kuwa kuna makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 80 ambayo data za Mamlaka ya Bandari inazo lakini katika mtandao wa TRA hayaonekani.

  JB Julius Bett
 524. HUKUMU YA PONDA: Mahakama mjini Morogoro yamwachia huru leo Sheikh Issa Ponda baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha makosa yake.

  JB Julius Bett
 525. FEDHA ZA UHURU: Rais John Magufuli ameamuru fedha zilizopaswa kutumika kugharamia shamra shamra za siku ya Uhuru sasa zitumike kufanya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es Salaam. Tayari fedha hizo kiasi cha Sh4 bilioni zimepelekwa Tanroads kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo.

  JB Julius Bett
 526. Mfuko wa kumsaidia mke, mtoto wa Mawazo kuanzishwa utaitwa Alphonce Mawazo Trust Fund

  JB Julius Bett
 527. SAKATA LA MAKONTENA: Maofisa Polisi, TRA washikilia makontena 9 Tangibovu, Dar baada ya kutilia shaka kuwa yalikuwa yanasafirishwa kinyemela usiku kuamkia leo.

  JB Julius Bett
 528. AJALI YA NDEGE: Ripoti ya wachunguzi Indonesia yasema leo hitilafu ndiyo sababu ya kuanguka ndege ya AirAsia iliyoanguka bahari ya Java 2014 na kuua watu 162.

  JB Julius Bett
 529. AJALI SINGIDA YAUA: Abiria 12 wafa, 18 wajeruhiwa baada ya basi la Takibrii likielekea Geita kugonga lori huko Kisonzo, Iramba usiku kuamkia leo, Polisi yasema.


  JB Julius Bett
 530. MGOMO DAR: Wafanyakazi kiwanda Urafiki, Kinondoni jijini Dar es Salaam wagoma na kufungia uongozi ndani leo wakitaka orodha ya wanaostahili malipo itolewe kama walivyokubaliana. Polisi wafika kuimarisha usalama

  JB Julius Bett
 531. MGOMO DAR: Polisi yatumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafanyakazi kiwanda cha nguo Urafiki ambao wameufungia uongozi ndani wakitaka orodha ya malipo itolewe.

  JB Julius Bett
 532. MGOMO DAR: DC Kinondoni Paul Makonda leo aamuru kufungwa kwa muda kiwanda cha Urafiki baada ya wafanyakazi kutoridhishwa na orodha ya watakaolipwa stahiki zao.

  JB Julius Bett
 533. KESI YA UPORAJI: Korti ya Misungwi yamuhukumu Mkazi wa Kahama, Ally Mohamed kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kuiba Sh32m katika kituo cha mafuta huko Misungwi mwaka jana.

  JB Julius Bett
 534. UNYAMA Z'BAR: Watu wasiofahamika wateketeza kwa moto Kituo cha Redio Hits FM usiku wa kuamkia leo, kujeruhi mtangazaji, meneja wa vipindi Juma Ayoub asema leo.

  JB Julius Bett
 535. TUHUMA MADIWANI MBEYA: Chadema wilayani Mbarali chaitaka Kamati Kuu ifute uanachama wa madiwani wawili kwa usaliti wakati wa uchaguzi mkuu, mwenyekiti P. Mwashiti asema.

  JB Julius Bett
 536. HUKUMU YA PISTORIUS: Mahakama ya Rufaa Afrika Kusini leo imemtia hatiani Mwanariadha Oscar Pistorius kwa mauaji, yatengua uamuzi wa awali kuua bila kukusudia.

  JB Julius Bett
 537. ZIARA BANDARINI: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa afanya ziara ya ghafla Shirika la Reli (TRL) na Bandari leo mchana kuangalia utekelezaji wa maagizo yake.

  JB Julius Bett
 538. MATOKEO CECAFA: Rwanda yaingia fainali ya michuano ya Cecafa leo baada ya kuifunga Sudan kwa penalti 4-2 huko Ethiopia. Wenyeji Ethiopia inaendelea muda huu.

  JB Julius Bett
 539. TZ YAPANDA FIFA: Tanzania imepanda kwa nafasi 3 na kuwa ya 132 kwa viwango vya Fifa vilivyotoka leo. Uganda kinara Afrika Mashariki (63), Kenya 98, Rwanda 101, Burundi 112.

  JB Julius Bett
 540. ADA 2016: Shule binafsi zimekatazwa kuongeza ada mwaka wa masomo 2016 hadi "Ada Elekezi" itakapotolewa, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo Profesa Sifuni Mchome asema leo Dar

  JB Julius Bett
 541. SHAMBULIO CAIRO: Takribani watu 12 wauawa, kadhaa wajeruhiwa leo katika shambulio la bomu lililotokea mgahawani kwenye mji mkuu wa Misri, Cairo, maofisa wasema.

  JB Julius Bett
 542. UTEUZI: Rais amteua Valentino Mlowola kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kuziba nafasi iliyoachwa Lilian Mashaka aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

  JB Julius Bett
 543. KORTINI DAR: Watuhumiwa 8 wa upotevu wa makontena 329 wafikishwa Mahakama ya Kisutu leo wakikabiliwa na makosa ya uhujumu uchumi, kusababisha hasara ya Sh12.7bn.

  JB Julius Bett
 544. KORTINI DAR: Watu 20 wapanda kizimbani leo katika mahakama ya Kisutu Dar wakituhumiwa kwa mauaji ya watu 2 yaliyotokea Buguruni, kesi itatajwa tena Disemba 17.

  JB Julius Bett
 545. KESI YA WACHINA MBEYA: Korti yawakuta na kesi ya kujibu wachina 4 wanaoshtakiwa kusafirisha pembe za faru zenye thamani ya Sh902m. Kuanza kujitetea wiki ijayo.

  JB Julius Bett
 546. UKWEPAJI KODI: TRA yakusanya zaidi ya Sh5bn za kodi ya makontena 329 yaliyotoweka bandarini. Kaimu Kamishna P. Mpango asema leo wafanyakazi 35 TRA wanashikiliwa

  JB Julius Bett
 547. WIZI TANESCO: Wafanyakazi 2 wa Tanesco Kagera, Wachina 2 wafikishwa kortini Bukoba leo kwa tuhuma za udanganyifu uliowawezesha kujipatia Sh1bn kutoka Tanesco.

  JB Julius Bett
 548. ANCELOTTI AITAKA UNITED: Kocha Carlo Ancelotti asema leo kuwa angependa kuifundisha Manchester United kama fursa ya kufanya hivyo itakuwepo.

  JB Julius Bett
 549. UFAFANUZI SIKU YA UHURU: Serikali imesema kesho sio siku ya mapumziko. Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue amesema wafanyakazi waende kazini au washiriki kwenye usafi.

  JB Julius Bett
 550. KESI YA UPORAJI: Mahakama ya Wilaya ya Tarime leo yamuhukumu Mkazi wa Nyabichune, Nchagwa Marwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kuiba Sh350,000 kwa kutumia silaha

  JB Julius Bett
 551. Rais John Magufuli amefanya usafi leo asubuhi eneo la feri kwa muda wa dakika 45 na kisha kuzungumza na wavuvi aliosaidiana nao kufanya usafi huku akiwaahidi kuwasaidia. Dk Magufuli alitoa ahadi hiyo baada ya kuwataka wavuvi hao kumueleza matatizo yanayowakabiri.

  JB Julius Bett
 552. SIKU YA UHURU: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa asubuhi hii awaongoza wafanyabiashara Kariakoo, Dar kufanaya usafi wa mazingira kutekeleza agizo la Rais Magufuli.

  JB Julius Bett
 553. SIKU YA UHURU: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa asubuhi hii awaongoza wafanyabiashara Kariakoo, Dar kufanaya usafi wa mazingira kutekeleza agizo la Rais Magufuli.

  JB Julius Bett
 554. PICHA: Mh Rais Magufuli na mkewe Janeth Magufuli wakiwa wanashiriki kwenye usafi maeneo ya feri jijini Dar es Salaam kwa muda wa dakika 45

  JB Julius Bett
 555. Rais mstaafu Jakaya Kikwete na mkewe Salma wakiwaongoza wananchi kutekeleza agizo la Rais John Magufuli la kufanya usafi kama sehemu ya kuadhimisha miaka 54 ya uhuru.

  JB Julius Bett
 556. SIKU YA UHURU: Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe akifanya Ufyekaji Zahanati ya Rusimbi, kata ya Rusimbi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji.

  JB Julius Bett
 557. SIKU YA UHURU: Rais mstaafu, Jakaya Kikwete leo amewaongoza wananchi wa Chalinze kufanya usafi wa mazingira katika Soko la Chalinze kuadhuimisha siku ya Uhuru.

  JB Julius Bett
 558. SIKU YA UHURU: Wakazi wa Mwanjelwa, Mbeya leo wazuia magari katika barabara ya Mbeya-Tunduma, washusha baadhi ya abiria kufanya usafi, polisi wafika eneo la tukio.

  JB Julius Bett
 559. Rais wa awamu ya tano, John Magufuli akifanya usafi katika eneo la Feri, Kivukoni, jijini Dar es Salaam leo, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho miaka 54 ya uhuru.

  JB Julius Bett
 560. SIKU YA UHURU: Wafanyakazi wa Tanesco kituo cha Tabata, Dar wakisafisha mazingira ofisini kwao leo kutekeleza agizo la Rais Magufuli. Picha na Beatrice Moses

  JB Julius Bett
 561. SIKU YA UHURU: Wafanyakazi wa Tanesco kituo cha Tabata, Dar es Salaam wakisafisha mazingira ofisini kwao leo kutekeleza agizo la Rais Magufuli. Picha na Beatrice Moses

  JB Julius Bett
 562. SIKU YA UHURU: wafanyabiashara mjini Handeni mkoani Tanga wamefunga maduka kupisha zoezi la kufanya usafi kuadhimisha siku ya Uhuru. (Picha na Rajabu Athuman)

  JB Julius Bett
 563. Wafanyabiashara Handeni, Tanga wamefunga maduka kupisha zoezi la kufanya usafi kuadhimisha siku ya Uhuru

  JB Julius Bett
 564. SIKU YA UHURU: Wafanyakazi wa mfuko wa GEPF wakifanya usafi katika Makaburi ya Mbaye wilayani Mtwara. Picha na Haika Kimaro

  JB Julius Bett
 565. SIKU YA UHURU: Wafanyakazi wa mfuko wa GEPF wakifanya usafi katika Makaburi ya Mbaye wilayani Mtwara. Picha na Haika Kimaro

  JB Julius Bett
 566. Baadhi ya wananchi walojitokeza leo kufanya usafi wa mazingira kwenye maeneo yao katika Bandari ya Zanzibar.

  JB Julius Bett
 567. SIKU YA UHURU: Wananchi kwa kushirikiana na Jeshi la wananchi JWTZ wakifanya usafi leo katika eneo la mtaa wa Roman, Mjini Tarime. Picha na Waitara Meng'anyi.

  JB Julius Bett
 568. Wananchi maeneo ya Jangombe, Zanzibar wakifanya usafi wa mazingira leo kuadhimisha siku ya Uhuru.

  JB Julius Bett
 569. Wapiga debe kwenye stendi ya mabasi Tarime wakimtaka mmoja wa wasafiri aliyeshuka kwenye basi ashiriki kufanya usafi

  JB Julius Bett
 570. Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisafisha mfereji wa maji machafu kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar leo

  JB Julius Bett
 571. Wananchi wa eneo la Kisimani mjini Tunduma wakiendelea kufanya usafi wa mazingira. Picha na Enea Mwanja

  JB Julius Bett
 572. PICHA: Wananchi wa eneo la Kisimani mjini Tunduma wakiendelea kufanya usafi wa mazingira.

  JB Julius Bett
 573. MAGENDO: Magogo na nguzo za umeme zaidi ya 1,300 zakamatwa Tunduma leo zikivushwa kuelekea Zambia, RC Mbeya A. Kandoro, RPC A. Msangi wafuatilia. Watu 7 mbaroni, mmoja atoweka.

  JB Julius Bett
 574. Rais Mstaafu Jakaya kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakishiriki kufanya usafi soko kuu la Chalinze leo

  JB Julius Bett
 575. Rais Mstaafu Jakaya kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakishiriki kufanya usafi soko kuu la Chalinze leo

  JB Julius Bett
 576. RADI YAUA KAGERA: Ng’ombe 19, kondoo 26 wauawa leo baada ya kupigwa na radi Kasange, Ngara kufuatia mvua kubwa kunyesha, afisa mifugo Richard Ngowi athibitisha.

  JB Julius Bett
 577. MAADILI YA TAIFA: Katibu Mkuu Kiongozi Sefue leo amewataka watanzania kuungana kutokomeza rushwa kama walivyoadhimisha siku ya Uhuru jana kwa usafi wa mazingira.

  JB Julius Bett
 578. Rais John Magufuli aitisha mkutano na waandishi wa habari Ikulu Jijini Dar es Salaam

  JB Julius Bett
 579. Rais John Magufuli atangaza Baraza la Mawaziri

  JB Julius Bett
 580. Nape Nnauye awa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na michezo

  JB Julius Bett
 581. #BarazaLaMawaziri Wizara ya Ardhi - William Lukuvi

  JB Julius Bett
 582. #BarazaLaMwaziri Wizara ya Mambo ya Nje na EAC/ Kimataifa - Augustino Mahiga, Naibu Waziri - Dk. Suzan Kolimba

  JB Julius Bett
 583. Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Waziri ni January Makamba #BarazaLaMawaziri

  JB Julius Bett
 584. Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Waziri ni Mwigulu Nchemba Naibu wake ni William Tate Ole Nashon #BarazaLaMawaziri

  JB Julius Bett
 585. Wizara ya maji na Umwagiliaji: Prof Makame Mbarawa

  JB Julius Bett
 586. Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Waziri wake ni Jenista Mhagama #BarazaLaMawaziri

  JB Julius Bett
 587. Wizara ya Nishati na Madini Waziri ni Sospeter Muhongo na Naibu Waziri wake ni Medard Kalemani #BarazaLaMawaziri

  JB Julius Bett
 588. PICHA: Rais John Magufuli alipokuwa akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo

  JB Julius Bett
 589. Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji-, Waziri ni Charles Mwijage.

  JB Julius Bett
 590. Rais wa awamu ya tano, John Magufuli amteuwa Dr Harrison Mwakyembe kuwa waziri Wizara ya Katiba na Sheria #BarazaLaMawaziri

  JB Julius Bett
 591. PICHA: Rais John Magufuli akirejea ofisini kwake baada ya kutangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo

  JB Julius Bett
 592. UMEYA: David Mwashilindi (Chadema) leo atangazwa meya wa jiji la Mbeya baada ya kupata kura 34 dhidi ya 14 za K. Mwasote (CCM). D. Ngogo (Chadema) awa naibu.

  JB Julius Bett
 593. MAPIGANO BURUNDI: Watu kadhaa wafa, wengine waumia baada ya watu wenye silaha kuvamia kambi za jeshi mjini Bujumbura usiku wa kuamkia leo, ofisa wa jeshi asema.

  JB Julius Bett
 594. UFISADI FIFA: Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) yatupilia mbali leo ombi la Rais wa UEFA Platini kutaka kifungo cha siku 90 kujihusisha na soka kiondolewe.

  JB Julius Bett
 595. UMEYA MUSOMA: Diwani wa Makoko (CCM) William Gumbo amshinda Lucas Katikiro (Chadema) kwa kura 20 kwa 5. Diwani wa Nyakato Shabani Kajala (CCM) awa Naibu Meya.

  JB Julius Bett
 596. UMEYA BUKOBA: Diwani wa Kahororo Chief Karumuna (Chadema) ashinda umeya Bukoba kwa kupata kura 13 dhidi ya mgombea wa CCM Almasoud Karumuna aliyepata kura 10.

  JB Julius Bett
 597. MAWAZIRI WAAPISHWA: Rais Dk John Magufuli awaapisha rasmi leo Mawaziri na Manaibu Waziri Ikulu jijini Dar baada ya kuwateua juzi.

  JB Julius Bett
 598. Waziri wa Habari, utamaduni, wasanii na michezo- Nape Nnauye alipokuwa akila kiapo mbele ya Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam leo

  JB Julius Bett
 599. Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu) Jenista Mhagama akila kiapo mbele ya Rais Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam leo

  JB Julius Bett
 600. Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi- akila kiapo mbele ya Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar leo

  JB Julius Bett
 601. Waziri wa Katiba na Sheria, Harrison Mwakyembe akila kiapo mbele ya Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar leo

  JB Julius Bett
 602. Naibu Waziri, Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na Watoto Hamis Kigwangalla afanya ziara ya kushtukiza Hospitali ya Amana

  JB Julius Bett
 603. Waziri, Wizara ya Ofisi ya makamu wa Rais, muungano na mazingira- January Makamba akila kiapo mbele ya Rais John Magufuli, Ikulu jijini Dar leo

  JB Julius Bett
 604. UCHAGUZI MDOGO: Wananchi wa Jimbo la Handeni na Arusha wameanza kupiga kura asubuhi hii kuwachagua wabunge baada ya uchuguzi huo kuahirishwa mwezi Oktoba.

  JB Julius Bett
 605. UCHAGUZI HANDENI: Mgombea ubunge wa Chama cha ADC, Doyo Hassani Doyo akipiga kura leo asubuhi katika kituo cha Mdoe, Handeni.

  JB Julius Bett
 606. UCHAGUZI ARUSHA: Polisi Arusha leo wanamshikilia Diwani wa Kata ya Ngarenaro (Chadema), Issaya Doita kwa tuhuma za kusababisha vurugu katika kituo cha kupigia kura.

  JB Julius Bett
 607. Polisi wakiimarisha ulinzi katika uchaguzi wa ubunge Jimbo la Arusha Mjini leo

  JB Julius Bett
 608. UCHAGUZI MDOGO: Upigaji kura katika uchaguzi wa wabunge Jimbo la Arusha na Handeni umekamilika, zoezi la kuhesabu kura linaendelea.

  JB Julius Bett
 609. MAPIGANO MVOMERO: Mapigano yazuka Turiani Morogoro kati ya wafugaji na wakulima, Waziri Mwigulu Nchemba aenda kwenye tukio, DC Betty Mkwasa aeleza, zaidi baadaye.

  JB Julius Bett
 610. MAPIGANO MVOMERO: Mtu mmoja auawa, wengine watatu wajeruhiwa kwenye mapigano kati ya wakulima na wafugaji kijiji cha Dihimba Turiani, DC Betty Mkwasa aeleza.

  JB Julius Bett
 611. MAPIGANO MVOMERO: Polisi yawakamata wakulima 3 na wafugaji 4 leo kwa tuhuma za kuhusika kwenye mapigano katika kijiji cha Dihimba Turiani, DC Betty Mkwasa asema

  JB Julius Bett
 612. MAPIGANO MVOMERO: Ng’ombe 79 wameuawa, 72 wajeruhiwa kwenye mapigano katika kijiji cha Dihimba Turiani, uchunguzi kuendelea. DC Betty Mkwasa asema amani yarejea

  JB Julius Bett
 613. AJALI TABORA: Watu 8 wafa, 14 wajeruhiwa leo baada ya basi la Allys toka Kaliua-Mwanza kupinduka huko Urambo, Kamanda wa Polisi Tabora, Hamis Issa athibitisha.

  JB Julius Bett
 614. PICHA: Waziri wa Mambo ya Nje Dk Augustine Mahiga katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan leo

  JB Julius Bett
 615. PICHA: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Jenista Mhagama kwenye kikao leo

  JB Julius Bett
 616. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Hussein Ali Mwinyi aanza kazi rasmi

  JB Julius Bett
 617. ZIARA: Waziri wa Afya Ummy Mwalimu azuru Hospitali ya Muhimbili leo na kukuta wagonjwa wakisubiri huduma huku CT Scan, MRI zikiwa mbovu. Aagiza zishughulikiwe.

  JB Julius Bett
 618. MAAFA: Watu 3 wafa, familia 70 hazina pa kuishi baada mafuriko kusomba nyumba zao, Mkurugenzi Arusha Vijijini, F. Lumato athibitisha leo. Mifugo 150 yapotea.

  JB Julius Bett
 619. KLABU BINGWA YA DUNIA: TP Mazembe ya DRC ikiwa na Watanzania; Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu yafungwa 2-1 na CF America katika mechi iliyomalizika mchana huu.

  JB Julius Bett
 620. BOTI YAWAKA: Abiria 300 wanusurika kifo bahari ya Hindi baada ya boti ya Royal toka Pemba kwenda Unguja kuwaka moto leo, Polisi yasema. Abiria warudishwa Pemba.

  JB Julius Bett
 621. HATIMA: Kocha Bayern Munich Pep Guardiola leo asema atatoa ufafanuzi wa hatima yake "wiki ijayo" huku tetesi za kuhamia klabu za England zikizidi kupamba moto.

  JB Julius Bett
 622. MALIPO KWA WAKULIMA: Waziri wa Kilimo, Mwigulu Nchemba leo ametoa saa 48 kwa kampuni ya Sparkway Ltd kulipa Sh3.4bn kwa wakulima wa korosho mkoani Pwani.

  JB Julius Bett
 623. KESI YA UCHAGUZI: Aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Ubungo (CCM), Dk. Didas Masaburi leo amefuta kesi ya uchaguzi ya kupinga ushindi wa Mbunge, Saed Kubenea.

  JB Julius Bett
 624. HOSEAH NJE: Rais John Magufuli leo ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dk. Edward Hoseah kutokana na kutoridhishwa na utendaji wa taasisi hiyo.

  JB Julius Bett
 625. Rais John Magufuli amemteua Valentino Mlowoka kuchukua nafasi ya Dr Edward Hosea (TAKUKURU)

  JB Julius Bett
 626. AJALI PWANI: Takribani watu wawili wafa, watatu wengine wamejeruhiwa mapema leo huko Chalinze katika ajali iliyohusisha lori na gari dogo, polisi wathibitisha.

  JB Julius Bett
 627. BOMOABOMOA DAR: Manispaa ya Kinondoni yaendesha operesheni asubuhi hii kubomoa majengo yaliyojengwa kwenye bonde la Mto Msimbazi eneo la Kinondoni Mkwajuni.

  JB Julius Bett
 628. UCHAGUZI MASASI: Wananchi wa Jimbo la Masasi mkoani Mtwara wameanza kupiga kura asubuhi hii kumchagua mbunge wao baada ya uchuguzi huo kuahirishwa mwezi Oktoba.

  JB Julius Bett
 629. UCHAGUZI LUDEWA: Wananchi Jimbo la Ludewa mkoani Njombe waanza zoezi la kupiga kura asubuhi hii kumchagua mbunge baada ya uchuguzi huo kuahirishwa mwezi Oktoba.

  JB Julius Bett
 630. UCHAGUZI MASASI: Wananchi wakiwa kwenye foleni kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa ubunge asubuhi hii katika kituo cha Msufini 1 shule ya msingi Kambarage, Masasi. Picha na Haika Kimaro

  JB Julius Bett
 631. WAHAMIAJI HARAMU: Polisi yawakamata zaidi ya watu 42 wanaosadikiwa kuwa wahamiaji haramu toka Somalia leo asubuhi wakiwa kwenye chumba 1 huko Kijitonyama, Dar.

  JB Julius Bett
 632. UCHAGUZI MASASI: Wasimamizi wa kituo cha hotel ya halmashauri namba 2 Kata ya Nyasa wakisubiri wapiga kura leo katika uchaguzi mdogo Jimbo la Masasi mkoani Mtwara.

  JB Julius Bett
 633. AJALI MAREKANI: Mtu mmoja afa wengine 36 wajeruhiwa baada ya gari moja kuacha njia na kuparamia waenda kwa miguu mjini Las Vegas, Marekani leo, mamlaka yaeleza.

  JB Julius Bett
 634. MAHABUSU WAGOMA: Mahabusu 6 wakaa barabarani mjini Geita wakipinga kesi zao kuchelewa, kubambikiwa kesi; Afisa Upelelezi Wilaya aahidi kushughulikia madai yao.

  JB Julius Bett
 635. MAHABUSU WAGOMA TARIME: Mahabusu kutoka Gereza la Tarime wagoma kushuka kwenye gari la polisi kwenye Mahakama ya Wilaya Tarime wakipinga kesi yao kuendelea wakati wenzao waliokuwa kundi moja wakiachiwa huru.

  JB Julius Bett
 636. MAFURIKO MWANZA: Mvua kubwa iliyopiga kwa takriban dakika 45 yasababisha Mto Mirongo kufurika na kulifunika daraja la Mabatini; abiria, waenda kwa miguu wakwama

  JB Julius Bett
 637. OPERESHENI 2016: Waziri wa Mambo ya Ndani Charles Kitwanga leo jijini Dar atangaza msako wa wahamiaji haramu kwenye makazi na maofisini. Asema utaanza Januari 1.

  JB Julius Bett
 638. Jumla ya watoto 79 wamezaliwa katika mkesha wa Sikukuu ya Krismasi katika hospitali za rufaa za mkoa wa Dar es Salaam.

  JB Julius Bett
 639. Kati ya watoto 79 walizaliwa usiku wa mkesha wa Krismasi, wawili ni njiti na kwa mujibu wa wataalam wa afya, watoto hao wanaendelea vema

  JB Julius Bett
 640. UJUMBE WA KRISMASI 2015: Papa Francis leo ataka dunia kuungana dhidi ya "matendo ya kikatili ya kigaidi" yanayoshuhudiwa katika nchi mbalimbali.

  JB Julius Bett
 641. CHEKA vs. MASHARI: Bondia Thomas Mashari kutoka Dar ampiga Francis Cheka kwa pointi mjini Morogoro katika pambano la raundi 10, uzito wa Kg 77.

  JB Julius Bett
 642. CHEKA vs. MASHARI: Majaji wamempa Mashari pointi 94, 96 na 97 wakati mwenyeji Cheka amepata pointi 96, 93 na 93.

  JB Julius Bett
 643. KODI: Serikali imepoteza sh48.77bn baada ya makontena 11,884, magari 2,019 kupitishwa badarini Dar bila kulipiwa, Waziri Mbarawa asema leo. 7 mbaroni, 8 wasakwa

  JB Julius Bett
 644. MKWAMO WA KISIASA Z’BAR: Cuf imesema leo Z’bar kuwa inaamini mazungumzo yanayofanywa na viongozi wastaafu yatazaa matunda. Yataka wananchi kumpa Rais John Magufuli nafasi kushughulikia suala hilo.

  JB Julius Bett
 645. MKWAMO WA KISIASA Z’BAR: Chama cha Wananchi (CUF) leo visiwani Z’bar kimewataka wananchi kupuuza taarifa za CCM zinazoitaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) irudie uchaguzi

  JB Julius Bett
 646. ADHA YA USAFIRI: Zaidi ya abiria 350 wakwama kwa muda Mtwara leo kufuatia mgomo wa madereva wanaopinga kukamatwa kwa wenzao 3 jana wakituhumiwa kwa mwendokasi.

  JB Julius Bett
 647. URASIMU: Waziri G. Simbachawene leo ameagiza Kaimu Afisa biashara Manispaa ya Ilala asimamishwe kazi kwa urasimu wa utoaji leseni unaoikosesha serikali mapato.

  JB Julius Bett
 648. NECTA YAPEWA SIKU 7: Waziri Ndalichako ataka apewe maelezo ya kisayansi kwa nini mfumo wa kupanga matokeo kwa GPA ni bora kuliko wa Divisheni uliotumika kabla.

  JB Julius Bett
 649. SHAMBULIO LIBYA: Watu 65 wauawa, kadhaa wajeruhiwa leo katika mlipuko wa bomu kwenye kituo cha mafunzo ya polisi mjini Zliten Magharibi mwa Libya, polisi wasema.

  JB Julius Bett
 650. MKAPA, WARIOBA IKULU: Rais Mstaafu B. Mkapa, Jaji Mstaafu J. Warioba wafanya mazungumzo na Rais Magufuli, Ikulu leo. Mkapa asema yupo tayari kumsaidia Magufuli.

  JB Julius Bett
 651. Rais John Magufuli @MagufuliJP akiagana na Waziri Mkuu mstaafu Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar leo.Picha na Ikulu

  JB Julius Bett
 652. MAGUFULI ‘AMFAGILIA’ SAMATTA: Rais J. Magufuli amempongeza Mbwana Samatta kwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora anayecheza ndani ya bara la Afrika, Ikulu yasema leo.

  JB Julius Bett
 653. AJALI YAUA DAR: Mtu 1 afa leo, 15 majeruhi baada ya lori la mchanga likiwa kwenye mwendokasi kugonga magari 4 huko Pugu. Majeruhi wakimbizwa Kisarawe Hospital.

  JB Julius Bett
 654. UBOMOAJI DAR: Mwanasheria NEMC afukuzwa kazi kwa kuondoa kesi kortini kinyemela kunusuru ubomoaji ghorofa la Mch. Lwakatare, Ofisi ya Makamu wa Rais yasema leo.

  JB Julius Bett
 655. KESI YA UMEYA: Korti Kuu Dar leo yaamuru uchaguzi wa meya Kinondoni kufanyika kesho na kutupilia mbali ombi la kuusimamisha hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa.

  JB Julius Bett
 656. KOMBE LA MAPINDUZI 2016: URA ya Uganda yaingia nusu fainali Kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Jamhuri 1-0 uwanja wa Amani leo, Zanzibar. Simba vs JKU baadaye

  JB Julius Bett
 657. JK AMPONGEZA SAMATTA: Rais Mstaafu Jakaya Kikwete leo akutana na Mbwana Samatta Dar na kumpongeza kwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora anayecheza ndani ya Afrika.

  JB Julius Bett
 658. MAPINDUZI Z’BAR: Marais John Magufuli, Mohamed Shein, viongozi mbalimbali wa serikali na wastaafu wako uwanja wa Amani katika sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi ya Z’bar. Makamu wa Rais (1) Maalim Seif hajahudhuria.

  JB Julius Bett
 659. Makundi ya wakulima wadogo wa mahindi, wafugaji wa kuku na wauzaji wa dawa za mifugo, wamepatiwa fursa ya kujiongezea kipato baada ya taasisi ya Brac-Maendeleo Tanzania kuwawezesha kupata fursa mbalimbali ikiwamo ya rasilimali fedha, utaalamu na masoko.

  JB Julius Bett
 660. Ukosefu wa miundombinu katika baadhi ya mikoa yenye vivutio vya utalii umetajwa kuwa kikwazo kwa watalii kufika kwenye maeneo hayo na kusababisha kukosekana kwa mapato.

  JB Julius Bett
 661. BANDARI TANGA YAUNDIWA KAMATI KUHIMIZA UTENDAJI: Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza ameahidi kuunda kamati ya watu 10 itakayoshughulikia masuala ya Bandari ya Tanga ili yaende kwa kasi inayotakiwa na Rais John Magufuli.

  JB Julius Bett
 662. VITAMBULISHO VYA TAIFA: BVR 5,000 za NEC kutumiwa na NIDA ili lengo la kutoa vitambulisho 15m hadi Juni lifikiwe, N/Waziri Mambo ya Ndani H. Masauni asema leo.

  JB Julius Bett
 663. WAKURUGENZI WASIMAMISHWA: Waziri George Simbachawene leo awasimamisha kazi wakurugenzi watendaji wa Manispaa ya Kigoma na Mpanda kwa kukiuka sheria ya manunuzi.

  JB Julius Bett
 664. ‪#‎SeminaElekezi‬ ‪#‎KutokaDodoma‬ Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu), Dk Possy Abdallah walipohudhuria semina ya Wabunge wa CCM katika ukumbi wa Whitehouse makao makuu ya chama hicho, mkoani Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 665. ‪#‎SeminaElekezi‬ ‪#‎Dodoma‬

  Wabunge wa Chama cha Mapinduzi wakiwa katika ukumbi wa Whitehouse Makao Makuu ya chama hicho mkoani Dodoma wakihudhuria semina elekezi ya siku mbili iliyoanza jana. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 666. ‪#‎KutokaDodoma‬ ‪#‎SeminaElekezi‬

  Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge akijisajili kwenye fomu za mahudhurio ya semina elekezi kwa wabunge wa CCM, katika ukumbi wa Whitehouse, makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 667. #‎KutokaDodoma‬ ‪#‎SeminaElekezi‬

  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (kulia) akiwaeleza jambo wabunge wa CCM walihudhuria semina elekezi kwa wabunge wa chama hicho, mjini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 668. RADI YAUA PWANI: Watu 3 wa familia 1 Mchukwi wafa baada ya kupigwa na radi wakiwa jikoni wakijikinga na mvua, DC Rufiji Nurdin Babu aenda kwenye tukio muda huu.

  JB Julius Bett
 669. VIDIC AONDOKA MILAN: Mlinzi Nemanja Vidic leo amevunja mkataba na Inter Milan kwa makubaliano ya pande zote 2 baada ya kushindwa kucheza tangu msimu huu kuanza.

  JB Julius Bett
 670. TAHARUKI DAR: Taharuki yatanda leo makutano ya mtaa wa Mchikichini/Livingstone huko Kariakoo baada ya moja ya ghorofa kuonesha dalili za kutitia.

  JB Julius Bett
 671. Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chadema, Leticia Nyerere aliyefariki dunia wiki iliyopita nchini Marekani umewasili Dar leo.

  JB Julius Bett
 672. TANZIA: Makamu M'kiti UWT-Z'bar Asha B. Makame afariki leo alfajiri Dubai akitoka India kutibiwa, Naibu Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo, Salama A. Talib athibitisha

  JB Julius Bett
 673. SERA: Shirika la Hakielimu lasema leo Dar, sera ya elimu bure inawachanganya wazazi na itachangia ELIMU kushuka kwani haimuliki uboreshaji miundombinu shuleni.

  JB Julius Bett
 674. VIPODOZI VYATEKETEZWA: Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Kanda ya Ziwa leo imeteketeza shehena ya vipodozi vyenye viambata vya sumu vya thamani ya Sh156m.

  JB Julius Bett
 675. ADHA YA USAFIRI: Wananchi wanaosafiri kati ya Turiani na Morogoro Mjini wakwama tangu saa saba mchana jana baada ya Mto Mburuni kujaa maji kutokana na mafuriko.

  JB Julius Bett
 676. KESI YA UCHAGUZI: Mahakama Kuu mjini Mbeya leo imeliondoa ombi la aliyekuwa mgombea wa Chadema kutaka kufungua kesi kupinga ushindi wa CCM jimbo la Mbarali.

  JB Julius Bett
 677. Rais Dk John Magufuli amemteua Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Kuwa Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam

  JB Julius Bett
 678. MAZIKO: RC Mara Assery Msangi leo aongoza viongozi, wananchi kumzika aliyekuwa mbunge wa Chadema Leticia Nyerere makaburi ya familia ya Mwl J. Nyerere Butiama.

  JB Julius Bett
 679. CHAN 2016: Congo DR yapata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Angola leo katika mechi ya Kundi B Michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani ya Afrika huko Rwanda.

  JB Julius Bett
 680. MATOKEO VPL: Magoli ya Jerry Tegete na Nizar Halfan yaipa Mwadui ushindi wa 2-1 dhidi ya Kagera Sugar leo. Mtibwa na African Sports ya Tanga zatoka sare ya 0-0.

  JB Julius Bett
 681. USHURU WA HUDUMA: Halmashauri ya Wilaya Tarime yagoma kupokea ushuru wa Sh 1.60bn kutoka mgodi wa North Mara (Acacia) hadi wajiridhishe kiwango sahihi wanachopaswa kulipwa na mgodi huo, M/Kiti wa Halmashauri Moses Misiwa aeleza leo.

  JB Julius Bett
 682. KESI YA UBUNGE: Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo imeiondoa kesi ya kupinga ubunge wa Ester Bulaya kwa kuwa waleta maombi hawana haki kisheria kufungua kesi hiyo

  JB Julius Bett
 683. MGOGORO WA BURUNDI: Burundi yatuma ujumbe jijini Arusha leo unaoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama tawala CNDD FDD Joseph Ntakirutimana ili kujibu hoja za mauaji na utesaji wananchi unaoendelea nchini humo.

  JB Julius Bett
 684. RAS ATIMULIWA: Rais Magufuli atengua uteuzi wa Eng. Madeni Kipande kabla hajathibitishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Katavi kutokana na utendaji kazi usioridhisha

  JB Julius Bett
 685. AMRI: Waziri wa Ardhi, William Lukuvi awaagiza polisi kuwakamata viongozi wa kijiji cha Mlilingwa wilayani Morogoro wanaotuhumiwa kuuza shamba la hekari 3500 kwa mwekezaji.

  JB Julius Bett
 686. BOSI NIDA ASIMAMISHWA: Rais Magufuli amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, maofisa wengine 4 kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha.

  JB Julius Bett
 687. Askari kanzu na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa kwenye Ukumbi wa Bunge ili kuwatoa kwa nguvu wabunge wa upinzani baada ya kukaidi amri ya Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge ya kuwataka waondoke bungeni mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 688. HABARI ZA SIKU TELE! Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (kulia) akipeana mkono na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kabla ya kuanza kwa mkutano na waandishi wa habari wakipinga kitendo cha kutolewa kwa nguvu katika Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 689. AJALI YA KIVUKO: Waziri Jenista Mhagama asema mtu 1 amepotea baada ya kivuko cha Kilombero kilichokuwa na abiria 31 kupinduka kwenye mto Kilombero jana usiku.

  JB Julius Bett
 690. AJALI YA KIVUKO: Watu 30 wameopolewa baada ya kivuko cha Kilombero kupinduka kwenye Mto Kilombero jana usiku, DC wa Kilombero Lephy Gembe athibitisha mapema leo

  JB Julius Bett
 691. BUNGENI DODOMA: Wabunge wa upinzani wametoka bungeni leo baada ya Naibu Spika, Tulia Ackson kuzuia miongozo na kuruhusu Bunge kuendelea kujadili hotuba ya Rais.

  JB Julius Bett
 692. KIBALI NCHINI: Afisa Utumishi Hosp ya KCMC, Alfa Chabakanga ameburuzwa kortini kwa kosa la kuajiri raia 3 wa Burundi ambao hawana kibali cha kufanya kazi nchini

  JB Julius Bett
 693. KESI YA MASHA: Mahakama ya Kisutu leo imeifuta kesi ya kutumia lugha ya matusi kwa polisi inayomkabili aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha.

  JB Julius Bett
 694. Baraza Kuu la uongozi la taifa CUF, limetangaza kuwa hawatashiriki kwenye uchaguzi uliotangazwa kufanyika Machi 20 mwaka huu, kwa kuwa siyo halali wameomba Wazanzibari wote wanaoheshimu katiba yao na sheria za nchi hiyo kutoshiriki uchaguzi huo, kwa kuwa CCM imeshapanga matokeo.

  JB Julius Bett
 695. MADAWA YA KULEVYA: Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Simoni Sirro akiri vita dhidi ya madawa ya kulevya ni ngumu, ataka wananchi kutoa taarifa, pia aonya bodaboda kupaki karibu na mabenki.

  JB Julius Bett
 696. AJALI YA MOTO MBEYA: Moto ambao chanzo chake hakijajulikana unaendelea kuteketeza ghala lenye bidhaa mbalimbali eneo la Maghorofani mjini Mbeya muda huu, zimamoto na polisi wawasili eneo la tukio.

  JB Julius Bett
 697. BUNGE: Hatimaye Waziri wa Fedha aendelea kuwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa 2016-2017 baada ya serikali kujikwamua kutoka vikwazo vya upinzani.

  JB Julius Bett
 698. MGOMO MBEYA: Abiria wahaha vituoni leo huku mgomo wa madereva ukiingia siku ya 2 kupinga agizo la RC Mbeya Abas Kandoro kutumia barabara ipitayo Rift Valley.

  JB Julius Bett
 699. HOFU YA ZIKA: Homa ya Zika inaathiri mimba changa na si tishio kama Ebola, N/Waziri Afya Dk Hamis Kigwangala asema bungeni. Asisitiza serikali imejipanga kuukabili.

  JB Julius Bett
 700. Ukuta wa Chuo cha Biashara, CBE-Mkoani Dodoma umesombwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

  JB Julius Bett
 701. Kakakuona aonekana leo hifadhi ya Kitulo Wilayani Makete Mkoa wa Njombe. Picha na Juma Mtanda

  JB Julius Bett
 702. MJADALA BUNGE: Mbunge wa Mwibara Kangi Lugola (CCM) leo asema atapinga Bajeti ya 2016/17 ikiwa haitabainisha Reli ya Kati itakavyoboreshwa kiwango cha "Standard Gauge".

  JB Julius Bett
 703. Gari ndogo mali ya benki ya CRDB tawi la Ifakara likiwa linaopolewa kwenye maji baada ya kutumbukia kufuatia ajali ya kupinduka kwa kivuko cha MV II Kilombero kilichokumbwa na dhuruba ya upepo mkali ikiambatana na mvua januari 27 mwaka huu na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine zaidi ya 35 kunusurika kifo mkoani Morogoro. Picha na Juma Mtanda

  JB Julius Bett
 704. Gari mali ya benki ya CRDB Ifakara likiwa linaopolewa kwenye maji baada ya kutumbukia kufuatia ajali ya kupinduka kwa kivuko cha MV II Kilombero kilichokumbwa na dhuruba ya upepo mkali ikiambatana na mvua januari 27 mwaka huu na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine zaidi ya 35 kunusurika kifo mkoani Morogoro. Picha na Juma Mtanda

  JB Julius Bett
 705. Gari ndogo mali ya benki ya CRDB tawi la Ifakara likiwa linaopolewa kwenye maji baada ya kutumbukia kufuatia ajali ya kupinduka kwa kivuko cha MV II Kilombero kilichokumbwa na dhuruba ya upepo mkali ikiambatana na mvua januari 27 mwaka huu na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine zaidi ya 35 kunusurika kifo mkoani Morogoro. Picha na Juma Mtanda

  JB Julius Bett
 706. Mwalimu anaefundisha darasa la awali katika shule ya Msingi Mwibagi kijiji cha Mwibaji Wilaya ya Butiama Mkoani Mara akisahihisha madaftari ya wanafunzi chini ya mti kufuatia chumba cha darasa kujaa hadi kukosa sehemu ya kuweka kiti.jumla ya wanafunzi ni zaidi ya 240 katika chumba kimoja. Picha na Flolence Wisso

  JB Julius Bett
 707. Baba mzazi wa Dastan Rwegasira, Francis Rwegasira anayedhaniwa kufa maji katika ajali ya kunduka kwa kivuko cha MV II Kilombero januari 27 mwaka huu wakifanya mila za kihaya kama ishara ya kumzika mtoto wao mara baada ya kumalizika kwa ibada ya mazishi iliyofanyika kando ya mto kilombero mita chache kutoka kilipopinduka kivuko hicho mkoani Morogoro. Picha Juma Mtanda

  JB Julius Bett
 708. Mama mzazi wa Dastan Rwegasira, anayedhaniwa kufa maji katika ajali ya kupinduka kwa kivuko cha MV II Kilombero januari 27 mwaka huu, Flora Hamadi akitulizwa na ndugu na jamaa mara baada ya kumalizika kwa ibada ya mazishi. Picha Juma Mtanda

  JB Julius Bett
 709. BUNGE: Waziri wa Mambo ya Nje, Augustine Mahiga asema uchunguzi umeanza kufuatia taarifa zilizoenea za kudhalilishwa wanafunzi wanaosoma nchini india hivi karibuni.

  JB Julius Bett
 710. BOMOA BOMOA BAA ZA DAGAADAGAA-SINZA

  Mahakama ya Kisutu ilitoa oda ya kubomolewa eneo hilo ambalo limekuwa maarufu kwa uuzaji wa Kitimoto, baada ya kesi ya msingi iliyonguruma toka mwaka 1993 kumalizika na hukumu ya kesi hiyo ilitoka Januari 25 mwaka huu ambapo Mahakama iliamuru eneo hilo kubomolewa. Kihalali linadaiwa kumilikiwa na Erick Cool Maker. Picha na Vicky Kimaro, Mwananchi

  JB Julius Bett
 711. BOMOA BOMOA BAA ZA DAGAADAGAA-SINZA

  Mahakama ya Kisutu ilitoa oda ya kubomolewa eneo hilo ambalo limekuwa maarufu kwa uuzaji wa Kitimoto, baada ya kesi ya msingi iliyonguruma toka mwaka 1993 kumalizika na hukumu ya kesi hiyo ilitoka Januari 25 mwaka huu ambapo Mahakama iliamuru eneo hilo kubomolewa. Kihalali linadaiwa kumilikiwa na Erick Cool Maker. Picha na Vicky Kimaro, Mwananchi

  JB Julius Bett
 712. BOMOA BOMOA BAA ZA DAGAADAGAA-SINZA

  Mahakama ya Kisutu ilitoa oda ya kubomolewa eneo hilo ambalo limekuwa maarufu kwa uuzaji wa Kitimoto, baada ya kesi ya msingi iliyonguruma toka mwaka 1993 kumalizika na hukumu ya kesi hiyo ilitoka Januari 25 mwaka huu ambapo Mahakama iliamuru eneo hilo kubomolewa. Kihalali linadaiwa kumilikiwa na Erick Cool Maker. Picha na Vicky Kimaro, Mwananchi

  JB Julius Bett
 713. BOMOA BOMOA BAA ZA DAGAADAGAA-SINZA

  Mahakama ya Kisutu ilitoa oda ya kubomolewa eneo hilo ambalo limekuwa maarufu kwa uuzaji wa Kitimoto, baada ya kesi ya msingi iliyonguruma toka mwaka 1993 kumalizika na hukumu ya kesi hiyo ilitoka Januari 25 mwaka huu ambapo Mahakama iliamuru eneo hilo kubomolewa. Kihalali linadaiwa kumilikiwa na Erick Cool Maker. Picha na Vicky Kimaro, Mwananchi

  JB Julius Bett
 714. BOMOA BOMOA BAA ZA DAGAADAGAA-SINZA

  Mahakama ya Kisutu ilitoa oda ya kubomolewa eneo hilo ambalo limekuwa maarufu kwa uuzaji wa Kitimoto, baada ya kesi ya msingi iliyonguruma toka mwaka 1993 kumalizika na hukumu ya kesi hiyo ilitoka Januari 25 mwaka huu ambapo Mahakama iliamuru eneo hilo kubomolewa. Kihalali linadaiwa kumilikiwa na Erick Cool Maker. Picha na Vicky Kimaro, Mwananchi

  JB Julius Bett
 715. BUNGE: M/kiti wa Bunge Andrew Chenge amsimamisha Mbunge (Chadema), Jesca Kishoa kutohudhuria vikao 2 kwa kushindwa kutoa ushahidi kuwa Dk.Mwakyembe alinunua mabehewa feki.

  JB Julius Bett
 716. Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Handeni na Kilindi Anold Kileo akisoma hotuba ya maadhimisho ya siku ya sheria wilaya ya Handeni inayofanyika viwanja vya Mahakama ya wilaya Handeni. Picha na Rajabu Athumani

  JB Julius Bett
 717. VIDEO: Mwanamuziki @diamondplatnumz awa Balozi wa @VodacomTanzania https://www.facebook.com/MwananchiNews/

  JB Julius Bett
 718. Mafuriko yavikumba vijiji kumi na mbili vilivyopo kandokando ya mto Rufiji.

  Zaidi ya hekari 3500 za mazao ya mahindi na mpunga vyasombwa na Maji na zaidi kaya 1700 zaathiriwa na mafuriko. Picha na Azory Gwanda

  JB Julius Bett
 719. MAWAZIRI VIVULI: Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ametangaza Baraza la Mawaziri Vivuli leo mjini Dodoma.

  JB Julius Bett
 720. Kivuko cha MV II Kilombero kikionekana nusu kufuatia juhudi za kukiibua kuzamisha maboya katika kazi inayoendelea baada ya kupinduka januari 27 mwaka huu na kusababisha zaidi ya watu 35 kunusuriki kifo huku kukiwa na taarifa za watu wawili wakipoteza maisha baada ya kukumbwa na dhuruba la upepo mkali na mvua kubwa mkoani Morogoro. Picha na Juma Mtanda, Mwananchi

  JB Julius Bett
 721. Kivuko cha MV II Kilombero kikionekana nusu kufuatia juhudi za kukiibua kuzamisha maboya katika kazi inayoendelea baada ya kupinduka januari 27 mwaka huu na kusababisha zaidi ya watu 35 kunusuriki kifo huku kukiwa na taarifa za watu wawili wakipoteza maisha baada ya kukumbwa na dhuruba la upepo mkali na mvua kubwa mkoani Morogoro. Picha na Juma Mtanda, Mwananchi

  JB Julius Bett
 722. Kivuko cha MV II Kilombero kikionekana nusu kufuatia juhudi za kukiibua kuzamisha maboya katika kazi inayoendelea baada ya kupinduka januari 27 mwaka huu na kusababisha zaidi ya watu 35 kunusuriki kifo huku kukiwa na taarifa za watu wawili wakipoteza maisha baada ya kukumbwa na dhuruba la upepo mkali na mvua kubwa mkoani Morogoro. Picha na Juma Mtanda, Mwananchi

  JB Julius Bett
 723. Kivuko cha MV II Kilombero kikionekana nusu kufuatia juhudi za kukiibua kuzamisha maboya katika kazi inayoendelea baada ya kupinduka januari 27 mwaka huu na kusababisha zaidi ya watu 35 kunusuriki kifo huku kukiwa na taarifa za watu wawili wakipoteza maisha baada ya kukumbwa na dhuruba la upepo mkali na mvua kubwa mkoani Morogoro. Picha na Juma Mtanda, Mwananchi

  JB Julius Bett
 724. KOMPYUTA ZA TRA: Polisi Dar yakamata magari 2 yanayosadikiwa kutumika kubeba kompyuta zilizoibwa kwenye ofisi ya aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Philip Mpango.

  JB Julius Bett
 725. UDHALILISHAJI INDIA: Maofisa polisi 3 Bangalore wasimamishwa kazi leo kwa kukataa kupokea malalamiko ya msichana wa Kitanzania aliyevuliwa nguo na kupigwa.

  JB Julius Bett
 726. BUNGE: Waziri Mkuu Majaliwa aliahirisha Bunge mjini Dodoma leo akitaka wananchi kutogawanywa kwa misingi ya ukabila, udini na siasa. Bunge kuendelea Aprili 19.

  JB Julius Bett
 727. BUNGENI DODOMA: Waziri Mkuu Majaliwa asema leo kuna waasi wenye silaha kutoka nchi jirani walioingia nchini kupita kambi ya Nyarugusu, ataka watu watoe taarifa

  JB Julius Bett
 728. SINGIDA ROAD ACCIDENT: A car overturns Saturday at Mkiwa in Ikungi District killing three police officers, injuring two others, RPC Thobias Sedoyeka confirms.

  JB Julius Bett
 729. TETEMEKO TAIWAN: Tetemeko kubwa la ardhi lapiga kusini mwa Taiwan leo alfajiri; watu 5 wathibitika kufa mpaka sasa, wengine mamia wajeruhiwa, mamlaka zaeleza.

  JB Julius Bett
 730. MAADHIMISHO CCM: Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) leo wameadhimisha mjini Singida miaka 39 tangu Kuzaliwa kwa Chama hicho mwezi Februari 5, 1977.

  JB Julius Bett
 731. CCM mkoani Iringa imewataka wabunge kuwasilisha na kujadili matatizo ya wananchi wanaowawakilisha bungeni, badala ya kutupiana maneno ya kejeli ambayo hayana tija.

  JB Julius Bett
 732. WAJAWAZITO WASHAURIWA KUHUSU POMBE: Wajawazito wameshauriwa kuacha kutumia pombe kwa kuwa inaweza kuwasababishia watoto madhara makubwa na vifo.

  Daktari Bingwa wa Akinamama wa Hospitali ya Rufaa Mawenzi, Dk Nanyaro Solomon amesema ushauri huo kwa wajawazito ni muhimu wakauzingatia.

  JB Julius Bett
 733. ALI KIBA AACHIA VIDEO MPYA: Ni ya kimataifa, wimbo huo unalenga kupinga ujangili wa tembo, alirekodia Marekani

  JB Julius Bett
 734. TFDA WAKAMATA JUISI, SODA CHOONI: Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) Kanda ya Kati imekamata shehena ya soda na juisi vilivyohifadhiwa chooni na mfanyabiashara mmoja katika Kata ya Kihonda Manispaa ya Morogoro.

  Mkaguzi wa TFDA, Dk Engdrybet Mbekenga amesema leo kuwa mfanyaniashara huyo aliwahi kukamatwa kwa kosa hilo na kutozwa faini ya Sh600,000.

  JB Julius Bett
 735. MIGOGORO YA ARDHI: Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Mwigulu Nchemba ametembelea Kijiji cha Kigurukwa mjini Morogoro kulikotokea mapigano ya Wakulima na Wafugaji yaliyosababisha kuuawa kwa mbuzi 75.

  Waziri Mwigulu ameagiza Kamati ya Ulinzi ya Mkoa kuhakikisha wote waliohusika katikla tukio hilo wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

  Pia ameagiza kutekelezwa haraka hukumu ya mahakama iliyotolewa mwaka 2005 iliyoagiza kuwekwa kwa mipaka kati ya eneo la wafugaji na wakulima.


  JB Julius Bett
 736. WATALII WA NDANI KUSHEREHEKEA PASAKA MLIMA KILIMANJARO: Kampuni ya Kili Base Adventures imeandaa tamasha la kusherehekea Sikukuu ya Pasaka kwa watalii wa ndani kupanda mlima Kilimanjaro. Mkurugenzi mwendeshaji wa kampuni hiyo, Sifael Hariohay, amesema leo kuwa lengo la kuandaa tamasha hilo ni kuhamasisha utalii wa ndani.

  JB Julius Bett
 737. MUHONGO: WAWEKEZAJI RUKSA KUUZA UMEME: Nishati inayozalishwa nchini ipo chini ya kiwango kinachohitajika.

  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo alitoa kauli hiyo jana kwenye kikao cha mameneja na watendaji wa Tanesco kilichowashirikisha wawekezaji wadogo nchini katika Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Mtera.

  JB Julius Bett
 738. WAKE KWA WAUME WALAZWA PAMOJA: Kituo cha Afya cha Ushetu cha Halmashauri ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, kinalaza wagonjwa wanawake na wanaume kwenye chumba kimoja kutokana na uhaba wa wodi.

  Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Isabela Chulumba amesema kwa sasa hawana fedha ya kujenga wodi nyingine kituoni hapo za kulaza wagonjwa.

  JB Julius Bett
 739. Gari aina ya Toyota Land-Cruiser lililokuwa limempakia mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Mama Tunu Pinda, likinyanyuliwa ili kupakizwa kwenye lori baada ya kupinduka eneo la Mkundi Sheri, Morogoro juzi. Picha na Lilian Lucas

  JB Julius Bett
 740. Jeshi la Polisi Zanzibar limewataka madaktari kuacha kuwahudumia watu wanaokwenda hospitali baada ya kupigwa na kikundi cha watu wasiojulikana cha mazombi bila ya kuwa na fomu ya matibabu (PF3).

  Mkurugenzi wa Upelelezi Zanzibar, Salum Msangi amesema matukio ya watu kujeruhiwa na kutopeleka taarifa polisi yanachangia kuendeleza uhalifu.

  JB Julius Bett
 741. Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akimfariji Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir aliyelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.

  JB Julius Bett
 742. KIPINDUPINDU IRINGA: Idadi ya wagonjwa wa kipindupindu katika kambi ya Mt. Luka, Pawaga imeongezeka na kufikia 85, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza athibitisha leo.

  JB Julius Bett
 743. HAKIMU KIZIMBANI: Takukuru leo yamfikisha kortini Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Manyoni, Mahando Sabato kwa tuhuma za kuomba rushwa ya Sh350,000 ili afute kesi ya wizi.

  JB Julius Bett
 744. AJALI TABATA MATAA: Wananchi eneo la tukio kushuhudia magari yaliyogongana kwenye barabara ya Mandela eneo la Tabata Mataa jijini Dar es Salaam leo. Picha na Anthony Siame

  JB Julius Bett
 745. HATUA: TPA yafungia makampuni 210 ya usafirishaji na uondoaji mizigo bandarini kwa kutowasilisha nyaraka za malipo, Meneja mawasiliano J. Ruzangi athibitisha leo

  JB Julius Bett
 746. Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, Mahmoud Kambona amewaagiza polisi kuwakamata viongozi wa kampuni ya TanzaniteOne kwa kukiuka maagizo yake na kuwafukuza wafanyakazi wa kampuni hiyo.

  Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Halfani Hayeshi amethibitisha kufukuzwa kazi kwa wafanyakazi hao 2O1 kwa kushiriki mgomo usio halali mwanzoni mwa wiki hii.

  JB Julius Bett
 747. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga imekusanya zaidi ya Sh185 milioni katika kipindi cha siku 100 za utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano zilizotokana na kutoza bidhaa zilizoingizwa kwa magendo nchini. Meneja wa TRA, Mkoa wa Tanga, Salehe Byalugaba asema leo

  JB Julius Bett
 748. UBADHIRIFU ATCL: Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Mbarawa leo amsimamisha kazi Meneja wa fedha wa ATCL kupisha uchunguzi wizi wa Sh.715 mil.

  JB Julius Bett
 749. WARUNDI 26 WAKAMATWA SIRARI: Raia 26 wa Burundi wakiwamo watoto 14 wamekamatwa katika kituo cha mabasi Sirari wilayani Tarime Mkoa wa Mara wakidaiwa kuingia nchini kinyemela na kutafuta hifadhi.

  Ofisa Uhamiaji Mfawidhi mpaka wa Sirari, Estomih Urio amesema Warundi hao walikuwa kwenye Kambi ya Kakuma Kenya, inayohifadhi wakimbizi kutoka Somalia.

  JB Julius Bett
 750. RADI YAUA: Wanafunzi watatu wa Shule ya Sekondari Kanazi wamekufa, 19 wajeruhiwa baada ya kupigwa na radi leo huko Ngara, DC Honoratha Chitanda athibitisha.

  JB Julius Bett
 751. AJALI TANGA: Watu kadhaa wahofiwa kufa baada ya basi la Simba Mtoto toka Tanga- Dar kugonga lori huko Muheza, polisi inaendelea kunasua walionasa ndani ya basi.

  JB Julius Bett
 752. Watu kadhaa wahofiwa kufa baada ya basi la Simba Mtoto toka Tanga- Dar kugonga lori huko Muheza, polisi inaendelea kunasua walionasa ndani ya basi.

  JB Julius Bett
 753. AJALI TANGA: Watu kadhaa wahofiwa kufa baada ya basi la Simba Mtoto toka Tanga- Dar kugonga lori huko Muheza, polisi inaendelea kunasua walionasa ndani ya basi.

  JB Julius Bett
 754. Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe amewakatia bima ya mfuko wa afya ya Jamii vijana 100 wa bodaboda

  JB Julius Bett
 755. AJALI TANGA: Watu 11 Wafa, 18 wajeruhiwa baada ya basi la Simba Mtoto toka Tanga kwenda Dar kugongana na lori huko Muheza, Kamanda Mihayo Msikhela athibitisha.

  JB Julius Bett
 756. MGOMO KAGERA: Polisi Karagwe leo watumi mabomu ya machozi kutawanya wafanyakazi wa kampuni inayojenga barabara ya Kyaka-Bugene wakidai malimbikizo ya mishahara.

  JB Julius Bett
 757. YANGA YAKWAMA DAR: Yanga yashindwa kuanza safari leo asubuhi kuelekea Mauritius baada ya ndege kupata hitilafu kabla ya kuondoka, uongozi wa klabu wathibitisha.

  JB Julius Bett
 758. Majeruhi 16 wa ajali ya Simba mtoto waruhusiwa kurudu nyumbani, Mganga Mfawidhi wa hospitali Teule Wilayani Muheza,Dr Rajab Malagio athibitisha

  JB Julius Bett
 759. Taasisi ya TZ One Billion Rising Movement inawaalika wanaume, wanawake na watoto wote kukusanyika kwa ajili ya matembezi ya kuunga mkono mabadiliko katika Tanzania ya leo. Siku hiyo imekusudiwa kuwatia moyo watu wote kujitokeza na kusisitizia umoja na kupinga unyanyasaji dhidi ya wanawake.

  Waandaaji wanawaalika wote kukusanyika kwenye Klabu ya New Msasani kuanzia saa 6 mchana na matembezi kuanza saa 8 mchana kupitia Barabara ya Mandazi.

  JB Julius Bett
 760. ZILIZOTUFIKIA: Wenje apata ajali
  Gari lililokuwa likiendeshwa na aliyekuwa Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje limepata ajali maeneo ya Magereza Bariadi mkoani Simiyu mchaba wa leo baada ya kuacha njia na kugonga mtaro na kisha kuanguka. Ndani ya gari hilo alikuwepo pia Mbunge wa VIti Maalumu (Chadema), Gimbi Masaba na Mwandishi wa habati wa Tanzania Daima, Sitta Tuma ambao wamepata michubuko kidogo.

  JB Julius Bett
 761. TAARIFA YA MALI TAKUKURU: Waziri Angellah Kairuki awataka wafanyakazi wote wa Takukuru kuwasilisha vielelezo vya mali wanazomiliki; aonya kuhusu udanganyifu.

  JB Julius Bett
 762. WAKURUGENZI WASIMAMISHWA: Waziri wa Afya Ummy Mwalimu awasimamisha kazi leo wakurugenzi 4 wa MSD kwa tuhuma za ubadhirifu wa shilingi bilioni 1.5.

  JB Julius Bett
 763. Waziri wa Elimu Sayansi, Teknolojia na ufundi, Prof Joyce Ndalichako amesitisha mkataba wa kazi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikop George Nyatenga. Pia amewasilisha kazi wakurugezi watatu wa Bodi hiyo ambao ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Yusufu Kisare, Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo Juma Chagonja na Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo. Prof amemwagiza Mkaguzi wa ndani Mkuu wa Serikali ahakiki maelezo na Nyaraka zilizowasiliwa na Bodi ya Mikopo pamoja na kufanya ukaguzi maalum kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi sasa.

  JB Julius Bett
 764. MSIBA BONGO 'FLEVA': Mwanamuziki Michael Mhina "John Walker" amefariki Muhimbili kuamkia leo, baba yake, Denis Mhina athibitisha. Mwili kusafirishwa kwenda Tanga kesho.

  JB Julius Bett
 765. COCOA YAITANGAZA KYELA KIMATAIFA

  Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Thea Ntara amesema cocoa imepata sifa ya ubora kutokana na kulimwa bila kutumia mbolea au dawa za viwandani. Asema kuwa, cocoa ya Kyela imeingia kwenye masoko ya kimataifa na kusababisha wanunuzi wengi kufika wilayani mwake. “Mwaka 2012 tani milioni tatu za cocoa zilizalishwa, lakini mwaka jana tani milioni 6.4 zimenunuliwa jambo linaloonyesha uzalishaji unaongezeka,” amesema. Miaka 20 iliyopita zao hilo halikupewa kipaumbele wilayani Kyela kutokana na kushuka kwa soko la zao hilo.

  JB Julius Bett
 766. Watanzania wameonywa kutumia simu zisizokidhi viwango vya ubora ambazo zimepigwa marufuku na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Mkuu wa Kitengo cha Vifaa vya Mawasiliano wa Kampuni ya Tigo, David Zakaria amesema: “Kwa mujibu wa maelekezo ya TCRA simu za mkononi ambazo namba zake za utambulisho wa kimataifa (IMEI) ni bandia zitapigwa marufuku kutumika kwa mitandao yote ya simu kuanzia Juni 16 mwaka huu.

  JB Julius Bett
 767. UKUSANYAJI TAKWIMU KUTUMIA GPS

  Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) imetoa mafunzo ya ukusanyaji wa takwimu za kilimo kwa kutumia mfumo wa kiteknolojia wa GPS (Global Position System).

  Mkurugenzi wa ofisi hiyo, Dk Albina Chuwa amesema mafunzo hayo kwa wadadisi 90 kutoka Dar es Salaam, Lindi, Mtwara na Pwani yana lengo la kuacha kutumia njia ya kizamani zilizokuwa zinagharimu fedha nyingi.

  JB Julius Bett
 768. Polisi imeanza kuwaita vigogo wa CUF siku chache baada ya Balozi Seif kusema kama kuna watu wanatishia kufanya vurugu watu wa mwanzo watakaoanzwa kukamatwa ni viongozi

  JB Julius Bett
 769. MAPAMBANO: Polisi leo yasambaratisha jamii za Wamasai, Wamang'ati mkoani Manyara wakiwa na silaha za jadi na moto wakijiandaa kupambana baada ya mifugo kudaiwa kutokea mauaji ya mwanamke na kuibwa kwa ng’ombe 23.

  JB Julius Bett
 770. HATUA:Kamishna wa Elimu Prof Bhalalusesa aagiza wakuu vituo vya Elimu ya Watu Wazima Dar, Mwanza, Dodoma kufukuzwa kwa uwepo upotoshaji katika udahili wanafunzi

  JB Julius Bett
 771. MBARONI: Polisi yawashikilia mwanasheria mkoa Katavi F. Seif, askari magereza 2 wakituhumiwa kumtorosha mtuhumiwa aliyetaka kumuua albino baada ya kuhongwa Sh3m.

  JB Julius Bett
 772. KWA HERI JANETH:Mke wa Rais Magufuli, Janeth leo awasili Shule ya Msingi Mbuyuni, Dar alikokuwa anafundisha kabla mumewe hajachaguliwa kuwa Rais, walimu wamuaga

  JB Julius Bett
 773. Mkazi wa wilaya ya Handeni,akichota Maji kwenye kisima kilichopo pembeni ya bwawa linalotumiwa na wakazi hao, Kutokana na maji ya kwenye bwawa kuwa machafu sana na kutofaa kwa matuminzi ya nyumbani hivyo kuwalazimu kuchimba visima pembeni ili kupata Maji safi yanayojichuja kutoka bwawani lakini sio salama.Picha kulia ni hali halisi ya maji ya bwawa hilo jinsi yalivyo machafu.Picha na Rajabu Athumani, Handeni.

  JB Julius Bett
 774. UCHAGUZI MKUU UGANDA: Upigaji kura katika maeneo mengi umeanza nchini Uganda ingawa kwa kuchelewa katika baadhi ya maeneo. Picha na Henry Lubulwa, Andrew Bagala, Rachel Mabala na Denis Edema.‪#‎UgandaDecides‬

  JB Julius Bett
 775. NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YALIYOPANGWA KWA MFUMO WA DIVISION.

  -Ufaulu umeshuka kwa asilimia 1.85 mwaka 2014 kwa mfumo wa GPA ambapo ufaulu ulikuwa ni asilimia 69.76 Mwaka 2015 ufaulu kwa mfumo wa division ni asilimia 67.91

  - Wasichana wachukua nafasi tatu za mwanzo katika kumi bora.‪#‎Mwananchi‬

  JB Julius Bett
 776. Waangalizi kutoka AU-African Union wakiwa kwenye moja ya vituo vya kupigia kura katika uchaguzi mkuu wa Uganda unaofanyika leo hii.‪#‎Ugandadecides‬

  JB Julius Bett
 777. Baadhi ya walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari Kaizirege iliyopo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera wakifurahia shule yao kuongoza Kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2015 yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani (Necta) leo. Picha na Phinias Bashaya

  JB Julius Bett
 778. Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Kaizirege iliyopo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera wakifurahia shule yao kuongoza Kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2015 yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani (Necta) leo. Picha na Phinias Bashaya

  JB Julius Bett
 779. Baadhi ya walimu wa shule ya sekondari Kaizirege iliyopo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera wakifurahia shule yao kuongoza Kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2015 yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani (Necta) leo. Picha na Phinias Bashaya

  JB Julius Bett
 780. VURUGU MWANZA: Polisi watumia mabomu ya machozi leo kutawanya waendesha bodaboda waliofunga barabara ya TX Igombe – U/Ndege kupinga agizo la serikali kuifunga.

  JB Julius Bett
 781. Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Alliance Girls ya jijini Mwanza, wakifurahi baada ya kutangaziwa wamekuwa nafasi ya pili kitaifa kwenye matokeo ya kidato cha nne.Picha na Michael Jamson

  JB Julius Bett
 782. MWALIMU ASHIKILIWA TAKUKURU KWA RUSHWA YA SH100,000

  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani Bukombe, Mkoa wa Geita imemkamata mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Umoja akituhumiwa kupokea rushwa ya Sh100,000.

  Mkuu wa Takukuru wilayani Bukombe, Shija Chuzela amesema mwalimu huyo alishawishi na kuomba rushwa kwa Marco Elias, aliyekuwa anamtafutia mtoto wake nafasi ya kuingia darasa la saba shuleni hapo.

  JB Julius Bett
 783. JELA MIAKA 30: Mahakama ya wilaya ya Ilala leo yamhukumu Riziki Ally (25) kwenda jela miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mvulana wa miaka 16.

  JB Julius Bett
 784. BOSI BMT 'OUT': Waziri wa Michezo Nape Nnauye amrejesha wizarani Katibu Mkuu wa BMT Henry Lihaya leo kutokana na utendaji usioridhisha, aagiza uteuzi mwingine.

  JB Julius Bett
 785. Butogwa Shija wa Shule ya Sekondari ya Canossa aliyeshika nafasi ya kwanza kitaifa katika mtihani wa kidato cha nne. Picha na Said Hamis

  JB Julius Bett
 786. Congcong Wang wa Shule ya Sekondari ya Feza Girls aliyeibuka mwanafunzi wa pili kitaifa matokeo ya kidato cha nne.

  JB Julius Bett
 787. Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Feza Girls wakimshangilia mwenzao, Congcong Wang (katikati)ambaye ni raia wa China aliyeibuka mwanafunzi wa pili kitaifa katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2015, yaliyotangazwa jana jijini Dar es Salaam. Picha na Said Khamis

  JB Julius Bett
 788. Mhitimu wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Marian Boys, Bright Mwang’onda akiwa amekumbatiwa na mama yake Hamida Kejo baada ya kupata taarifa kuwa miongoni mwa wanafunzi 10 bora kitaifa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne jijini Dar es Salaam jana. Picha na Doris Maliyaga

  JB Julius Bett
 789. RUNGU LA TCU: Tume ya Vyuo Vikuu leo imefuta hati ya kuanzisha vyuo viwili vya elimu vya Chuo Kikuu cha Mt. Joseph TZ Songea kwa kutoa viwango duni vya elimu.

  JB Julius Bett
 790. RUNGU LA TCU: Vyuo vya Mt. Joseph vilivyofutiwa hati ni Chuo Kishiriki cha Sayansi ya Kilimo na Teknolojia na Chuo Kishiriki cha Tehama vilivyopo mjini Songea.

  JB Julius Bett
 791. RUNGU TCU: Wanafunzi 2046 wanaosoma shahada, stashahada katika vyuo 2 vilivyofutiwa hati watahamishiwa kwenye vyuo vingine. Watajulishwa kupitia tovuti ya TCU.

  JB Julius Bett
 792. UCHAGUZI UGANDA: Yoweri Museveni atangazwa mshindi leo kwa kupata kura 5,617, 503 (60.7%) dhidi ya Dk. Kizza Besigye wa FDC aliyepata kura 3,270,290 (34.18%).

  JB Julius Bett
 793. KIDATO CHA NNE: Wanafunzi 59 Sekondari ya Kihanga wilayani Karagwe wanyimwa matokeo kwa madai ya kutolipia mitihani; Wazazi wapinga na kuandamana hadi kwa Afisa Elimu wakiwa na risiti za malipo.

  JB Julius Bett
 794. BIDHAA ZAKAMATWA DAR: Shehena ya mizigo iliyosafirishwa kwa jahazi kutoka Z'bar yakamatwa bandarini jijini Dar kwa madai ya kutolipiwa kodi, Polisi wathibitisha

  JB Julius Bett
 795. MKUU UTUMISHI ASIMAMISHWA: Waziri Angellah Kairuki amsimamisha kazi leo Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Said Nassor kutokana na utendaji usioridhisha.

  JB Julius Bett
 796. MUGABE ATIMIZA MIAKA 92, KUWANIA TENA URAIS 2018

  Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametimiza umri wa miaka 92 huku chama chake kikisema atawania tena urais 2018.


  Mnadhimu wake mkuu amesema kiongozi huyo ambaye ameongoza nchi tangu mwaka 1980, bado ana uwezo kamili wa kuongoza Serikali licha ya tetesi kwamba hawezi kuongoza kutokana na umri

  JB Julius Bett
 797. AJALI YAUA MARA: Watu 3 wafa, 19 wajeruhiwa leo asubuhi baada ya basi la Nata Raha toka Serengeti kuacha njia na kugonga nyumba Kwa Sabato, Bunda. Uokoaji waendelea.

  JB Julius Bett
 798. AJALI MARA: Vifo vyafikia 5 baada ya basi kugonga nyumba huko Bunda leo, Mganga Mkuu wa wilaya Nicholas Machochota athibitisha. 4 taabani, wakimbizwa Bugando Hospital, mkoani Mwanza.

  JB Julius Bett
 799. Wanafunzi 926 wa shule ya msingi Nyakanazi kata ya Lusahunga wilayani biharamulo mkoani Kagera wakisomea kwenye uwanja na kuandika chini kwa kukosa vyumba vya madarasa shuleni hapo.

  Leo kutakuwa na mkutano wa kukabiliana na changamoto hiyo baada ya mkuu wa mkoa wa kagera kutoa agizo kujenga madarasa na vyoo ambapo shule inao wanafunzi 4200

  Picha na Shaaban Nasibu Ndyamukama

  JB Julius Bett
 800. Wanafunzi 926 wa shule ya msingi Nyakanazi kata ya Lusahunga wilayani biharamulo mkoani Kagera wakisomea kwenye uwanja na kuandika chini kwa kukosa vyumba vya madarasa shuleni hapo.

  JB Julius Bett
 801. Wanafunzi 926 wa shule ya msingi Nyakanazi kata ya Lusahunga wilayani biharamulo mkoani Kagera wakisomea kwenye uwanja na kuandika chini kwa kukosa vyumba vya madarasa shuleni hapo.

  Leo kutakuwa na mkutano wa kukabiliana na changamoto hiyo baada ya mkuu wa mkoa wa kagera kutoa agizo kujenga madarasa na vyoo ambapo shule inao wanafunzi 4200


  JB Julius Bett
 802. NJOMBE HATARINI KUKUMBWA NJAA

  Mkoa wa Njombe uko katika hatari ya kukumbwa na baa la njaa, kutokana na ardhi kubwa kutumika katika kilimo cha miti, huku zao la viazi mviringo linalotegemewa kwa chakula na biashara, likikumbwa na ugonjwa wa kuungua ambao haujafahamika kitaalamu.

  Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dk Rehema Nchimbi ameziagiza halmashauri mkoani humo kutenga maeneo kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula na wataalamu wa kilimo kufanya utafiti ili kubaini ugonjwa unaoshambulia viazi na kusababisha kukauka.

  JB Julius Bett
 803. SAMIA KUWAPA USHIRIKIANO WAWEKEZAJI WA CHINA

  Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu amewahakikishia wawekezaji kutoka China kuwa Serikali itawapa ushirikiano kutekeleza miradi ya maendeleo watakayowekeza nchini.

  Samia ametoa ahadi hiyo ofisini kwake alipokutana na ujumbe wa Kampuni ya Gezhouba kutoka China.

  JB Julius Bett
 804. TFA KUUBURUTA UONGOZI KORTINI

  Baadhi ya wanachama wa Chama cha Wakulima cha Tanganyika (TFA), wametishia kuuburuza uongozi wao wa muda mahakamani kwa tuhuma za kuuza mali za chama bila ya kuwashirikisha na kutaka uitishwe mkutano mkuu wa dharura wa wafanyakazi. Mwenyekiti wa bodi ya muda ya chama hicho, Meynad Swai amekiri kupokea taarifa hizo akisema kuna wanachama wanatumika kutaka kuuvuruga uongozi wao. Meneja wa TFA, Sarah Lyimo amesema masuala yanayozua utata yatajadiliwa katika mkutano mkuu ili wakulima wapate haki yao.

  JB Julius Bett
 805. Mkuu wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Amani Mwenegoha ametakiwa kuitisha harambee kwa wadau wa elimu ili kuchangia madawati kabla ya Juni 30.

  JB Julius Bett
 806. Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi Communications Limited, Bakari Machumu akimweleza jambo Mkurugenzi wa Rasilimali Watu katika Sekretarieti ya Mtukufu Aga Khan, Marc Brazier (katikati) alipotembelea ofisi za MCL zilizopo Tabata, jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Francis Nanai. Picha na Salim Shao

  JB Julius Bett
 807. MAMA MBARONI KWA KUUA MWANAYE

  Jeshi la Polisi wilayani Kibaha limefukua maiti ya mtu anayedaiwa kuuawa na mama yake, ili kuifanyia uchunguzi wa kitabibu, baada ya kuzikwa kinyemela.

  Mama wa mtoto huyo, Navonoiwa Mndeme, ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Kongo wilayani Bagamoyo na wanaye wawili walikamatwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga hadi kumuua Salehe Hassan na kisha kuuzika mwili huo.

  JB Julius Bett
 808. Mbunge wa Segerea, Bonna Kaluwa amejenga madarasa matano katika Shule ya Msingi Kinyerezi Jica, ikiwa ni mkakati wake wa kukabiliana na upungufu wa madarasa jimboni humo.

  Kaluwa amesema baada ya Rais John Magufuli kutangaza elimu bure, mwitikio wa wanafunzi umekuwa mkubwa tofauti na matarajio. Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Charles Shao amesema shule yake mpya baada ya kugawanywa, ilikumbwa na changamoto ya upungufu wa madarasa, hivyo msaada huo utasaidia kumaliza tatizo hilo.

  JB Julius Bett
 809. Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya inakusudia kukusanya Sh55 bilioni kwa mwaka wa fedha wa 2016/17 kutoka Serikali Kuu na vyanzo vyake vya ndani vya mapato.

  JB Julius Bett
 810. Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu amewahakikishia wawekezaji kutoka China kuwa Serikali itawapa ushirikiano kutekeleza miradi ya maendeleo watakayowekeza nchini.

  Samia alitoa ahadi hiyo ofisini kwake alipokutana na ujumbe wa Kampuni ya Gezhouba kutoka China.

  JB Julius Bett
 811. Vyuo vya Mamlaka ya Mafunzo na Ufundi Stadi (Veta), vimetakiwa kuongeza idadi ya wanafunzi ili kupunguza wimbi la vijana wanaoingia mitaani kila mwaka wasiokuwa na kazi.

  JB Julius Bett
 812. HUDUMA KWA KADI

  Mtangaziji Kituo cha Redio cha EFM, Gadner Habash (wa pili kulia), akiwekewa mafuta gari yake kwa malipo ya kadi (Airtel Money Tap Tap) baada ya Airtel na Total kuingia ubia na kuzindua kadi hiyo kwa ajili ya malipo ya bidhaa mbalimbali. Picha na Mpigapicha Wetu

  JB Julius Bett
 813. Naibu Waziri wa Kazi, Ajira Anthony Mavunde akizungumza na baadhi ya wafanyakazi 201 wa kampuni ya TanzaniteOne waliofukuzwa kazi kwenye kampuni hiyo. Picha na Joseph Lymo

  JB Julius Bett
 814. Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Tanzanite waliofukuzwa kazi, wakimsikiliza Naibu Waziri Anthony Mavunde aliyetembelea mgodi huo leo. Picha na Joseph Lymo

  JB Julius Bett
 815. Chuo Kikuu cha St. Joseph (Arusha) chafungwa kwa muda usiojulikana kufuatia mgomo wa wanafunzi, makamu mkuu wa chuo S.Balasingh athibitisha

  JB Julius Bett
 816. RANGI MCHANGANYIKO: Wanawake hawa wameonekana leo asubuhi katika kituo cha mabasi cha Kimara wakionesha mitindo yao ya uvaaji wa hijab.

  JB Julius Bett
 817. Mwanasiasa mkongwe nchini, Steven Wasira jana alimvamia mpigapicha wa gazeti la Mwananchi aliyekuwa akichukua picha zake wakati akitoka mahakamani, lakini akashindwa kutimiza azima yake ya kufuta picha.

  JB Julius Bett
 818. Naibu Spika, Dk Tulia Ackson akiwaaga wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Loleza, Mbeya jana baada ya kufanya ziara shuleni hapo. Alisoma Loleza kidato cha kwanza hadi cha nne (1991 - 1994). Habari zilizopatikana baadaye jana zilisema kuwa Dk Ackson alinusurika kwenye ajali baada ya gari lake kugongwa na gari jingine kwenye tairi la mbele katika Kijiji cha Mpandapanda wilayani Rungwe wakati akitokea Mbeya kwenda Tukuyu. Picha na Godfrey Kahango

  JB Julius Bett
 819. Kivuko cha MV Kilombero II kikiingizwa majini kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya kuwasha injini ili kufanyiwa majaribio, mkoani Morogoro jana. Picha na Juma Mtanda

  JB Julius Bett
 820. MAREKANI YATANGAZA VIVUTIO NGORONGORO:

  Kituo cha Television cha Marekani cha ABC juzi kilirusha matangazo ya moja kwa moja kwa saa tatu, kuonyesha vivutio vya utalii katika Hifadhi ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha.

  Matangazo hayo ambayo yalionekana katika kipindi cha Goodmorning America, yalirushwa kuanzia saa moja asubuhi hadi saa tatu asubuhi kwa muda wa Marekani wakati Tanzania ilikuwa saa tisa alasiri hadi saa kumi na moja jioni.

  JB Julius Bett
 821. Kamishina wa Sekretarieti ya maadili ya Viongozi Jaji mstaafu Salome Kaganda ameahidi kumkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa majina ya mawaziri na Manaibu Waziri ambao hawajaza fomu za mali wanazomiliki licha ya kutakiwa kufanya hivyo tangu walipochaguliwa.

  Jaji Kaganda alitoa ahadi hiyo kwenye semina kwa mawaziri na manaibu kuhusu mwongozo wa maadili ya viongozi wa umma na utekelezaji wa ahadi ya uadilifu. Jaji Kaganda amesema Sekretarieti hiyo inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwamo ukosefu wa fedha ambao imesababisha washindwe kufanya uhakiki wa mali za viongozi kwa miaka mitatu sasa. Hali hiyo inakwamisha kubaini viongozi wenye uadilifu au waliowadanganyfu kutokana na fomu za mali walizojaza.

  JB Julius Bett
 822. BAYPORT YAZINDUA MIKOPO YA VIWANJA: Viko kwenye maeneo ya Bagamoyo, Chalinze , Temeke, Kilwa na Morogoro.

  PICHA: Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga (kulia), akisisitiza jambo katika uzinduzi wa miradi ya mikopo ya viwanja katika maeneo sita ya Kilwa, Bagamoyo, Kigamboni, Chalinze, Kibaha na Morogoro. Kulia kwake ni Zahra Moore, Mkurugenzi wa Uzalishaji wa BlackWood akifuatiwa na Tibiita Muganga, mwanasheria wa Blackwood.

  JB Julius Bett
 823. Fastjet imepunguza safari zake kwa njia ya Kilimanjaro Tanzania na Nairobi Kenya kuanzia Februari 15, mwaka huu.

  JB Julius Bett
 824. Akina mama wanaofanya kibarua cha kusomba maji ya ujenzi wa mtaro wa barabara ya kiwango cha lami Mugumu wilayani Serengeti wakiwa wamelala kama walivyokutwa, picha na Anthony Mayunga

  JB Julius Bett
 825. Chama cha Wananchi (CUF) kimesema kwamba kinaidai Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), zaidi ya Sh3 bilioni ikiwa ni malimbikizo ya ruzuku kwa takriban miaka 18.

  JB Julius Bett
 826. MRADI WA KIHISTORIA WANUKIA TANZANIA

  Ujenzi wa kiwanda cha uchakataji na usindikaji wa gesi kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi ambacho kitajengwa Lindi utakapokamilika, utakuwa miongoni mwa miradi mikubwa ambayo imewahi kutekelezwa nchini tangu Tanzania ipate uhuru.
  Ili kufanikisha azma hiyo, Serikali imewataka wawekezaji kwenye sekta ya gesi kuharakisha mradi huo ili Tanzania ianze kusafirisha bidhaa hiyo.

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa kiwanda hicho cha gesi kitakachogharimu Dola za Marekani 30 milioni (zaidi ya Sh60 trilioni), thamani yake inafanana na miradi ya reli ya Tazara au bomba la mafuta la Tazama.

  Profesa Muhongo amesema hayo alipokutana na wawekezaji hao Dar es Salaam na kubainisha kuwa mbali na kiwanda hicho, pia kutakuwa na vingine viwili vya mbolea huko Kilwa na Mtwara.

  JB Julius Bett
 827. UCHAGUZI Z'BAR: Chama cha Wananchi (CUF) leo kimesema kitazindua maadamano ya nchi nzima Jumatatu ijayo mkoani Kagera kupinga kurudiwa kwa uchaguzi mkuu Z'bar.

  JB Julius Bett
 828. MATANGAZO YA BUNGE TBC: Mfuko wa Habari Tanzania TMF leo umesema uko tayari kutoa msaada wa fedha ili kuiwezesha TBC kutangaza moja kwa moja mwenendo wa Bunge.

  JB Julius Bett
 829. VIGOGO DART KORTINI: Maofisa waandamizi 3 wa mradi wa mabasi yaendayo kasi (DART) wapanda kizimbani leo katika mahakama ya Kisutu Dar, taarifa zaidi kukujia.

  JB Julius Bett
 830. Makamu mweyekiti wa CUF taifa na mbunge Viti maalum kupitia chama hicho mh Savelina Mwijage akitangaza uzinduzi wa maandamano mkoani KAGERA kupinga uchaguzi Zanzibar wakati akiwa ofisi za CUF zilizopo mtaa wa uswahilini manispaa ya Bukoba

  JB Julius Bett
 831. Makamu mweyekiti wa CUF taifa na mbunge Viti maalum kupitia chama hicho mh Savelina Mwijage akitangaza uzinduzi wa maandamano mkoani KAGERA kupinga uchaguzi Zanzibar wakati akiwa ofisi za CUF zilizopo mtaa wa uswahilini manispaa ya Bukoba

  JB Julius Bett
 832. Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa Tanzania, Yassin Abdallah Ustaadh akiwa na Rais wa Shirikisho la Ngumi ulimwenguni(WBF) Howard Goldberg, ambaye amewasili akiwa na mkanda ambao bondia Francis Cheka ataugombea mwishoni mwa wiki hii. Kushoto kwa Goldberg ni mwamuzi wa pambano hilo Eddie Marshall. Picha na Charles Abel

  JB Julius Bett
 833. Timu ya Cercle de Joackim kutoka Mauritius imewasili jioni hii na ndege ya shirika la ndege la South Africa. Klabu hiyo inatarajia kuumana na Yanga, Jumamosi hii katika mchezo wa marudiano ya raundi ya awali ya mashindano ya Ligi ya mabingwa Africa baada ya mchezo wa kwanza kufungwa nyumbani kwa bao 1-0

  JB Julius Bett
 834. Serikali imeendelea kushikwa na kigugumizi baada ya kushindwa kutamka lini itawalipa posho baadhi ya walimu kwa kusimamia mitihani ya taifa ya kidato cha nne mwaka jana.

  JB Julius Bett
 835. Wakulima kutoka mikoa minane nchini wamesema changamoto inayowakabili katika sekta ya kilimo ni kuwapo kwa pembejeo feki na kusababisha baadhi ya kukithiri kwa umaskini kwa kukosa mazao ya kutosha.

  Wakulima hao wamesema leo kwenye semina ya iliyo andaliwa na shirika la kimataifa la Marekani la Catholic Relief Serves CRS, kwa ufadhili wa shirika la maendeleo la watu wa Marekani USAID iliyofanyika mjini Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro.

  JB Julius Bett
 836. Uhai wa watoto njiti wanaozaliwa wilayani Pangani uko mashakani baada ya Hospitali ya Wilaya hiyo kukosa mashine ya kuwahifadhi.

  JB Julius Bett
 837. Naibu Waziri wa Kazi, Anthony Mavunde ameingilia kati mgogoro wa Kampuni ya Tanzanite One na wafanyakazi 201

  JB Julius Bett
 838. Tanzania imefanikiwa kutoa washiriki 24 kwenye mashindano ya kuwania tuzo za vivutio vya utalii, yanayoratibiwa na World Travel Awards (WTA) kwa nchi za Afrika na India.

  JB Julius Bett
 839. Rais John Magufuli akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa walipokuwa wakizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam jana. Picha na Ikulu

  JB Julius Bett
 840. WASIRA AFICHUA KILICHOMKERA: Mwanasiasa mkongwe nchini, Stephen Wasira amesema kilichomfanya aamue kumvamia mwandishi wa gazeti la Mwananchi juzi ni kitendo cha kupigwa picha nyingi alizoona zimekithiri.

  Wasira, ambaye aliingia kwenye siasa mwaka 1970, alipigwa picha hizo wakati akitoka kwenye jengo la Mahakama Kuu, Kitengo cha Biashara mjini Mwanza ambako shauri la wakazi wa Bunda waliokuwa wakitaka kukata rufaa ya kupinga ushindi wa Mbunge Ester Bulaya wa Chadema katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, 2015, lilitupwa.

  JB Julius Bett
 841. Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) inakabiliwa na upungufu wa chupa 60 za damu kila siku kwa ajili ya kuwaongezea wagonjwa ili kuokoa maisha yao.

  JB Julius Bett
 842. MAZISHI YA MAPILI: Marehemu Kassim Mapili aliyefariki Dar jana atazikwa jioni leo katika makaburi ya Kisutu, asema Rais wa Shirikisho la Muziki, Addo Novemba.

  JB Julius Bett
 843. AJALI SHINYANGA: Watu 4 wafa, 8 wajeruhiwa Alhamisi jioni baada ya basi la Mashimba Express lililokuwa linasafiri toka Kahama - Mwanza kugongana na gari dogo.

  JB Julius Bett
 844. MAADILI: Rais JPM awataka mawaziri 4 na naibu waziri 1kujaza na kuwasilisha fomu Sekritarieti ya Maadili kufikia jioni leo vinginevyo watakuwa wamejifuta kazi.

  JB Julius Bett
 845. MAADILI: Waziri Mkuu Majaliwa amewataja mawaziri hao kuwa ni Charles Kitwanga, January Makamba, Augustine Mahiga na Joyce Ndalichako. N/Waziri ni Luhaga Mpina.

  JB Julius Bett
 846. BULAYA: SIASA ZIMEISHA, TUGEUKIE MAENDELEO

  Mbunge wa Bunda Mjini (Chadema), Ester Bulaya amewataka wakazi jimboni humo kuachana na siasa kwa kuwa uchaguzi umepita na kuangalia namna bora ya kuharakisha kujiletea maendeleo.

  Bulaya alitoa kauli hiyo juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyikia katika Kitongoji cha Mbugani, Kata ya Nyamakokoto mjini Bunda.

  JB Julius Bett
 847. UBAKAJI DAR: Mtuhumiwa mmoja tu kati ya 63 wa matukio ya ubakaji Dar amehukumiwa miaka 30 jela, TAMWA yasema leo. Kesi 43 kortini, 17 hazijasajiliwa, 2 zafutwa.

  JB Julius Bett
 848. DROO EUROPA: Liverpool kucheza na Manchester United raundi ya 16 Europa, Tottenham v. Dortmund, Athletic v. Valencia, Basel v. Sevilla, Leverkusen v. Villarreal.

  JB Julius Bett
 849. UCHAGUZI RAIS FIFA: Mgombea urais wa Fifa, Tokyo Sexwale, raia wa Afrika Kusini, ajitoa leo, muda mfupi kabla ya kura kupigwa nchini Uswisi, wabaki wagombea 4.

  JB Julius Bett
 850. MGOMO MWANZA: Wafanyakazi wa kiwanda cha samaki (Vic Fish) jijini Mwanza wagoma kufanya kazi wakidai nyongeza ya malipo kutoka Sh 3,800 hadi Sh. 10,000 kwa siku

  JB Julius Bett
 851. AGIZO: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aagiza maduka yote ya dawa yanayoizunguka Hospitali ya Rufaa Ligula- Mtwara kufungwa kwa kuwa wagonjwa wanaelekezwa kununua dawa huko

  JB Julius Bett
 852. VURUGU ZA UMEYA: Polisi wazingira nyumba ya Mbunge wa Kawe H. Mdee ili kumfikisha Kituo Kikuu cha Polisi kwa mahojiano, Afisa Habari Chadema T. Makene aeleza.

  JB Julius Bett
 853. UCHAGUZI KILOMBERO: Polisi wamemkamata Mbunge wa Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali baada ya kutaka kushiriki kwenye uchaguzi wa M/kiti wa halmashauri hiyo.

  JB Julius Bett
 854. UCHAGUZI KILOMBERO: Baadhi ya wanahabari wazuiwa kuripoti uchaguzi wa M/kiti wa halmashauri ya Kilombero, waruhusiwa walioambatana na mkuu wa mkoa wa Morogoro.

  JB Julius Bett
 855. UCHAGUZI KILOMBERO: Diwani wa Sanje (CCM), David Ligazo achaguliwa kuwa M/kiti wa Halmashauri ya Kilombero kwa kura 19 dhidi ya Godrey Lwena (Chadema) kura 18.

  JB Julius Bett
 856. TFDA imesema leo imekamata kiwanda bubu kinachotengeneza marashi feki chapa ya 'Same' huko Temeke, Dar kinyume cha sheria, katika kiwanda hicho kumekutwa shehena ya tani 82 ya marashi hayo yakiwa katika hatua za kufungashwa.

  Katika hatua nyingine, TFDA pia imekamata marashi hayo yakiuzwa katika duka moja la vipodizi huko Sinza, jijini Dar. Katika duka hilo kulipatikana chupa zaidi ya 5,000 za marashi hayo zenye thamani ya Sh100 milioni.

  PICHA:Kaimu Meneja, Mawasiliano na Uhusiano wa Umma, kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania TFDA- Gaudensia Simwanza.

  JB Julius Bett
 857. Naibu Waziri wa Afya Dk Hamis Kigwangalla, amewasimamisha kazi wauguzi sita wa Hospitali ya Rufaa Wilaya ya Temeke kwa kosa la kuomba rushwa kwa wajawazito. Wauguzi waliosimamishwa kazi ni pamoja na Hadija Salum, Beatrice Temba, Agnes Mwampashe, Elizabeth Mwilawa, Mariam Mohamed na Marion Said. Akizungumza leo alasiri baada ya kufanya ziara ya ghafla Hospitalini hapo, Kigwangalla amesema wauguzi hao waliokuwa katika zamu ya asubuhi wanapaswa kusimama kazi mpaka Baraza la wauguzi na wakunga Tanzania litakapokaa‪#‎Mwananchi‬

  JB Julius Bett
 858. MKUTANO WA EAC: Rais John Magufuli leo amefungua mkutano wa 17 wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaofanyika jijini Arusha.

  JB Julius Bett
 859. HUDUMA BORA: Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo imezitoza faini kampuni tano za simu za mkononi kwa kushindwa kutoa huduma bora kwa wateja.

  JB Julius Bett
 860. RUNGU LA TCRA:TCRA yaisimamisha Kampuni ya Azam Marine kutoa huduma za kiposta kusafirisha vifurushi na vipeto,kulipa Sh5m kwa kuendesha huduma hizo bila leseni

  JB Julius Bett
 861. Mwenyekiti wa EAC, Rais Dk John Magufuli ameidhinisha nchi ya Sudani Kusini kuwa mwanachama wa 6 wa EAC.

  JB Julius Bett
 862. EAC yamchagua Liberat Mfumukeko kutoka Burundi kuwa katibu mkuu wake baada ya Richard Sezibera kufikia kikomo cha uongozi wake.

  JB Julius Bett
 863. KESI YA KUBENEA: Korti ya Kisutu leo yamkuta mbunge wa Ubungo Saed Kubenea na kesi ya kujibu katika kesi ya kumtolea lugha ya matusi DC wa Kinondoni P. Makonda.

  JB Julius Bett
 864. UTANGAMANO EAC: Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo wamezindua jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Arusha-Holili/Taveta yenye urefu wa km 234.3.

  JB Julius Bett
 865. MAUAJI KIGOMA: Walinzi 2 wa Hifadhi ya Msitu wa Makere wilayani Kasulu wauawa, 3 waumia katika mapambano baada ya wafugaji kuvamia msitu huo, polisi wasema leo.

  JB Julius Bett
 866. ICU MPYA MUHIMBILI: Naibu Waziri wa Afya H. Kigwangalla azindua leo chumba kipya cha wagonjwa mahututi chenye vitanda 25 badala ya wodi ya awali yenye vitanda 8.

  JB Julius Bett
 867. HAFLA MAALUM KWA AJILI YA KUKUTANA NA WADAU MBALIMBALI WA KAMPUNI YA MWANANCHI ILIYOFANYIKA JANA KATIKA HOTEL YA SERENA, DAR ES SALAAM.

  Naibu Waziri, Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura akiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa National Media Group, Joe Muganda wa pili kutoka (kushoto), Mwenyekiti wa MCL, Leonard Mususa (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Francis Nanai (kulia) na Mkurugenzi wa Idara Habari MAELEZO, Assah Mwambene. Picha na Anthony Siame #Mwananchi

  JB Julius Bett
 868. Sumatra imesema mabaharia wanapaswa kupata mafunzo zaidi ili kuimarisha huduma za usafiri majini.

  JB Julius Bett
 869. Wakulima wa Kijiji cha Masanga Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, wameiomba Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) kuharakisha mpango wa kuwagawia mashine ya kuchambua zao hilo ili waweze kupanga madaraja ya mazao yao kulingana na ubora.

  JB Julius Bett
 870. Serikali imesema itaendelea kuwabana wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi na ushuru ili ikusanye fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo nchini.

  JB Julius Bett
 871. Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa ujenzi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi, katika hafla iliyofanyika Tengeru, Arusha.Kutoka kulia ni Makamu wa Rais wa Burundi, Joseph Botare, Makamu wa Rais wa Sudan Kusini, James Wani Igga, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Rais John Magufuli, Rais wa Uganda, Yoweri Museven, Waziri wa Afrika Mashariki wa Rwanda, Valentine Rugwabiza na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein. Picha na Ikulu

  JB Julius Bett
 872. UTEUZI: Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Jenister Mhagama atengua uteuzi wa kaimu bosi mpya wa NSSF Dk Carina Wangwe muda mfupi baada ya kuteuliwa hapo jana.

  JB Julius Bett
 873. AJALI MANYARA: Watu 7 walazwa hospitali ya wilaya ya Kiteto baada ya kuumia katika ajali ya lori iliyotokea mapema leo wakati ikielekea mnadani Kata ya Kijungu.

  JB Julius Bett
 874. SILAHA ZAKAMATWA ARUSHA: Silaha 4 za kivita, risasi 164 zakamatwa wilayani Ngorongoro katika operesheni kukabili mapigano ya kikabila, asema leo RPC L. Sabas.

  JB Julius Bett
 875. AJALI ZIMBABWE: Watu 30 wafa, 36 wajeruhiwa baada ya basi kupasuka tairi kisha kugongana na basi lingine kwenye barabara kuu ya Harare-Bulawayo, polisi wasema.

  JB Julius Bett
 876. Shirika la Afya Duniani (WHO) limetaka wananchi wasibughudhiwe katika mapambano dhidi ya kipindupindu, badala yake waelimishwe njia za kujikinga.

  JB Julius Bett
 877. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, limemuua mtu anayedhaniwa kuwa ni jambazi aliyekuwa akifanya jaribio la kupora fedha kwenye kituo cha mafuta cha Olympic kilichopo Igoma jijini Mwanza

  JB Julius Bett
 878. Watu wawili wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa baada ya kutokea mapambano kati ya maofisa wa Idara ya Misitu wilayani Kasulu mkoani Kigoma kushirikiana na mgambo kuvamia hifadhi ya Msitu wa Makere ili kukabiliana na wafugaji.

  JB Julius Bett
 879. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina ameahidi kufuatilia na kuchukua hatua dhidi ya Kiwanda cha Mount Meru kilichopo Bunda ambacho kinadaiwa kutiririsha maji yenye kemikali katika makazi ya wananchi wa Stoo mjini humo.

  JB Julius Bett
 880. UCHAGUZI BENIN: Zoezi la kuhesabu kura za urais linaendelea nhini Benini ambapo wagombea urais 33 wanachuana kumrithi Thomas Boni Yayi, mamlaka husika yaeleza.

  JB Julius Bett
 881. KATIBU KIONGOZI: Rais John Magufuli amwapisha Balozi Mhandisi John Kijazi kushika rasmi wadhifa wa Katibu Mkuu Kiongozi , Ikulu jijini Dar.

  JB Julius Bett
 882. BUNGE KUANZA: Bunge la Afrika Mashariki kuanza vikao vyake vya wiki 2 kesho Dar ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atalifungua rasmi, Spika Daniel Kidega aeleza

  JB Julius Bett
 883. UJENZI WA BOMBA: Ujenzi wa bomba la kusafirishia mafuta (1,403KM) kutoka Uganda hadi Bandari ya Tanga kuanza mwezi Agosti; litagharimu dola 4bn, TPDC waeleza.

  JB Julius Bett
 884. Mamlaka ya Utambulisho wa Taifa (Nida) imevunja mikataba ya wafanyakazi wake 597 kwa sababu za ufinyu wa bajeti unaosababishwa na idadi kubwa ya wafanyakazi hao, pia kuwa na ufanisi mdogo katika kuzalisha vitambulisho vya Taifa.

  Mamlaka hiyo itapitia upya majukumu ya wafanyakazi wengine 802 wa kudumu ili kuendana na majukumu yaliyopo. Kama itabainika idadi bado ni kubwa, wafanyakazi hao watarudhishwa wizara ya utumishi kwa ajili ya kupangiwa majukumu mengine.

  JB Julius Bett
 885. MAUAJI YA ALBINO: Takribani watu 30 waliokutwa na hatia ya mauaji ya albino watanyongwa kwa mujibu wa sheria, Waziri wa Sheria Mwakyembe asema leo kupitia TBC.

  JB Julius Bett
 886. AFYA YA MAALIM SEIF: Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad leo amesema afya yake inaendelea vizuri baada ya kulazwa katika hospital ya Hindu Mandal, Dar jana.

  JB Julius Bett
 887. FEDHA ZA HDFI KUKUZA UBUNIFU: Mfuko wa ruzuku kwa ubunifu unaoleta mabadiliko kwenye jamii Tanzania (HDIF), umetenga zaidi ya Dola 5 milioni za Marekani (Sh10.75 bilioni) kwa kukuza ubunifu wa teknolijia wa kijamii.

  Ofisa Mtendaji wa HDIF, David Mcginty amewaambia waandishi wa habari kuwa fedha hizo zimetengwa wakati wanapoelekea kwenye maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu inayoanza Machi 13 hadi 19.

  JB Julius Bett
 888. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema inatambua mchango unaotolewa na taasisi za fedha zikiwamo benki kuleta maendeleo na kupunguza umaskini nchini.Waziri wa Fedha na Uchumi wa Zanzibar, Omar Yussuf Mzee ametoa kauli hiyo wakati akizindua tawi jipya la Benki ya Afrika (BOA), Mlandege mjini Unguja.

  JB Julius Bett
 889. AJALI DAR: Watu kadhaa wahofiwa kufa leo asubuhi baada ya daladala kugongana na malori mawili eneo la Matumbi jijini Dar. Taarifa zaidi kukujia.

  JB Julius Bett
 890. Watu kadhaa wahofiwa kufa leo asubuhi baada ya daladala kugongana na malori mawili eneo la Matumbi jijini Dar.

  JB Julius Bett
 891. AJALI DAR: Watu 4 wafa, 25 wajeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha magari 3 mapema leo huko Matumbi, Dar, daktari Hospitali ya Amana Stanley Binagi athibitisha.

  JB Julius Bett
 892. Wawakilishi wa TZ katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Yanga yaondoka asubuhi hii kuelekea mjini Kigali Rwanda kuikabili APR ya huko Jumamosi hii.

  JB Julius Bett
 893. 2 KORTINI MWANZA: Maofisa wa Mifugo, Ugavi wilayani Misungwi wapandishwa kizimbani leo kwa kutumia vibaya madaraka yao, kuisababishia serikali hasara ya Sh27m.

  JB Julius Bett
 894. Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imebuni mfumo maalum wa kupata taarifa za ujuzi na huduma za maendeleo ya biashara kupitia intaneti na simu za mkononi utakaotumiwa na wafanyabishara wadogo na wa kati.

  JB Julius Bett
 895. Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), inaendelea na mazungumzo na Benki ya Uwekezaji (TIB) kwa lengo la kupata mkopo wenye riba nafuu wa Sh213 bilioni ili kutekeleza miradi ya kuongeza vichwa 19 na mabehewa ya mizigo 260. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Masanja Kadogosa amesema kuwa mkopo huo utaisaidia kupata mtaji wa mafuta ili kutekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa(BRN).

  JB Julius Bett
 896. Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu za Mkononi Tigo, Kanda ya Ziwa, Ally Maswanya amesema wamepanua mawasilino kwa kuwafikishia wateja wa Mwanza huduma ya 4G LTE.

  JB Julius Bett
 897. MALI ZA SHKUBA MAREKANI: Marekani yashikilia mali za Mtanzania Ali K. Haji Hassan “Shkuba” na mtandao wake baada ya kumtaja kinara mkuu wa dawa za kulevya duniani.

  JB Julius Bett
 898. MAGUFULI ‘AVAMIA’ BOT: Rais John Magufuli afanya ziara ya kushtukiza leo Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar; afanya kikao na menejimenti ya taasisi hiyo.

  JB Julius Bett
 899. ZIARA YA MAGUFULI BOT: Ikulu yasema Rais Magufuli ameiagiza Benki Kuu ya Tanzania kusitisha malipo ya malimbikizo ya Sh925.6 bilioni hadi Hazina iyahakiki.

  JB Julius Bett
 900. KUBENEA KORTINI: Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea apandishwa kizimbani mahakama ya Kisutu asubuhi leo, aunganishwa kwenye kesi ya vurugu za uchaguzi wa meya Dar.

  JB Julius Bett
 901. DAWA ZA KULEVYA: Polisi Uwanja wa Ndege Dar jana wamekamata kifurushi chenye gramu 596 za Heroin kilichotumwa toka Morogoro kisafirishwe kwa DHL kwenda Canada.

  JB Julius Bett
 902. UCHAGUZI UMEYA DAR: Waziri Simbachewene aagiza Arusha leo uchaguzi wa umeya Dar ufanyike kabla ya Machi 25, ataka vyama husika kuheshimu misingi ya kidemokrasia.

  JB Julius Bett
 903. MBAKAJI AFUNGWA:Mahakama wilayani Misungwi leo imemhukumu kifungo cha miaka 30 mkazi wa kijiji cha Busagara kwa kukutwa na hatia ya kumbaka binti wa miaka 11.

  JB Julius Bett
 904. Wakala wa Huduma za Misitu TZ umewataka wakazi wa Tarafa ya Kahunda wilayani Buchosa kuwa walinzi wa hifadhi ya shamba la miti la Buhindi

  JB Julius Bett
 905. Vituo 12 vya afya mikoa ya Mwanza na Mara vimekabidhiwa vifaa vya tiba vyenye thamani zaidi ya Sh20 milioni kwa ajili ya wanawake na watoto.

  JB Julius Bett
 906. Mkoa wa Mwanza umetoa Sh181 milioni kati ya mwaka 2013/14 kwa vikundi 230 vya wanawake ili kuwaendeleza kiuchumi.

  JB Julius Bett
 907. Tanesco Sengerema wapewa siku saba kukamilisha kazi. Ni ya kufunga umeme katika taasisi za umma zilizopo kwenye mradi wa Rea

  JB Julius Bett
 908. DC AWATUMBUA MAJIBU WATENDAJI WAWILI

  Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amewasimamisha kazi kwa siku saba watendaji wawili wa Kijiji cha Igula kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za miradi ya kijiji.

  JB Julius Bett
 909. Meli za kivita kutoka Afrika Kusini, China na Pakistan zikiwa zimetia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam. Picha na Said Khamis

  JB Julius Bett
 910. Hatimaye Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara imepata gari na kufungua ofisi ya Kikosi cha Zimamoto ili kukabilana na majanga ya moto.

  JB Julius Bett
 911. Mzee wa miaka 80 amekutwa amekufa ndani ya choo cha Msikiti wa Ibadhi uliopo Bopwe karibu na Ofisi za Baraza la Wawakilishi Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

  JB Julius Bett
 912. BOSI NEWCASTLE 'ATUMBULIWA': Kocha Newcastle Steve McCLaren amefukuzwa kazi leo baada ya kudumu miezi 9 kutokana na matokeo mabaya, klabu hiyo yathibitisha leo.

  JB Julius Bett
 913. POCHETTINO, FORSTER WANG'ARA: FA ya England yamtangaza Mauricio Pochettino wa Tottenham kocha bora, kipa Forster Fraser wa Southampton mchezaji bora wa Februari

  JB Julius Bett
 914. Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga akisaidiwa kunyanyuka na Ofisa Maliasili Mkoa wa Kilimanjaro, Emmanuel Kiyengi na polisi baada ya kutumbukia kwenye mfereji wa maji alipokuwa akikagua uharibifu wa mazingira unaofanywa katika msitu wa Rau, Moshi. Picha na Dionis Nyato

  JB Julius Bett
 915. MOTO Z'BAR: Watu wasiojulikana wateketeza kwa moto Kituo cha afya Kiuyu Pemba, nyumba 2 za wananchi na ofisi ya CCM usiku wa kuamkia leo, taarifa zaidi baadaye.

  JB Julius Bett
 916. MBUNGE MBARONI: Mbunge Esther Bulaya anashikiliwa Kituo Kikuu cha polisi Mwanza baada ya kukamatwa jana saa saba usiku, taarifa kamili baadaye, T. Makene aeleza

  JB Julius Bett
 917. UCHAGUZI MAREKANI: Rais Barack Obama awaonya wagombea urais kuepuka kauli za chuki baada ya vurugu kuzuka kwenye mkutano wa Donald Trump mjini Chicago.

  JB Julius Bett
 918. GSM YAFADHILI: Kampuni ya GSM yakubali kujenga jengo la upasuaji na kufunga vifaa vyote muhimu Hosp. ya Mwananyamala Dar kufuatia ombi la DC Paul Makonda.

  JB Julius Bett
 919. UTEUZI: Rais John Magufuli ateua wakuu wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara; kati yao 13 wapya; Paul Makonda awa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Ikulu yathibitisha.

  JB Julius Bett
 920. KIAPO CHA WAKUU WA MIKOA: “Watanzania wafanye kazi, kama hawawezi kufanya kazi kwa kuambiwa, wafanye kazi kwa lazima” Rais John Magufuli

  JB Julius Bett
 921. “Nyinyi mna mamlaka ya kuwaweka watu ndani hata masaa 48 wekeni watu ndani ili wajue mnatakiwa kuheshimiwa.” Rais John Magufuli #kiapoChaWakuuWaMikoa

  JB Julius Bett
 922. Rais John Magufuli awaapisha wakuu 25 wa mikoa Ikulu, jijini Dar leo. Awapa siku 15 kuhakikisha wafanyakazi hewa wanaondolewa serikalini.

  JB Julius Bett
 923. MAAGIZO YA RAIS KWA WAKUU WA MIKOA:

  1. AGIZO LA JPM KWA MA- RC: Kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa kwenye maeneo yao ikiwamo kukabiliana na ujambazi

  2. AGIZO LA JPM KWA MA-RC: Kukabiliana na baa la njaa

  3. AGIZO LA JPM KWA MA-RC: Watu wafanye kazi na wasio na ajira watafutiwe kazi za kufanya kwa maaana “asiyefanya kazi na asile.”

  4. AGIZO LA JPM KWA MA-RC: Ametoa siku 15 kuhakikisha wafanyakazi hewa wanaondolewa serikalini kwa maana “wapo waliokufa, wamefungwa na waliofukuzwa kazi” lakini wanalipwa mishahara

  5. AGIZO LA JPM KWA MA-RC: Kusimamia kikamilifu walioko chini yao (wakuu wa wilaya, makatibu tarafa, kata) ili kuboresha utendaji na kuinua elimu

  JB Julius Bett
 924. VURUGU Z'BAR: Nyumba kadhaa ikiwemo ya Kamishna Polisi Z'bar H. Makame zaharibiwa baada ya kutokea mlipuko, Polisi yasema leo. Watu 31 mbaroni kwa tukio hilo.

  JB Julius Bett
 925. Bingwa wa zamani wa ngumi za kulipwa duniani, Mike Tyson amejitokeza hadharani kumuunga mkono bilionea wa New York, Donald Trump

  JB Julius Bett
 926. REDKNAPP ATUA JORDAN: Kocha wa zamani Tottenham Harry Redknapp akubali kuifundisha timu ya taifa Jordan kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Bangladesh na Australia.

  JB Julius Bett
 927. MRADI WA UMEME: Rais John Magufuli leo azindua ujenzi wa kituo cha kufua umeme wa Megawati 240 wa Kinyerezi II jijini Dar ambao utaigharimu serikali USD 344m.

  JB Julius Bett
 928. SIASA ZANZIBAR: Kaimu mkurugenzi wa uenezi CUF Hamad Masoud anashikiliwa na Polisi, naibu mkurugenzi haki za binadamu wa chama hicho, Pavu Abdallah athibitisha.

  JB Julius Bett
 929. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani Bukombe, imeagizwa kuchunguza uandikishaji wa wanafunzi waliohamia wakiwa darasa la tano, sita na saba katika shule za msingi ili kubaini iwapo walimu wakuu walijihusisha na rushwa.

  JB Julius Bett
 930. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa siku tano kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera kujieleza kwa kuuza bila kibali yaliyokuwa majengo ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wakimbizi (UHCR).

  JB Julius Bett
 931. MKATABA WA SHAMBA WA SERIKALI, MWEKEZAJI KUCHUNGUZWA

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo kupitia upya mkataba kati ya Serikali na mwekezaji katika shamba lenye hekta 36 wilayani Karagwe ili kubaini kama ametekeleza masharti.

  JB Julius Bett
 932. WAJASIRIAMALI KAHAMA WAKOPESHWA MAMILIONI

  Wanawake 10 wa kikundi cha ujasiriamali wamenufaika na mkopo wa Sh400 milioni uliotolewa kwa masharti nafuu na Benki ya CRDB Tawi la Kahama mkoani Shinyanga.

  Meneja wa tawi hilo, Luther Mneney amesema

  JB Julius Bett
 933. ZIARA YA PM: Waziri Mkuu Majaliwa ameagiza aliyekuwa mkurugenzi H/wilaya ya Ngara C. Ngudung, afisa ardhi E. Mponzi warudi wilayani humo kujibu tuhuma za kuuza ardhi za wananchi.

  JB Julius Bett
 934. Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimetaka jitihada za kutoa elimu bure ya msingi na sekondari ziendane na uboreshaji wa masilahi ya walimu.

  JB Julius Bett
 935. MWAPACHU ARUDI CCM: Balozi Juma Mwapachu leo ametangaza kurudi CCM, miezi mitano tangu akihame na kuunga mkono upinzani, asema alikosea kufanya maamuzi hayo.

  JB Julius Bett
 936. AJALI MBEYA: Watu wawili wafa, kumi wajeruhiwa leo huko Uyole baada ya basi la Ndenjela kuigonga Hiace, Afisa Uuguzi Hospitali ya Rufaa Mbeya amethibitisha.

  JB Julius Bett
 937. OPERESHENI TOKOMEZA 2: Serikali yawaambia wadau Arusha kuwa operesheni kukabili ujangili awamu ya 2 imesitishwa, Bodi ya Utalii kupewa uwezo wa kiintelejensia.

  JB Julius Bett
 938. MSAKO MIKOA 9: Maduka ya dawa 432 kati ya 648 yaliyokaguliwa mikoa 9 yamefungwa kwa sababu kadhaa ikiwemo kuuza dawa za serikali, Baraza la Famasia lasema leo.

  JB Julius Bett
 939. Walimu wa Shule ya Msingi Jitegemee katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani wamesema wanaomba msaada wa kujisaidia kwenye nyumba za majirani kwa kukosa vyoo.

  JB Julius Bett
 940. APR WATUA DAR: Mabingwa wa Rwanda APR watua Uwanja wa Ndege Dar leo jioni kwa ajili ya kuikabili Yanga Jumamosi katika mchezo wa marudiano Klabu Bingwa Afrika.

  JB Julius Bett
 941. ANAPA WAJA NA UTALII WA BAISKELI

  Hifadhi ya Taifa ya Arusha (Anapa) inatarajia kuanzisha utalii wa ndani wa baiskeli ili kuwavutia watalii zaidi kutoka ndani na nje ya nchi.

  Kaimu Mhifadhi Mkuu wa hifadhi hiyo, Neema Mollel amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari hifadhini hapo.

  JB Julius Bett
 942. Kampuni ya Saruji mkoani Mbeya ya Lafarge Tanzania, imetoa mifuko 1,000 ya saruji na vifaa vingine kwa Shule ya Sekondari ya Iyunga kwa ajiili ya ujenzi wa mabweni yaliyoungua moto hivi karibuni.

  JB Julius Bett
 943. KORTINI MWANZA: Muuguzi hosp. ya wilaya ya Misungwi Masalu Kangalukwi apandishwa kizimbani leo kwa kuomba rushwa ya Sh45, 000/-, kusababisha kifo cha kichanga.

  JB Julius Bett
 944. UHAMISHO UHAMIAJI: Maofisa uhamiaji wa mikoa 14 wahamishwa vituo vya kazi, wengine zaidi ya 200 kuhamishwa kama alivyoagiza waziri Kitwanga, Idara yasema leo.

  JB Julius Bett
 945. ROBO FAINALI UEFA: Wolfsburg v Real Madrid; Bayern Munich v Benfica; FC Barcelona v Atletico Madrid na PSG v Man City, droo iliyofanyika Uswis leo yaonyesha.

  JB Julius Bett
 946. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Morogoro, imeshindwa kuwafikia zaidi ya nusu ya wafanyabiashara wanaopaswa kutumia mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFD) kutokana na changamoto mbalimbali na baadhi yao kugoma kuzitumia.


  Meneja wa TRA mkoani humo, Phillip Kimune amesema leo mamlaka hiyo inajipanga kuchukua hatua kwa mfanyabiashara atakayekaidi agizo la kutumia mashine hizo.

  JB Julius Bett
 947. USAJILI WA SILAHA: Mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda atoa siku 90 kwa wamiliki wa silaha kusajili upya silaha zao kwani baada ya hapo msako mkubwa kuanza.

  JB Julius Bett
 948. 'MZUNGU WA UNGA': Kamanda wa Polisi Dar Simon Sirro asema kinara wa dawa za kulevya Hussein Halili amekamatwa baada ya mwenzake kukutwa na kilo moja ya heroini.

  JB Julius Bett
 949. WACHINA JELA: Mahakama Kisutu yawatupa Wachina 2 jela miaka 30 kila mmoja au wote kulipa faini ya Sh100.87 bilioni kwa kukutwa na vipande 726 vya meno ya tembo.

  JB Julius Bett
 950. DROO YA EUROPA: Liverpool kucheza dhidi ya Borussia Dortmund robo fainali michuano ya Europa. Braga vs Shakhtar Donetsk, Villarreal vs Sparta, Bilbao vs Sevilla

  JB Julius Bett
 951. RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT JOHN POMBE MAGUFULI AMEFANYA UTEUZI WA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI TATU ZA SERIKALI KWA MUJIBU WA MAMLAKA ALIYONAYO.

  --> Rais Magufuli amemteua Profesa Godius Kahyarara kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

  ---> Pia Rais Magufuli amemteua Dkt Ayub Rioba Chacha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

  ---> Rais amemteua Dkt Mussa Iddi Mgwatu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO).

  Uteuzi wa watendaji wote watatu umeanza mara moja

  JB Julius Bett
 952. UCHAGUZI Z’BAR: Mgombea wa urais wa TADEA, Juma Ali Khatibu amepiga kura mapema leo katika kituo cha Kiembe Samaki, Unguja kwenye uchaguzi wa marudio Zanzibar.

  JB Julius Bett
 953. UCHAGUZI Z’BAR: Mgombea urais wa Chama cha ADC, Hamad Rashid na mgombea wa Chama cha AFP Said Soud Said wamepiga kura katika kituo cha Wawi kisiwani Pemba.

  JB Julius Bett
 954. UCHAGUZI Z’BAR: Wananchi wakiwa katika foleni wakisubiri kupiga kura katika kituo cha Wawi B, kisiwani Pemba.

  JB Julius Bett
 955. SAHIHISHO: Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimempa jukumu la usemaji wa chama Christopher Ole Sendeka ambaye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), atamsadia majukumu ya usemaji Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye. Ole Sendeka hajateuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM.

  JB Julius Bett
 956. Mtaa wa Darajani na Soko kuu la Darajani maarufu kama Markiti maeneo ambayo huwa na msongamano wa watu leo hii biashara zimefungwa na kuna watu wachache wanaopita njia

  JB Julius Bett
 957. Zoezi la kuhesabu kura limeanza kwenye kituo cha Shule ya Msingi Kiembe Samaki.

  JB Julius Bett
 958. UCHAGUZI Z'BAR: Dr Ali Mohamed Shein aongoza matokeo ya awali ya urais majimbo ya Chonga kura 3598, Ziwani (2890), Wawi (4147), Ole (3818), Chake Chake (4551).

  JB Julius Bett
 959. Dk Ali Mohamed Shein ametangazwa mshindi wa urais wa Zanzibar kwa kupata asilimia 91 ya kura zote halali zilizopigwa katika uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20, 2016.

  JB Julius Bett
 960. #MabadilikoMaelezo Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof Elisante Gabriel amemteua Zamaradi Kawawa kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari - Maelezo.

  Kawawa ameteuliwa kushika wadhifa huo baada ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari – Maelezo, Assah Mwambene kuhamishiwa Wizara ya Mambo ya NJe Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa ambapo atapangiwa kazi nyingine.

  JB Julius Bett
 961. BUNGE KUVUNJWA: Waziri Mkuu wa Australia Malcolm Turnbull atishia kulivunja Bunge na kuitisha uchaguzi mpya endapo halitapitisha maboresho ya miswada 2 ya kazi.

  JB Julius Bett
 962. SARAH DUMBA AAGA DUNIA: Mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Mganga Mfawidhi Hospitali ya Wilaya ya Njombe ya Kibena, Dk Celina Nyoni athibitisha.

  JB Julius Bett
 963. MILIPUKO UBELGIJI: Watu wasiopungua 10 wafa, 30 wajeruhiwa baada ya milipuko 2 kutokea uwanja wa ndege wa Zaventen jijini Brussels. Safari za ndege zasitishwa.

  JB Julius Bett
 964. MEYA WA JIJI: Wajumbe 158 wamaliza kupiga kura leo mchana katika uchaguzi wa kumpata meya wa jiji la Dar. Kura zaanza kuhesabiwa muda huu.

  JB Julius Bett
 965. ZITTO AJIUZULU: Mbunge Zitto Kabwe (ACT) atangaza kujiuzulu ujumbe Kamati ya Huduma za Jamii baada ya wajumbe wake kutuhumiwa kwa rushwa. Ataka Bunge lichunguze

  JB Julius Bett
 966. MABADILIKO BUNGENI: Spika wa Bunge, Job Ndugai leo amefanya mabadiliko ya wajumbe kwenye baadhi ya Kamati za Kudumu za Bunge. Wenyeviti wa Kamati za Bunge waliovuliwa uongozi leo ni pamoja na Mary Mwanjelwa (Ardhi) Martha Mlata (Nishati) na Richard Ndassa (PIC).

  JB Julius Bett
 967. DIWANI JELA SINGIDA: Diwani kata ya Siuyu (Chadema), Jared Jastin ahukumiwa kifungo cha miezi 6 jela kwa kumzuia mkusanya ushuru na kuikosesha serikali mapato.

  JB Julius Bett
 968. RADI YAUA KAGERA: Watoto 2 wa familia moja wafa leo baada ya kupigwa na radi wakiwa nyumbani wilayani Ngara, uongozi wa Hospitali ya Murusagamba wathibitisha.

  JB Julius Bett
 969. Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akiwa amebebwa na madiwani na wafuasi wa Ukawa baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi uliofanyika Dar es Salaam jana. Picha na Said Khamis

  JB Julius Bett
 970. Wabunge waliobadilishwa kwenye kamati za kudumu za bunge

  JB Julius Bett
 971. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi (Dart), utaanza kufanyiwa majaribio ndani ya wiki moja

  JB Julius Bett
 972. UKAGUZI: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza mama lishe wakati alipotembelea soko la samaki la Feri jijini Dar es salaam jana. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  JB Julius Bett
 973. Viongozi wa Chama cha Akiba na Mikopo (Saccos) ya Sanya wamesomewa mashtaka 127 yakiwamo ya kughushi, wizi wa kuaminiwa na kula njama za kuiba Sh155 milioni.

  JB Julius Bett
 974. Ng’ombe wakiwa katika machinjio ya Vingunguti jijini Dar es Salaama baada ya wafanyabiashara kugoma kuchinjwa jana kwa lengo la kushinikiza kufunguliwa kwa machinjio ya Ukonga ili kupunguza msongamano machinjioni hapo. Picha na Kalunde Jamal

  JB Julius Bett
 975. AJALI TABORA: Watu kadhaa wajeruhiwa baada ya basi la Super Sami toka Mwanza kwenda Dar kupinduka Igogo, Igunga wakati likikwepa ng’ombe. Taarifa zaidi kukujia.

  JB Julius Bett
 976. ASKARI WASIMAMISHWA: N/Waziri wa Mambo ya Ndani H. Masauni aagiza kusimamishwa kazi askari 3 wa Jeshi la Zimamoto kwa tuhuma za wizi kwenye uwanja wa ndege Dar.

  JB Julius Bett
 977. JELA MIAKA 50: Korti wilayani Misungwi leo imewahukumu watu watano kifungo cha miaka 50 jela kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya wizi kwa kutumia silaha.

  JB Julius Bett
 978. KUAPISHWA RAIS MTEULE ZANZIBAR: Rais mteule Dkt Ali Mohamed Shein ameapishwa kwenye uwanja wa Amaan leo kuwa rais wa saba wa Serikali ya Mapindizi ya Zanzibar.

  JB Julius Bett
 979. KASHFA UVUNAJI WA MAGOGO: Waziri wa Maliasili J. Maghembe asimamisha kazi wakurugenzi 4 wa Huduma za Misitu leo kwa uvunaji na usafirishaji holela wa magogo.

  JB Julius Bett
 980. HOTUBA YA RAIS SHEIN: Rais wa Z'bar Dkt Ali Mohamed Shein amesema Serikali yake italinda haki za raia, kuhimiza uwajibikaji na usawa pasipo kubagua mtu yeyote.

  JB Julius Bett
 981. BALAA MALIASILI: Waziri Maghembe amsimamisha kazi leo Mkurugenzi Msimamizi Wanyamapori Charles Mlokozi kwa kutoa vibali vya kusafirisha tumbili kwenda Albania.

  JB Julius Bett
 982. NYONGEZA VITI MAALUM: Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewapitisha Ritha Kabati na Oliver Semuguru wa Chama cha Mapinduzi na Lucy Owenya kutoka Chadema kuwa wabunge Viti Maalum, Mwenyekiti Jaji Damian Lubuva atangaza leo jijini Dar es Salaam.

  JB Julius Bett
 983. MGOMO ARUSHA: Wafanyakazi kiwanda cha bidhaa za plastiki, Best Pack jijini Arusha wagoma leo wakiudai uongozi mishahara ya Machi, makato NSSF na kiinua mgongo baada ya kuachishwa kazi.

  JB Julius Bett
 984. Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akimuombea dua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipomtembelea kiongozi huyo wa dini leo. Makonda ameanza ziara ya kuwatembelea viongozi wa dini na wastaafu jijini ili kupata ushauri mbalimbali.

  JB Julius Bett
 985. UGAIDI: Wanamgambo 60 wa kundi la Kiislamu la IS wauawa kaskazini mwa Sinai, Jeshi nchini Misri laeleza leo.

  JB Julius Bett
 986. NMB NGARA: Wateja Benki ya NMB Ngara wajaa viwanja vya benki hiyo baada ya kukosa huduma za kipesa kupitia ATM, Mawakala, M-Pesa tangu jana, uongozi uko kimya.

  JB Julius Bett
 987. VITI MAALUM Z’BAR: Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yatangaza majina 22 ya wajumbe wa viti maalum.

  JB Julius Bett
 988. IBADA YA PASAKA: Askofu Valentino Mokiwa aongoza Ibada ya Pasaka kitaifa katika Kanisa la Mt. Albano Upanga jijini Dar, Mkuu wa Mkoa Paul Makonda naye ahudhuria

  JB Julius Bett
 989. IBADA YA PASAKA: Askofu Mokiwa asema chuki, makundi, biashara, uchochezi, kusemana, wivu kati ya wachungaji, mapadre, maaskofu na waumini yanalibomoa kanisa.

  JB Julius Bett
 990. AJALI YAUA IRINGA: Watu 6 wamekufa, 38 wajeruhiwa baada basi la Lupondije walilokuwa wakisafiria (Mwanza-Iringa) kupinduka Mlima Ipogoro, Iringa, polisi waeleza

  JB Julius Bett
 991. GALLAWA AAPISHWA: Rais John Magufuli leo amemwapisha Mkuu wa Mkoa mpya wa Songwe, Chiku Gallawa ambaye hakuwepo wakati wakuu wa mikoa mingine wakiapishwa.

  JB Julius Bett
 992. RIPOTI YA CAG: Rais Magufuli leo amepokea taarifa ya ukaguzi wa hesabu za serikali kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad.

  JB Julius Bett
 993. NDEGE YATEKWA: Ndege ya Shirika la Egyptair ikiwa na abiria 80 yatekwa mara baada ya kutoka Alexandria ikielekea Cairo, Misri. Yalazimika kutua Larnaca, Cyprus.

  JB Julius Bett
 994. TRILIONI YAYEYUKA: TZ yakosa karibu Sh1trilioni za miradi ya maendeleo baada ya MCC USA kuamua kutoshirikiana na serikali. Uchaguzi Z'bar miongoni mwa sababu.

  JB Julius Bett
 995. Imebainika kwamba polisi waliokufa, wastaafu na kufutwa kazi bado wanaendelea kulipwa mishahara na marupurupu kila mwezi kutoka Serikali ya Kenya.

  JB Julius Bett
 996. AL SHABAAB 100 WAUAWA KWENYE MAPIGANO YA SIKU NNE SOMALIA

  Galmudug. Kiongozi wa jimbo la Galmudug nchini Somalia amesema wanajeshi wa jimbo hilo wamewaua zaidi ya wapiganaji 100 wa al-Shabab kwenye mapigano yaliyodumu siku nne.

  JB Julius Bett
 997. UDHALILISHAJI MTWARA: Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara Henry Mwaibambe asema watu 2 wanaotuhumiwa kumpiga daktari hospitali ya mkoa wamekamatwa kuamkia leo wakitoroka nchi, 3 wasakwa. Waziri wa Afya Ummy Mwalimu awasili hospitali hiyo na kuzungumza na madaktari.

  JB Julius Bett
 998. Wagonjwa wakiwa wamekaa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara ya Ligula leo baada ya wahudumu kusitisha huduma.

  JB Julius Bett
 999. Wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara ya Ligula leo baada ya wahudumu kusitisha huduma.

  JB Julius Bett
 1000. PICHA: Wagonjwa wakiwa wamekaa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara ya Ligula leo baada ya wahudumu kusitisha huduma.

  JB Julius Bett
 1001. Baadhi ya watoa huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara ya Ligula wakishangilia baada ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kuwasili hospitalini hapo. (Picha na Haika Kimaro)

  JB Julius Bett
 1002. KUPIGWA KWA DAKTARI MTWARA:

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu (aliyesimama) akizungumza na wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara ya Ligula (hawako pichani) kushoto ni katibu tawala mkoa,Alfred Luanda, Mganga mkuu wa mkoa,Shahibu Maarifa.Kulia ni kaimu mkuu wa Mkoa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Mtwara,Fatuma Ally.(Picha na Haika Kimaro)

  JB Julius Bett
 1003. Waziri wa Afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto,Ummy Mwalimu (aliyesimama) akizungumza na wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mtwara ya Ligula (hawako pichani) kushoto ni katibu tawala mkoa,Alfred Luanda,mganga mkuu wa mkoa,Shahibu Maarifa.Kulia ni kaimu mkuu wa Mkoa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Mtwara,Fatuma Ally akifuatiwa na Mganga mkuu wa serikali,Prof Mohammad Kambi. (Picha na Haika Kimaro)

  JB Julius Bett
 1004. BURUNDI: Serikali ya Burundi inatarajia kuiburuza mahakamani Rwanda kwa madai ya kuwaunga mkono waasi na kusababisha mauaji ya raia wake wasiokuwa na hatia kutokana na machafuko yanayoendelea kutokea nchini humo.

  Akizungumza na Shirika la DW la Ujerumani, Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Alain-Aime Nyamitwe amesema kila nchi ina haki ya kwenda mahakamani iwapo itaona uhuru wake unakiukwa.

  Amesema Burundi ina ushahidi unaoonyesha kuwa Rwanda imekiuka uhuru na utu wa raia wake.

  JB Julius Bett
 1005. Waziri wa Tamisemi George Simbachawene asema kupitia Clouds TV leo asubuhi kwamba ajira za walimu zitatoka baada ya bajeti kupita kuepuka mishahara kucheleweshwa.

  JB Julius Bett
 1006. MATATANI KWA 'KUBETI': FA ya England leo yamfungulia beki wa Man City Martin Demichelis mashtaka 12 yanayohusiana na 'kubeti' kati ya Januari 22-28, mwaka huu.

  JB Julius Bett
 1007. MAGARI YA TFF YAKAMATWA: Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yakamata magari matano ya TFF kutokana na malimbikizo ya kodi ya Sh1.118bn, TRA imethibitisha leo.

  JB Julius Bett
 1008. KORTINI MWANZA: Muuguzi Amon Shija apandishwa kizimbani leo kwa kuomba rushwa ya Sh100, 000 ili amhudumie mjamzito baada ya mimba kuharibika.

  JB Julius Bett
 1009. WABUNGE KORTINI: Taasisi ya Kuzuia, Kupambana na Rushwa (Takukuru) leo imewafikisha mahakama ya Kisutu wabunge 3 inaowatuhumu kwa rushwa, taarifa zaidi kukujia.

  JB Julius Bett
 1010. BEI YA UMEME YASHUKA: Bei kwa watumiaji wadogo ni Sh100/- kwa Uniti. Watumiaji wa Kati ni Sh292/- toka Sh298/-, wafanyabiashara wadogo ni Sh195/- toka Sh200/-.

  JB Julius Bett
 1011. BEI YA UMEME: Bei kwa wafanyabiashara wa Kati ni Sh157/- toka Sh159/-, wanaonunua kwa wingi (Bulk) ni Sh152/- toka Sh156/-. Service Charge yafutwa kuanzia leo.

  JB Julius Bett
 1012. NDASSA NAYE KORTINI: Mbunge wa Sumve Richard Ndassa apandishwa kizimbani mahakama ya Kisutu leo akituhumiwa kuomba rushwa ya Sh30m akiwa kwenye Kamati za Bunge.

  JB Julius Bett
 1013. KIZIMBANI MWANZA: Maofisa 2 TASAF, watumishi 2 wa wilaya wafikishwa mahakama ya Misungwi leo, wasomewa mashtaka ya kudanganya kaya masikini na kujipatia Sh1.2m.

  JB Julius Bett
 1014. Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TDFA), imeyafunga machinjio ya Manispaa ya Tabora kwa muda usiojulikana kutokana na kukithiri kwa uchafu.

  JB Julius Bett
 1015. KIWANDA CHAFUNGWA: Kiwanda cha Mount Meru Miller Ltd cha Bunda kimefungwa, chapigwa faini Sh 12m kwa kukiuka sheria ya mazingira, NEMC Kanda ya Ziwa waeleza.

  JB Julius Bett
 1016. BOMOABOMOA PWANI: Wakala wa Taifa wa Barabara (Tanroads) wabomoa leo nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya barabara mjini Kibiti ikiwemo ya mbunge Ally Ungando.

  JB Julius Bett
 1017. MATOKEO EPL: Chelsea yaifunga Aston Villa bao 4-0 huko Villa Park leo na kukwea hadi nafasi ya tisa kwenye msimamo. Mechi nyingine Saba kupigwa baadaye leo.

  JB Julius Bett
 1018. UPANGAJI MATOKEO: Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu TFF Jerome Msemwa amesema hukumu kwa timu za FDL zinazotuhumiwa kwa upangaji matokeo itatolewa kesho.

  JB Julius Bett
 1019. MECHI YA KIRAFIKI: Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) yawafunga bao 2-1 wenzao wa umri huo kutoka Misiri. Timu hizo zitarudiana Jumanne.

  JB Julius Bett
 1020. MATOKEO VPL: Mtibwa Sugar yaifunga Mwadui 2-1 Kambarage Stadium mjini Shinyanga. Mbeya City 4-0 Coastal Union. Mechi nyingine Saba zinatarajiwa kupigwa kesho.

  JB Julius Bett
 1021. MAFURIKO DODOMA: Abiria wanaosafiri kati ya Dar es Salaam na Kanda ya Ziwa wakwama eneo la Pandambili Dodoma baada ya maji kukatiza barabara kwa kasi.

  JB Julius Bett
 1022. KIKAO CHAVUNJIKA: Kikao cha Baraza la Madiwani jijini Tanga chavunjika baada ya Madiwani wa CUF kutomtambua Meya Suleiman Mustapha kwa madai hakushinda kihalali

  JB Julius Bett
 1023. KESI YA UBUNGE: Agustino Mrema wa TLP ameondoa mahakamani kesi ya kupinga ushindi wa ubunge wa James Mbatia Jimbo la Vunjo baada ya kukubaliana naye.

  JB Julius Bett
 1024. SHAW AREJEA: Beki wa kushoto wa Manchester United Luke Shaw leo arejea uwanja wa mazoezi Carrington kwa mara ya kwanza tangu Septemba, 2015 alipovunjika mguu.

  JB Julius Bett
 1025. AJALI MWANZA: Watu 2 wathibitika kufa, 18 wajeruhiwa eneo la Ukiliguru, nje kidogo ya jiji la Mwanza baada ya basi la Dar Lux kupinduka kuamkia leo.

  JB Julius Bett
 1026. AJALI MWANZA: Vifo ajali ya Dar Lux vyafikia 3, majeruhi 8 wahamishiwa Bugando Hospital huku 20 wakiruhusiwa, Polisi yathibitisha. Mwendokasi chanzo cha ajali.

  JB Julius Bett
 1027. ----> Hotuba ya Rais Shein katika Baraza la Wawakilishi

  VIPAUMBELE VYA SHEIN

  .. Kuboresha barabara visiwani Zanzibar na kuwa ya njia nne (4 ways)

  …Kukabiliana na migogoro ya ardhi, atahadharisha watendaji kuhakikisha kero hii inatatuliwa

  …Kukabiliana na uharibifu wa mazingira; kukata miti hovyo, usafi wa bahari

  …Kuinua kilimo hususani zao la karafuu kwa kugawa miche ya zao hilo bure ili hatimaye kuinua pato la nchi na kuinua maisha ya Wazanzibar

  …Kukuza utalii kwa kutoa elimu ya tasnia hiyo kwa kiwango cha shahada itakayotolewa na Chuo Kikuu cha SUZA

  …Kuongeza fursa za ajira kwa kupanua sekta ya viwanda na utalii. Saccos kuimaimarishwa

  …Kuimarisha maslahi na mishahara ya wafanyakazi ILA waongeze ufanisi katika uzalishaji, nidhamu

  JB Julius Bett
 1028. HOTUBA YA SHEIN: Rais Shein asema ndani ya Baraza la Wawakilishi kuwa hatoteua Makamu wa Kwanza wa Rais kwa kuwa hakuna chama cha upinzani kilichokidhi matakwa ya kikatiba.

  JB Julius Bett
 1029. HOTUBA YA SHEIN: Rais Shein apiga marufuku safari nje ya Z’bar zisizo za lazima na kuondoa posho wakati wa muda wa kawaida wa kazi kupunguza matumizi ya serikali. Azindua rasmi Baraza la Wawakilishi.

  JB Julius Bett
 1030. WAFANYAKAZI HEWA: Jumla ya wafanyakazi hewa 4,317 wamebainika katika mamlaka za mikoa nchini, Waziri wa Utumishi A. Kairuki asema leo. Zoezi bado laendelea.

  JB Julius Bett
 1031. Wakazi wanne wa Kijiji cha Kitawasi wilayani Tarime Mkoa wa Mara, akiwamo mama na mwanawe wa miaka 18 wamefariki dunia baada ya kuugua kipindupindu.

  JB Julius Bett
 1032. UFAFANUZI: Wafanyakazi hewa waliobainika toka mwezi Januari hadi jana ni 7795 na si 4317, waisababishia serikali hasara ya Sh7.5bn, Waziri A. Kairuki asema leo.

  JB Julius Bett
 1033. AL AHLY WATUA DAR: Timu ya Al Ahly kutoka Misri yawasili uwanja wa ndege Dar leo alfajiri kwa ajili ya kuikabili Yanga Jumamosi mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

  JB Julius Bett
 1034. KIFUSI CHAFUKIA 4: Watu 4 wafukiwa na kifusi Mkwamani, Kawe Dar baada ya udongo kuporomoka leo asubuhi. Zimamoto, wananchi waendelea kutafuta miili

  JB Julius Bett
 1035. MWELEKEO WA BAJETI: Serikali kutumia Sh29 trilioni kwenye Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/17 kutoka Sh22 trilioni mwaka wa Fedha 2015/16, Waziri P. Mpango asema.

  JB Julius Bett
 1036. BOSI TFF ANG'ATUKA: Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano Shirikisho la Soka nchini (TFF) Martin Chacha amejiuzulu kwa sababu za kifamilia na kikazi, TFF yathibitisha.

  JB Julius Bett
 1037. MWALIMU MBARONI SINGIDA: Takukuru inamshikilia mwalimu mkuu shule ya msingi Manispaa ya Singida kwa tuhuma za kuomba rushwa ya ngono ili atoe barua ya uhamisho.

  JB Julius Bett
 1038. NGAWAIYA KORTINI DAR: Aliyekuwa mbunge Moshi Vijiji, T. Ngawaiya afikishwa Kisutu akituhumiwa kutumia wakandarasi wasiosajiliwa kujenga hoteli ya Sh500m Magomeni

  JB Julius Bett
 1039. Rais John Magufuli na Rais Paul Kagame wazindua rasmi daraja la Rusumo, mpakani mwa Tanzania na Rwanda.

  JB Julius Bett
 1040. UMEYA TANGA: Mgogoro wa umeya umekwamisha maendeleo Tanga, serikali inapaswa kuingilia kati kuutatua, Naibu Katibu Mkuu CUF-Bara Magdalene Sakaya asema leo Dar.

  JB Julius Bett
 1041. TZ YASHUKA FIFA: Tanzania yashuka kwa nafasi 5, yawa ya 130 viwango Fifa vilivyotolewa leo. Uganda ya 72, Rwanda 87, Kenya 115, Burundi 122. Argentina kileleni.

  JB Julius Bett
 1042. #SIMIYU: Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Simiyu, imeokoa Sh63.6 milioni zilizorejeshwa na baadhi ya watumishi wilayani Bariadi waliobainika kuzitumia kinyume cha sheria.

  JB Julius Bett
 1043. #BUKOBA: Kuanza kwa msimu wa senene maeneo ya Mkoa wa Kagera, umeanza kuwatia hofu wafanyabiashara wa samaki Manispaa ya Bukoba, wakihofia mauzo kupungua.

  JB Julius Bett
 1044. #MUSOMA: Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Manispaa ya Musoma mkoani Mara kimesema walimu wanaidai Serikali zaidi ya Sh257 milioni za malimbikizo ya posho, uhamisho, nyongeza ya mishahara na stahiki mbalimbali.

  JB Julius Bett
 1045. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella ametoa siku 38 kwa uongozi wa Wilaya ya Misungwi kukamilisha mchakato wa ujenzi wa gereza la wilaya hiyo.

  JB Julius Bett
 1046. #KYELA: Serikali imesema iko katika hatua ya mwisho za kukamilisha utengenezaji wa mradi wa meli tatu utakaogharimu Sh27 bilioni.

  JB Julius Bett
 1047. DAR ES SALAAM: Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imetaja mambo saba yatakayofanikisha ndoto ya Rais John Magufuli ya uchumi wa viwanda ikiwamo ya kuwekeza katika sayansi na teknolojia.

  JB Julius Bett
 1048. Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dk Joel Bendera amemsimamisha kazi Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ Filex Mabula akidaiwa kusababisha upotevu wa zaidi ya sh600 milioni na ubadhirifu wa fedha.

  JB Julius Bett
 1049. TANZIA: Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Christina Lissu Mughwai amefariki dunia leo Hosp. ya Aga Khan Dar akitibiwa kansa, familia yathibitisha.

  JB Julius Bett
 1050. UBUNGE NYAMAGANA: Korti Kuu Mwanza leo yaifuta kesi ya kupinga matokeo ya ubunge Nyamagana iliyofunguliwa na Ezekia Wenje kwa kushindwa kuthibitisha madai yake.

  JB Julius Bett
 1051. KANE, RANIERI WANG'ARA: Straika Tottenham Harry Kane, meneja wa Leicester City Claudio Ranieri watangazwa kuwa mchezaji bora na kocha bora kila mmoja wa Machi.

  JB Julius Bett
 1052. MCHINA KORTINI: Mfanyabiashara Mchina Huifang Ma afikishwa kortini Ilala, Dar; ashtakiwa kwa kutotumia mashine za EFD, kutojisajili VAT. Polisi yasaka mwingine.

  JB Julius Bett
 1053. BOSI MPYA HAI: Rais Magufuli amemteua Gelasius Byakanwa kuwa mkuu mpya wa Wilaya ya Hai kujaza nafasi ya Antony Mtaka aliyeteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu.

  JB Julius Bett
 1054. WATUMISHI HEWA WAMPONZA KILANGO: Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela na Katibu Tawala wa mkoa huo kwa kutoa taarifa za uongo kuwa mkoa huo hauna watumishi hewa baada ya tume nyingine kuchunguza na kubaini uwepo wa watumishi hewa 45.

  JB Julius Bett
 1055. SEIF AONDOLEWA ESKOTI: Aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad aondolewa eskoti na kubaki na gari moja tu, CUF Z’bar wathibitisha.

  JB Julius Bett
 1056. BUNGE LABANA MATUMIZI: Bunge lamkabidhi Rais Magufuli Sh 6bn baada ya kubana matumizi, zitatumika kutengeneza madawati, kila mbunge wa Jimbo kupata madawati 600

  JB Julius Bett
 1057. ASKOFU AFARIKI: Askofu mstaafu Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Askofu Mathias Issuja (87) amefariki dunia kuamkia leo hospitalini Mt. Gaspar Itigi, TEC yathibitisha.

  JB Julius Bett
 1058. AJALI LINDI: Watu 20 wajeruhiwa leo baada ya basi la Halifa kutoka Liwale kwenda Mtwara kupinduka Nangoo-Masasi, Polisi yathibitisha. Wakimbizwa Ndanda Mission.

  JB Julius Bett
 1059. BUNDI NDANDA: Wachezaji wa Ndanda FC watishia kugoma wakidai kutolipwa mishahara tangu Machi, Katibu Selemani athibitisha. Asema Sh13m zahitajika kuokoa jahazi.

  JB Julius Bett
 1060. MGOMO MWANZA: Wafanyakazi 100 wa kampuni ya ujenzi ya CRJE wagoma leo jijini Mwanza wakishinikiza kulipwa stahiki zao, wamtaka Rais John Magufuli kuingilia kati.

  JB Julius Bett
 1061. Wakulima wa Wilaya za Misungwi na Sengerema mkoani Mwanza wametakiwa kuacha tabia ya kuuza mazao shambani ili kuepuka kukumbwa na njaa.

  JB Julius Bett
 1062. Mkazi wa wilayani Mbogwe Mkoa wa Geita, Manyanda Kumalilwa (22) na mtoto wake aliyekuwa na miezi tisa, Rosemary Manyanda wamefariki dunia kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba wakati wakiwa wamelala.Ofisa Mtendaji wa Kata ya Masumbwe, Alex Makoye amesema ukuta huo umeanguka wakati mvua kubwa ikinyesha jana usiku.

  JB Julius Bett
 1063. KUBENEA AHUKUMIWA: Korti ya Kisutu yampa Mbunge wa Ubungo S.Kubenea adhabu ya kutojihusisha na kutoa lugha chafu kwa miezi 3 kwenye kesi dhidi ya RC, P. Makonda

  JB Julius Bett
 1064. TAHADHARI KUTOKA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA: Vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa Leo 13 Aprili, 2016 hadi 16 Aprili, 2016

  JB Julius Bett
 1065. Vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24 vinatarajiwa Leo 13 Aprili, 2016 hadi 16 Aprili, 2016

  JB Julius Bett
 1066. ANGALIZO KUNYESHA KWA MVUA KUBWA: Mikoa ya Tanga,Dar es salaam,Pwani na Morogoro pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba wanashauriwa kuchukua tahadhari na hatua stahiki.

  MAELEZO YA ZIADA: Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo kila itakapobidi.

  JB Julius Bett
 1067. MOROGORO: Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero inatarajia kufanya mnada wa kuuza magari saba kwa siku mbili kuanzia kesho kutwa Jumamosi hadi Jumapili.

  Watakaoshinda kwenye zabuni hiyo watapaswa kulipa asilimia 25 papo hapo na itakayobaki ndani ya wiki mbili.

  Watakaoshindwa kulipa ndani ya muda huo, watakuwa wamepoteza sifa ya ununuzi, hivyo itauzwa tena na hawatarejeshewa asilimia 25 waliolipia awali.

  JB Julius Bett
 1068. SIMU MPYA YA SMART YAINGIA SOKONI TANZANIA: Ikiwa imesalia miezi miwili kabla ya Mamlaka ya Mawasiliano TCRA kuzima simu feki, aina mpya ya simu smart imeingia sokoni kukidhi matakwa ya Watanzania.


  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Amoli Group, Vikash Shah amesema bidhaa hiyo imetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu iliyozingatia viwango vya ubora. Amesema ni simu itakayomsaidia Mtanzania.

  JB Julius Bett
 1069. BATILDA KURUDI: Balozi wa Tanzania huko Japan Dk Batilda Burian kurudi nchini muda wowote baada ya kukwama kutokana na ukata, Wizara ya Mambo ya Nje yathibitisha leo jijini Dar es Salaam.

  JB Julius Bett
 1070. Kamati ya Miundombinu imeitaka Serikali kuchukua hatua kwa wote waliohusika na kufungwa kwa flowmeter za Mamlaka ya Bandari TPA.

  Kadhalika Kamati hiyo imeridhishwa na kiwango cha bajeti ya 4 trilioni zilizotengwa kwa ajili ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Kadhalika Wameitaka iongeze upembuzi katika uteuzi wa watendaji wakuu kwenye idara na taasisi ili kuzuia kupata viongozi wasio waaminifu ambao wamekuja wakifanya au kuruhusu ufisadi wa kutafunwa kwa fedha za Serikali hivyo.

  JB Julius Bett
 1071. DARAJA LA KIGAMBONI KUANZA KAZI WIKI IJAYO

  Rais John Magufuli Jumanne ya Aprili 19, 2016 atafungua rasmi Daraja la Kigamboni lenye urefu wa mita 680 na barabara unganishi (approach roads) upande wa Kurasini na Kigamboni.

  Rais Magufuli pia ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya juu (Flyover) katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela (Tazara Flyover) siku ya Jumamosi ya tarehe 16, Aprili 2016, Taarifa ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imesema leo.

  JB Julius Bett
 1072. USALAMA BARABARANI: Wanafunzi Shule ya Msingi Mzambarauni, Ukonga Dar wafunga barabara, washinikiza matuta kuwekwa eneo hilo baada ya mwenzao kufa kwa ajali jana

  JB Julius Bett
 1073. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli ametengua uteuzi wa Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Gabriel Nderumaki.

  Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 14 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, taarifa hiyo kutoka Ikulu imeeleza kuwa Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia tarehe 18 Machi, 2016.

  Kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Tuma Abdallah kukaimu nafasi hiyo.


  Tuma Abdallah ni Mhariri Mtendaji Msaidizi wa Magazeti ya Serikali (TSN)

  JB Julius Bett
 1074. Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amevunja bodi ya Soko la Machinga Complex lililopo Ilala Mchikini Dar es Salaam na kulikabidhi kwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.

  Akizungumza leo katika mkutano wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini (JWT), Simbachawene amesema wazo la kuanzishwa kwa soko hilo lilikuwa zuri lakini Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeshindwa kulitekeleza.

  Jengo hilo lilikamilika kujengwa mwaka 2010 likiwa na uwezo wa kuchukua wafanyabiashara 4206, lakini Waziri Simbachawene alisema limeishia kuwa makazi ya popo

  JB Julius Bett
 1075. SHERIA YA MAKOSA MTANDAONI: Kijana Izack Emil afikishwa mahakamani Arusha leo asubuhi kwa tuhuma za kumtukana Rais Magufuli kupitia ukurasa wake wa Facebook.

  JB Julius Bett
 1076. ZIARA YA RAIS KIIR: Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir awasili Dar asubuhi, atarajiwa kusaini mkataba wa nchi yake kujiunga EAC iliyo chini ya M/kiti Dk. Magufuli.

  JB Julius Bett
 1077. MWANACHAMA MPYA: Sudan Kusini yapokelewa rasmi kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya Rais Kiir kusaini mkataba wa kujiunga leo chini ya M/kiti Dk Magufuli.

  JB Julius Bett
 1078. KADA CHADEMA AHAMA: Aliyekuwa M/kiti wa Chadema mkoa wa Mwanza Mhandisi Adrian Tizeba leo ajiunga rasmi na CCM. Apokelewa katika tawi la Lugata, Sengerema.

  JB Julius Bett
 1079. DROO YA UEFA: Manchester City itacheza na Real Madrid katika nusu fainali ya UEFA wakati Bayern Munich watakabiliana na Atletico Madrid ya Hispania katika hatua hiyo.

  JB Julius Bett
 1080. ‘WATUMISHI HEWA’ KORTINI:Mhasibu H/shauri Singida Imani Abdul (44) afikishwa kortini leo akituhumiwa kupokea Sh29.4m za wafanyakazi hewa 57 tangu 2013 hadi 2014

  JB Julius Bett
 1081. OFISA ATIMULIWA MARA: DC Tarime Glorius Luoga leo amfuta kazi ofisa mifugo Theodul Akaro kwa madai ya kutoza wachinjaji hadi Sh7,500 badala Sh1,500 kwa ng'ombe mmoja.

  JB Julius Bett
 1082. MACHINJIO VINGUNGUTI YAFUNGULIWA

  Mawaziri wawili wenye dhamana ya afya na ufugaji, Ummy Mwalimu na Mwigulu Nchemba, wameruhusu machinjio ya Vingunguti kufanya kazi kwa muda kuanzia leo usiku ili kukidhi haja ya upatikanaji nyama.

  Hatua hiyo imekuja baada ya mawaziri hapo kutembelea eneo hilo, ikiwa ni zaidi ya mwezi mmoja tangu wafungie machinjio hayo kwa kutofuata kanuni za kiafya.

  JB Julius Bett
 1083. MWENGE: Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan awasili Uwanja wa Jamhuri Morogoro kwa ajili ya kuzindua mbio za Mwenge wa Uhuru.

  JB Julius Bett
 1084. MOTO CHALINZE: Moto wateketeza moja ya mabweni katika shule ya Sekondari Bwilingu Halmashauri ya Chalinze, M/Kiti wa Halmashauri Said Zingatimu athibitisha.

  JB Julius Bett
 1085. UTEUZI: Rais John Magufuli amemteua Mathias Chikawe kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan, Ikulu yaeleza.

  JB Julius Bett
 1086. DAWA ZA KULEVYA: Mtanzania Musa Yange, Mzambia Zuber Nyirenda wakamatwa nchini Botswana wakituhumiwa kusafirisha tembe 141 za dawa za kulevya aina ya Mandrax.

  JB Julius Bett
 1087. UZINDUZI DARAJA KIGAMBONI: Serikali ilianza usanifu miaka ya 1970

  JB Julius Bett
 1088. UZINDUZI DARAJA KIGAMBONI: 1982 mkandarasi alipatikana kwa gharama ya Sh252m, serikali ikaachana na mradi huo kwa sababu za ukosefu wa fedha

  JB Julius Bett
 1089. UZINDUZI DARAJA KIGAMBONI: 2002 walionyesha nia ya kujenga daraja la Kigamboni kupitia mfumo wa PPP. Wakawasilisha andiko serikalini

  JB Julius Bett
 1090. UZINDUZI DARAJA KIGAMBONI: Daraja limeshikiliwa na nyaya (cables) zinazounganisha na nguzo. Haliwezi kubomoka kwa miaka 100

  JB Julius Bett
 1091. UZINDUZI DARAJA KIGAMBONI: Daraja hilo litapunguza adha ya usafiri kwa wakazi wa Kigamboni

  JB Julius Bett
 1092. Daraja la Kigamboni litakuwa chini ya NSSF, sekta binafsi hadi serikali itakapokabidhiwa, Waziri wa Uchukuzi Ngonyani asema. Rais Magufuli kuzindua punde

  JB Julius Bett
 1093. UZINDUZI DARAJA KIGAMBONI: Mwalimu Nyerere alianza mkakati ujenzi Daraja la Kigamboni 1979 ila ilishindikana kutokana na uhaba wa fedha, Rais Magufuli asema

  JB Julius Bett
 1094. UZINDUZI DARAJA KIGAMBONI: Rais Magufuli asema Daraja la Kigamboni lenye urefu wa mita 980 ni la kipekee Afrika Mashariki

  JB Julius Bett
 1095. UZINDUZI DARAJA KIGAMBONI: Rais Magufuli apendekeza daraja la Kigamboni lililogharimu Sh254bn liitwe "Daraja la Nyerere" kama ishara ya kuutambua mchango wa Hayati Mwalimu Nyerere.

  JB Julius Bett
 1096. UZINDUZI DARAJA KIGAMBONI: Rais Magufuli asema watakaopita daraja la Kigamboni kwa bajaji, baiskeli, magari lazima walipe na watembea kwa miguu watapita bure.

  JB Julius Bett
 1097. UZINDUZI DARAJA KIGAMBONI: Rais Magufuli amewataka wananchi kulitumia daraja hilo kujinasua kiuchumi. Ataka watu wafungue maduka kando ya barabara bila kuvamia hifadhi ya barabara

  JB Julius Bett
 1098. MKURUGENZI JIJI ASIMAMISHWA: Rais Magufuli amsimamisha kazi mkurugenzi Dar Wilson Kabwe anayetuhumiwa kuingia mikataba iliyosababisha hasara ya zaidi ya Sh3bn.

  JB Julius Bett
 1099. UNYAMA RUFIJI: Polisi wanamshikilia Afisa Tarafa ya Kibiti, Suleimani Mpangile kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la 6 wa Shule ya Msingi Kitundu, kufikishwa kortini kesho.

  JB Julius Bett
 1100. BUNGE LA BAJETI 2016/17: Serikali yawasilisha Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano (2016/17-2020/21) bungeni mjini Dodoma leo asubuhi.

  JB Julius Bett
 1101. AJALI DAR: Gari aina ya Hiace ikiwa na watu 2 kwenye kivuko kuelekea Kigamboni yatumbukia Bahari ya Hindi. Mwili wa dereva wapatikana, Zimamoto wanaendelea kuutafuta mwili wa mwanamke mmoja.

  JB Julius Bett
 1102. WAHAMIAJI HARAMU: Wachina 9 mbaroni kwa kufanya kazi Kyerwa bila vibali halali, Mkuu Uhamiaji Kagera A. Towo athibitisha. Warundi 353 na Wanyarwanda 137 wanaswa.

  JB Julius Bett
 1103. KESSY STOP: Simba yamfungia Hassan Kessy kutocheza mechi 5 kwa kumchezea rafu Christopher Edward wa Toto na kutolewa kwa kadi nyekundu, msemaji Haji Manara athibitisha.

  JB Julius Bett
 1104. AJALI DAR: Mwili wa mwanamke,Nice Karago umepatikana baada ya Hiace kutumbukia Bahari ya Hindi ikielekea Kigamboni mapema leo, jitihada za kuopoa gari zaendaleo

  JB Julius Bett
 1105. AJALI SINGIDA: Watu 2 wajeruhiwa leo baada ya Fuso kugonga treni ya mizigo huko Manyoni mkoani Singida, Kamanda T. Sedoyeka athibitisha. Fuso lateketea kwa moto.

  JB Julius Bett
 1106. MOTO MARA: Bweni la wasichana shule ya sekondari ya Issenye huko Serengeti limeteketea kwa moto leo, Zimamoto wasema wanafunzi wanusurika. Chanzo hakijajulikana.

  JB Julius Bett
 1107. MRITHI WA MAKONDA: Mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda leo amwapisha DC wa Kinondoni, Salum Hapi na kumpa vipaumbele 7 vikiwemo afya, rushwa na mgogoro wa ardhi.

  JB Julius Bett
 1108. MATAPELI JELA MWANZA: Mahakama Misungwi leo yawahukumu watu 5 kwenda jela miaka 36 kila mmoja kwa kutapeli viwanja huko Usagara, Nyashishi na kujipatia Sh11.4m.

  JB Julius Bett
 1109. NAIBU MEYA DAR: Diwani kata ya Kiwalani (CUF), Mussa Kafana leo achaguliwa kuwa naibu meya jiji la Dar baada kupata kura 10 dhidi ya 6 za Mariam Lulida (CCM).

  JB Julius Bett
 1110. DROO SHIRIKISHO CAF: Yanga yapangwa kucheza na G.D. Sagrada Esperanca ya Angola raundi ya 2 hatua ya 8. TP Mazembe v. St Gabesien na Merrikh v. Kawikab.

  JB Julius Bett
 1111. DALADALA DAR: Daladala zote zifanyazo safari katikati ya jiji zatakiwa kuondoka ifikapo Mei 2 kupisha mabasi ya mwendokasi, msemaji DART Sabri Mabrouk asema leo

  JB Julius Bett
 1112. BUNGE LA BAJETI DODOMA: Waziri Jenista Mhagama awasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu, upinzani wawasilisha maoni bungeni leo Dodoma.

  JB Julius Bett
 1113. MAUAJI GEITA: Watu wasiojulikana wamuua kwa kumkatakata kwa mapanga muuguzi zahanati ya Kagu, Elizabeth Misango kuamkia leo, RPC Mponjoli Lotson athibitisha.

  JB Julius Bett
 1114. TAHADHARI KABLA YA HATARI: Mkuu wa wilaya ya Mtwara Fatuma Ally leo amhamisha daktari zahanati ya Mkunywa, Isabella Tiliana na kumpeleka kituo cha afya Mahurunga kumwepusha na kipigo baada ya kutuhumiwa kuwatukana wagonjwa.

  JB Julius Bett
 1115. YANGA YATUA: Yanga yawasili uwanja wa ndege Dar baada ya kutolewa Ligi ya Mabingwa Afrika huko Misri. Kocha msaidizi Mwambusi asema wanajipanga kuivaa Coastal.

  JB Julius Bett
 1116. MSAKO WA TFDA: Tani 10 za vipodozi vinavyodaiwa kuingizwa nchini bila kibali vyakamatwa katika ghorofa Na.55 Kariakoo baada ya maofisa TFDA kufanya ukaguzi jijini Dar leo.

  JB Julius Bett
 1117. MGOMO DALADALA MORO: Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Steven Kebwe amesimamisha kazi afisa mfawidhi wa Sumatra mkoani humo, Rahimu Kondo kwa tuhuma za kuwatoza madereva wa daladala faini kubwa.

  JB Julius Bett
 1118. VIGOGO NHIF NJE: Waziri U. Mwalimu awasimamisha kazi maofisa wakuu 4 wa Mfuko wa Bima ya Afya kwa tuhuma za wizi wa zaidi ya Sh2bn katika akaunti ya NHIF Mara.

  JB Julius Bett
 1119. VIGOGO WALIOSIMAMISHWA NHIF: Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Michael Mhando, Mkurugenzi wa Fedha, D. Rutazaa, Mkurugenzi wa Habari, A. Othman na Mkaguzi Mkuu, A. Maneno.

  JB Julius Bett
 1120. Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa, Dk Vicent Mashinji akifungua rasmi Kongamano la BAVICHA na CHASO Leo Dodoma

  JB Julius Bett
 1121. GOGORO SYRIA: Rais B. Obama wa Marekani akataa kupeleka majeshi ya ardhini nchini Syria akisema nguvu za kijeshi pekee haziwezi kumaliza mgogoro nchini humo.

  JB Julius Bett
 1122. Write an update ...

  BUNGE ‘LIVE’:BUNGE ‘LIVE’: Kutokana na ubora wa habari zinazotolewa na Bunge kuwa duni, Jukwaa la Wahariri wataka Bunge kufikiria upya hatua yake ya kufunika shughuli za Bunge.

  JB Julius Bett
 1123. WAJIUNGA CCK: Viongozi wawili wa UDP, Salum Makunganya na Joachim Mwakitiga wahamia Chama cha Kijamii (CCK) wakidai kuchoshwa na ukiukwaji wa taratibu za chama.

  JB Julius Bett
 1124. TISHIO LA NYUKLIA: Rais Obama apuuza madai ya Korea Kaskazini ya kuzijaribu silaha zake za nyuklia endapo Marekani haitaacha mazoezi ya kijeshi na Korea Kusini.

  JB Julius Bett
 1125. FURSA YA BIASHARA: Wauzaji wa bidhaa za ndani watakiwa kujaza fomu za kushiriki kongamano la kibiashara nchini Rwanda mwezi ujao, TANTRADE na TCCIA waeleza.

  JB Julius Bett
 1126. Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema wamewakamata ombaomba 45 na kuwapeleka 17 gerezani.

  Akizungumza leo na waandishi wa habari Sirro amesema jeshi hilo kwa kushirikiana na ustawi wa jamii wanafanya utaratibu wa kuhakikisha watu hao wanarudishwa mikoani kwao badala ya kuendelea kuombaomba.

  JB Julius Bett
 1127. MAGUFULI AMTEUA ANDENGENYE KAMISHA ZIMAMOTO: Rais wa Dk John Magufuli amemteua Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye kuwa Kamishna Mkuu wa Jeshi la Zimamoto nchini.

  JB Julius Bett
 1128. SUMBAWANGA: Ukosefu wa madawati 12,600 kwa shule za msingi Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, kunasababisha zaidi wanafunzi 37,000 kukaa chini.

  JB Julius Bett
 1129. MIAKA 52 YA MUUNGANO: Miaka 52 iliyotuleta pamoja kama taifa la Tanzania. Tuzidi kukumbuka nasaha za waasisi wa Muungano.

  JB Julius Bett
 1130. MSAMAHA WA JPM: Rais Magufuli atangaza msamaha kwa wafungwa 3,551; kati yao 580 huru, 2,971 wapunguziwa vifungo kama sehemu ya maadhimisho miaka 52 ya Muungano

  JB Julius Bett
 1131. MKE WA RAIS AFARIKI: Mke wa Rais mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki, Lucy Kibaki afariki hospitalini Cromwell, London, UK alikokuwa anatibiwa, Rais Kenyatta asema leo

  JB Julius Bett
 1132. Tunawatakia Watanzania wote maadhimisho mema ya miaka 52 ya Muungano wa Tanzania

  JB Julius Bett
 1133. Dk Magufuli amtema mkurugenzi TCRA: Rais John Magufuli amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk Ally Simba.

  JB Julius Bett
 1134. MTOTO AJIUA SINGIDA: Mwanafunzi wa darasa la 4 shule ya msingi Manyoni, A. Vicent (13) ajinyonga hadi kufa kwenye mti, uongozi hospitali ya Manyoni wathibitisha

  JB Julius Bett
 1135. TAHADHARI YA MVUA: Mamlaka ya Hali ya Hewa yatoa tahadhari ya mvua kubwa na upepo mkali katika ukanda wa Pwani na Z'bar inayotarajiwa kuanza leo hadi Ijumaa.

  JB Julius Bett
 1136. MTOTO AJIUA SINGIDA: Mwanafunzi wa darasa la 4 shule ya msingi Manyoni, A. Vicent (13) ajinyonga hadi kufa kwenye mti, uongozi hospitali ya Manyoni wathibitisha

  JB Julius Bett
 1137. MRITHI WA MWIGAMBA: Chama cha ACT- Wazalendo kimemteua Juma Saanani kuwa Kaimu Katibu Mkuu baada ya Samson Mwigamba kung’atuka wiki iliyopita.

  JB Julius Bett
 1138. PICHA: Mhariri mtendaji wa gazeti la Mwananchi ‪#‎FrankSanga‬ kwenye‪#‎KuperuziNaKudadisi‬ Ya Power BreakFast-Clouds FM ‪#‎MwananchiLeo‬


  Picha na Clouds Digital

  JB Julius Bett
 1139. PICHA: Mbunge wa jimbo la Ileje mkoani Songwe Janeth Mbene, akiuliza swali Bungeni kuhusu maswala ya wanawake

  JB Julius Bett
 1140. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenister Mhagama akipitia nyaraka zake tayari kwa kujibu hoja mbalimbal za wabunge walizotoa wakati wa kuchangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2016/17 muda huu. Kulia ni Mwanasheria mkuu George Masaju

  JB Julius Bett
 1141. KUTOKA BUNGENI: Naibu spika wa Bunge Dk Tulia Ackson akijibu miongozo mbalimbali iliyotolewa leo Bungeni, Moja ya miongozo hiyo ni pamoja na swala la Wabunge wa upinzani kupokea posho ya Bunge, wakati hawachangii chochote Bungeni.

  JB Julius Bett
 1142. WAZIRI MKUU AMJIBU MBOWE: Waziri Mkuu kassim Majaliwa, amemjibu kiongozi wa upinzani Bungeni Freeman Mbowe, aliyehoji siku za hivi karibuni kitendo cha Serikali kutotoa hati maalumu ya mwongozo (Instrument) inayoitambulisha serikali iliyopo madarakani kwa mujibu wa sheria.

  “Instrument ipo, na tayari imeshasainiwa na rais kwa mujibu wa sheria, kwa sasa mchakato wa kuitangaza kwenye magazeti ya Serikali inaendelea” amesema Waziri Mkuui Majaliwa

  Amesema viongozi wote wa serikali wapo kwa mujibu wa sheria na kanuni za serikali.

  Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema haya wakati alipokuwa akihitimisha hotuba yake ya kulitaka bunge likubali kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi yake kwa mwaka wa fefdha 2016/17

  JB Julius Bett
 1143. Mbunge wa jimbo la Kigoma mjini, Zitto Kabwe akihoji kuhusu kutoonekana kwa fedha kiasi cha Sh50milioni kwenye vitabu vya bajeti ofisi ya Waziri Mkuu, fedha hizo zinatarajiwa kutolewa kwa kila kijiji nchini, . hata hivyo Naibu Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson amemtaka awe na subira

  JB Julius Bett
 1144. UTEUZI TFF: TFF leo yamteua Alfred Lucas kuwa afisa habari na mawasiliano kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Baraka Kizuguto ambaye amepewa kazi nyingine.

  JB Julius Bett
 1145. UHABA WA SUKARI: Waziri Mkuu Majaliwa asema bungeni serikali imeagiza sukari nje ya nchi kuukabili uhaba wa bidhaa hiyo. Ataka uchunguzi kufichua wanaohujumu.

  JB Julius Bett
 1146. BUNGE LA BAJETI: Wabunge mjini Dodoma wapitisha bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2016/17.

  JB Julius Bett
 1147. KESI YA KITILYA: Korti Kisutu, Dar yafuta shtaka la kutakatisha fedha dhidi ya aliyekuwa bosi wa TRA, Harry Kitilya, wengine 2. Mawakili sasa wanaomba dhamana.

  JB Julius Bett
 1148. VIPIMO KWA WACHEZAJI: Wachezaji 30 wa timu ya Taifa under-17 chini usimamizi wa TFF wanafanyiwa vipimo vya MRI hospitali ya Muhimbili kubaini umri wao halali.

  JB Julius Bett
 1149. MAKATIBU TAWALA WAAPISHWA: Rais John Magufuli leo awaapisha makatibu tawala wa mikoa 10, Ikulu, Dar leo. Watia saini ahadi ya uadilifu.

  JB Julius Bett
 1150. SILVA SHAKANI: David Silva wa Manchester City shakani kuikabili Real Madrid mechi ya marudio UEFA baada ya kuumia misuli ya paja, kocha Manuel Pellegrini asema.

  JB Julius Bett
 1151. Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Edwin Ngonyani amesema kuwa Serikali imeanza mchakato wa ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya Ifakara – Mlimba kwa kuanza na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina.

  JB Julius Bett
 1152. Waziri wa Katiba na Sheria Dk Harrison Mwakyembe amesema Serikali inatarajia kupeleka bungeni muswada wa sheria utakaowalazimisha wazazi na wahusika kuwasomesha watoto wao wa kike katika shule za msingi hadi sekondari.

  JB Julius Bett
 1153. PANYA ROAD DAR: Polisi Temeke yawakamata vijana zaidi ya 18 maarufu kama ‘Panya Road’ kwa tuhuma za kufanya uhalifu wilayani humo, Kamanda Gilles Muroto asema.

  JB Julius Bett
 1154. BUNGENI DODOMA: Waziri Mkuu Majaliwa asema leo serikali itawarudishia wananchi silaha zilizochukuliwa wakati wa “Operesheni Tokomeza” baada ya uhakiki kufanyika.

  JB Julius Bett
 1155. UAMUZI WA JPM: Rais Magufuli atengua uteuzi wa mkurugenzi mtendaji TIC Julieth Kairuki kwa sababu kadhaa ikiwemo kutochukua mshahara tangu Aprili 2013 hadi sasa

  JB Julius Bett
 1156. MAUAJI MBEYA: Watu 3 wanaotuhumiwa kwa ujambazi wauawa katika ya majibizano ya risasi baina yao na polisi Chunya, Jeshi la Polisi Mbeya lathibitisha leo mchana.

  JB Julius Bett
 1157. Mwili wa aliyekuwa mwanamuziki nguli wa Congo Jules Shungu maarufu kama Papa Wemba aliyefia huko Abidjan, Ivory Coast, wawasili leo huko Kinshasa

  Picha na Mtandao

  JB Julius Bett
 1158. ASKOFU MPYA GEITA: Papa Francis amteua mhadhiri chuo kikuu Stella Maris Flavian Kassala kuwa askofu Jimbo Kuu Katoliki Geita, balozi wake nchini Askofu Francisco Padilla atangaza.

  JB Julius Bett
 1159. Chato. Dawa za Serikali ya Uganda, zimekamatwa wilayani Chato, Mkoa wa Geita baada ya kuingizwa na wafanyabiashara kinyume na sheria.

  JB Julius Bett
 1160. Sengerema: Mbunge wa Buchosa, Dk Charles Tizeba amesema mradi wa maji wenye thamani ya Sh1.6 bilioni unaoratibiwa na Wizara ya Maji kuanzia Lumeya hadi Nyehunge katika halmashauri hiyo, umekwama kukamilika tangu ulipoanza mwaka 2012.


  JB Julius Bett
 1161. BUNDA: Mkuu wa Wilaya ya Bunda mkoani Mara, Joshua Mirumbe amewataka wanaume kujengea tabia ya kuwapeleka watoto wao kliniki ili nao wapate elimu juu ya kujikinga na ugonjwa wa malaria.

  JB Julius Bett
 1162. MAAFA KENYA: Jengo la ghorofa 7 laanguka mjini Nairobi kutokana na mvua, watu 7 wafa, wengine wengi wafunikwa na kifusi, uokoaji unaendelea, polisi wathibitisha.

  JB Julius Bett
 1163. NDEGE YAACHA NJIA: Abiria wanusurika kifo baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kutoka Mwanza kuacha njia wakati ikitua Uwanja wa Bukoba, taarifa zaidi baadaye.

  JB Julius Bett
 1164. AJALI MBEYA: Watu 5 wamekufa, wengine 29 wamejeruhiwa baada ya Basi la HBS walilosafiria kutoka Mbeya kwenda Tabora kuanguka Mbeya Vijijini, polisi wathibitisha.

  JB Julius Bett
 1165. ALIYEJIFANYA OFISA USALAMA WA JK ATUPWA JELA MIAKA 12:

  Mahakama ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, imemhukumu kwenda jela miaka 12, Qasama Machibya aliyejifanya ofisa usalama wa Taifa kwenye ziara ya Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete mwaka 2013.

  JB Julius Bett
 1166. MEI MOSI: Rais Magufuli ashusha kodi ya mapato ya mshahara kwa wafanyakazi kutoka asilimia 11 hadi asilimia tisa.

  JB Julius Bett
 1167. KANISA LAUNGUA: Kanisa Katoliki Kigango cha Nyarwele Jimbo la Kayanga mkoani Kagera lateketea kwa moto, chanzo hakijajulikana, Padre N. Rutahiwa athibitisha.

  JB Julius Bett
 1168. MGOMO DAR: Wafanyakazi wa Pepsi wagoma kufanya kazi wakidai kupewa mikataba ya ajira, nyongeza ya mishahara; polisi wafika kwenye tukio, taarifa zaidi baadaye

  JB Julius Bett
 1169. BOMOABOMOA: Nyumba 100 kati ya 400 zimeshabomolewa eneo la Iloganzila, Jimbo la Kibamba jijini Dar kufuatia amri ya Mahakama Kuu, ubomoaji unaendelea.

  JB Julius Bett
 1170. UTAPELI MWANZA: Polisi wilayani Misungwi wamemkamata Martin John kwa kujifanya Afisa Usalama wa Taifa na kutaka kuwatepeli waganga wa jadi Sh. 2,070,000.

  JB Julius Bett
 1171. BUNGE LA BAJETI: Naibu Waziri Uchukuzi Edwin Ngonyani asema serikali inatafakari kanuni ya kupiga marufuku matairi ya “Super Single” yanaodaiwa kuharibu barabara

  JB Julius Bett
 1172. NZEGA: Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Jackline Liana amewataka watu wanaokwenda kuwasalimia wagonjwa katika hospitali ya wilaya hiyo, kutumia mapipa yaliyopo kutupa uchafu ili kuepuka mlipuko wa magonjwa kama kipindupindu.

  JB Julius Bett
 1173. MWANZA: Hatima ya madaktari watano na wauguzi watano wa Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana ya Butimba na ile ya Mkoa wa Mwanza ya Sekou-Toure waliosimamishwa kazi kwa tuhuma za uzembe uliosababisha vifo vya watoto watatu, itajulikana kabla ya Mei 15.

  JB Julius Bett
 1174. DAR ES SALAAM: Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi amesema Shule za

  msingi Manispaa ya Kinondoni zinakabiliwa na upungufu wa madawati 19,386, vyumba vya madarasa 2,235 na matundu ya vyoo 6,788, huku akitoa rai kwa mashirika na sekta binafsi kusaidia kutatua kero hiyo.
  JB Julius Bett
 1175. DODOMA: Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu ya CCM, (Nec), imeteuwa wabunge wanne kuwania nafasi ya ukatibu wa Kamati ya wabunge wote wa CCM.

  JB Julius Bett
 1176. SNURA AFUNGIWA KUJIHUSISHA NA SANAA, TCRA WAAGIZWA KUIFUTA VIDEO YA CHURA

  Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo leo imetangaza kumfungia Snura kujihusisha na masuala ya sanaa.

  Akiongea na waandishi wa habari, Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa wizara hiyo, Zawadi Msalla, amewaonya watu kutousambaza wimbo huo kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo WhatsApp. Amedai kuwa wale watakaokiuka agizo hilo watashtakiwa kwa kutumia sheria ya makosa ya mtandao. ‪#‎MwananchiLeo‬

  JB Julius Bett
 1177. MWALIMU AJINYONGA: Mwalimu wa Shule ya Msingi Buzebazeba mkoani Kigoma, Victoria Wiso ajinyonga kwa kamba hadi kufa jikoni kwake, sababu haijajulikana, polisi wathibitisha.

  JB Julius Bett
 1178. Rais John Magufuli amemteua Dk Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza

  JB Julius Bett
 1179. BAGAZA AFARIKI: Rais Mstaafu wa Burundi J. Bagaza afariki dunia nchini Ubelgiji alikokuwa akitibiwa. Alitawala mwaka 1976 hadi 1987; Serikali yathibitisha.

  JB Julius Bett
 1180. WAFANYAKAZI HEWA: RC wa Singida M. Mtigumwe amsimamisha kazi Mkurugenzi H/Shauri ya Singida Simion Mumbee kwa kudanganya hakuna wafanyakazi hewa. RC awabaini 19.

  JB Julius Bett
 1181. SAKATA LA SNURA: Mwimbaji wa muziki wa Mduara nchini Snura Mushi ameomba radhi kwa umma wa Watanzania kwa kosa la kutengeneza, kuzindua na kuweka mitandaoni video ya udhalilishaji wa mwanamke na isiyozingatia maadili ya Kitanzania ya muziki unaoitwa "Chura".

  JB Julius Bett
 1182. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Walemavu, Antony Mavunde amekifunga kwa muda kiwanda cha kutengeneza mbao nyepesi cha S & Y Company Ltd na kuwatoza wamiliki faini ya papo hapo ya Sh4 milioni na kuwataka raia 10 wenye asili ya China kujisalimisha Uhamiaji.

  JB Julius Bett
 1183. RUNGU LA TFF: Azam FC yanyang'anywa pointi 3 na mabao 3 na kupewa Mbeya City baada ya Azam kumchezesha Erasto Nyoni aliyekuwa na kadi 3 za njano, TFF yaeleza.

  JB Julius Bett
 1184. MOROGORO: Polisi mkoani Morogoro inawasaka watu sita kwa tuhuma za kufyatua risasi iliyosababisha kifo cha Joseph Abubakar walipovamia duka alilokuwa ananunua mahitaji yake katika eneo la Mkundi katika Manispaa ya Morogoro.

  Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Ulrich Matei amesema tukio hilo lilitokea Aprili 30, mwaka huu, saa tatu usiku, pale majambazi hayo yalivamia duka la Derigo Joseph kwa lengo la kuiba na ndipo yalipofyatua risasi.

  JB Julius Bett
 1185. Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally amewataka Watanzania halali ili kujipatia ridhiki.

  Amesema Mwenyezi Mungu ameagiza waja wake kujitafutia ridhiki ambayo inayotokana na kazi halali hivyo kuwataka viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) kuwasisitiza hilo waumini na wafuasi wao.

  JB Julius Bett
 1186. Rais John Magufuli amemuapisha Dk Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

  Hafla ya kuapishwa kwa Dk Asha-Rose Migiro imefanyika leo katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma, na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.

  JB Julius Bett
 1187. Mkazi wa Makongo Dar esalaam Oliver Erasto (22) pamoja na mtoto wake Emmanuel Frowin( 3) wameuawa kinyama kwa kuchinjwa shingo na kisha miili yao kutelekezwa kwenye kichaka kilichopo Kaole kata ya Dunda wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

  JB Julius Bett
 1188. AJALI K'NJARO: Watu 6 wajeruhiwa leo baada ya basi la Chakito toka Dar-Arusha kugongana na lori huko Shirimatunda mjini Moshi, Kamanda Wilbroad Mutafungwa asema

  JB Julius Bett
 1189. MATUKIO YA UBAKAJI: Waziri Harrison Mwakyembe ameliambia Bunge kuwa kuna matukio 19 ya ubakaji na ulawiti nchini kila siku. Mashauri yafikia 2,031 kati ya Jan-Machi, 2016.

  JB Julius Bett
 1190. BUNGENI: Wabunge wanawake Ukawa watoka nje ya Bunge wakipinga kauli iliyotolewa na Mbunge Goodluck Mlinga kuwa viti maalum Ukawa hutolewa kwa rushwa ya ngono.

  JB Julius Bett
 1191. KESI YA KITILYA: Mahakama Kuu Dar yatupilia mbali rufaa ya DPP dhidi ya Kitilya na wenzake, yaishauri Jamhuri kurudi Kisutu kufanya marekebisho ya shtaka hilo.

  JB Julius Bett
 1192. BARIADI: Walimu watano wamepigwa na kung’olewa mazao yao mashambani na wanakijiji kwa madai ya kuwazuia kuchungia mifugo katika maeneo ya shule.

  Katibu wa Chama cha Walimu nchini (CWT) wilayani Bariadi, Baraka Owawa amewaambia waandishi wa habari baada ya kutokea tukio la kati shule za msingi Giriku, Nkindwabiye, Sapiwi na Nyamikoma.

  JB Julius Bett
 1193. MAUAJI SERENGETI: Mtu mmoja apigwa risasi na kufa baada ya wananchi Kisaka kuvamia kituo cha polisi Borenga wakitaka kumuua mtuhumiwa wa mauaji, polisi waeleza.

  JB Julius Bett
 1194. FIFA YAISHUKIA SIMBA: Fifa yaipiga faini ya Sh4m Klabu ya Simba kwa kushindwa kumlipa kwa wakati mchezaji Donald Musoti Omanua raia wa Kenya baada ya kuvunja mkataba wake.

  JB Julius Bett
 1195. SAKATA LA SUKARI: Mamlaka ya Mapato (TRA) Lindi imetaifisha na kugawa sukari mifuko 5,319 toka Brazil yenye thamani ya Sh 373.5 milioni na kuigawa kwa taasisi mbalimbali mkoani humo ikiwa ni sehemu ya shehena iliyokamatwa ikiingizwa kimagendo nchini mwezi Februari 2016.

  Taasisi zilizopata sukari hiyo ni magereza, shule maalumu, kambi ya wazee, shule za kawaida,hospitali na magereza.

  JB Julius Bett
 1196. MGOMO SIMBA: Wachezaji 7 wa kigeni klabu ya Simba wagoma kwenda Songea kuikabili Majimaji keshokutwa wakidai mishahara yao, baadhi ya wanasoka hao wathibitisha.

  JB Julius Bett
 1197. OFISA AJINYONGA KAGERA: Ofisa Utumishi Idara ya Elimu Muleba, Manase Mkumbo ajinyonga shambani kwake Kyamyorawa, DC Francis asimamia uondoaji mwili asubuhi hii.

  JB Julius Bett
 1198. MAUAJI MWANZA: Watu wasiojulikana wamuua kwa kumchinja mkulima Ibwenge Erasto (45) kijijini Kolomije, Misungwi kuamkia leo, Polisi yathibitisha. Msako waanza.

  JB Julius Bett
 1199. NAULI MPYA DAR: Sumatra yatangaza rasmi nauli za mabasi ya mwendo kasi ambazo ni kati ya Sh400 hadi Sh800 kulingana na umbali. Wanafunzi kuendelea kulipa Sh200.

  JB Julius Bett
 1200. SAKATA LA SUKARI: Uhaba wa sukari unatokana na agizo la Rais Magufuli kuzuia uagizaji wa bidhaa hiyo nje, Waziri Kivuli wa Biashara Anthony Komu asema Dodoma.

  JB Julius Bett
 1201. WATUMISHI HEWA: Hadi leo watumishi hewa 248 wamebainika Dar, waleta hasara ya Sh3.7bn, RC Paul Makonda asema. Waajiriwa 11 wazua utata, Ofisa asimamishwa Ilala.

  JB Julius Bett
 1202. ANG'ATUKA UEFA: Rais wa UEFA Michel Platini atangaza kujiuzulu leo baada ya rufaa yake ya kuitaka FIFA kumwondolea marufuku ya miaka sita kugonga mwamba.

  JB Julius Bett
 1203. UCHUMI WA VIWANDA: Rais Magufuli azindua majengo ya NSSF na PPF leo Arusha, aagiza mifuko ya hifadhi ya jamii nchini kuwekeza kwenye viwanda na si majengo pekee

  JB Julius Bett
 1204. BUNGE LA BAJETI: Waziri wa Ulinzi Hussein Mwinyi awasilisha bajeti ya wizara yake leo, aomba Bunge liidhinishe Sh1.73trn; matumizi Sh1.48trn, maendeleo Sh248bn.

  JB Julius Bett
 1205. SAKATA LA SUKARI: Mfanyabiashara Dar akamatwa akituhumiwa kuficha sukari tani 4 iliyokamatwa Kinondoni. Kiongozi wa mtaa mbaroni akidaiwa kuhongwa afiche siri.

  JB Julius Bett
 1206. Polisi wanamshikilia mfanyabiashara Bushir Haroun kwa tuhuma za kuficha kilo 4,000 za sukari katika ghorofa lake Hananasaf, Kinondon Dar es Salaam.

  JB Julius Bett
 1207. Madiwani wa Halmashauri ya Gairo wameziomba mamlaka husika kumchukulia hatua Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Mbwana Maguto kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za miradi hali iliyosababisha miradi yote inayotekelezwa katika halmashauri hiyo kuwa chini ya kiwango.

  JB Julius Bett
 1208. Kamati Kuu ya Chadema itakutana mjini Dodoma katika kikao chake cha kikatiba kuanzia Mei Jumatano na Alhamisi kitakachojadili mwenendo wa Serikali ya CCM chini ya Rais John Magufuli.

  JB Julius Bett
 1209. Aliyekuwa askari wa jeshi la polisi wilayani hai mkoani Kilimanjaro, Kuyani Mkunjera (36) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi kwa kupokea mshahara huku akiwa ameacha kazi miezi saba iliyopita.

  JB Julius Bett
 1210. DARAJA LA NYERERE: Serikali leo imetangaza viwango vya tozo kwa watumiaji daraja la Nyerere, Kagamboni. Bodaboda kulipia Sh600,magari madogo 1500 kuanzia J'mosi

  JB Julius Bett
 1211. JELA MAISHA K'NJARO: Mahakama ya wilaya ya Hai leo imewahukumu Obedia Daniel na Joblate Moshi kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji.

  JB Julius Bett
 1212. UCHAGUZI BUNGENI: Wabunge wamemchagua Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu kuwa Mwenyekiti wa Bunge jioni hii mjini Dodoma.

  JB Julius Bett
 1213. MASWI ATUMBUA WALIMU WAWILI KITETO: Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Eliakim Maswi amemvua madaraka mkuu wa shule ya sekondari Lesoit, Pekoslid Kambi ya Kata ya Lengatei kwa kudaiwa kufanya mapenzi na wanafunzi wa kidato cha pili na cha nne wa shule hiyo.

  JB Julius Bett
 1214. Ofisa mtendaji wa kijiji cha Bwenda, Lameck Kisusi amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu baada ya Mahakama ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita kumtia hatiani na kosa la kuomba rushwa ya Sh4 milioni na kupokea Sh1.7 milioni.

  JB Julius Bett
 1215. Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro imevipatia vikundi 39 vya wanawake na vijana mikopo ya jumla ya Sh23.8 milioni.

  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amesema bunge kuwa vikundi hivyo vyenye wanachama 295 vimepata mikopo hiyo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na Wanawake.

  JB Julius Bett
 1216. Miaka 30 waliyokaa uraiani vijana wawili wakazi wa Machane Shari imekoma leo baada ya Mahakama ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro kuamuru wamalizie muda uliosalia wa maisha yao wakiwa jela.

  Vijana hao, Obadia Daniel Mkulima (30) na Jubiliti Mushi (30) wamehukumia kifungo hicho cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya kubaka kwa zamu mwanamke anayewazidi umri kwa miaka 10, ambaye pia ni mkazi wa Machame Shari.

  JB Julius Bett
 1217. Nyumba nne kati ya nane za upasuaji wajawazito wanaojifungua zilizojengwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa hazifanyi kazi tangu zikabidhiwe Juni mwaka juzi.

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Dk Ellen Mkondya amesema nyumba hizo zimeshindwa kufanya kazi kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo ukosefu wa gari la kubebea wagonjwa, huduma ya maji na wataalamu, hasa madaktari

  JB Julius Bett
 1218. KINYAMBE AFARIKI: Mchekeshaji Mohamed Abdallah “Kinyambe” afariki dunia kuamkia leo hospitali ya mkoa Mbeya akipatiwa matibabu, uongozi Vituko Show wathibitisha

  JB Julius Bett
 1219. MAJANGA EPL: Norwich, Newcastle zashuka daraja rasmi baada ya Sunderland kuifunga Everton 3-0 na kubaki EPL. Hatima ya Rafael Benitez kubaki Newcastle shakani.

  JB Julius Bett
 1220. WABUNGE WAJITOA: Wabunge 53 wanawake wanaotokana na Umoja wa Katiba ya Wananchi wamejitoa rasmi katika Umoja wa Wabunge Wanawake (TWPG) wakipinga kauli za udhalilishaji.

  JB Julius Bett
 1221. SAKATA LA SUKARI: Polisi mkoani Arusha wanawashikilia watu tisa kwa kosa la kuuza sukari tofauti na bei elekezi ya Sh1800 kwa kilo, Kamanda Charles Mkumbo asema

  JB Julius Bett
 1222. SAKATA LA SUKARI: Aliyekuwa M/kiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba asema agizo la kuzuia sukari toka nje limesababisha uhaba nchini, uzalishaji wa ndani haukidhi mahitaji

  JB Julius Bett
 1223. NG'OMBE WATAIFISHWA: Mahakama ya wilaya ya Bukombe imetaifisha ng'ombe 603 waliokamatwa wakichungwa ndani ya pori la akiba la Kigosi wilayani humo bila kibali.

  JB Julius Bett
 1224. NANYUMBU: Halmashauri ya wilaya Nanyumbu imebaini watumishi 11 zaidi hewa ambao wamesababisha hasara kiasi ya Sh57,756,984.20 baada ya uhakiki.

  Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Nanyumbu, Idris Mtandi Katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya Nanyumbu kinachoendelea sasa.

  JB Julius Bett
 1225. ARUSHA: Ibrahim Kathembe (33), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha kwa tuhuma za kufanya utapeli wa kukusanya ushuru wa mabango.

  JB Julius Bett
 1226. Vyama vya ushirika nchini vimetakiwa kutoa elimu kwa wanachama wake kuhusu matumizi sahihi ya mikopo ili iwapatie tija kuondokana na lindi la umaskini.

  JB Julius Bett
 1227. JPM ASHTUKIZA: Rais Magufuli akitokea Uganda atua uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, Dar leo, akuta mashine za ukaguzi hazifanyi kazi. Ataka hatua zichukuliwe.

  JB Julius Bett
 1228. MAKOCHA WAPYA AZAM FC: Kocha Mkuu Zebenzui Hernandez, msaidizi Jonas Garcia toka Hispania watua Dar leo kuchukua nafasi za makocha Stewart Hall, Mario Marinica katika benchi la ufundi la Azam FC.

  JB Julius Bett
 1229. DART DAR: Wananchi kupitia ITV walalamikia utaratibu mbovu wa mabasi ya mwendokasi ikiwemo ugumu wa kupata tiketi, msongamano vituoni, mabasi kuchelewa vituoni.

  JB Julius Bett
 1230. BUNGENI DODOMA: Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu ataka Kamati ya Kanuni za Bunge kufuatilia kama hotuba ya Upinzani Wizara ya Mambo ya Ndani inakidhi kanuni za Bunge.

  JB Julius Bett
 1231. UBAKAJI DAKAWA: Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ataka watuhumiwa waliombaka mwanamke eneo la Dakawa mkoani Morogoro na video yake kusambazwa wafikishwe mahakamani haraka.

  JB Julius Bett
 1232. BUNGENI DODOMA: Bunge laahirishwa kabla ya muda wake hadi saa kumi ili Kamati ya Kanuni iendelee kupitia hotuba ya upinzani iliyopaswa kuwasilishwa na Godbless Lema.

  JB Julius Bett
 1233. KESI YA UCHAGUZI: Mbunge wa Momba mkoani Songwe David Silinde (Chadema) ashinda kesi ya uchaguzi iliyofunguliwa na Dk Luca Siame (CCM)Mahakama Kuu Kanda y Mbeya

  JB Julius Bett
 1234. BUNGENI: Upinzani wakataa kusoma hotuba kuhusu wizara ya mambo ya ndani baada ya mwenyekiti Mussa Zungu kuwaelekeza waondoe baadhi ya maneno aliyodai yanakwenda kinyume na kanuni za bunge

  JB Julius Bett
 1235. KESI YA UCHAGUZI: Mbunge Kigoma Kusini Hasna Mwilima kupitia tiketi ya CCM ameshinda kesi ya uchaguzi iliyofunguliwa na David Kafulila (NCCR-Mageuzi) Korti Kuu Kanda ya Tabora.

  Mahakama hiyo imesema Kafulila na mashahidi wake wameshindwa kuthibitisha madai kwamba alimshinda mpinzani wake, hivyo Mwilima ndiye mshindi halali.

  Hata hivyo, Kafulila amesema hakubaliana na hukumu hiyo na kuahidi kukata rufaa, jambo linaloungwa mkono na wafuasi wa chama chake na Ukawa kwa ujumla.

  Wafuasi wa CCM wamefurahia hukumu hiyo wakisema Mahamaka Kuu Kanda ya Tabora imetenda haki kwa kumpa ushindi Mwilima.

  Baada ya hukumu hiyo, Mwilima amesema ngungu zake sasa anaelekeza kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo lake.

  JB Julius Bett
 1236. UCHAFUZI WA MAZINGIRA: Maofisa wa TFDA, TRA na NEMC wakifunga kiwanda ‘bubu’ cha kuchakata samaki kwa kutolipa kodi, kuchafua mazingira eneo la Gerezani, Dar.

  JB Julius Bett
 1237. BUNGE LA BAJETI: Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa aomba Bunge liidhinishe mpango wa mapato, matumizi ya Sh4.9trn mwaka wa fedha 2016/17.

  JB Julius Bett
 1238. Wachumi nchini wamesema ni hatari kwa Serikali kufanya uamuzi bila kushirikisha wafanyabiashara au vyama vyao kwa kuwa wanaweza kuwa kiini cha nchi kuyumba kiuchumi.

  Baadhi ya wasomi hao, wakijenga hoja zao kwa kuonyesha wazi tofauti za kimtazamo wa biashara na uchumi wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne iliyokuwa chini ya Jakaya Kikwete, na ya awamu hii ya Dk John Magufuli, wamesema maamuzi yanayowashirikisha wadau yana afya zaidi na ni mtaji mzuri kwa Serikali kuweza kujipanga. Walishauri Serikali itumie mbinu za ushirikishwaji badala ya mbinu ya mapambano.

  JB Julius Bett
 1239. KAHAMA: Kukosekana kwa chumba cha kuhifadhi maiti katika kituo cha Afya cha Bulungwa wilayani Ushetu Mkoa wa Shinyanga kumesababisha wagonjwa kulala chumba kimoja na maiti, inapotokea mtu kafariki usiku.

  Kaimu Mganga Mkuu wa kituo hicho, Dk Peter Dalali amesema wanalazimika kuwachanganya na maiti hadi ndugu wa marehemu wanapowachukua.

  JB Julius Bett
 1240. SERENGETI: Polisi mkoani Mara inamshikilia mganga wa zahanati katika Kijiji cha Rwamchanga kwa madai ya kushindwa kumhudumia mjamzito aliyejifungua mapacha na kusababisha kifo mtoto mmoja.

  JB Julius Bett
 1241. MWANZA: Wakulima wa pamba kutoka mikoa mbalimbali nchini wameiomba Serikali kuingilia kati sekta hiyo ili iwanufaishe.

  JB Julius Bett
 1242. KIGOMA: Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Paulo Malala amesema wamejipanga kudhibiti biashara holela ya ununuzi na usafirishaji wa mazao ya muhogo na mahindi kwenda nchi jirani ya Burundi.

  JB Julius Bett
 1243. MWANZA: Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania(TFDA) Kanda ya Ziwa, imeteketeza bidhaa feki zenye thamani ya zaidi ya Sh171 milioni zilizokamatwa wakati wa operesheni iliyofanyika Januari hadi Mei, mwaka huu.

  JB Julius Bett
 1244. AVEVA AOMBA RADHI: Rais wa Simba, Evance Aveva leo amewaomba radhi wanachama, mashabiki baada ya klabu hiyo kushindwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na FA.

  JB Julius Bett
 1245. MASHINDANO YA AIFF: Timu ya Taifa (U17) Serengeti Boys leo imeshinda goli 3-1 dhidi ya wenyeji India katika mashindano ya vijana huko Goa nchini India.

  JB Julius Bett
 1246. MOTO DAR: Moto wateketeza Shule ya Sekondari ya wasichana ya Dar es Salaam Islamic huko Ilala kuamkia leo, polisi yathibitisha. Chanzo na hasara havijajulikana.

  JB Julius Bett
 1247. SAKATA LA UBAKAJI DAKAWA: Watu 6 wafikishwa katika korti ya wilaya Morogoro kwa tuhuma za kumbaka mwanamke, kusambaza picha za video kwenye mitandao ya kijamii.

  JB Julius Bett
 1248. MAUAJI MWANZA: Watu wasiojulikana wavamia msikitini wa Ramadhani, Mkolani na kuua watu 3, kujeruhi mmoja kuamkia leo, Polisi yathibitisha. Taarifa zaidi kukujia.

  JB Julius Bett
 1249. NDEGE YA EGYPTAIR YAPOTEA: Ndege ya Shirika la EgyptAir la Misri ikitoka Paris kwenda Cairo yatoweka kwenye rada ikiwa na watu 69. Utafutaji unaendelea.

  JB Julius Bett
 1250. AJALI SINGIDA: Lori lagonga na kuua punda 16 kati ya 19 waliokuwa wanaswagwa toka Singida Vjijini kuelekea Dodoma kuamkia leo, RPC Thobias Sedoyeka athibitisha.

  JB Julius Bett
 1251. AJALI SINGIDA: RPC Seyodeka asema polisi wanachunguza lori lililogonga, kuua punda 16 kuamkia leo baada ya kukutwa na sukari tani 1.5 iliyokuwa inapelekwa Arusha.

  JB Julius Bett
 1252. JOHANESBURG: Mwanamuziki Ali Kiba asaini mkataba na Sony Music ya nchini Marekani

  JB Julius Bett
 1253. DAKTARI APIGWA: Muuguzi Hospitali ya Rufaa Mara amepigwa leo akituhumiwa kuchelewa kumtibu mtoto wa miezi 7 ambaye amekufa, uongozi wa hospitali hiyo wasema.

  JB Julius Bett
 1254. KESI YA UCHAGUZI: Aliyekuwa mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni (CCM), Idd Azzan leo amefuta kesi ya uchaguzi ya kupinga ushindi wa mbunge, Maulid Mtulia (CUF).

  JB Julius Bett
 1255. MTOTO ALIYEIBWA ARUSHA: Ndugu wa mtoto wa siku 5 aliyeibwa hospitalini Arusha miezi 2 iliyopita leo wameandamana toka Semanjiro hadi ofisini kwa RPC, C. Mkumbo

  JB Julius Bett
 1256. FIDIA KWA WANAFUNZI: DC Arumeru, Wilson Nkambaku aamuru Chuo Kikuu Mount Meru mkoani Arusha kuwafidia wanafunzi 54 wa ualimu baada ya serikali kufuta kozi hiyo.

  JB Julius Bett
 1257. TUZO ZA BET 2016: Diamond Platnumz msanii pekee Afrika Mashariki aliyeteuliwa kuwania tuzo za BET zitakazofanyika Juni, Marekani. Zawajumuisha Drake, Beyonce na Rihanna. Mtanzania huyo anawania tuzo hiyo katika kipengele za ‘Centric’.

  JB Julius Bett
 1258. MAUAJI PWANI: Watu waliokuwa na pikipiki wamuua kwa risasi askari usalama barabarani Ally Kinyogoli huko Mkuranga, Pwani kuamkia leo, Kamanda Usalama Barabarani Mohamed Mpinga athibitisha leo asubuhi.

  JB Julius Bett
 1259. YANGA YATUA: Ndege iliyobeba wachezaji wa Yanga toka Angola yatua uwanja wa ndege, Dar. Mashabiki wafurika kuwalaki baada ya kufuzu robo fainali Shirikisho CAF.

  JB Julius Bett
 1260. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameziagiza halmashauri za manispaa za Temeke, Ilala na Kinondoni kujenga machinjio za kisasa ili nyama ziuzwe katika maduka makubwa.

  JB Julius Bett
 1261. SHINYANGA: Polisi Mkoa wa Shinyanga, wamekamata magunia 35 ya bangi yenye jumla ya kilo 1,820 kwenye Kijiji cha Nyida, Barabara ya Iska- Tinde wilayani Shinyanga, yakiwa yanasafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam.

  JB Julius Bett
 1262. GEITA: Zaidi ya watu 90 wengi wakiwa wajawazito na watoto, wamepoteza maisha

  kwa miaka mitatu wilayani Geita kutokana na upunggufu wa damu unaoikabili hospitali ya wilaya.

  Vifo hivyo vimetokea kati ya mwaka 2013 na 2015. Imeelezwa kuwa, tatizo la upungufu wa damu katika hospitali hiyo linasababishwa na ugonjwa wa homa ya ini inayodaiwa kuwakumba wananchi wengi wilayani Geita.

  JB Julius Bett
 1263. Chama cha Wananchi(CUF) kimemtaka Waziri Mkuu Kassim Majaliwa awaombe radhi watanzania kwa kuwadhalilisha kuwa hawapendi kufanya kazi, badala yake wanashinda kuangalia Bunge, hali ambayo imeisababisha lisirushwe moja kwa moja.

  JB Julius Bett
 1264. Watu 14 wanashikiliwa na polisi wakihusishwa na tukio la kuuwawa kwa askari wa kikosi cha usalama barabarani F 1839 Sajent Ally Salumu maarufu Kinyogori aliyeuawa usiku wa kuamkia jana.


  JB Julius Bett
 1265. Mkazi wa Kitongoji cha Kapembo, Kijiji cha King’wangoko wilayani Kaliua, Mkoa wa Tabora, anadaiwa kumuua mama yake mzazi.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issa amesema kijana huyo anatuhumiwa kumnyonga mama yake, Kiziko Lukambwe kisha mwili wake kuuning’’iniza ndani ya nyumba, ili ichukuliwe kuwa amejinyonga.

  JB Julius Bett
 1266. TANZIA: Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Meya wa Jiji la Dar Isaya Mwita athibitisha.

  JB Julius Bett
 1267. UTORO KAZINI: Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Handeni lawafukuza kazi watumishi 5 kwa kosa la utoro wa muda mrefu kazini, M/Kiti R. Diliwa aeleza.

  JB Julius Bett
 1268. MGOGORO BURUNDI: Msuluhishi wa Mgogoro wa Burundi, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa awasili ukumbi wa mikutano wa AICC jijini Arusha ili kufungua mkutano huo.

  JB Julius Bett
 1269. LIGI KUU BARA: Pazia Ligi Kuu Bara lafungwa leo kwa timu za Coastal Union, Mgambo JKT na African Sports kushuka daraja huku Azam wakishika nafasi ya pili.

  JB Julius Bett
 1270. BUNGENI: Swali lililomng’oa Waziri Charles Kitwanga kuhusu nyumba za polisi na magereza, limejibiwa upya leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni.

  JB Julius Bett
 1271. MAUAJI MWANZA: Watu wasiojulikana wampiga risasi na kumuua M/Kiti wa Mtaa wa Bulale mkoani Mwanza Alphonce Nyinzi na kumjeruhi mama mmoja, polisi wathibitisha.

  JB Julius Bett
 1272. VAN GAAL NJE: Kocha Louis van Gaal atimuliwa rasmi Manchester United ikiwa ni siku mbili baada ya kuiongoza timu hiyo kuchukua taji la FA.

  JB Julius Bett
 1273. BOTI YAZAMA: Watu wapatao 12 wahofiwa kufa baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kutoka Mbaba Bay kwenda Malawi kuzama Ziwa Nyasa, polisi wanafuatilia.

  JB Julius Bett
 1274. MKUU MPYA TALIBAN: Kundi la Taliban Afghanistan lamteua Mawlawi Akhundzada kuwa kiongozi mpya kuziba pengo la Mullah Mansour aliyeuawa kwa shambulizi la ndege.

  JB Julius Bett
 1275. MOTISHA KWA WALIMU: Waziri wa Elimu Prof Ndalichako asema serikali ipo kwenye mchakato wa kutoa motisha kwa walimu wa darasa na 1 na 2 wanaofanya vizuri.

  JB Julius Bett
 1276. MENEJA MPYA AJAX: Ajax Amsterdam leo yamtangaza Mdachi Peter Bosz kuwa meneja mpya baada ya kusaini mkataba wa miaka 3 kuziba nafasi iliyoachwa na Frank de Boer

  JB Julius Bett
 1277. HATI YA KUKAMATWA: Mahakama ndogo Sweden yasema haitafuta hati ya kukamatwa kwa mwasisi wa mtandao wa Wikileaks Julian Assange, kesi yapelekwa korti ya rufaa.

  JB Julius Bett
 1278. MAKUNDI CAF: Yanga inafanya mazungumzo na serikali ili kupata ndege kwa ajili ya mechi za ugenini hatua ya makundi Kombe la Shirikisho kwa lengo la kupunguza gharama za usafiri, mkuu wa kitengo cha mawasiliano Jerry Muro athibitisha.

  JB Julius Bett
 1279. MAKUNDI CAF: Yanga inafanya mazungumzo na serikali ili kupata ndege kwa ajili ya mechi za ugenini hatua ya makundi Kombe la Shirikisho, Jerry Muro athibitisha.

  JB Julius Bett
 1280. Baadhi ya wabunge wa bunge la Afrika ya Mashariki (EALA), wameeleza kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli,kupambana na rushwa na kurejesha uwajibikaji serikalini huku wakimuomba kukutana nae.

  JB Julius Bett
 1281. PINDA ATEULIWA: Rais Magufuli amteua Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kuchukua nafasi ya Dk. Asha-Rose Migiro

  JB Julius Bett
 1282. ZIARA YA SHEIN: Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein anaondoka leo jioni kwenda Muungano wa Visiwa vya Comoro kwa ziara ya siku 2 kumuwakilisha Rais Magufuli

  JB Julius Bett
 1283. KIBALI CHA BIASHARA: Maofisa Uvuvi wakamata vifaranga 5,000 vya kuku na mayai ya samaki Uwanja Wa Ndege Dar leo, yanayodaiwa kutokea Malawi bila kibali.

  JB Julius Bett
 1284. KOMBE LA KAGAME 2016: Rais wa TFF Jamal Malinzi asema Tanzania haitoandaa michuano ya Kombe la Kagame mwaka huu kutokana na ratiba ya kimataifa kubana.

  JB Julius Bett
 1285. MREMA AIBUKA: TLP inalaani hatua ya Katibu Mkuu CUF Maalim Seif kutangaza kumwondoa Rais Z'bar Shein madarakani kabla ya 2020, M/kiti Augustine Mrema asema leo.

  JB Julius Bett
 1286. Wasanii Aisha Ramadhani maarufu Isha Mashauzi na kundi la muziki wa hip hop la Weusi wanatarajiwa kuhamasisha mapambano dhidi ya ugonjwa malaria katika mradi unaojulikana kama ‘Kliniki ya chandarua’

  JB Julius Bett
 1287. KUFUZU AFCON 2017: CAF imemteua Michael Wambura kuwa kamishna wa mchezo kati ya Rwanda na Msumbiji kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika Juni 3, TFF yathibitisha.

  JB Julius Bett
 1288. Watu wawili mume na mke wameuawa kwa kuchinjwa shingo na watu wasiofahamika wakati wakiwa wamelala nyumbani kwao usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Mmazami Kata ya Bukabwa Wilaya ya Butiama Mkoani Mara.

  Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Jackson Kitukuru amewataja waliouawa kuwa ni Saidi Somba(48) na mke wake Kadogo Ehicho(47) wote wakazi wa kijiji cha Mmazami.

  JB Julius Bett
 1289. DAR ES SALAAM: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amefanya ziara ya kushtukiza kwenye kituo kikubwa cha mabasi yaendayo haraka Kimara Mwisho

  JB Julius Bett
 1290. Mbunge wa Temeke (CUF), Abdallah Mtolea ameibana Serikali akiitaka kusitisha uchimbaji wa mafuta kwa kuwa haijawa na wataalamu wa kutosha.

  Mtolea ametoa kauli hiyo katika swali la nyongeza ambapo amehoji ni kwa nini Serikali ilitangaza kuanza uchimbaji wa mafuta wakati hakuna wataalamu waliozalishwa na vyuo vya ndani.

  JB Julius Bett
 1291. Mbunge wa Temeke (CUF), Abdallah Mtolea ameibana Serikali akiitaka kusitisha uchimbaji wa mafuta kwa kuwa haijawa na wataalamu wa kutosha.

  Mtolea ametoa kauli hiyo katika swali la nyongeza ambapo amehoji ni kwa nini Serikali ilitangaza kuanza uchimbaji wa mafuta wakati hakuna wataalamu waliozalishwa na vyuo vya ndani.

  JB Julius Bett
 1292. Wanawake 19 wanaojishughulisha na kilimo kidogo cha vyakula nchini wameteuliwa kushiriki shindano la Mama Shujaa wa Chakula msimu wa tano, linalotarajiwa kufanyika katika Kijiji cha Enguiki, Monduli mkoani Arusha.

  JB Julius Bett
 1293. Tatizo la wananchi kuendelea kutumia maji ya madimbwi ambayo siyo salama na kujisaidia vichakani kwa kutokuwa na vyoo, kunatokana na uzembe wa maofisa wa afya na wahandisi wa maji.

  Mkuu wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Amani Mwenegoha amesema wahandisi wa maji husubiri kufanya kazi za miradi badala ya kwenda vijijini kuwahamasisha wananchi kuchimba visima vya maji safi pamoja na matumizi bora ya vyoo.

  JB Julius Bett
 1294. AJALI DAR: Mabasi ya Maning Nice na Ibra Line yakisafiri Dar-Mtwara yagongana eneo la Ubungo External Dar leo na kujeruhi watu wawili, Polisi wathibitisha.

  JB Julius Bett
 1295. BOTI YAZAMA DAR: Watu 5 wafa baada ya boti ndogo toka Magogoni kwenda Kigamboni kuzama Bahari ya Hindi kuamkia leo, Polisi yathibitisha. Vikosi vya Zimamoto na Uokoaji vinaendelea kutafuta miili zaidi.

  JB Julius Bett
 1296. MAUAJI DAR: Mtu anayetuhumiwa kuwa jambazi auawa katika mapambano na wananchi Buguruni, jijini Dar leo, mwingine atoweka, polisi wamsaka. Bastola 2 zaokotwa

  JB Julius Bett
 1297. BUNGENI: Wabunge wa upinzani watoka nje ya Bunge wakipinga kuapishwa kwa wabunge watano wa CCM kutoka Zanzibar.

  JB Julius Bett
 1298. MAKOSA BARABARANI: Polisi jijini Dar yakusanya Sh 500 milioni kutokana na makosa ya usalama barabarani kwa mwezi huu, Kamanda Simon Sirro aeleza.

  JB Julius Bett
 1299. UTEUZI: Rais John Magufuli amemteua Jaji Shaban Ally Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Taarifa ya Ikulu yasema leo.

  JB Julius Bett
 1300. MAKINDA ATEULIWA: Rais John Magufuli leo amemteua aliyekuwa Spika wa Bunge, Anne Makinda kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

  JB Julius Bett
 1301. UTEUZI: Rais John Magufuli leo amemteua Profesa Apollinaria Pereka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT).

  JB Julius Bett
 1302. BUNGENI: Naibu Spika wa Bunge T.Ackson amewatoa wabunge wa upinzani bungeni jioni hii baada ya kutaka kujadili hoja ya kufukuzwa wanafunzi Chuo Kikuu cha Dodoma.

  JB Julius Bett
 1303. KIAPO CHA UAMINIFU: Wabunge wa upinzani watoka nje ya Bunge leo asubuhi wakipinga kuapishwa kwa mbunge wa CCM kutoka Zanzibar.

  JB Julius Bett
 1304. Wabunge wote wa upinzani wametoka nje kususia kikao cha Bunge ikiwa ni kutekeleza azimio lao la kutokuwa na imani na Naibu Spika, Tulia Ackson.

  Baada tu ya kusomwa dua ya kufungua Bunge asubuhi wabunge hao wametoka nje.

  Juzi kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, Freeman Mbowe akizungumza na wabunge wa upinzani alisema kuwa hawana imani na Dk Tulia hivyo watakuwa wakisusia vikao vyote vitakavyokuwa vikiongozwa na kiongozi huyo

  JB Julius Bett
 1305. TUZO KWA WAZALISHAJI: Rais John Magufuli anatarajiwa kutoa tuzo kwa ajili ya wenye viwanda hapa nchini katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Asema hatowaangusha na atawatetea maslahi yao.

  JB Julius Bett
 1306. TUZO KWA WAZALISHAJI: Rais John Magufuli asema hawachukii matajiri kwani wana mchango katika uchumi. Atarajiwa kutoa tuzo kwa wenye viwanda punde jijini Dar.

  JB Julius Bett
 1307. MGOMO UDSM: Wanafunzi wa chuo kikuu cha cha Dar es salaam mpaka sasa wamegoma wakiishinikiza bodi ya mikopo kutoa fedha kwa ajili ya kujikimu.

  JB Julius Bett
 1308. LHRC yawakingia kifua wabunge walioadhibiwa .

  Siku moja baada ya kuibuka vurugu bungeni, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) leo kimetoa tamko lenye maagizo matano ikiwamo wabunge wote waliosimamishwa kurejeshwa bungeni ili kuendelea na majukumu yao.

  JB Julius Bett
 1309. Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia watuhumiwa wawili kwa tuhuma za kukutwa na bangi misokoto 1,082.

  JB Julius Bett
 1310. BUKOBA: Ahadi ya Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda imehojiwa na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera kuhusu ujenzi wa jengo la upasuaji katika Hospitali Teule ya Izimbya.

  JB Julius Bett
 1311. TABORA: Watu watano wanashikiliwa na polisi baada ya mtu kukutwa amejinyonga mtini muda mfupi baada ya kutoka katika sherehe mjini Tabora.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issa amesema watu hao wanashikiliwa kutokana na mtu aliyetambuliwa kwa jina moja la Musa kukutwa amejinyonga kwenye tawi la mti.

  JB Julius Bett
 1312. Shirika la Viwango nchini (TBS), limejipanga kuendesha msako wa mikoa yote nchini kubaini vilainishi vya magari, nondo na matairi yanayouzwa bila kuwa na viwango vinavyohitajika kisheria.

  Ofisa Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile amesema leo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika banda la shirika hilo lililopo kwenye maonyesho ya biashara jijini Tanga.

  JB Julius Bett
 1313. Mkazi wa Karakata mpya jijini Dar es Salaam, Athuman Rajabu (19) ameanguka na kupoteza fahamu katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kulawiti na kumbaka mfanyakazi wake wa ndani wa miaka 13.

  JB Julius Bett
 1314. Watanzania 408 wanatumikia vifungo nje ya nchi na wengine kukabiliwa na adhabu ya kifo baada ya kusafirisha dawa za kulevya.

  Taarifa hiyo imetolewa bungeni leo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga alipokuwa akiwasilisha makadirio ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/17.

  JB Julius Bett
 1315. Sekretarieti ya Ajira ya Utumishi wa Umma, imesema tangu kuanzishwa kwa mfumo wa utumaji maombi kwa elekroniki umesaidia kupungua muda wa mchakato wa utumaji maombi kutoka siku 90 hadi 52.

  JB Julius Bett
 1316. Naibu waziri wa Mambo ya Nje, Dk Susan Kolimba amesema serikali inatarajia kufungua balozi katika nchi za Qatar, Korea Kusini, Namibia, Uturuki na Israel katika mwaka ujao wa fedha.

  JB Julius Bett
 1317. BUNGE LA BAJETI: Waziri wa Fedha Philip Mpango awasilisha bajeti ya wizara yake Dodoma leo, aomba Bunge lidhinishe Sh9.4trn kwa mwaka wa fedha 2016/17.

  JB Julius Bett
 1318. KORTI YA MAFISADI: Serikali yawasilisha muswada bungeni kuanzishwa kitengo cha Mahakama Kuu kitakachoshughulikia kesi za ufisadi na wahujumu uchumi bungeni leo.

  JB Julius Bett
 1319. BUNGENI DODOMA: Naibu msemaji upinzani Wizara ya Fedha David Silinde agoma kusoma maoni ya kambi hiyo kupinga namna Naibu Spika Tulia Ackson anavyoliendesha Bunge na kukandamiza upinzani.

  JB Julius Bett
 1320. Msemaji wa Kambi ya upinzani kwa Wizara ya Fedha na Mipango, David Silinde amegoma kusoma hotuba ya kambi hiyo bungeni kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa Naibu Spika, Tulia Ackson katika kuliendesha Bunge.

  JB Julius Bett
 1321. Wanafunzi walioandaa mgomo wa jana Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) huenda wakakumbwa na hatua za kinidhamu kwa kosa la kukikuka sheria ndogo ya Chuo kwa kuandaa mkusanyiko pasipo kibali cha Menejimenti.

  JB Julius Bett
 1322. Wananchi wa Kijiji cha Ipera Asilia wilayani Malinyi wameuomba uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Morogoro kuunda kamati maalumu ya uchunguzi ili kuupatia ufumbuzi mgogoro wa wafugaji na wakulima uliosababisha kifo cha mtu mmoja.

  JB Julius Bett
 1323. DODOMA: Kamati ya Bajeti imesema moja ya eneo ambalo Serikali ina changamoto kubwa ya kutatua madeni yake katika mifuko ya jamii yanayofikia zaidi ya Sh6 trilioni.

  JB Julius Bett
 1324. Hifadhi ya Taifa ya Selous iliyopo kusini mwa Tanzania imepoteza asilimia 90 ya tembo waliopo katika hifadhi hiyo kutokana na ujangili uliokithiri.

  JB Julius Bett
 1325. Serikali itakosa mchango wa dawa zenye jumla ya gharama ya dola za Marekani 375 milioni sawa na Sh787 trilioni, ambazo zimekuwa zikichangiwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID).

  JB Julius Bett
 1326. Idara ya Uhamiaji wilayani Temeke, inawashikilia wahamiaji haramu 71 kutoka Ethiopia kwa tuhuma za kuingia na kuishi nchini kinyume cha sheria.

  JB Julius Bett
 1327. Balozi wa EU Tanzania, Roeland van de Geer,akizindua Kitabu cha masuala ya nishati, kuhusu ukuaji na maendeleo endelevu ya nishati kwa Tanzania.

  Kitabu hicho kimeeleza kwa ufupi mchango wa EU uliotoka kwa miaka 10 kwa Tanzania katika kusukuma maendeleo ya sekta ya nishati nchini.

  JB Julius Bett
 1328. Mvua kubwa iliyonyesha Kusini mwa Ujerumani imesababisha eneo hilo kukumbwa na mafuriko makubwa hali iliyoifanya Serikali ya nchi hiyo kutangaza hali ya hatari.

  JB Julius Bett
 1329. Serikali imewasilisha muswada bungeni wa kuanzishwa kwa Mahakama Maalumu ya Rushwa.

  Watakaokutwa na hatia ya makosa ya rushwa au uhujumu uchumi, watafungwa kifungo kisichopungua miaka 20 na kisichozidi miaka 30.

  JB Julius Bett
 1330. Mchezaji kimataifa wa Tanzania anayecheza mpira wa kikapu nchini Marekani, Hasheem Thabeet ametembelea Bunge leo na kujionea jinsi wabunge wanafofanya kazi zao, pichani anaonekana akiingia katika ukumbi wa Bunge na nyingine akiwa amekaa akisikiliza wabunge walipokuwa wakiuliza maswali kwa wizara mbalimbali. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 1331. Kampuni ya Twiga cement yatoa msaada wa vyandarua Boko-Basihaya kata ya Bunju

  JB Julius Bett
 1332. Msanii Naseeb Abdul (Diamond Platinumz) akibalishana mkataba na Msanii Richard Martin (Rich Mavoko) ambaye ameingia katika lebo ya wasafi WCB

  JB Julius Bett
 1333. UCHAGUZI YANGA: Wanachama 9 wakiwemo Bakari Malima na Aaron Nyanda wasimamishwa baada ya kuchukua fomu za uongozi TFF badala ya ofisi za Yanga. Kamati kuwahoji.

  JB Julius Bett
 1334. TANZANIA YASHUKA VIWANGO FIFA: Tanzania yaporomoka kwa nafasi 7 kutoka 129 hadi 136 katika viwango vya Fifa vilivyotoka leo. Algeria yaongoza Afrika, Uganda kinara A. Mashariki.

  JB Julius Bett
 1335. Mke wa rais, Janeth Magufuli ametaka misaada yote inayotolewa kwaajili ya wazee na watu wenye mahitaji maalumu kuhakikisha inawafikia walengwa katokana na kuwepo kwa malalamiko mengi ikiwemo mkoa wa Mwanza .

  Mama Magufuli ameyasema hayo Leo katika kijiji cha Kaseka wilaya ya Masasi wakati alipokwenda kutoa msaada katika kambi ya wazee na walemavu wa ukoma katika kambi ya kaseka.

  Amewataka viongozi wanaohusika kuhakikisha walengwa wanafaidika na misaada hiyo katokana na kupokea malalamiko mengi kutoka mkoa wa Mwanza alikopeleka msaada na kusema vitendo hivyo vinavunja moyo.

  Mama Magufuli kwa kushirikiana na mke wa waziri mkuu,Mary Majaliwa wamekabidhi vyakula mbalimbali,nguo,saruji,vitanda na magodoro ambavyo vimetolewa na watu mbalimbali akiwemo TB Joshua, kampuni ya Super Doll, Dangote na viongozi wanawake wa mkoa wa Mtwara.

  JB Julius Bett
 1336. Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya (EU-EOM), umewasilisha ripoti yake kamili yenye mapendekezo ya marekebisho ya kuboresha mchakato wa uchaguzi, ikiwamo la kutaka Tanzania iruhusu mgombea binafsi wa urais.

  Mwangalizi Mkuu wa Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa EU, Judith Sargentini amesema licha ya uchaguzi wa Oktoba 25, 2015 kuonyesha dhamira ya Watanzania ya kuzingatia mfumo wa kikatiba na kuheshimu misingi ya demokrasia, kulikuwa na kasoro kadhaa.

  JB Julius Bett
 1337. Zaidi ya wanafunzi 30 wanaosoma kidato cha pili na tatu sekondari za Igogo na Mapango, Kata ya Igogo jijini Mwanza, wamenaswa katika msako dhidi ya wahalifu wanaoendesha vitendo vya uporaji maeneo yanayozunguka shule hizo.

  JB Julius Bett
 1338. BUKOMBE: Mkuu wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Amani Mwenegoha ameagiza kufutwa kwa sheria kandamizi ya kuwatoza wafugaji kiasi cha Sh50, 000 kwa kila ng’ombe inayoingia shambani kwa mtu na kulisha mazao.

  JB Julius Bett
 1339. Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe ameomba Jumuiya ya Kimataifa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupiga vita ujangili.
  Profesa Maghembe amesema hayo leo, eneo la Matambwe Selous kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya ndege maalumu nane zisizo na rubani zilizotolewa na Mfuko wa Uhifadhi Wanyamapori na Mazingira Duniani (WWF).

  JB Julius Bett
 1340. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Watanzania wanaoishi Papur New Guinea katika ukumbi wa Airways Hotel mjini Guinea baada ya kukamilisha ziara yake ya kikazi ya kumwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific uliojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu. (Picha na OMR)

  JB Julius Bett
 1341. Katibu mkuu wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo,Prof Elisante Gabriel akiwa na moja ya kikundi cha sanaa cha Mundu Art cha mkoani Mtwara. (Picha na Haika Kimaro)

  JB Julius Bett
 1342. Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu watatu wakazi wa maeneo ya Kabangaja–Mnarani, Kata ya Bugongwa wilayani Ilemela wakijihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya na pombe aina ya gongo.

  JB Julius Bett
 1343. Mwanamuziki nyota nchini, Lady Jay Dee leo ametembelea bungeni kilipokuwa kikiendelea kikao cha 36 cha Bunge, mjini Dodoma ambapo baadae alifanya mazungumzo na wabunge na mawaziri mbalimbali. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 1344. Mwanamuziki nyota nchini, Lady Jay Dee leo ametembelea bungeni kilipokuwa kikiendelea kikao cha 36 cha Bunge, mjini Dodoma ambapo baadae alifanya mazungumzo na wabunge na mawaziri mbalimbali. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 1345. Mwanamuziki nyota nchini, Lady Jay Dee leo ametembelea bungeni kilipokuwa kikiendelea kikao cha 36 cha Bunge, mjini Dodoma ambapo baadae alifanya mazungumzo na wabunge na mawaziri mbalimbali. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 1346. Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika leo imetupilia mbali rufaa ya wastaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya maombi yao kukosa nguvu kisheria kutokana na kukiuka taratibu za uwasilishaji maombi yao.

  Kwa mujibu wa mahakama hiyo iliyopo jijini Arusha, kesi hiyo ilitakiwa kuwasilishwa kwenye mahakama za ndani na kutolewa maamuzi kabla ya kuwasilishwa kwenye korti hiyo ya juu zaidi Afrika.

  Aidha mahakama hiyo imesema ushahidi wa magazeti na kauli ya serikali uliowasilishwa kortini hapo haukujitosheleza hivyo kuamua kuitupilia mbali kesi hiyo.

  Awali, Frank Omary na wenzake waliwasilisha shauri lao katika mahakama hiyo wakiitaka serikali ya Tanzania kuwalipa stahiki zao baada ya kuitumikia Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyovunjika rasmi mwaka 1977.

  JB Julius Bett
 1347. Serikali imesisitiza kuzima simu zote feki itakapofika June 16, mwaka huu, hayo yamesema leo na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani alipokuwa akitoa maelezo bungeni alipopewa nafasi na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kujibu muongozo wa spika ulioombwa na Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola akitaka Bunge lijadili hatua ya serikali kuzima simu bandia ifikapo Juni 16 mwaka huu. waziri Ngonyani alisisitiza kuwa simu bandia ni lazier zizimwe kwa sababu zina madhara makubwa kiafya na kiusalama. Picha na Edwin Mhwahuzi

  JB Julius Bett
 1348. Zaidi ya kaya 900 zinazozungukwa na shamba la mradi mkubwa wa kilimo cha miwa wilayani Bagamoyo (Eco Energy) wamesema wamepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kusitishwa kwa mradi huo iliyotolewa bungeni na Waziri Mkuu Kassim Mjaliwa, wakisema hawajalipwa fidia na hawajui hatima yao.

  JB Julius Bett
 1349. Baadhi ya wakazi wa Kata ya Kigogo jijini Dar es Salaam wamelalamikia uchafuzi wa mazingira katika Bonde la Mto Msimbazi unaosababishwa na viwanda na makazi ya watu.

  JB Julius Bett
 1350. BONDIA AFARIKI: Bondia wa kimataifa Muhammad Ali afariki dunia nchini Marekani kwa maradhi ya upumuaji. Familia yake yathibitisha.

  JB Julius Bett
 1351. AGIZO: Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Wilson Nkumbaku aagiza wananchi waliojenga kwenye chanzo cha maji Kiranyi kubomoa nyumba zao mara moja.

  JB Julius Bett
 1352. UBADHIRIFU KINONDONI: Meya wa Kinondoni Boniface Jacob awasimamisha kazi watendaji kata wawili na kuwatimua wengine wawili kwa ubadhirifu wa Sh400 milioni.

  JB Julius Bett
 1353. Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ahamed Msangi amesema pamoja na kuwaachia watu ambao hakutaja idadi yao, bado wanafuatilia wengine ambao wanaonekana kuhusika na tukio hilo, bila kutaja idadi ya watu waliochiwa.

  JB Julius Bett
 1354. Mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli akikabidhi zawadi ya mbuzi na kuku kwa Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ulemavu wa Ngozi Mkoa wa Lindi, Hemed Said alipomtembelea leo asubuhi Ikulu ndogo mkoani Lindi.Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa. Picha na Maelezo

  JB Julius Bett
 1355. BUNGENI: Kwa siku ya tano mfululizo leo, wabunge wote wa upinzani wametoka nje ya Ukumbi wa Bunge wakigomea kushiriki vikao vinavyoongozwa na Naibu Spika.

  JB Julius Bett
 1356. KIPINDUPINDU: Ugonjwa wa kipindupindu waigharimu serikali Sh900m kuanzia Novemba hadi sasa, Waziri wa Afya asema ugonjwa bado upo, ataka wananchi kuwa makini.

  JB Julius Bett
 1357. MAZINGIRA: Wajumbe kutoka mataifa 16 ya Afrika na Asia wakutana Dar kujadili umuhimu wa kutunza mazingira ili kunusuru vyanzo vya maji, Dk. M. Ulisubisya aeleza

  JB Julius Bett
 1358. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewakabidhi wakazi wa Kijiji cha Upare, shamba la Kibaranga lililokuwa likimilikiwa na Mamlaka ya Mkonge nchini (TSA) baada ya hati yake kufutwa na Rais John Magufuli hivi karibuni.

  JB Julius Bett
 1359. Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa zinazosambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa imetangaza sifa na vigezo vitakavyotumika katika uchambuzi wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

  JB Julius Bett
 1360. CHADEMA WAPIGWA ‘STOP’: Jeshi la polisi limepiga marufuku mkutano wa hadhara wa Chadema uliotarajiwa kufanyika leo mjini Kahama mkoani Shinyanga.

  JB Julius Bett
 1361. Rais John Magufuli leo amemteua Jaji Ferdinand Wambali kuwa Jaji Kiongozi.

  Jaji Wambali anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Shaaban Lila aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

  Kabla ya uteuzi huo, Jaji Wambali alikuwa Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, mkoani Tanga. Uteuzi huu unaanza mara moja leo.

  JB Julius Bett
 1362. MKUTANO ULIOPIGWA 'STOP': Polisi wanawazuia wananchi wanaoelekea kwenye uwanja wa CDT Kahama mjini uliokuwa umeandaliwa kufanyika mkutano wa hadhara wa Chadema.

  JB Julius Bett
 1363. MKUTANO ULIOPIGWA 'STOP': Polisi watumia mabomu ya machozi kutawanya wananchi waliokusanyika katika uwanja wa CDT mjini Kahama kusubiri mkutano wa hadhara.

  JB Julius Bett
 1364. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo amezindua Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango, mjini Dodoma. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 1365. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo amezindua Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano

  JB Julius Bett
 1366. BAKI LA UCHAGUZI: Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo imemkabidhi Rais Magufuli hundi ya Sh12bn zilizobaki baada ya Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka jana.

  JB Julius Bett
 1367. JELA MIAKA 25: Korti Kuu Mbeya yamuhukumu raia wa Afrika Kusini, Vuyo Jack miaka 25 jela na kulipa faini ya Sh3b kwa kusafirisha dawa za kulevya zenye thamani ya Sh1b.

  JB Julius Bett
 1368. ZITTO POLISI: Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe awasili Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam kuhojiwa. Taarifa zaidi kukujia.

  JB Julius Bett
 1369. KESHI AFARIKI DUNIA: Nahodha na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria Stephen Keshi (54) afariki dunia mapema leo jijini Benin katika jimbo la Edo State.

  JB Julius Bett
 1370. Kanisa Katoliki Tanzania kesho litatumia maadhimisho ya kongamano la Ekaristi Takatifu kuliombea Taifa amani.

  Kongamano hilo linaloanza kesho, litahitimishwa Jumamosi, linafanyika kitaifa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza.

  JB Julius Bett
 1371. MAKOSA MTANDAONI: Mahakama Arusha yamhukumu Isaac Emily jela miaka 3 au kulipa faini ya Sh7m kwa kumtukana Rais Magufuli kupitia Facebook. Akubali kulipa faini.

  JB Julius Bett
 1372. Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara, umeziondoa kaya 448 za vijiji 97 katika mpango wa kunusuru kaya maskini baada ya kukosa sifa.

  JB Julius Bett
 1373. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amepiga marufuku uuzwaji wa shamba lenye ekali 455 la Chama cha Ushirika cha Usambara lililoko eneo la Bumbuli wilayani Lushoto Mkoa wa Tanga.

  JB Julius Bett
 1374. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango akiwasilisha bungeni hali ya uchumi wa taifa kwa mwaka 2015 na mpango wa maendeleo wa taifa kwa mwaka wa fedha 2016/2017, mjini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 1375. VIONGOZI CHADEMA KORTINI: Viongozi 22 wa Chadema wapandishwa kortini Kahama, Shinyanga leo wakituhumiwa kufanya kusanyiko lisilo halali. Wakana mashtaka.

  JB Julius Bett
 1376. Imeelezwa kuwa wasomi wanaoishi mijini ndiyo wavunjaji wa sheria zinazohusu watoto kwa kuwaaajiri kwenye nyumba zao na hivyo kukwamisha mpango wa Serikali wa kupambana na ajira za watoto

  Akizungumza leo, Mkurugenzi wa Utafiti wa kupunguza umaskini (Repoa), Dk Abel Kinyondo amesema mapambano dhidi ya ajira za watoto yanakwamishwa na wasomi.

  JB Julius Bett
 1377. BAJETI 2016/17: Mafanikio ya bajeti ya 2015/16 ni pamoja na kuongezeka makusanyo ya kodi hadi wastani wa sh1.02 trilion kwa mwezi #BajetiTz16

  JB Julius Bett
 1378. BAJETI 2016/17: Mafanikio mengine ni kuongezeka kwa wanafunzi wanaonufaika na mikopo ya elimu ya juu hadi kufikia 123,789 #BajetiTz16

  JB Julius Bett
 1379. BAJETI 2016/17: Hadi Machi 2016 deni la Taifa ni USD 20.94bn ikilinganishwa na USD 19.69 Juni, 2015 #BajetiTz16

  JB Julius Bett
 1380. BAJETI 2016/17: Shabaha na misingi ya bajeti ya 2016/17 ni kukuza pato la taifa hadi asilimia 7.2 kutoka asilimia 7.0 mwaka 2015 #BajetiTz16

  JB Julius Bett
 1381. BAJETI 2016/17: Bajeti ya mwaka 2016/17 inalenga kukuza mapato ya ndani kufikia asilimia 16 ya pato la taifa kutoka asilimia 14.8 #BajetiTz16

  JB Julius Bett
 1382. BAJETI 2016/17: Bajeti inalenga kuwa na akiba ya fedha za kigeni kukidhi mahitaji ya uagizaji bidhaa na huduma kutoka nje kwa miezi mine

  JB Julius Bett
 1383. BAJETI 2016/17: Ili kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato Serikali itadhibiti na kupunguza misamaha ya kodi isiyo na tija. #BajetiTz16

  JB Julius Bett
 1384. BAJETI 2016/17: Serikali imetenga Sh5.5trilioni kukarabati reli, barabara na viwanja vya ndege. #BajetiTz16

  JB Julius Bett
 1385. BAJETI 2016/17: Elimu imetengewa Sh4.8trilioni sawa na asilimia 22.1 ya bajeti kugharamia elimu bure, chakula, vitabu nk #BajetiTz16

  JB Julius Bett
 1386. BAJETI 2016/17: Serikali imetenga Sh59 bilioni kutimiza ahadi yake ya kutoa Sh50 milioni kila kijiji. #BajetiTz16

  JB Julius Bett
 1387. BAJETI 2016/17: Agizo la Rais Magufuli kupunguza kodi ya mishahara kutoka asilimia 11 hadi 9 kuanza kutekelezwa Julai Mosi. #BajetiTz16

  JB Julius Bett
 1388. BAJETI 2016/17: Ushuru vinywaji baridi isipokuwa maji ya chupa umepanda kutoka Sh55 kwa lita hadi Sh58 #BajetiTz16

  JB Julius Bett
 1389. BAJETI 2016/17: Ushuru wa bia inayotengenezwa kwa nafaka inayozalishwa nchini umepanda kutoka Sh694 hadi Sh729 kwa lita #BajetiTz16

  JB Julius Bett
 1390. BAJETI 2016/17: Ushuru wa vinywaji vikali umepanda kutoka Sh3,157 hadi Sh3,315 kwa lita. #BajetuTz16

  JB Julius Bett
 1391. BAJETI 2016/17: Ushuru wa sigara inayotumia angalau asilimia 75 ya tumbaku ya TZ umepanda kutoka Sh26,689 hadi Sh28,024 #BajetiTz16

  JB Julius Bett
 1392. BAJETI 2016/17: Serikali kutoza asilimia 10 ada ya zinazotozwa kwa watoa huduma wa kutuma, kupokea fedha kwa njia ya simu #BajetiTz16

  JB Julius Bett
 1393. BAJETI 2016/17: Kodi ya usajili wa gari moja umepanda kutoka Sh150,000 - Sh250,000, pikipiki kutoka Sh45,000 - Sh95,000.#BajetiTz16

  JB Julius Bett
 1394. BAJETI 2016/17: Wakala na taasis zote za usimamizi na udhibiti kuchangia asilimia 15 ya pato lake ghafi serikalini. #BajetiTz16, #Mwananchi

  JB Julius Bett
 1395. BAJETI 2016/17: Waagizaji wa sukari ya viwandani watalipa ushuru zaidi kwa hatua hadi kufikia asilimia 25 mwaka 2018/19 #BajetiTz16

  JB Julius Bett
 1396. BAJETI 2016/17: Hakuna msamaha kwenye ushuru wa wa Barabara, Ushuru wa Petroli na Ushuru wa Bidhaa kwenye mafuta ya petrol #BajetiTz16

  JB Julius Bett
 1397. BAJETI 2016/17: Misamaha ya kodi kwa majeshi ya Ulinzi na Usalama itafutwa, Wanajeshi kupatiwa posho wanunue mahitaji yao wenyewe #BajetiTz16

  JB Julius Bett
 1398. BAJETI 2016/17: Serikali inalenga kukusanya mapato ya ndani Sh18.4 trilioni sawa na asilimia 62.5 ya bajeti yote. #BajetiTZ16

  JB Julius Bett
 1399. BAJETI 2016/17: Serikali kukopa Sh7.4 trilioni kutoka vyanzo vya ndani ili kuziba nakisi ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2016/17 #BajetiTZ16

  JB Julius Bett
 1400. BAJETI 2016/17: Serikali kutumia Sh17.7 trilioni kwa matumizi ya kawaida na Sh11.8 trilioni kwa matumizi ya maendeleo #BAJETITZ2016

  JB Julius Bett
 1401. “Lengo la misaada ni kujazia uwezo wa taifa kutekeleza miradi, upande mwingine misaada inaweza kuwa sumu ya maendeleo” – Mpango #BajetiTZ16

  JB Julius Bett
 1402. KUDHIBITI MISAMAHA: Ili kudhibiti misamaha ya kodi inayotolewa kwa wafanyabiashara, watumishi wa umma, mashirika ya dini na taasisi zisizo za serikali, kuanzia mwaka ujao wa fedha, watalazimika kulipa kodi kwanza kwa bidhaa watakazoagiza, kodi hiyo itarejeshwa kwa wanufaikaji baada ya serikali kujiridhisha bidhaa hizo zimetumika kwa lengo lililokusudiwa. #BajetiTZ16

  Wanaonufaika na misamaha ya kodi, sasa watalipa kodi ya bidhaa walizoagiza kwanza, fedha kurudishwa bidhaa ikitumika ilivyokusudiwa #BajetiTZ16

  JB Julius Bett
 1403. Awamu ya kwanza ya ujenzi wa mradi wa umeme wa Backbone utakaounganisha nchi za Zambia na Kenya unatarajiwa kukamilika Septemba, mwaka huu na kuiwezesha Tanzania kuwa na umeme wa uhakika.

  JB Julius Bett
 1404. Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara imetupilia mbali kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa Jimbo la Newala Mjini iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa CUF, Juma Manguya,dhidi ya mbunge wa jimbo hilo,George Mkuchika (CCM).

  JB Julius Bett
 1405. WATUMISHI HEWA: Mkoani Mbeya kumebainika watumishi hewa 170 ambao wamesababisha hasara ya Sh773.8m, RC Amos Makalla asema leo. Watumishi hao wakopa Sh481m benki.

  JB Julius Bett
 1406. Balozi za Tanzania nchini India na Malaysia zimeiomba wizara ya mambo ya nje ipeleke msaada katika nchi hizo ili iweze kuwarejesha nchini Watanzania waliotelekezwa katika nchi hizo walipokwenda kusaka ajira.

  JB Julius Bett
 1407. Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero imepiga marufuku mbinu zinazotumiwa na baadhi ya wafanyabiashara wasiowaminifu za kununua mazao kwa njia za lumbesa hali inayofanya wakulima kuendelea kudidimia kiuchumi.

  JB Julius Bett
 1408. Vijana, wadau na wanaharakati wamefungua vikundi vya mtandao wa kijamii kwa ajili ya kuchanga fedha za kumsaidia kijana wa Arusha aliyepatikana na hatia ya kumtukana Rais na kuhumiwa faini ya Sh7 milioni au kifungo.

  JB Julius Bett
 1409. Chama cha Wakulima wa Miwa wa bonde la Ruhende (RCGA) wilayani Kilosa, wameziomba mamlaka husika kutatua mgogoro wa muda mrefu wa chama hicho unaosababishwa na tuhuma za ubadhirifu.

  JB Julius Bett
 1410. BUNGENI: Kwa siku ya 9 mfululizo leo, wabunge wote wa upinzani wametoka nje ya Ukumbi wa Bunge wakigomea kushiriki vikao vinavyoongozwa na Naibu Spika.

  JB Julius Bett
 1411. MAUAJI DODOMA: Mkazi mmoja wa Kijiji cha Chololo, Dodoma amemuua kwa kumchinja mke wake usiku wa kuamkia leo, Diwani Christina Mulugu athibitisha.

  JB Julius Bett
 1412. AJALI TABORA: Basi la Kisbo kutoka Mwanza kwenda Dar lapata ajali Igunga Tabora leo, hadi sasa hakuna vifo, majeruhi wapelekwa Hospitali ya wilaya Igunga.

  JB Julius Bett
 1413. Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imedhamiria kumsaka nyoka aina ya chatu anayeishi karibu na Mto Mzinga ambaye amekuwa tishio kwa wakazi wa eneo la Lubakaya, Kata ya Zingiziwa.

  Nyoka huyo amekuwa akionekana kati ya saa 12 hadi saa 1 jioni akitokea kwenye mto huo na kuelekea kwenye makazi ya watu kula mifugo, jambo ambalo linahatarisha maisha ya wakazi wa eneo hilo.
  JB Julius Bett
 1414. TAMKO LA CHADEMA: Viongozi wa kitaifa Chadema waafikiana jijini Mwanza kufungua kesi Korti Kuu kupinga zuio la mikutano, N/Katibu Mkuu-Z’bar Salum Mwalimu asema.

  JB Julius Bett
 1415. Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), amewataka Watanzania kutoa taarifa katika ofisi hizo wanapoona kuna miradi iliyotekelezwa chini ya viwango au hewa ili iweze kufanyiwa
  ukaguzi.

  JB Julius Bett
 1416. Rais John Magufuli amemwapisha Jaji Shaaban Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Ikulu jijini Dar es salaam.

  Taarifa iliyotolewa leo na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, imesema kabla ya kuteuliwa na kuapishwa kuwa Jaji wa Mahakama yaRufani, Jaji Lila alikuwa Jaji Kiongozi.

  Wakatihuohuo, RaisMagufuli amemwapisha Jaji Ferdinand Wambali kuwa Jaji Kiongozi.

  Kabla ya kuteuliwa na kuapishwa Jaji Wambali alikuwa Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto mkoani Tanga na anachukua nafasi ya Jaji Lila.

  JB Julius Bett
 1417. SUGU KIKAANGONI BUNGENI

  Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ameitaka Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuchunguza tuhuma dhidi ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu anayedaiwa kuwaonyeshea kidole cha kati wabunge wa CCM.

  Sugu anadaiwa kufanya kitendo hicho June 6, mwaka huu alipokuwa akitoka katika ukumbi wa Bunge baada ya kuwasilisha maoni ya kambi ya upinzani kuhusu azimio la bunge kuridhia mkataba wa kimataifa wa udhibiti wa matumizi ya dawa na mbinu za kuongeza nguvu michezoni.

  Naibu Spika ameitaka kamati hiyo kumchukulia hatua kali kama watamkuta na hatia ya kufanya kitendo hicho.

  Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 1418. WABUNGE CCM WAICHARUKIA SERIKALI
  KWA KUTAKA KUKATA KODI MAFAO YAO

  Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamezugumza kwa hisia kali walipokuwa wakipinga hatua ya serikali kutaka kuwakata kodi mafao yao watakapomaliza kazi ya ubunge mwaka 2020.

  Wabunge hao wamesema hawatakubali kuona wanakatwa kodi mafao yao na serikali walipokuwa wakichangia mjadala bungeni wa kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017, mji Dodoma leo.

  Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 1419. AJALI SAME: Watu 6 wafa, 8 wajeruhiwa baada ya Hiace walilosafiria kuligonga lori eneo la Njoro usiku wa kuamkia leo, Dk Casto Mlay Hosp. ya Same athibitisha.

  JB Julius Bett
 1420. MNADA WA NG’OMBE: Ng’ombe 603 waliokamatwa mwezi Machi kwenye hifadhi ya Kigosi wilayani Bukombe wanapigwa mnada leo kwa amri ya Mahakama ya Wilaya hiyo.

  JB Julius Bett
 1421. Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), imekanusha taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa imesitisha ajira za ualimu kwa mwaka wa fedha 2016/17.

  Hivi karibuni taarifa hizo zilieleza kuwa utafiti uliofanywa na Tamisemi umebaini kuwapo kwa ziada ya walimu 7,988 wa masomo ya sanaa na biashara hivyo haitaajiri walimu hao badala wataajiri wa masomo sayansi na hisabati.

  JB Julius Bett
 1422. Mfanyabiashara raia wa Nigeria, Joachim Ikechukwu Ike (36), amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha kilo 6,969.38 za dawa za kulevya aina ya Heroin.

  JB Julius Bett
 1423. UTEUZI WA JPM: Rais John Magufuli leo amteua Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa mambo ya ndani, Charles Tizeba anakua waziri wa Kilimo.

  JB Julius Bett
 1424. MEDEYE AHAMIA UDP: Kada wa Chadema na mbunge wa zamani wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye leo ametangaza kuhamia UDP,asema inasimamia haki na demokrasia

  JB Julius Bett
 1425. KONGAMANO LA BAJETI: Polisi Dar yazuia Kongamano la kujadili bajeti lililopangwa kufanyika leo kwa uratibu wa Chama cha ACT Wazalendo, sababu hazijaelezwa

  JB Julius Bett
 1426. BUNGENI: Kwa wiki ya tatu mfululizo leo, wabunge wote wa upinzani wametoka nje ya Ukumbi wa Bunge wakigomea kushiriki vikao vinavyoongozwa na Naibu Spika.

  JB Julius Bett
 1427. MWENDO KASI DAR: Baadhi ya madereva wa mabasi ya mwendo kasi wamegoma wakipinga kulipwa mshahara wa Sh 400,000 badala ya Sh 800,000 walizokubaliana na uongozi.

  JB Julius Bett
 1428. MAWAZIRI WAAPISHWA: Rais John Magufuli awaapisha Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba na Waziri wa Kilimo Charles Tizeba Ikulu Dar.

  JB Julius Bett
 1429. BREAKING: Prof Ibrahim Lipumba leo ametangaza nia ya kurudia wadhifa wake wa Mwenyekiti Taifa wa CUF, amemuomba Katibu Mkuu atengue maamuzi yake ya kung’atuka katika wadhifa huo mwaka jana.

  JB Julius Bett
 1430. Watu watatu wamekufa maji baada ya boti yao ya uvuvi kuzama ndani ya Ziwa Victoria kutokana na dhoruba kali lililowapiga katika eneo la Nyamkazi Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera.

  Mwenyekiti wa mtaa wa Nyamukazi lilipotokea tukio hilo, Andason Lazaro amesema wavuvi hao waligundulika kuzama maji baada ya kutoonekana tangu Juni 9, mwaka huu.

  JB Julius Bett
 1431. POLISI YACHUNGUZA SUMU OFISINI KWA MEYA: Jeshi la polisi limeanzisha uchunguzi kubaini dhidi ya madai ya kupuliziwa hewa ya sumu ofisini kwa Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza, James Bwire.

  Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema leo kuwa jeshi hilo tayari limewahoji watu kadhaa kuhusiana na tukio hilo lililotokea Juni 13, mwaka huu.

  JB Julius Bett
 1432. KIGODA CHA MWALIMU: Mjadala unapaswa kuwepo kujadili upatikanaji Katiba mpya ilivyokwama, Rais mstaafu Benjamin Mkapa asema UDSM, Tamasha la 8 la J.K Nyerere.

  JB Julius Bett
 1433. Shauri la kupinga amri ya polisi ya kupiga marufuku maandamano na mikutano ya kisiasa iliyofunguliwa na Chadema katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza inaanza kusikilizwa mchana huu baada ya kupangiwa jaji.

  JB Julius Bett
 1434. Mwanaharakati Jenerali Ulimwengu amesema Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete anapaswa kushtakiwa kama viongozi wengine walioisababishia hasara Serikali.

  Akizungumza katika tamasha la Nane la Kigoda cha Mwalimu Nyerere leo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ulimwengu amesema fedha nyingi zimepotea wakati wa kuunda Katiba Mpya ambayo haikupatikana.

  JB Julius Bett
 1435. Serikali imesema zaidi ya Sh1.5 bilioni zilizotakiwa kutumika kwa ajili ya fainali za michuano ya wanafunzi wa shule za msingi (Umiseta) na Sekondari (Umitashumta) zitaelekezwa kwenye utengenezaji wa madawati, baada ya michuano hiyo kusimamishwa.

  JB Julius Bett
 1436. Kutokana na kukua kwa teknolojia ya mtandao, Bodi ya Utalii (TTB) imeamua kuwafuata watalii mtandaoni kwa kuanzisha tovuti na apps ili kutangaza vivutio kwa urahisi.

  Kaimu mkurugenzi wa masoko wa TTB, Philip Chitaunga amesema matangazo yatakayowekwa katika tovuti hiyo yatamsaidia mtalii kujua namna atakavyoweza kusafiri, lakini pia yatahamasisha watalii wengi zaidi kuzuru Tanzania.

  JB Julius Bett
 1437. Watoto wawili wa familia moja kwenye kitongoji cha Nadosoito wilayani Simanjiro wamefariki dunia na wengine wawili kunusurika baada ya kula maandazi yanayosadikiwa kuwa na sumu.

  JB Julius Bett
 1438. Jukwaa la Katiba (Jukata) limeitaka Serikali kutangaza kwenye gazeti la Serikali tarehe ya kuanza upya kwa mchakato wa Katiba mpya.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Jukata, Deus Kibamba amewaeleza waandishi wa habari leo kuwa Serikali pia inatakiwa ipeleke bungeni miswada miwili ili kuhuisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 pamoja na Sheria ya Kura za Maoni 2013.

  JB Julius Bett
 1439. Wanafunzi wa Shule ya Msingi Levolosi, iliyoko kata ya Levolosi mkoani Arusha wakiandamana katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika leo. Picha na Filbert Rweyemamu.

  JB Julius Bett
 1440. POLISI KWA GWAJIMA: Polisi 6 ndani ya Landcruiser wako nje ya nyumba ya Askofu Josephat Gwajima huko Salasala, jijini Dar muda huu. Wasema wamegonga geti bila kufunguliwa. Zaidi kukujia

  JB Julius Bett
 1441. AJALI DAR: Watu 2 wajeruhiwa baada ya gari dogo kutoka Mwenge kwenda Tegeta kugonga bajaj leo eneo la Makonde na kukimbia. Majeruhi wakimbizwa Lugalo Hospital.

  JB Julius Bett
 1442. MAJALIWA: KILA MKOA UUNDE KAMATI YA AMANI

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza kila mkoa kuunda kamati ya amani kwa lengo la kudumisha amani na utulivu nchini.

  JB Julius Bett
 1443. MATOKEO EURO 2016: Daniel Sturridge afunga bao dakika za majeruhi na kuipa England ushindi wa 2-1 dhidi ya Wales. Bale aifungia Wales, Jamie Vardy akasawazisha.

  JB Julius Bett
 1444. Tanzania itafungua ofisi ya ubalozi nchini Qatar kwa lengo la kuendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo.

  Rais John Magufuli amesema hayo leo alipokutana na na balozi wa Qatar nchini, Abdallah Jassim Al Maadadi.

  JB Julius Bett
 1445. URATHI WA NYERERE:Waziri Mkuu Mstaafu Salim A. Salim azindua kitabu cha insha 3 za falsafa za Mwl Nyerere, jijini Dar katika kongamano la urathi wa Mwl Nyerere.

  JB Julius Bett
 1446. UHAMIAJI HARAMU: Wahamiaji Haramu 58 raia wa Ethiopia wamekamatwa usiku wa kuamkia leo Makurunge Bagamoyo wakiwa kwenye shimo, Diwani wa Makurunge athibitisha.  JB Julius Bett
 1447. WABUNGE WASIMAMISHWA:Bunge limewasimamisha wabunge wa Chadema Suzan Lyimo kutohudhuria vikao 5 na Anatropia Theonest vikao 3 kwa kosa la kusema uongo Bungeni.

  JB Julius Bett
 1448. UZINDUZI WA UDHAMINI WA SPORTS EXTRA NDONDO CUP KUPITIA GAZETI LA MWANASPOTI

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) Francis Nanai (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 50 kwa Mratibu wa michuano ya Ndondo, Shafii Dauda wakati wa hafla ya uzinduzi wa udhamini wa Sports Extra Ndondo Cup kupitia Gazeti la Mwanaspoti jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kushoto ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwanaspoti, Abdul Mohamed na Katibu wa DFRA, Msanifu Kondo. Picha na Venance Nestory

  JB Julius Bett
 1449. Meneja Masoko wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) Sara Munema akizungumza wakati wa uzinduzi wa udhamini wa Sports Extra Ndondo Cup kupitia Gazeti la Mwanaspoti jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa MCL. Francis Nanai, Mratibu wa michuano ya Ndondo, Shafii Dauda, Katibu wa DFRA,Msanifu Kondo. Picha na Venance Nestory

  JB Julius Bett
 1450. Meneja Masoko wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) Sara Munema akizungumza wakati wa uzinduzi wa udhamini wa Sports Extra Ndondo Cup kupitia Gazeti la Mwanaspoti jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja wa Chumba cha Habari MCL, Daniel Mwaijeha, Mkurugenzi Mtendaji wa MCL. Francis Nanai, Mratibu wa michuano ya Ndondo, Shafii Dauda, Katibu wa DFRA,Msanifu Kondo na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwanaspoti, Abdul Mohamed. Picha na Venance Nestory

  JB Julius Bett
 1451. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) Francis Nanai akizungumza wakati wa uzinduzi wa udhamini wa Sports Extra Ndondo Cup kupitia Gazeti la Mwanaspoti jijini Dar es Salaam leo. Kushoto Meneja Masoko wa MCL, Sara Munema Mratibu wa michuano ya Ndondo, Shafii Dauda, Katibu wa DFRA, Msanifu Kondo na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwanaspoti, Abdul Mohamed. Picha na Venance Nestory

  JB Julius Bett
 1452. LIPUMBA KUREJEA CUF: Mwenyekiti Kamati ya uongozi CUF Taifa, leo amesema Prof.Lipumba hana haki ya kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu, ili kurejea nafasi yake.

  JB Julius Bett
 1453. MZAMBIA AIKUBALI YANGA: Straika raia wa Zambia, Obrey 'Cholo' Chirwa usiku huu amesaini mkataba wa miaka miwili kuichazea klabu ya Yanga, uongozi wathibitisha.

  JB Julius Bett
 1454. TEMBO SERENGETI: Makundi ya tembo yavamia vijiji vitatu wilayani Serengeti, waua mtu 1 na kuharibu mazao, juhudi za kuwaondoa zinaendelea, DC Maftah Ally aeleza.

  JB Julius Bett
 1455. POLISI WATAWANYA MAHAFALI YA WANAFUNZI WA CHADEMA WA VYUO VIKUU VYA DODOMA

  Jeshi la Polisi mkoani Dodoma leo limewatawanya wanafunzi ambao ni wafuasi wa Chama cha Chadema wanaosoma vyuo vikuu mkoani humo walikuwa wakishiriki hafla ya mahafali katika Hotel ya African Dream.

  Katika hafla hiyo mgeni rasmi alitalajiwa kuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ambapo baadhi ya wanafunzi walikamatwa baada ya kuwambiwa watawanyike na kurudi majumbani kwao.

  Picha na Edwin Mjwahuzi

  JB Julius Bett
 1456. MAHAFALI DODOMA: Polisi mkoani Dodoma wawatawanya wanafunzi wa vyuo vikuu wanachama wa Chadema kwa kufanya mahafali bila kibali ukumbi wa African Dream.

  JB Julius Bett
 1457. Zaidi ya watoto 100 wilayani Kibaha mkoani Pwani wanatarajia kuingizwa kwenye akaunti ya watoto kupitia Benki ya CRDB Tawi la Kibaha, lengo likiwa ni kuwawezesha kuwa na uhakika wa kumudu gharama za masomo kwa kipindi cha baadaye.

  JB Julius Bett
 1458. Mtu anayesadikiwa kuwa jambazi ameuawa kwa kupigwa risasi wakati akifanya jaribio la kuwatoroka polisi waliomkamata akiwa na silaha ya kivita aina ya AK 47 aliyoficha kwenye mfuko wa kuwekea kompyuta mpakato.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo amemtaja aliyekamatwa na silaha hiyo kuwa alitambulika kwa jina la Benjamin Wales (Singano).

  JB Julius Bett
 1459. Machafuko ya kisiasa yanayoendelea nchini Burundi yametajwa kuathiri ujio wa watalii wa nje katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi iliyopo wilayani Mpanda mkoani Katavi.

  Kaimu Mhifadhi Mkuu wa hifadhi hiyo, Fredrick Mofulu ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea hifadhi hiyo ambayo ni moja ya zilizopo Kanda ya Magharibi inayopakana na nchi za Rwanda na Burundi .

  JB Julius Bett
 1460. Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli amekabidhi chakula kwa ajili ya futari wakati huu wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa vituo vinne vya kulea watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu Jijini Dar es salaam.

  Vyakula hivyo vimekabidhiwa leo katika ofisi ya Mke wa Rais Ikulu jijini Dar es salaam vinajumuisha mchele kilo 500, sukari kilo 500 na tende kilogramu 28.

  JB Julius Bett
 1461. U/KITI CCM: CCM imetangaza kuwa mkutano mkuu wa kufanya makabidhiano ya Uenyekiti wa chama kutoka kwa Kikwete kwenda kwa Rais Magufuli utafanyika Julai 23, 2016

  JB Julius Bett
 1462. BUNGENI: Wabunge wa upinzani waziba midomo yao kwa karatasi na utepe na kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge wakigomea kushiriki vikao vinavyoongozwa na Naibu Spika.

  JB Julius Bett
 1463. AJALI MOROGORO: Watu 5 wamekufa, 27 wajeruhiwa leo baada ya basi la NBS toka Dar kwenda Tabora kupinduka huko Chakwale wilayani Gairo, polisi yathibitisha.

  JB Julius Bett
 1464. JELA MAISHA: Korti ya Wilaya ya Ilala leo imemuhukumu kifungo cha maisha jela, Siasa R. Mwinyi (40) baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka 9.

  JB Julius Bett
 1465. HAKIJAELEWEKA CHADEMA: Chadema wapeleka Korti Kuu Mwanza ombi la kufungua upya shauri kupinga polisi kuzuia mikutano baada ya ombi la awali kutupiliwa mbali.

  JB Julius Bett
 1466. RISASI ZANASWA MORO: Polisi wakamata risasi 853 zikiwa zimefichwa pembeni mwa mto Ngerengere mijini Morogoro, kaimu kamanda Leonce Rwegasira athibitisha.

  JB Julius Bett
 1467. BOSI MPYA TSN: Rais John Magufuli leo amemteua Dk Jim James Yonazi kuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Ikulu yasema.

  JB Julius Bett
 1468. Kanisa Kuu la Pentekoste katika Mamlaka ya Mji Muleba mkoani Kagera, ambalo lilikuwa limefikia hatua ya kuezekwa limeporomoka kutokana na madai ya kujengwa chini ya kiwango.

  JB Julius Bett
 1469. Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella ametaka wawekezaji wababaishaji kwenye sekta ya madini wasipewe nafasi, kwani wanaweza kuzuia maeneo makubwa bila kuyatumia na kusababisha migogoro na wananchi.

  JB Julius Bett
 1470. Naibu Spika, Dk Tulia Ackson leo ameonekana kuchoka kitendo cha wabunge wa Ukawa kususia vikao vyake na kuwataka watoke haraka bungeni kama hawahitaji kuendelea na kikao.

  JB Julius Bett
 1471. AJALI YAUA KAGERA: Wanyarwanda 3 wateketea kwa moto baada ya lori la mafuta likielekea Rwanda kupinduka na kuwaka moto leo Rusumo, Ngara, polisi yathibitisha.

  JB Julius Bett
 1472. HOFU YA ZIKA: Mcheza gofu namba 3 kwa ubora duniani Rory McIlroy ajiondoa kushiriki michezo Rio Olympics mwaka huu huko Brazil akihofia ugonjwa wa Zika.

  JB Julius Bett
 1473. KESI YA MWANGOSI: Mahakama Iringa yamkuta askari Kikosi cha Kutuliza Ghasia, Pasificus Simon na kesi ya kujibu kwenye Kesi ya mauaji ya mwandishi wa habari Daudi Mwangosi.

  JB Julius Bett
 1474. RIPOTI YA UCHAGUZI: Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi NEC Jaji Damian Lubuva leo amekabidhi ripoti ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa Rais Magufuli Ikulu

  JB Julius Bett
 1475. Mwenyekiti wa NEC amesema mchakato wa kura ya maoni upo palepale na kwa sasa tume ya uchaguzi itajikita zaidi katika kuboresha mchakato huo.

  JB Julius Bett
 1476. RIPOTI YA UCHAGUZI: Rais Magufuli amesema Sh12b zilizopatikana kama chenji baada ya uchaguzi zitatumika kujenga Jengo jipya la Tume ya Uchaguzi mjini Dodoma.

  JB Julius Bett
 1477. RIPOTI YA UCHAGUZI: Rais Magufuli amesema kuwa marais wastaafu nchini watalindwa dhidi ya tuhuma zote na kuhakikisha hawanyayasiki baada ya kustaafu.

  JB Julius Bett
 1478. NYARA ZA SERIKALI: Korti ya Manyara imemhukumu kwenda jela miaka 20 mkazi wa Kondoa Dodoma baada ya kukutwa na nyara za Serikali zenye thaman ya Sh 5.3m.

  JB Julius Bett
 1479. Shule mbalimbali za msingi katika Manispaa ya Ilemela, Mwanza zimegawiwa madawati 2600 kwa ajili ya kuepuka wanafunzi kukaa sakafuni.

  Akikabidhi madawati hayo, Meya wa Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga amesema manisapaa hiyo ina kata 19 na shule za msingi 74.

  JB Julius Bett
 1480. Mkazi wa Kijiji cha Nyangamalila wilaya ya Buchosa mkoani Mwanza, Mariam Mathias (35), amekutwa amekufa katika mazingira ya kutatanisha kwenye Msitu wa Buhindi uliopo Wilaya ya Buchosa mkoani Mwanza.

  JB Julius Bett
 1481. KIZIMBANI KWA UTAPELI: Waganga 3 wafikishwa kortini Kisutu, Dar leo, wadaiwa kumtapeli mwanamke Sh260m kwa ahadi ya kumwezesha kupata watoto, kuolewa, biashara.

  JB Julius Bett
 1482. VARDY KUBAKI KINGS POWER: Leicester City yatangaza mshambuliaji wake Jamie Vardy amekubali kuongeza mkataba wa miaka 4 kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya EPL.

  JB Julius Bett
 1483. MAAFA CHINA: Watu 51 wafa, kadhaa wajeruhiwa leo baada ya kimbunga kupiga mji wa Yancheng uliopo katika jimbo la Jiangsu, chombo cha serikali ya China charipoti.

  JB Julius Bett
 1484. UINGEREZA KUJITOA EU: Matokeo yaonesha asilimia 52% ya Waingereza wamepiga kura kutaka kujitoa katika Umoja wa Ulaya huku 48% wakitaka kubaki katika umoja huo

  JB Julius Bett
 1485. UINGEREZA KUJITOA EU: Paundi ya Uingereza yaanguka dhidi ya dola ya Marekani baada ya kura ya kujitoa EU, anguko hilo halijapata kutokea tangu mwaka 1985.

  JB Julius Bett
 1486. SERIKALI KUMILIKI TTCL: Airtel Tanzania leo imesaini makubaliano kuuza asilimia 35 ya hisa zake ndani ya TTCL na kuiachia Serikali umiliki wa asilimia 100.

  JB Julius Bett
 1487. Uimarishaji wa Mfumo wa Rufaa kupitia Mitandao ya Simu ya Mkononi - CCBRT & Timu ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam yazindua mradi

  Mpango mpya umezinduliwa leo, 24 Juni 2016, kuimarisha mfumo wa rufaa jijini Dar-es-Salaam na kuboresha mawasiliano kati ya vituo vya huduma za afya, ili kuhakikisha akina mama na watoto wachanga wanapata huduma bora na matibabu wanayohitaji. Kamati ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam, ikishirikiana na CCBRT, wanapambana na tatizo la mawasiliano hafifu kati ya zahanati, vituo vya afya na hospitali. Hii hupelekea rufaa ya wagonjwa usio na mpangilio na ucheleweshaji wa huduma na matibabu. Mpango huu utatumia teknolojia ya simu ya mkononi na mfumo maalum wa watumiaji [Closed User Group (CUG)]. Vituo 23 na magari ya wagonjwa saba (7) yataunganishwa na mfumo huu wa simu, pamoja na ofisi za waganga wakuu wa wilaya na mratibu wa timu ya afya ya mkoa. Hii itasaida wawakilishi wa vituo vidogo na vituo vikubwa vya huduma za afya kuwasiliana kupitia mfumo huu na kuwapa taarifa wafanyakazi wa vituo husika kuwa kuna mgonjwa yuko njiani, wanaweza pia kupata ushauri wa kitaalam jinsi ya kumhudumia mgonjwa njiani, kutoa taarifa ya mgonjwa, kusaidia kufanya maamuzi kwa pamoja kwa kuzingatia viwango na kuwasiliana moja kwa moja na magari ya wagonjwa. Watumiaji wa simu kutoka vituo 23 na madereva wa magari saba (7) ya wagonjwa wamepewa mafunzo ya siku moja na CCBRT kuhusu namna ya kutumia simu na jinsi ya kupanga vigezo vya rufaa. Mfumo huu maalum pia itasaidia kuimarisha mfumo mzima kwa kutoa taarifa na kuelimisha vituo vingine kuhusu mpango huu ndani ya vituo hivi 23 kupitia ujumbe na picha za Whatsapp

  JB Julius Bett
 1488. UZINDUZI DAR: Rais John Magufuli azindua rasmi kituo cha mawasiliano cha polisi jijini Dar.

  JB Julius Bett
 1489. UZINDUZI DAR: Rais Magufuli ashangaa kutomuona Meya wa Kinondoni Boniphace Jacob (Chadema) kwenye uzinduzi wa Mpango wa Usalama wa Jamii Viwanja vya Biafra Dar.

  JB Julius Bett
 1490. FAINALI ZA AFRIKA: Timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys yaifunga Shelisheli goli 3-0 Uwanja wa Taifa, ni mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika.

  JB Julius Bett
 1491. KITWANGA AKABIDHI: Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga leo amekabidhi rasmi ofisi kwa waziri mpya wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba.

  JB Julius Bett
 1492. VURUGU DAR: Polisi watumia mabomu ya machozi kutawanya mashabiki waliovunja mageti uwanja wa Taifa kuona Yanga v. Mazembe. Mageti yafungwa baada ya uwanja kujaa

  JB Julius Bett
 1493. AJALI MWANZA: RPC Msangi asema majeruhi 5 wamekimbizwa Bugando Hospital, 8 wanatibiwa Misungwi baada ya basi la Super Sami kuanguka. Abiria walalamika kuporwa.

  JB Julius Bett
 1494. AJALI YAUA MWANZA: Watu 5 wafa, 13 wajeruhiwa kuamkia leo baada ya basi la Super Sami toka Dar-Mwanza kugonga mawe na kuanguka Misungwi, RPC Msangi athibitisha.

  JB Julius Bett
 1495. NI KUFA AMA KUPONA TAIFA: 🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥

  MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, JCB aliwahi kuimba Ukisikia Paaa.. Ujue imekukosa, kwani aliyekulenga hana shabaha....!

  Ndivyo ambavyo jioni ya leo inatarajiwa kutokea kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Wawakilishi wa Tanzania, Yanga itakapoumana na TP Mazembe katika pambano la kukata na soka la michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
  Hilo litakuwa pambano la pili kwa timu hizo zilizopo Kundi A pamoja na timu za MO Bejaia ya Algeria na Medeama ya Ghana.

  JB Julius Bett
 1496. YANGA v. TP MAZEMBE: Msemaji wa TFF Alfred Lucas asema uwanja wa Taifa Dar umejaa, hivyo walioko nje warudi kwao. Ataka walioko nyumbani wasiende Taifa.

  JB Julius Bett
 1497. Juma Mahadhi anaziba pengo la Simon Msuva, Obrey Chirwa anaanza mbele na Ngoma, Kiraka Twite anazuia kushoto.

  JB Julius Bett
 1498. KESI YA UCHAGUZI: Korti Kuu Mbeya yamtangaza Saul Amon (CCM) kuwa ni mbunge halali wa Rungwe baada ya kushinda kesi iliyofunguliwa na John Mwambigija (Chadema).

  JB Julius Bett
 1499. LISSU KORTINI: Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu na wenzake 3 wamepandishwa katika Korti ya Kisutu leo na kusomewa mashtaka ya uchochezi.

  JB Julius Bett
 1500. 10' Kona ya kwanza kwa Yanga, Juma Mahadhi aliambaa na mpira kabla ya kutolewa kwenye reli na kuwa kona mfu.

  JB Julius Bett
 1501. Yanga 0 - 0 TP Mazembe | Mchezo ni dakika ya 37 kipindi cha kwanza.

  JB Julius Bett
 1502. LISSU POLISI: Mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chadema, Tundu Lissu aitwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar kwa mahojiano. Taarifa zaidi kukujia.

  JB Julius Bett
 1503. MAGARI YA TOYOTA: Kampuni ya magari ya Japan, Toyota yaagiza magari 1.43 milioni aina ya Prius, Lexus kurejeshwa kiwandani kutokana na hitilafu ya mfumo wa hewa

  JB Julius Bett
 1504. VIAPO IKULU: Uteuzi DC Serengeti Emile Ntakamulenga watenguliwa baada ya kuteuliwa kimakosa, Nurdin Babu ajaza nafasi. Rais Magufuli awaapisha ma- RC wateule.

  JB Julius Bett
 1505. NANGOLE APOTEZA UBUNGE: Korti Kuu Arusha yamvua ubunge wa Longido Onesmo Ole Nangole (Chadema), yabainika fujo zilitokea katika chumba cha kujumlishia matokeo.

  JB Julius Bett
 1506. LISSU RUMANDE: Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu apelekwa rumande baada ya kuhojiwa na polisi Dar kutokana na maneno aliyotoa dhidi ya Rais Magufuli

  JB Julius Bett
 1507. SUGU AADHIBIWA: Bunge limemsimamisha Mbunge Joseph Mbilinyi kutohudhuria vikao 10 vya Bunge la 11 kwa kosa la kutukana kwa kuonesha kidole cha kati bungeni.

  JB Julius Bett
 1508. KUBENEA AADHIBIWA: Bunge limemsimamisha Mbunge Saed Kubenea kutohudhuria vikao 5 vya Bunge la 11 kwa kosa la kusema uongo Bungeni.

  JB Julius Bett
 1509. OLE MILLYA AADHIBIWA: Bunge limemsimamisha Mbunge James Ole Millya kutohudhuria vikao 5 vya Bunge la 11 kwa kosa la kusema uongo bungeni.

  JB Julius Bett
 1510. CHINI YA ULINZI: Watu watatu wakamatwa leo mahakamani Kisutu, Dar wakituhumiwa kubeba mabango yenye ujumbe wa kulikashifu Jeshi la Polisi.

  JB Julius Bett
 1511. MURO MATATANI: Msemaji wa Jerry Muro aitwa kujieleza akituhumiwa kupingana na maamuzi, kuishambulia TFF kwenye vyombo vya habari, Katibu Mkuu Mwesigwa asema.

  JB Julius Bett
 1512. HATUA TBS: Waziri wa Viwanda Mwijage awasimamisha kazi Mkurugenzi TBS Joseph Masikitiko, Meneja Fedha E. Ntelya kupisha uchunguzi. Dk Mubofu wa UDSM akaimu ukuu

  JB Julius Bett
 1513. WATUMISHI HEWA: Machi hadi Juni, jumla ya watumishi hewa 274 wamebainika Kagera, wagharimu Sh3.3bn, RC Salum Kijuu asema leo. Idara ya Afya kinara kwa kuwa watumishi hewa 139, ambao pekee wamesababisha hasara ya Sh2.1bn.

  JB Julius Bett
 1514. AJALI MOROGORO: Watu 11 wafariki na wengine kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha lori la mafuta na basi la Ota, Dakawa Morogoro leo alfajiri Polisi yathibitisha.

  JB Julius Bett
 1515. KAGAME ATUA DAR: Rais wa Rwanda Paul Kagame amewasili asubuhi hii jijini Dar kwa ziara maalum ya siku 2 nchini, kufungua Maonyesho ya Kimataifa ya Sabasaba leo.

  JB Julius Bett
 1516. SAKATA LA DC: RC wa Songwe Chiku Galawa athibitisha kupata taarifa kutoka Ikulu ya kumwapisha John Palingo kuwa DC wa Mbozi, asema hana taarifa za Ally Maswanya

  JB Julius Bett
 1517. TANZIA: Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kilindi-Tanga, Beatrice Shelukindo amefariki dunia jana usiku Arusha, M/Kiti CCM Wilaya Kilindi Bakari Kingalangala athibitisha.

  JB Julius Bett
 1518. AJALI RUVUMA: Watu tisa wahofiwa kufa, 40 waokolewa baada ya boti walilosafiria kuvuka Mto Ruvuma kuzama jana usiku, Kamati ya Ulinzi Mkoa yaenda kwenye tukio.

  JB Julius Bett
 1519. AJALI YA SINGIDA: Mabasi 12 ya kampuni ya City Boy ambayo magari yake 2 yalihusika kwenye ajali iliyoua watu 30 jana Manyoni yamefungiwa, Sumatra yatangaza leo.

  JB Julius Bett
 1520. JUNO YATUA JUPITER: Satelaiti Juno ya shirika la anga la Marekani, NASA yatua sayari ya Jupiter leo alfajiri kwa ajili ya kuichunguza. Satelaiti hiyo imesafiri kwa miaka mitano na inatarajiwa kuwa kwenye sayari hiyo kubwa zaidi ulimwenguni, Jupiter, kwa takribani mwaka mmoja na nusu.

  JB Julius Bett
 1521. Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB Prof. William Lyakurwa.

  JB Julius Bett
 1522. RUNGU LA TCRA: Mamlaka ya Mawasiliano ya (TCRA) leo yatangaza kuzipiga faini ya Sh642 milioni kampuni 6 za simu kwa madai ya kuuza namba za simu bila kuzisajili

  JB Julius Bett
 1523. Siku moja baada ya kutokea ajali ya mabasi iliyosababisha vifo vya watu 30 na majeruhi kadhaa, Kampuni ya mabasi ya City Boy imefungiwa kufanya biashara hiyo kwa muda usiojulikana.

  JB Julius Bett
 1524. Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (Rahco), imetoa notisi ya siku 30 kwa wananchi waliovamia maeneo ya reli jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza wakati kazi hiyo ikifanyika leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Rahco, Dk Mussa Mgwatu amesema hatua hiyo ni kutekeleza Sheria ya Reli Na.4 ya Mwaka 2002 inayokataza watu kujenga karibu na njia za reli.

  JB Julius Bett
 1525. RISITI ZA EFD: Korti ya Ilala yawahukumu wafanyabiashara 2 wa Kariakoo kifungo cha miaka 3 jela kila mmoja kwa kuuza bidhaa bila kutoa risiti za Kieletroniki.

  JB Julius Bett
 1526. UJAMBAZI NGARA:Watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi usiku wa kuamkia leo wameteka kijiji cha Benako mkoani Kagera na kupora fedha, mmoja ajeruhiwa, polisi yasema

  JB Julius Bett
 1527. MAMEYA WAADHIBIWA: Korti ya Ufaransa imewahukumu kifungo cha maisha mameya wawili wa zamani wa Rwanda kwa hatia ya kuhusika na mauaji ya kimbari mwaka 1994.

  JB Julius Bett
 1528. Rais John Magufuli leo tarehe 07 Julai, 2016 amefanya uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri za majiji 5, Manispaa 21, Miji 22 na Wilaya (DC) 137 za Tanzania Bara.

  JB Julius Bett
 1529. MAREKEBISHO YA UTEUZI: Ikulu yatangaza marekebisho madogo ya uteuzi wa wakurugenzi uliofanyika leo, Dk Leonard Massale atabaki kuwa DC wa Ilemela, awali aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Manispaa ya Dodoma.

  JB Julius Bett
 1530. AJALI YA SINGIDA: Mmoja wa madereva wa mabasi ya City boys yaliyohusika katika ajali iliyoua abiria 32 Maweni Singida, afikishwa mahakamani leo asubuhi

  JB Julius Bett
 1531. Rais John Magufuli amemteua Dk Leonard Lutegama Maboko kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS).

  JB Julius Bett
 1532. UHAKIKI WA VYETI: Wakurugenzi wapya walioteuliwa na Rais Magufuli wametakiwa kupeleka Ikulu vyeti vyao halisi vya taaluma kwa uhakiki, taarifa ya Ikulu yasema leo

  JB Julius Bett
 1533. MALIPO HEWA:Katibu Mkuu Mambo ya Ndani amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Frank Msaki kwa madai ya kulipa malipo hewa.

  JB Julius Bett
 1534. DAKTARI FEKI ANASWA: Mkazi wa Tungi mjini Morogoro anayesadikiwa kuwa daktari feki akamatwa leo katika Hospitali ya Rufaa Morogoro, Kamanda Ulrich Matei asema.

  JB Julius Bett
 1535. USAFIRI WA ANGA: Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Anga itatumia fedha zake kununua na kufunga rada mbili za kisasa Dar na Mwanza katika mwaka huu wa fedha, Mkurugenzi Mkuu Hamza Johari amesema

  JB Julius Bett
 1536. KIAPO CHA UADILIFU: Wakurugenzi wateule 185 walioteuliwa na Rais Magufuli leo wamekula kiapo cha uadilifu kwa maadili ya viongozi wa umma Ikulu jijini Dar.

  JB Julius Bett
 1537. UKUSANYAJI MAPATO: Rais Magufuli leo amewataka Makatibu Wakuu wa wizara zote kusambaza mashine za EFD kila wizara ili zitumike kukusanya mapato ya serikali.

  JB Julius Bett
 1538. KITUO CHAFUNGIWA: Serikali imefungia kliniki ya Fore Plan inayomilikiwa na Tabibu Juma Mwaka kwa kosa la kujitangaza kutoa tiba za kisasa badala ya tiba asili.

  JB Julius Bett
 1539. UDHAMINI LIGI KUU: Kampuni ya Azam Media Limited imeingia makubaliano na TFF kuendelea kudhamini Ligi Kuu Tanzania Bara kwa miaka mitano kwa Sh 23 bn.

  JB Julius Bett
 1540. Baadhi ya wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro wanakabiliwa na wakati mgumu baada ya kutangaza kusitisha rasmi mgawo wa chakula uliokuwa ukifanyika kila siku kwa zaidi ya miaka 10.

  JB Julius Bett
 1541. Chama cha Mapinduzi kimeitaka Serikali kuwafikisha mahakamani mafisadi na watumishi wote wa umma waliofukuzwa kazi kwa sababu mbalimbali, ikiwamo kuisababishia hasara kutokana na watumishi hewa.

  JB Julius Bett
 1542. Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda 305 kwa kukiuka sheria za barabarani kwa kutovaa kofia ngumu, kutokuwa na leseni na kupakia abiria zaidi ya mmoja maarufu kama mishikaki.

  JB Julius Bett
 1543. UKWEPAJI KODI: Mfanyabiasha anayedaiwa kukwepa kodi na kuingiza Milion 7 kwa dakika amefikishwa Korti ya Kisutu mchana huu atasomewa mashtaka baadae.

  JB Julius Bett
 1544. UNUNUZI WA RADA: Mamlaka ya Usafiri wa Anga itanunua na kufunga rada mbili za kisasa Dar na Mwanza mwaka huu wa fedha, Mkurugenz Mkuu, Hamza Johari amesema leo.

  JB Julius Bett
 1545. KESI YA UCHAGUZI: Mahakama ya Rufani leo yaamuru Korti Kuu Mwanza isikilize upya kesi iliyofunguliwa na wananchi kupinga ushindi wa Mbunge wa Bunda Mjini (Chadema), Ester Bulaya.

  JB Julius Bett
 1546. Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula amesema serikali itaanzisha mamlaka itakayodhibiti na kusimamia waendelezaji wa majengo.

  Mabula amesema mamlaka hiyo itakuwa ikitoa miongozo ya uuzaji na upangishaji wa nyumba nchini.

  JB Julius Bett
 1547. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali imelipa Sh36 bilioni, sawa na asilimia 40 kwa ajili ya kununua ndege mbili za shirika la ndege la ATCL.

  JB Julius Bett
 1548. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina amekipa siku 30 Kiwanda cha Saruji cha Twiga kilichopo Wazo jijini Dar es Salaam, kurekebisha mfumo wa utoaji taka.

  Akiwa katika ziara yake ya kutembelea kiwanda hicho, Mpina amesema kinatakiwa kurekebisha mfumo wa utoaji taka ili kunusuru uharibifu wa mazingira na maisha ya viumbe hai.

  JB Julius Bett
 1549. Mwalimu wa Shule ya Msingi Geitasamo, Kata ya Rung'abure wilayani Serengeti Mkoa wa Mara, Raphael Charles (22) amenusurika kifo kwa kucharangwa mapanga kwa tuhuma za kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Ikorongo.

  Mwenyekiti wa Kijiji cha Geitasamo, Marwa Meng’anyi amesema alikatwa mapanga na kaka wa mwanafunzi waliochukizwa na kitendo cha dada yao (jina linahifadhiwa) kukatishwa masomo kwa kupewa ujauzito.

  JB Julius Bett
 1550. Wafuasi wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini, Steven Wassira wamembwaga mahakamani mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Ester Bulaya wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika rufaa yao ya kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kutupilia mbali kesi yao.

  Wafuasi hao, Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Escietik Malagila walifungua kesi ya uchaguzi kupinga ushindi wa Bulaya katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, wakijitambulisha kama wapigakura.

  JB Julius Bett
 1551. Mahakama ya Wilaya ya Ilala imetupilia mbali maombi ya kuzikwa mkoani Tanga mwili wa marehemu Andrew Daffa aliyefariki dunia Jumatano wiki iliyopita katika Hospitali ya Amana, Dar es Salaam.

  JB Julius Bett
 1552. Mazungumzo ya kusaka amani ya mgogoro wa kisiasa ulioikumba nchi ya Burundi yamekumbwa na sintofahamu baada Serikali ya nchi hiyo kugoma kuendelea na awamu ya pili wakiwatuhumu watu watatu wanaotakiwa kukamatwa kwa kusababisha vurugu nchini humo kuwa miongoni mwa wajumbe.

  JB Julius Bett
 1553. MABADILIKO YA TABIANCHI: Itakuwa ndoto Tanzania kuwa ya viwanda iwapo kutakosekana sera thabiti kulinda vyanzo vya asili, Rais mstaafu Kikwete asema jijini Dar.

  JB Julius Bett
 1554. MRADI WA MADAWATI: Naibu Spika Tulia amkabidhi Rais Magufuli madawati 53,450 jijini Dar leo; yatakayosambazwa maeneo yenye upungufu baada ya Bunge kujibana na kuokoa Sh6bn. Rais ayataka majeshi ya Magereza na JKT kukamilisha madawati zaidi ya 60,000 haraka. Fedha hizo zinatarajiwa kufanikisha upatikanaji wa madawati 120,000.

  JB Julius Bett
 1555. Wanafunzi 2,739 mbalimbali hawakujitokeza kuhakikiwa wakati Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ilipofanya shughuli hiyo katika vyuo 26 nchini.

  JB Julius Bett
 1556. WATUMISHI HEWA: Watumishi hewa 315 ambao wameigharimu serikali Sh2.2 bilioni wamebainika Morogoro, RC Kebwe asema. Wilaya ya Kilosa kinara kwa watumishi hewa 98

  JB Julius Bett
 1557. MAGAZETI 473 YAFUNGIWA: Serikali leo imefuta usajili wa magazeti 473 ambayo hayajachapishwa kwa kipindi cha miaka mitatu, Waziri wa Habari, Nape Nnauye atangaza

  JB Julius Bett
 1558. DPP APATA AJALI: Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga anusurika kufa leo baada ya gari alilokuwa akisafiria kupinduka huko wilayani Chato mkoani Geita.

  JB Julius Bett
 1559. VIWANGO FIFA: Tanzania yapanda kwa nafasi 13 na kuwa ya 123 katika viwango FIFA vilivyotoka leo, Uganda 69, Kenya 86, Rwanda 111, Burundi 125. Argentina kinara.

  JB Julius Bett
 1560. SHAMBULIO UFARANSA: Watu 84 wamekufa mapema leo baada ya Lori kugonga kundi la watu katika sherehe za kitaifa za Bastile mjini Nice Ufaransa

  JB Julius Bett
 1561. AJALI SINGIDA: Watu 3 wamekufa huko Manyoni baada ya kugongwa na basi la Osaka leo wakati wakilinda lori lililokuwa limeharibika, polisi kutoa taarifa zaidi baadae.

  JB Julius Bett
 1562. UFISADI MWANZA: RC Mwanza John Mongella amemtaka Waziri wa Kilimo kuivunja bodi ya chama cha ushirika Nyanza kwa madai ya kula pesa za uendeshaji.

  JB Julius Bett
 1563. AJALI SINGIDA: Watu 2 wamekufa na wengine 2kujeruhuiwa baada ya gari aina ya Fuso kugonga gari aina ya Noah Manyoni Singida, polisi kutoa taarifa zaidi baadae

  JB Julius Bett
 1564. MATOKEO YA MTIHANI: Katibu Mkuu Baraza la Mitihani leo ametangaza matokeo ya kidato cha sita, kiwango cha ufaulu kikionesha kushuka kwa 0.93% kulinganisha na matokeo ya mwaka jana.

  JB Julius Bett

 1565. UFISADI MWANZA: Waziri Charles Tizeba amefuta vibali vya kusafirisha mchele nje ya nchi na kuisimamisha Bodi ya Nyanza, aagiza Takukuru kuanza uchunguzi haraka.

  JB Julius Bett
 1566. ZIARA YA KUSTUKIZA: Waziri Nape Nnauye leo amefanya ziara ya ghafla katika jengo linalodaiwa kudurufu CD la Aguster lililopo Kariakoo Dar es Salaam, aagiza duka hilo kufungwa.

  JB Julius Bett
 1567. MSANII POLISI: Msanii Bongo Fleva Emmanuel Elibariki "Ney wa Mitego" ahojiwa na Polisi, Kamanda Kanda Maalum Dar Simon Sirro athibitisha leo bila maelezo zaidi.

  JB Julius Bett
 1568. KOMBE LA SHIRIKISHO: Yanga yashindwa kutumia vema uwanja wake wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Medeama, mechi ya kombe la Shirikisho.

  JB Julius Bett
 1569. KIAPO CHA UADILIFU: Makamanda wa Polisi waliopandishwa vyeo wala kiapo cha uadilifu kwa maadili ya viongozi wa umma Ikulu jijini Dar.

  JB Julius Bett
 1570. M/kiti wa Bodi ya Parole Taifa, Augustine Mrema ataka wananchi wapime utendaji wake ndani ya siku 100. Aahidi kubadilisha tabia za wahalifu

  JB Julius Bett
 1571. KIAPO CHA UADILIFU: Rais Magufuli amtaka IGP Mangu kuwaondoa raia wote wasiowaadilifu wanaofanyakazi ndani ya Jeshi la Polisi.

  JB Julius Bett
 1572. KIAPO CHA UADILIFU: Rais Magufuli awashangaa polisi kushindwa kumkamata Mhasibu aliyejilipa mamilioni ya fedha kupitia wafanyakazi hewa ndani ya Jeshi lao.

  JB Julius Bett
 1573. MOTO MOROGORO: Moto unateketeza Kiwanda cha Nguo cha 21st Century cha Morogoro asubuhi hii, chanzo na hasara hivijajulikana. Zimamoto wapo eneo la tukio.

  JB Julius Bett
 1574. BWANA AFYA ANASWA: Mkuu wa Wilaya Songwe, S. Opulukwa leo awaamuru polisi kumkamata Bwana Afya Kata ya Mkwajuni,H. Matingo baada ya kumkuta amelewa muda wa kazi

  JB Julius Bett
 1575. 382 WAITWA UDOM: Wanafunzi 382 kati ya 7,805 waliokuwa wanasoma Stashahada Maalum Chuo Kikuu Dodoma warejeshwa chuoni kuendelea na masomo, Waziri Ndalichako asema.

  JB Julius Bett
 1576. Balozi wa Uturuki nchini, Yasemin Eralp amelaani mapinduzi ya kijeshi yaliyoshindikana nchini humo akisema yaliandaliwa na kikundi cha kigaidi cha 'Feto’ kinachopigana na Serikali ya Uturuki kwa muda mrefu.

  JB Julius Bett
 1577. Hata wiki haijapita tangu Shule ya Sekondari Kisimiri iibuke ya kwanza kitaifa kwenye matokeo ya Kidato cha Sita imeanza kunufaika na juhudi hizo kwa kupewa misaada.

  Shule hiyo ambayo wanafunzi wake wote 63 waliibuka na ushindi wa daraja la kwanza na la pili, imepata msaada wa nyaya maalumu kwa ajili ya kuwekea uzio kuzunguka shule hiyo.

  JB Julius Bett
 1578. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amesema nafasi hiyo hakuipenda sana lakini kwa kuwa aliombwa na wazee kuchukua nafasi hiyo ya utendaji mkuu wa chama alikuwa hana jinsi.

  JB Julius Bett
 1579. MAUAJI MANYARA: Watu wasiojulikana wamemuua Ofisa wa Takukuru Wilaya ya Kiteto, Evanjelina Samson akiwa nyumbani kwake huko Kibaya, Kamanda Fransis Massawe athibitisha.

  JB Julius Bett
 1580. JIWE LA MSINGI DODOMA: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameweka Jiwe la Msingi la ukarabati na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Dodoma utakaogharimu Sh 11.8bn.

  JB Julius Bett
 1581. UHUJUMU UCHUMI: Waziri Dkt Mwakyembe emesema tangu mwaka 2015 hadi sasa Serikali imepokea kesi 176 za uhujumu uchumi ,watu 12 wameshahukumiwa na faini Sh 29bn

  JB Julius Bett
 1582. KESI YA MWANGOSI: Mahakama kuu Iringa imeahirisha hukumu ya kesi ya mauaji ya Mwandishi Daudi Mwangosi inayomkabili askari Pasificus Simon hadi Julai 25, 2016.

  JB Julius Bett
 1583. UHAKIKI: Watumishi 3600 wa serikali mkoani Pwani hatarini kukosa mishahara ya Agosti kutokana na mapungufu kwenye taarifa zao, Waziri Kairuki amesema leo.

  JB Julius Bett
 1584. OLYMPIC 2016: Korti ya usuluhishi wa Michezo imeikataa rufaa ya kamati ya Olympic ya Urusi kupinga kufungiwa wanariadha wake 68 kushiriki Olympic nchini Brazil

  JB Julius Bett
 1585. Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), John Mnyika (kushoto) na Wakili wa chama hicho, John Mallya wakiwa kwenye ofisi Msajili wa Mahakama ya Afrika Mashariki jijini Arusha kufungua kesi dhidi ya Serikali kwa kupiga marufuku mikutano ya kisiasa. Picha na Filbert Rweyemamu

  JB Julius Bett
 1586. KUNDAMBANDA AFARIKI: Mgombea Ubunge Jimbo la Masasi kupitia CUF 2015 Ismail Makombe “Kundambanda” amefariki usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake Masasi Mtwara CUF yathibitisha

  JB Julius Bett
 1587. MGOMO BUKOBA: Sumatra waingilia kati na kumaliza mgomo ulioanza wa madereva wa mabasi yaendayo mikoani waliopinga wenzao kukamatwa kwa makosa ya mwendokasi.

  JB Julius Bett
 1588. UENYEKITI CCM: Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM waanza kuingia ukumbi wa mkutano kwa ajili ya kupiga kura ya kumchagua mwenyekiti mpya wa chama hicho.

  JB Julius Bett
 1589. MKUTANO MKUU CCM: Mbali na TLP vyama vilivyohudhuria ni Chauma, UDP, ADC, UMD, Jahazi Asilia, Chausta, Updp, AFP, DP, CCK na SAU #Dodoma

  JB Julius Bett
 1590. MKUTANO MKUU CCM: "Wajumbe 2398 kati ya 2412 wamehudhuria mkutano huo ambao ni sawa na asilimia 99.4" Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana

  JB Julius Bett
 1591. Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete ameanza kwa vijembe dhidi ya wenzao ambao hakuwataja kwamba hawana wazee

  JB Julius Bett
 1592. “CCM watarejesha upendo maradufu kwa viongozi wa vyama vya siasa kama walivyoonyesha upendo kwa CCM” Jakaya Kikwete

  JB Julius Bett
 1593. "Hakukuwepo na mkakati wowote wa mimi kukataa kutoka kwenye uenyekiti, vyombo vya habari vilieneza uongo" Kikwete

  JB Julius Bett
 1594. MKUTANO MKUU MAALUM WA CCM: Mkutano Mkuu wa CCM umemchagua Rais John Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho kwa jumla ya kura zote 2,398 zilizopigwa

  JB Julius Bett
 1595. ADHABU YA MGOMO: Polisi yawafutia leseni madereava 18 wa mabasi waliogoma mkoani Kagera juzi; Sumatra watoa siku 7 kwa wamiliki kujieleza kwa nini wasifutiwe leseni za biashara.

  JB Julius Bett
 1596. UHAMIAJI HARAMU: Idara ya Uhamiaji Mtwara inawashikilia wahamiaji 18 raia wa Ethiopia kwa kuingia nchini bila kibali Naibu Kamishna Uhamiaji Mtwara athibitisha.

  JB Julius Bett
 1597. MGOMO WA DALADALA: Madereva daladala Mwanza leo wamegoma kusafirisha abiria baada ya kuzuiwa kuegesha chini ya bango Nyegezi, abiria watumia Pikipiki kusafiri.

  JB Julius Bett
 1598. MGOMO WA DALADALA: Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza leo limelazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya madereva wa daladala waliokua wakifanya mgomo

  JB Julius Bett
 1599. KOFFI OLOMIDE AKAMATWA: Mwanamuziki mashuhuri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Koffi Olomide amekamatwa akiwa nyumbani kwake mjini Kinshasa.

  JB Julius Bett
 1600. MAWAKILI WAANDAMANA: Mawakili Mkoani Arusha wameandamana wakipinga kukamatwa kwa wakili Shilinde Ngalula aliyekwenda Loliondo kuwatetea watuhumiwa wa uchochezi.

  JB Julius Bett
 1601. KESI YA MWANGOSI: Korti Kuu Iringa leo imemuhukumu askari, Pasificus Simon kifungo cha miaka 15 jela baada ya kumtia hatiani kwa mauaji ya bila kukusudia ya Daud Mwangosi.

  JB Julius Bett
 1602. KESI YA MASHA: Mahakama wilayani Mpanda yamwachia huru Lawrence Masha na wenzake baada ya kuona hawana hatia, Wakili Albert Msando asema.

  JB Julius Bett
 1603. UJAMBAZI NGARA: Polisi Ngara inamshikilia mtu mmoja anayedaiwa kusafirisha majambazi waliovamia kijiji cha mabawe na kuua mtu mmoja na kumjeruhi mwanafunzi usiku wa kuamkia leo.

  JB Julius Bett
 1604. MPIGA PICHA MKONGWE JOSEPH SENGA AFARIKI DUNIA: Joseph Senga alikuwa mpiga picha bora 2012 kwa kupiga picha ya kuuawa kwa Daudi Mwangosi akiwa Kampuni ya Free Media

  JB Julius Bett
 1605. AJALI MULEBA KAGERA:Wanafunzi watatu wa Shule ya Sekondari Gwanseri Muleba wamekufa baada ya kugongwa na gari wakielekea shuleni leo asubuhi Polisi yathibitisha

  JB Julius Bett
 1606. KESI YA UCHAGUZI: Mbunge wa Pangani, Juma Aweso ameshinda kesi ya kupinga ushindi wake iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea jimbo hilo kupitia CUF, Amina Mwidau.

  JB Julius Bett
 1607. UWEKEZAJI SIMBA: Mohammed Dewji amesema yupo tayari kusimamia mchakato wa usajili Simba iwapo wanachama watakubali mfumo wa uwekezaji wa hisa kwenye klabu hiyo.

  JB Julius Bett
 1608. KESI YA UCHAGUZI: Wabunge wa Chadema Peter Lijualikali wa Kilombero na Suzan Kiwanga wa Mlimba wameshinda kesi za kupinga matokeo ya ushindi wao.

  JB Julius Bett
 1609. MIKUTANO YA SIASA: Katibu Mkuu wa Chadema Dkt Vicent Mashinji leo amesema mkakati wa Chadema kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima Septemba 1 uko palepale.

  JB Julius Bett
 1610. MAHAFALI YAZUIWA: Uongozi wa chuo kikuu cha Muhimbili umewazuia wahitimu wa kikristo chuoni hapo kufanya mahafali ambayo mgeni rasmi alikuwa Edward Lowassa leo.

  JB Julius Bett
 1611. MKURUGENZI ATENGULIWA: Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo Azimina Mbilinyi kwa kutoridhishwa na utendaji wake wa kazi.

  JB Julius Bett
 1612. MREMA AAGIZA: M/kiti wa Bodi ya Parole, A. Mrema leo awapa siku 7 waendesha bodoboda Kinondoni kuorodhesha majina ya polisi wanaowalazimisha kutoa rushwa ili ayakabidhi kwa rais Magufuli.

  JB Julius Bett
 1613. Meneja wa mwanamuziki wa kimataifa Diamond Platnumz, Hamis Tale Tale maarufu kwa jina la ‘Babu Tale’ hivi sasa yupo mikononi mwa polisi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

  Babu Tale amekamatwa leo na kufikishwa mahakamani hapo ili ajieleze ni kwa nini asifungwe kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya Mahakama iliyomwamuru alipe fidia ya Sh250 milioni kwa makosa ya kuvunja sheria ya Hakimiliki.

  Babu Tale anatakiwa alipe fedha hizo kutokana na kuvunja mkataba kati yake na Shekhe Mbonde, kwa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya shekhe huyo, jambo ambalo ni kinyume na haki miliki.

  JB Julius Bett
 1614. AJALI KAGERA: Watu 2 akiwemo askari wa JWTZ wamefariki baada ya gari walilopanda kuacha njia na kupinduka huko Kanazi wilayani Ngara, Polisi yathibitisha leo.

  JB Julius Bett
 1615. USAJILI SIMBA: Mfanyabiashara na mwanachama wa timu ya Simba, Mohammed Dewji leo amekabidhi hundi ya Sh100m kwa uongozi wa klabu hiyo kusaidia usajili.

  JB Julius Bett
 1616. AJALI YAUA DODOMA: Watu 4 wafa, 29 wajeruhiwa wakitokea msibani kuamkia leo kijiji cha Dino, kata ya Kolo wilayani Kondoa baada ya basi dogo walilokodi kuelekea Moshi, Kilimanjaro kupata ajali Kondoa.

  JB Julius Bett
 1617. MOTO ARUSHA: Moto waunguza mabweni 2 katika Shule ya Sekondari Nanja iliyopo wilayani Monduli leo asubuhi, muda ambao wanafunzi walikuwa madarasani. Viongozi watarajiwa kuzuru eneo la tukio huku uchunguzi wa tukio hilo ukianza.

  JB Julius Bett
 1618. TUHUMA MBEYA: Kamanda wa Polisi Zahir Kidavashari asema vijana 2; Mosses Mwaifunga na Meshack Mgaya wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuandaa na kusambaza ujumbe kupitia mitandao ya kijamii ukihamasisha watu wakachome ofisi za CCM za mkoa wa Mbeya.

  JB Julius Bett
 1619. ZIARA YA WAZIRI MKUU MOROGORO: Wanakijiji wa Nguruandege wilayani Mvomero wasimamisha msafara wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wamtaka atatue kero za ardhi, maji, elimu ambazo zinawakabili. PM aagiza Halmashauri ya Mvomero kuzitatua.

  JB Julius Bett
 1620. Ndege ya Shirika la Emirati iliyokuwa ikijiandaa kutua katika Uwanja wa Kimataifa wa Dubai imewaka moto na kusababisha taharuki kubwa kwa abiria waliokuwamo kwenye ndege hiyo.

  Ndege hiyo Boeing 777 ilikuwa na abiria 282 na wafanyakazi 18 na hakuna aliyejeruhiwa. Abiria wote waliokolewa kupitia mlango wa dharura wa ndege hiyo iliyouwa ikiruka kutoka Trivvandrum, India.

  JB Julius Bett
 1621. Rais wa Ufaransa, Francois Hollande amemshambulia hadharani mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump akiyataja matamshi yanayotolewa na mgombea huyo kama yanayotia kichefuchefu.

  Hollande amemshutumu Trump kutokana na matamshi yake makali dhidi ya wazazi wa mwanajeshi wa Marekani aliyefia vitani nchini Iraq akisema yanatia fedheha.

  JB Julius Bett
 1622. Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limemnyima kibali cha kutengeneza video vya wimbo mpya mwanamuziki, Snura Mushi kwa madai kuwa hajatimiza masharti aliyopewa baada ya kufungiwa miezi mitatu iliyopita.

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam mwanamuziki huyo alisema ameshindwa kutengeneza video ya wimbo wake mpya Shindu baada ya Basata kumnyima kibali mpaka atakapotimiza masharti aliyopewa, moja likiwa ni kutengeneza video mpya ya wimbo Chura.

  JB Julius Bett
 1623. Waziri wa Kilimo, Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba amesema Serikali itaanza mchakato wa kutafuta mwekezaji ndani na nje ya nchi ili kufufua kiwanda cha chai cha Dabaga kilichosimamisha shughuli zake miaka 20 iliyopita.

  Kusimama kwa kiwanda hicho kumesababisha wakulima wa chai wilayani humo ambao wanamiliki zaidi ya hekta 9,000 za mashamba ya chai kukosa soko la kuuza malighafi ya zao jambo lililosababisha hasara kutokana na mazao yao kuharibikia shambani.

  JB Julius Bett
 1624. Askari polisi mstaafu wa kituo cha polisi Nansio wilayani Ukerewe, mkoani Mwanza Msafiri Bundala (52) amefariki dunia kambini kwake akisubiri stahiki zake tangu alipostaafu miaka miwili iliyopita.

  Askari huyo alistaafu Julai 2014 lakini hadi anapatwa na mauti hayo Agosti Mosi mwaka huu alikuwa akiishi katika kambi ya polisi mjini Nansio.

  Mjane wa marehemu, Paulina Ramadhan (43) aliyeachiwa watoto wanne alisema mumewe aliishiwa nguvu ghafla wakati anarejea nyumbani juzi usiku na alikufa muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali.

  JB Julius Bett
 1625. AVEVA ASHIKILIWA: Raisi wa Simba, Evans Aveva afikishwa polisi na maofisa wa Takukuru jijini Dar, Polisi Kinondoni yasema sababu za kukamatwa kutajwa baadae.

  JB Julius Bett
 1626. AJALI DAR: Mtu mmoja amekufa leo baada ya kugongwa na treni wakati akijaribu kuidandia ikiwa katika mwendo eneo la Kamata jijini Dar, Polisi Ilala yathibitisha.

  JB Julius Bett
 1627. Mahabusi wawili kati ya saba, waliotoroka wakiwa chini ya ulinzi wa polisi eneo la Mahakama ya Hakimu mkazi mjini Moshi, wametiwa mbaroni na kufungwa miaka miwili jela.

  Kutoroka kwa mahabusi hao, kulisababisha polisi 10 waliokuwa wakiwalinda kushikiliwa na polisi kwa mahojiano.

  Mahabusi hao ni Lucas Akaro (26) ambaye alijisalimisha mwenyewe kwa uongozi wa Gereza la Karanga na Charles Malenge (24), aliyekamatwa na Polisi akiwa amejificha nyumbani kwake.

  JB Julius Bett
 1628. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Yusuf Masauni ametangaza mikakati ya kupambana na ajali za barabarani nchini kwa kipindi cha miezi sita.

  JB Julius Bett
 1629. Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mwanza, Juma Sweda, ameagiza polisi wilayani humo, kumuweka ndani Ofisa Mazingira, Richard Charles kwa kosa la kuchelewa kufika kwenye eneo la mgogoro kati ya mkulima na wana kitongoji wa Mtindo “B”.

  JB Julius Bett
 1630. Mlinzi wa Shule ya Msingi Medeli katika Manispaa ya Dodoma, Zebedayo Bendera jana aliwafungia ofisini walimu kwa zaidi ya saa mbili akishinikiza kulipwa madeni ya mshahara yanayofikia Sh300,000.

  Tukio hilo lililotokea saa mbili asubuhi ni la nne shuleni hapo na kwa jana, mlinzi huyo alifanya hivyo wakati walimu walipokuwa ofisini wakijiandaa kuingia madarasani.

  Mmoja wa walimu aliyepatwa na mkasa huo, Neema Kurwa alisema kabla ya kuwafungia, mlinzi huyo aliingia ofisini kwao na kudai mshahara wake.

  JB Julius Bett
 1631. AFRIKA KUSINI. Chama cha African National Congress (ANC) kinaongoza katika matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika jana licha ya kuwa bado kinakabiliwa na hatari ya kupoteza viti katika miji muhimu.

  Chama hicho ambacho kimeiongoza Afrika Kusini tangu kumalizika kwa enzi ya ubaguzi wa rangi mwaka 1994, kinakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa vyama vya upinzani katika uchaguzi huo.

  JB Julius Bett
 1632. Wadhamini wa Ligi kuu, Kampuni ya Vodacom imekabidhi vifaa vyenye thamani ya Sh514 milioni kwa klabu 16 tayari kwa ajili ya msimu mpya wa 2016/2017.

  Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano wa Vodacom, Nandi Mwiyombella alikabidhi vifaa hivyo ambavyo ni jezi, soksi, vilinda ugoko, glovu, nguo za mazoezi, nguo za kawaida na vifaa vingine tayari kwa msimu mpya wa ligi.

  Nandi alisema Vodacom inaendelea kudhamini ligi kuu kwa kuwa soka ni mchezo unaoongoza kuwa na mashabiki si tu hapa nchini, bali duniani kote.

  JB Julius Bett
 1633. Madiwani wa halmashauri za Mkoa wa Simiyu kupitia kamati za fedha, wamepiga kauli ya mkuu wa mkoa huo Anthony Mtaka kuhusiana na ushuru wa asilimia mbili zinazotoza kwa ajili ya mfuko mmoja wa mkoa.


  JB Julius Bett
 1634. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amewasimamisha vigogo wawili wa Shirika la Ndege Tanzania (ATC) kwa tuhuma za kufanya figisufigisu katika masuala ya uteuzi wa marubani wanaotakiwa kwenda kusoma nje ya nchi.

  JB Julius Bett
 1635. Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amefikishwa Kituo Kikuu cha Polisi (Central) jijini Dar es Salaam leo saa 7.46 huku ulinzi ukiimarishwa katika maeneo yanayozunguka kituo hicho.

  Mara baada ya kufikishwa kituoni hapo, watu wengine ambao wanafika hapo kwa shida nyingine wamekuwa wakihojiwa na kisha kukaguliwa kabla ya kuruhusiwa kuingia.

  JB Julius Bett
 1636. UHABA WA VITANDA: Naibu Waziri wa Afya Hamisi Kigwangalla atoa siku 30 kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kuhakikisha Hospitali ya Mwananyamala inakuwa na vitanda 350

  JB Julius Bett
 1637. Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imesema kuwa itaanza kuwabana wenye nyumba za kupanga ili waweze kulipa kodi.

  Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

  JB Julius Bett
 1638. Benki Kuu Tanzania(BoT), imesema tatizo la noti bandia nchini ni kubwa hasa kwenye maeneo ya vijijini hali inayosababishwa na watu kutokuwa na elimu ya utambuzi wa noti halisi.

  JB Julius Bett
 1639. ZIARA YA KUSHTUKIZA: Naibu Waziri wa Afya Dk Hamisi Kigwangalla afanya ziara ya kushtukiza kwenye Kliniki ya Dk. Mwaka, asubiri kibali cha polisi ili kufanya ukaguzi.

  JB Julius Bett
 1640. AJALI MORO: Watu watatu wamekufa, nane wamejeruhiwa katika ajali ya Basi la Kisbo toka Tabora kwenda Dar iliyotokea Dumila usiku wa kuamkia leo, RPC athibitisha

  JB Julius Bett
 1641. DAWA ZA KULEVYA: Mtu mmoja amekamatwa na Polisi akiwa na dawa za kulevya kete190 za Heroin akiwa ameficha kweye chandarua huko Kingolwira Morogoro, RPC athibitisha.

  JB Julius Bett
 1642. Mahakama ya rufaa amemuondolea adhabu ya kunyongwa, Nicodemu Daudi(32) ambaye alitiwa hatiani kwa kuwaua watu wawili kwa shoka wakati alipokuwa akigomabana nao kuwadai ujira wa Sh 50,000 .

  JB Julius Bett
 1643. Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu amefikisha Mahakamani ya Kisutu saa 8. 46 huku mahakamani hapo kukiwa na ulinzi mkali.

  Ulinzi umeimarishwa katika mahakamani hapo muda mrefu wakati wakimsubiria Lissu akitokea katika kituo cha polisi kanda maalumu.

  JB Julius Bett
 1644. MKUTANO WA YANGA: Wajumbe watatu wa kamati ya utendaji ya Yanga wamevuliwa uanachama leo baada ya kudaiwa kushindwa kufanya kazi na Mwenyekiti Yusuph Manji.

  JB Julius Bett
 1645. MKUTANO WA YANGA: Wajumbe watatu waliovuliwa uanachama ni Salum Mkemi, Ayoub Nyenzi na Hashim Abdallah, mjumbe Siza Lymo amejitetea na kubakishwa kwenye kamati

  JB Julius Bett
 1646. MKUTANO WA YANGA: Mwenyekiti Yusuph Manji leo ameomba akodishwe timu hiyo kwa miaka kumi, na klabu itakuwa inapata mgawo wa 25% huku hasara zote zikiwa juu yake

  JB Julius Bett
 1647. SIMBA 'DAY': Simba yatambulisha kikosi cha wachezaji wake muda mfupi kabla ya kuanza mechi ya kirafiki kati ya klabu hiyo na AFC Leopards ya Kenya jijini Dar.

  JB Julius Bett
 1648. VURUGU DAR: Kundi la watu lavamia ofisi za NSSF zilizoko Ilala na Posta leo, Dar wakidai mafao yao baada ya kuacha kazi. Wadai kero yao ni ya muda mrefu.

  JB Julius Bett
 1649. DE BOER ASAINI: Aliyekuwa kocha wa Ajax Amsterdam Frank de Boer (46) asaini mkataba wa miaka 3 wa kuifundisha Inter Milan, uongozi wa Milan wathibitisha leo

  JB Julius Bett
 1650. MKURUGENZI MAELEZO: Waziri wa Habari Nape Nnauye leo amtangaza Hassan Abbas wa Ofisi ya Rais-Matokeo Makubwa Sasa (BRN) kuwa mkurugenzi idara ya Habari Maelezo kuziba nafasi ya Assah Mwambene, aliyehamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje.

  JB Julius Bett
 1651. STONES ATUA CITY: Manchester City yathibitisha kumsajili beki wa Everton John Stones (22) baada ya kusaini mkataba wa miaka 6 kwa ada ya pauni 47.5m. Aweka rekodi ya kuwa beki ghali zaidi England.

  JB Julius Bett
 1652. MADAI YA MAFAO: Kampuni ya ulinzi ya Optima Aviation ambayo wafanyakazi wake wameandamana ofisi za NSSF Dar leo haijawasilisha makato zaidi ya Sh100m, NSSF yasema.

  JB Julius Bett
 1653. Shule ya Msingi ya Putini iliyoko halmashauri ya jiji la Tanga yenye wanafunzi 143 wanasoma chumba kimoja baada ya shule hiyo kuwa mwalimu mmoja, chumba kimoja cha kusomea na uhaba wa madawati.

  Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Antony Saimon amesema wanafunzi hao wanalazimika kukaa darasa moja na kufundisha baada ya kukosa chumba cha kufundishia na kufundisha kwa awamu.

  Amesema hulazimika kufundisha kwa awamu tatu ambapo wanafunzi hulazimika kuja asubuhi kwa wakati kisha kukaa maeneo ya shule ili kusubiri wenzao kumaliza kipindi jambo ambalo limekuwa gumu hasa kutokana na kuwa mwalimu pekee.

  JB Julius Bett
 1654. RUNGU LA TCRA: Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania leo imevitoza faini ya jumla Sh19m vituo vya utangazaji, ITV, Clouds TV na Redio Clouds kwa kukiuka kanuni za utangazaji.

  JB Julius Bett
 1655. MSETO LAFUNGIWA: Waziri Nape Nnauye amelifungia gazeti la Mseto kwa miaka 3 kwa kudaiwa kuchapisha habari ya kugushi kuhusu N/Waziri wa Ujenzi Edwin Ngonyani.

  JB Julius Bett
 1656. KOMBE LA SHIRIKISHO: Goli la Amis Tambwe dakika 4 laipa Yanga ushindi wa 1-0 dhidi ya Mo Bejaia uwanja wa Taifa, Dar leo. Yanga yafikisha pointi 4.

  JB Julius Bett
 1657. BASATA LAMWACHIA NAY: Basata limemfungulia mwanamuziki Nay wa Mitego aliyefungiwa mwezi uliopita kwa kuimba wimbo wa ‘pale kati’, ila wimbo bado umefungiwa.

  JB Julius Bett
 1658. MAJAMBAZI MBARONI MBEYA: Polisi mkoani Mbeya wamewakamata watu 10 wanaodhaniwa kuwa majambazi, mmoja akutwa na risasi 10 za SMG na sare za Jeshi la Wananchi.

  JB Julius Bett
 1659. AKILIMALI APIGWA 'STOP': Umoja wa matawi ya Yanga umemsimamisha uanachama Katibu wa Baraza la Wazee, Ibrahim Akilimali kwa kosa la kumdhalilisha mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Manji.

  JB Julius Bett
 1660. MOTO SHULENI: Moto waunguza bweni la wavulana katika Shule ya Sekondari Mlangiri iliyopo wilaya ya Arumeru, Arusha leo, polisi yawahoji watu 4 wakiwemo walimu 2

  JB Julius Bett
 1661. SARE ZA POLISI: Wasanii wa kundi la vichekesho la Orijino Komedi watachukuliwa hatua za kisheria kwa tuhuma za kuvaa sare za polisi kwenye harusi ya mwenzao Emmanuel Mgaya ‘Masanja’, Jeshi la Polisi lasema leo.Chat Conversation End

  JB Julius Bett
 1662. UJAMBAZI KAGERA: Watu 2 wamejeruhiwa kwa kupigwa risasi baada ya kuvamiwa na majambazi wakiwa nyumbani katika kijiji cha Makulinzi wilayani Ngara, Kamanda Augustine Olomi athibitisha.

  JB Julius Bett
 1663. WANAFUNZI HEWA: Mkuu wa wilaya ya Arusha, Mrisho Gambo amesema wilaya hiyo imebaini wanafunzi hewa 907 katika shule za Msingi 12 ambao wamesababisha hasara ya Sh3.9m. Ameagiza wakuu wa shule hizo wajieleze.

  JB Julius Bett
 1664. UTEUZI WA JPM: Rais Magufuli amemteua Mrisho Gambo kuwa mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha na kuchukua nafasi ya Felix Ntibenda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

  JB Julius Bett
 1665. UMILIKI ARDHI: Waziri Lukuvi amefuta umiliki wa ardhi ya raia wa Uingereza George Rogers Bukoba Kagera na kuagiza Uhamiaji kuchunguza kibali chake kuishi nchini

  JB Julius Bett
 1666. Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Ally Hapi amemuagiza mkurugenzi wa manispaa hiyo kumsimamisha kazi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala, Delila Mushi kutokana na kuwapandishia wagonjwa bei ya kadi ya kumuona daktari.

  JB Julius Bett
 1667. IGP AWAAGA ASKARI 14 WA KIKOSI MAALUM CHA POLISI (S.F.U)-IGP Ernest Mangu awaaga askari 14 wa kikosi maalum cha Jeshi la Polisi wanaokwenda Jordan kwa kozi maalum ya kupambana na uhalifu na wahalifu.

  -->

  1.Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akimuuaga PC Prosper Yenda yenda wa kikosi maalum cha Jeshi la Polisi ( S.F.U) ambaye ni miongoni mwa askari 14 wanaokwenda nchini Jordan kwa kozi maalum ya kupambana na uhalifu na wahalifu (Picha na Tamimu Adam- Jeshi la Polisi).

  JB Julius Bett
 1668. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akiwa katika picha ya pamoja na askari 14 wa kikosi maalum cha Jeshi la Polisi (S.F.U) ambao wanaokwenda nchini Jordan kwa kozi maalum ya kupambana na uhalifu na wahalifu. (Picha na Tamimu Adam- Jeshi la Polisi)

  JB Julius Bett
 1669. MALIPO HEWA: Polisi Arusha yathibitisha kumshikilia mwenyekiti wa zamani wa chama cha wakulima Tanganyika Meinard Swai akidaiwa kuidhinisha Sh 58m malipo hewa.

  JB Julius Bett
 1670. KESSY RASMI YANGA: Kamati ya Sheria na Hadhi ya wachezaji yapitisha usajili wa timu za Ligi Kuu na kumuidhinisha Hassan Kessy kuichezea Yanga , TFF yathibitisha

  JB Julius Bett
 1671. KIBALI CHA UWEKEZAJI: Waziri Lukuvi aagiza kituo cha uwekezaji TIC kumfutia kibali cha uwekezaji raia wa Uingereza George Rogers akidai kilitolewa kimagendo.

  JB Julius Bett
 1672. BI SHAKILA AFARIKI: Mwimbaji mkongwe wa Taarabu, Bi Shakila Said amefariki dunia ghafla akiwa nyumbani kwake huko Mbagala Charambe kuamkia leo, Rais wa Shirikisho la Muziki Addo November athibitisha.

  JB Julius Bett
 1673. BODI YA WADHAMINI: Waziri wa Afya Ummy Mwalimu awateua wajumbe saba wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, asema uteuzi huu ni wa miaka 3.

  JB Julius Bett
 1674. SEPTEMBA MOSI: Msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi asema wanasiasa wanaojiandaa na maandamano ya Septemba Mosi, mwaka huu kusubiri hatma ya meza ya mazungumzo Agosti 29-30 yanayoratibiwa na Baraza la Vyama vya Siasa.

  JB Julius Bett
 1675. UJAMBAZI DAR: Askari 4 wameuawa baada ya majambazi 14 kuvamia benki ya CRDB, tawi la Mbande, Temeke. Kamanda Sirro asema kadhaa wamekamatwa, msako waendelea.

  JB Julius Bett
 1676. MAAFA ITALIA: Watu wasiopungua 6 wafa, wengi wafukiwa kwenye vifusi baada ya tetemeko la kipimo cha Richter 6.2 kutokea jijini Perugia, Italia leo asubuhi

  JB Julius Bett
 1677. UTEUZI MPYA: Rais John Magufuli amewateua Dk Modestus Kipilimba kuwa mkurugenzi mkuu, Robert Msalika naibu mkurugenzi mkuu Idara ya Usalama wa Taifa, taarifa Ikulu yasema leo. Dk Kipilimba kuapishwa leo mchana.

  JB Julius Bett
 1678. MAAFA ITALIA: Maofisa Italia wasema vifo vyafikia 20 huku utafutaji wa miili mingine iliyofukiwa kwenye vifusi ukiendelea baada ya tetemeko kutokea Perugia

  JB Julius Bett
 1679. AJALI GEITA: Watu watatu wahofiwa kupoteza maisha baada ya gari lililokuwa limebeba soda kuwagonga katika eneo la Nyamigota Geita leo, taarifa zaidi kukujia.

  JB Julius Bett
 1680. MKURUGENZI NIDA: Rais Magufuli leo amemteua Andrew Wilson Massawe kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)

  JB Julius Bett
 1681. LEMA ASHIKILIWA: Mbunge Godbless Lema anashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kukamatwa akiwa nyumbani kwake alfajiri ya leo, Meya wa Jiji Arusha athibitisha.

  JB Julius Bett
 1682. UJAMBAZI DAR: Kumeripotiwa majibizano ya risasi kati ya Polisi na watu wanaodaiwa kuwa majambazi huko Vikindu Dar, yadaiwa askari mmoja auawa, taarifa zaidi kukujia

  JB Julius Bett
 1683. TAARIFA ZA ARDHI: Wizara ya ardhi yazindua mfumo wa kielektroni wa taarifa za ardhi mkoani Dar, Waziri Lukuvi asema mfumo huo utadhibiti utapeli kwenye ardhi.

  JB Julius Bett
 1684. UJAMBAZI MKURANGA: Majambazi ambao idadi yao haijajulikana wanadaiwa kuuawa katika mapigano na polisi huko Vikindu Mkuranga, Polisi waanza kutoka eneo la tukio.

  JB Julius Bett
 1685. KUPATWA KWA JUA: Bodi ya Utalii (TTB) yasema tukio la kupatwa kwa jua Sept 1 litakaloshuhudiwa vizuri Mbeya, Njombe litafungua milango utalii Nyanda za Juu Kusini

  JB Julius Bett
 1686. KUPATWA KWA JUA: Watalii na watafiti kutoka nje na ndani wataelekea Njombe na Mbeya kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua Septemba Mosi, mwaka huu.

  JB Julius Bett
 1687. UJAMBAZI MKURANGA UPDATE: Polisi yaweka kizuizi cha barabara eneo la Kongowe, wilayani Mkuranga, magari yote yanayotoka na kuingia Dar yanapekuliwa.

  JB Julius Bett
 1688. Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa uliokuwa ufanyike Agosti 29-30 kujadili hali ya kisiasa nchini umesogezwa mbele hadi Septemba 3-4 ili kutoa fursa kwa wazee mashuhuri kuhudhuria.

  JB Julius Bett
 1689. LEMA AGOMA KULA: Mbunge Godbless Lema amegoma kula chakula tangu jana baada ya kudaiwa kunyimwa dhamana, Mwenyekiti wa Chadema Arusha Amani Golugwa asema leo.

  JB Julius Bett
 1690. POMBE YENYE SUMU: Watu 52 wamelazwa katika zahanati ya Lyangwenyi Songea kwa kudaiwa kunywa pombe aina ya togwa yenye sumu, Mkuu wa Wilaya ya Songea athibitisha

  JB Julius Bett
 1691. LEMA MAHAKAMANI: Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema afikishwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kwa makosa ambayo bado hayajajulikana, taarifa zaidi baadaye.

  JB Julius Bett
 1692. REDIO ZAFUNGIWA: Waziri wa Habari Nape Nnauye amevifungia vituo vya redio vya Magic FM na Redio 5 ya Arusha kwa madai ya uchochezi.

  JB Julius Bett
 1693. SAKATA LA CUF: Baraza Kuu la CUF limesitisha uanachama wa Prof Lipumba na wengine kumi akiwemo Magdalena Sakaya kwa tuhuma mbalimbali, watakiwa kujieleza.

  JB Julius Bett
 1694. CHADEMA WAZINGIRWA: Polisi wamezingira Hoteli ya Giraffe jijini Dar kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Chadema mchana huu, wataka kikao hicho kivunjwe, Afisa Habari Tumaini Makene asema.

  JB Julius Bett
 1695. LEMA AACHIWA: Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha leo imemuachia Mbunge wa Arusha, Godbless Lema kwa dhamana baada ya kulala mahabusu kwa siku tatu bila kula.

  JB Julius Bett
 1696. CHADEMA WAAHIRISHA UKUTA: Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe leo ametangaza kuahirisha mikutano yote ya kisiasa na maandamano kwa muda wa mwezi mmoja.

  JB Julius Bett
 1697. JPM ATEUA: Rais John Magufuli leo amemteua Doto James kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango kuchukua nafasi ya Dk Silvacius Likwelile.

  JB Julius Bett
 1698. Kitendo cha wabunge wa upinzani kutoka Bungeni haikuwa maaamuzi ya Chadema pekee bali maamuzi ya UKAWA
  -Mwenyekiti CHADEMA, FREEMAN MBOWE
  JB Julius Bett
 1699. Viongozi mbalimbali wametuomba na wametusihi kusitisha UKUTA
  -Mwenyekiti CHADEMA,Freeman Mbowe
  JB Julius Bett
 1700. UTHIBITISHO: Rais John Magufuli amemthibitisha Gerson Msigwa kuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, Ikulu yaeleza.

  JB Julius Bett
 1701. MADENI YA NHC: Madalali wa NHC watoa nje vifaa vya gazeti la Tanzania Daima leo kutokana na deni analodaiwa mmiliki wake F.Mbowe, Mhariri Mtendaji athibitisha.

  JB Julius Bett
 1702. KINACHOENDELEA RUJEWA ASUBUHI HII

  --Umati wa watu wamiminika Rujewa, Mbarali kushuhudia kupatwa kwa jua kipete

  JB Julius Bett
 1703. KUPATWA KWA JUA TZ: 11:03 Takribani theluthi moja ya jua imefunikwa na mwezi

  JB Julius Bett
 1704. KUPATWA KWA JUA: 11:33 Zaidi ya nusu ya jua imekwishafunikwa, kaubaridi kameanza.

  JB Julius Bett
 1705. KUPATWA KWA JUA TZ: Waheshimiwa Chiku Galawa na Amos Makalla wakishuhudia

  JB Julius Bett
 1706. KUPATWA KWA JUA: RC Makalla: Wanafunzi wamejifunza na watu wazima wameshuhudia kupatwa kwa Jua Tanzania . Hii ni fursa kwa utalii Mbeya

  JB Julius Bett
 1707. KUPATWA KWA JUA TZ: RC Makalla awaaga wananchi Rujewa baada ya kupatwa kwa Jua Tanzania. Awataka waendelee kuburudika baada ya tukio hilo la kihistoria

  JB Julius Bett
 1708. KUPATWA KWA JUA TZ: Kuapatwa kwa Jua tena kunaelezwa na wataalam wa anga kuwa kutatokea 2032

  JB Julius Bett
 1709. Katika kile kinachoonekana kutaka kuwadhibiti watu wanaodaiwa kuficha fedha, Rais John Magufuli amesema kwa mamlaka aliyonayo anaweza kuamua kubadili fedha ili zile zinazofichwa na watu hao wakose mahali pa kuzipeleka.

  JB Julius Bett
 1710. Taasisi ya Twaweza imefanya utafiti na kubaini kwamba mwaka 2014, mwalimu mmoja alikuwa anafundisha darasa lenye wastani wa wanafunzi 83 licha ya sera ya elimu na mafunzo kupendekeza mwalimu mmoja afundishe wanafunzi 45.

  JB Julius Bett
 1711. Shirika la Maji Safi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO) limetangaza kuzima mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Juu kwa wakazi wa Dar es salaam na Mji wa Kibaha Pwani kwa saa 14 kesho Ijumaa kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa tano usiku.

  JB Julius Bett
 1712. Rais John Magufuli atua Pemba muda mfupi uliopita akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli baada ya mapokezi yaliyombatana na kikundi cha ngoma, ameenda kuzulu kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais, Dk Omary Ali Juma. Baadaye saa tisa alasiri atafanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa Gombani ya Kale, Pemba. Picha na Ikulu

  JB Julius Bett
 1713. DENI LA NHC: Madalali wa NHC leo wameendelea kutoa vifaa kwenye jengo la Club Bilicanas inayomilikiwa na F. Mbowe kutokana na deni la Sh1 bilioni analodaiwa.

  JB Julius Bett
 1714. Rais John Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli waweka mashada ya maua katika kaburi la Marehemu Dk Omary Ali Juma katika Kijiji cha Wawi Bigilini - Pemba

  JB Julius Bett
 1715. Mke wa Rais Magufuli, Mama Janeth Magufuli aweka mashada ya maua katika kaburi la Marehemu Dk Omary Ali Juma katika Kijiji cha Wawi Bigilini - Pemba

  JB Julius Bett
 1716. HITILAFU YA SIMU: Kampuni ya Samsung imeagiza kurudishwa kiwandani simu zake mpya za Galaxy Note 7 baada ya kuripotiwa hitilafu ya kulipuka wakati zinapochajiwa

  JB Julius Bett
 1717. ZIARA YA JPM Z’BAR: Rais John Magufuli leo wakati wa ziara huko Pemba atahadharisha watu wanaovuruga amani nchini, aahidi kuwashughulikia.

  JB Julius Bett
 1718. ZIARA YA JPM Z’BAR: Rais John Magufuli leo amemuomba rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kupunguze ‘upole’ katika utendaje wake.

  JB Julius Bett
 1719. UJAMBAZI TANGA: Majambazi wafunga barabara kwa magogo eneo la Michungwani wilayani Handeni usiku wa kuamkia leo na kuwapora abiria simu na fedha, polisi waeleza

  JB Julius Bett
 1720. ZIARA YA JPM Z'BAR: Rais wa Zanzibar Dkt Shein leo amesema hakutakua na Serikali ya mpito Zanzibar na serikali yake ni halali kikatiba kwa mujibu wa uchaguzi.

  JB Julius Bett
 1721. MKUTANO WA CUF DAR: Polisi wapiga risasi hewani kuwatawanya wafuasi wanaodaiwa kuwa wa Prof Lipumba waliotaka kuingia kwenye mkutano huo.

  JB Julius Bett
 1722. MTAKATIFU TERESA: Baba Mtakatifu Francis amemtangaza Mama Teresa kuwa Mtakatifu katika Ibada ya Misa inayofanyika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican.

  JB Julius Bett
 1723. JAFO APATA AJAL